Zitto: Taarifa ya TRA kukusanya trilioni 2 ni ya kubumba

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,143
2,000
Zitto Kabwe ameandika hivi kwenye ukurasa wake wa Twitter

“Taarifa ya makusanyo ya kodi iliyotolewa na TRA leo kuwa Desemba wamekusanya shs 2T naamini ni ya kubumba.

Nachambua Taarifa za Benki Kuu za mapato kulinganisha na Taarifa ya TRA.

Nitaonyesha kwa ushahidi kuwa TRA wamedanganya Umma.”

291D0433-4E7A-46FE-8BA2-9B8469748169.jpeg


Soma >> TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,443
2,000
Taarifa ya makusanyo ya kodi iliyotolewa na TRA leo kuwa Desemba wamekusanya shs 2T naamini ni ya kubumba. Nachambua Taarifa za Benki Kuu za mapato kulinganisha na Taarifa ya TRA. Nitaonyesha kwa ushahidi kuwa TRA wamedanganya Umma.
Hakuna muujiza wowote ule. Kilichofanyika sasaivi ni hela zote za serikali zinakusanywa na TRA. Kama hadi mamlaka za Ngorongoro na Tanapa na uhamiaji zimenyang’anywa kukusanya mapato ya utalii na imepelekewa TRA hizo figures wala hazishangazi.

Tena utalii ukirudi kwenye hali yake tutakuja kutangaziwa imefikia hata trillion 4 na washamba wakashangaa kumbe hizo hela zilikuwepo tangu zamani sema zilikuwa zinaingia serikalini kupitia taasisi nyingine.
 

King klax

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
3,128
2,000
Kwa Nchi kama Tz najua ni tarakimu tu hizo,, mwache mgema asifiwe kidogo,,tutaona baada ya utawala huu kuisha
 

Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,412
2,000
Taarifa ya makusanyo ya kodi iliyotolewa na TRA leo kuwa Desemba wamekusanya shs 2T naamini ni ya kubumba. Nachambua Taarifa za Benki Kuu za mapato kulinganisha na Taarifa ya TRA. Nitaonyesha kwa ushahidi kuwa TRA wamedanganya Umma.
Leo kwakuwa zito amepinga kazi nzuri za serikali, huko ufipani kawa shujaaa gafla. Ndiomaaana mumekimbia hapa kuposti fastaa
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,852
2,000
Hakuna muujiza wowote ule. Kilichofanyika sasaivi ni hela zote za serikali zinakusanywa na TRA. Kama hadi mamlaka za Ngorongoro na Tanapa na uhamiaji zimenyang’anywa kukusanya mapato ya utalii na imepelekewa TRA hizo figures wala hazishangazi. Tena utalii ukirudi kwenye hali yake tutakuja kutangaziwa imefikia hata trillion 4 na washamba wakashangaa kumbe hizo hela zilikuwepo tangu zamani sema zilikuwa zinaingia serikalini kupitia taasisi nyingine.
Kwani TRA kukusanya mapato kwenye hizo mamlaka wameanza mwezi uliopita wa December? kama walikuwa wanakusanya toka miezi iliyotangulia kwanini hayo mapato TRA wakawa hawayatangazi kila mwezi wanavyopenda sifa? ukweli ni kwamba mapato yalishuka.

Hata hiyo sekta ya utalii unayoizungumzia imeathirika sana kwa janga la Corona, hakuna wageni, ni kipi kilichowainua mwezi wa December mpaka mapato yao yaongezeke hivyo?
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,948
2,000
2T sio ajabu kwa kuwa sasa hivi hata pesa zilizokuwa zinapitia TANAPA huko wanakusanya hawa watu. Zitto hata asipoteze muda wake kujaribu kudadavua data.
Ukizingatia ,pesa yetu kwa Sasa haina thamani zisi ya $.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom