Zitto tena kachafua hali ya hewa bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto tena kachafua hali ya hewa bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hon.MP, Aug 1, 2012.

 1. H

  Hon.MP Senior Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu kila mara wanajiuliza kwa nini kila siku, kila mara, kila mahala ni Zitto, Zitto, Zitto hadi inatia kichefuchefu
  Ukweli ni kwamba ni yeye anapenda iwe hivyo kwa kuwa hajakamilisha kazi aliyotumwa. Mpaka pale itakapokamilika, tutaendelea kusikia vitimbwi na show mbalimbali za huyu kijana.


  Akihitimisha mchango wako Bungeni, Zitto kasema, “ nilipewa mchango na Tundu Rissu lakini mwandiko wake ni mbaya sana kwa hiyo nimeshindwa kuusoma”. Tujiulize:


  1. Je, kweli kulikuwa na ulazima wa yeye kutamka au kutoa taarifa hiyo Bungeni? Faida yake ni nini maana haiongezi chochote (katika mchango wake) wala hawezi kuwahi nafasi kwamba pengine Rissu akirudi basi akute nafasi aliyo ‘bukiwa’ na mwenzake.


  2. Hata kama ilikuwa lazima aseme, Je, ilikuwa lazima atamke sababu na kuchagua maneno ‘mwandiko mbaya sana?' angalia kuna kivumishi ‘sana’ kama vile ‘mbaya’ haingetosha!


  Si kwamba Zitto ni mzito wa kuelewa, la hasha, anafanya makusudi akijua kuwa mambo kama haya ya kuwadhalilisha wenzake yanaweza kuleta vurugu ndani ya chama na hivyo kukisambaratisha.


  Amenihudhi sana, kama si kweli yanayosemwa juu yake, kwa nini asingekaa tu na kutulia kisha aje amweleze Rissu sababu iliyofanya asiwasilishe ujumbe wake. Au kama kwa hekima yake ambayo inashangaza bado aliona ni lazima kutoa taarifa hiyo ya makabidhiano ambayo Wabunge wengine hawahusiki na wala haiongezi chochote cha maana kwenye hansad ,kwa nini asingesema tu kuwa ‘nilipewa mchango na Mbunge mwenzetu lakini kwa bahati mbaya nimeshindwa kuusoma’ .  Kweli sasa tunaaamini, kazi ya double agency ni ya kipuuzi sana maana ni ya kutekeleza kile usichoamini na kuamini kile usichotekeleza! Zitto hawezi kuaminika tena katika jamii ya wasema kweli.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  Hayo ndio Matatizo Madogo Madogo ya ZITTO KABWE - HE THINKS HE's ALL THAT(HATARI KWA MWANA SIASA); UUMPE NCHI kweli hizo

  kejeli zake wako ambao watazichukua kiukweli na atasababisha Madhara; Afadhali huyu tuliliyenaye Sasa Jakaya Kikwete - Hasemi

  Chochote hatujui Msimamo Wake tunavurugana... lakini yuko bubu... ZITTO KABWE ataibebe Tanzania na kuigeuza up-side down...

  * Hafurahi TUNDU LISSU hakumtaja kati ya Wabunge Mafisadi? Hiyo Ndio Shukrani? Kumtangaza kuwa Maandishi yake Mabovu...?
   
 3. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama anamwandiko mbaya kweli asiseme?
   
 4. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  twendeni tukachangie mambo ya maana kwenye Thread nyingine....
   
 5. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hon.MP, Rissu ndiyo nani?
   
 6. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Nape kwani nae yumo??? Shiiit!!! hii nchi nimebaki mimi tu kutangaza nia
   
 7. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nashukuru kuona na wewe umesikia hivyo ndugu. Maana kuna uzi nilianzisha watu wakanitukana kweli kweli na kuomba nipigwe ban. Mpaka nikahisi nilikuwa nasikiza mzimu au!!. na uzi ukafutwa!. Sijui kama na huu utakuwa na muda mrefu. Sidhani kama hapa kuna suala la Ugamba au Ugwanda. ndivyo alivyosema. Kama mtu utapigwa ban kwa kuandika ukweli humu JF basi sina haja ya kuwa member tena hapa JF.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Guys u need to have a great sense of humour.. Ur so sensitive nyie watu
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  To the public? for what reason? Huyu siku 3 zilizopita aliwataja MAFISADI wa Tanesco hakumtaja ZITTO KABWE sababu

  Haamini kuwa Mwanachama Mwenzake ni Sisimizi wa ulaji Mchafu; wa kiuhaini wa kulaghai nchi nzima...

  Yeye ni kubwatuka - Oh Mwandiko Mbaya... Yeye chochote ni Ubwatukaji... NDIO APEWE URAIS????
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,953
  Trophy Points: 280
  Ule ulikuwa utani wa kibunge tuu,kwanza muda wake ulikuwa umekwisha na pia alitaka watu wajue kuwa kuna kawaida ya kupeana mawazo mtu anapochangia. Hakuna baya hapo.
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  U QUICK TYPO ERROR it was ZITTO KABWE; LOL -- TOO QUICK TO MAKE A MISTAKE? LOVE JAMII FORUMS!!!
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Zitto una kera sana! Unajiona wewe ndio wewe! Are you parfect? I hate u kwakweli.
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Hiki cheo cha urais CDM kitawatafuna mpaka muishe, na kweli waacheni wafu wawazike wafu wenzao. Na Mh. Rissu , ndio nani?
   
 14. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ZITTO KABWE hafai CCM,CHADEMA,TLP,NCCR,UDPP,SERIKALINI na popote pale kwani hekima, busara na uwezo wa kupima mambo ni muhimu kwa binadamu yeyote kwani ulimi unauwezo wa kuondoa amani katika jamii yoyote kwa muda mfupi sana.aende zake hukohuko kwa KAGAME.
   
 15. M

  Mpwechekule JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla ya hii ya leo nilikuwa najua zito ana mtazamo fulani ambao unapishana na wenzake, kumbe ni janga naviongozi wa chadema kaeni vizuri maana itakuwa ngumu 2015 kama kuna mamluki kama huyu na bila ana wenzake humo
   
 16. m

  manucho JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hakika katumwa huyo, mwisho wake umefika kama hataki akamuulize Masumbuko Lamwai
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Zitto ni mwanasiasa anayekufa huku akijiona.
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Usijali mkuu unajua watu walikuwa hawaamini kama kweli Zitto anaweza kuongea mambo ya kitoto kiasi hicho kutoka na kumu amini sana. Na mimi ni melaani sana kitendo alicho fanya zitto eti wengine wanamtetea eti alikuwa ana tania. Usivunjike moyo kwenye wengi kuna mengi!
   
 19. ha ha ha

  ha ha ha JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 641
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Niliiona kama kauli ya kimbea flani hivi, HEAVY amebadilika anajifanya ndo kila kitu kwenye siasa, alikuwa tishio zaman. Wasiwasi wangu ni kuwa anaweza akadhani anatumika kuarbu chama kumbe wanamtumia yeye kujiaribia binafsi. Kiukweli TL ana uwezo wa uelewa ukimlinganisha na Nzito,mara kadhaa TL ameitwa kutoa mawazo kwenye tribunals za kimataifa,hoja ya Nzito ya mwandiko ni ya kitoto na haikuwa na jipya. Tunanmwangalia mwanasiasa huyu kijana tunapata dalili mbaya juu yake. Mda unao jirekebishe.
   
 20. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Nilifikiri sijasikia vizuri hiyo kauli!Ni heri awe anafanya utani ambao hatukuuelewa.
   
Loading...