Zitto surgery tayari na anaendelea vizuri

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
MADAKTARI wa Hospitali ya Apollo India, wamefanikiwa kumfanyia operesheni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alipelekwa huko wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kipanda uso.

Kaka wa Mbunge huyo, Salum Mohammed aliliambia gazeti hili jana kuwa operesheni hiyo iliyotumia muda wa saa nne, ilifanyika salama na hali yake inaendelea vizuri. "Walianza kumfanyia operesheni saa 4:00 asubuhi na ilikamilika kwenye saa 8:00 mchana. Kwa sasa (Zitto) anaendelea vizuri.

Tayari amezinduka, amekunywa juisi na sasa (jana) amepumzika," alisema Mohammed. Alisema operesheni ilifanywa na jopo la madaktari lililoongozwa na Dk Sunil Narayan Dutt ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya kinywa, njia ya kupumua na kichwa na pia ndiye mkuu wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Appolo. Mohammed alisema madaktari hao walieleza kwamba aina ya operesheni hiyo huwa haihusishi upasuaji wa fuvu.

"Walichokifanya ni kuingiza chombo maalumu puani na kwa kutumia kompyuta, waliweza kuona kila kitu na ndipo wakaanza kufanya operesheni kwa kuona kupitia kompyuta," alisema Mohammed.

Alisema operesheni ilifanyika kikamilifu na Naibu Katibu Mkuu huyo wa Chadema anaendelea vizuri na hakuna tatizo lolote ambalo linamsibu kutokana na upasuaji huo.

"Hadi sasa anaendelea vizuri na hakuna tatizo lolote ambalo limempata kutokana na upasuaji huo. Mheshimiwa Zitto anaendelea vizuri ingawa anaonekana kuchoka kutokana na shughuli hiyo," alisema Mohammed.

Zitto alipelekwa India kwa matibabu baada ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) iliyokuwa ikimpatia matibabu kupendekeza rufaa hiyo.

Alipelekwa MNH akitokea katika Hospitali ya Aga Khan ya Dar es Salaam akitibiwa ugonjwa wa malaria.
 
So the whole thing took four hours which tells something on how serious an infliction was.

Altogether thanks God that the process went successfully and the vibrant politico has yet another lifeline to continue his campaign against irresponsible CCM. His contribution to the nation is extremely important especially during this period when everything goes chaotic.

Hoping will come back to put more pressure on the crook Mkulo until he steps down.
 
Absolute Mwita, your comment saluted.
 
Get well soon Zitto!
Hiyo process inaitwa 'ENDOSCOPY' na inafanywa kwa kutumia kifaa chenye camera iliyounganishwa na computer. Hata hivyo pale wanapopitisha hicho kifaa huacha majeraha na full recovery huchukua muda kidogo.
 
So the whole thing took four hours which tells something on how serious an infliction was.

Altogether thanks God that the process went successfully and the vibrant politico has yet another lifeline to continue his campaign against irresponsible CCM. His contribution to the nation is extremely important especially during this period when everything goes chaotic.

Hoping will come back to put more pressure on the crook Mkulo until he steps down.
safi mwita25 kumbe una akili sana wewe
 
Mungu amsaidie apone haraka.

Jamani haya ni maradhi yepi "kipanda uso"? Jee ndio hayo tunayoyafaham kama "sinus" au mengine?

Namuombea dua za kheri, arudi salama aendelee na shughuli zake za kila siku kwa amani na furaha.

Kumbe ilikuwa si Malaria pekee kama alivyotangaza mwanzo? kweli "binaadam hujafa hujaumbika".

Nawapa pole wote wa karibu yake wanaomuuguza Mheshimiwa Zitto Mwenyeezi Mungu awape imani ya ziada na awape wepesi mumuhudumie mgonjwa kwa kila hali.
 
kwahyo Mhimbil walitupga changa la macho na vijidudu 150 vya malaria?
Inaonekana baadhi ya watu hamsomi vizuri habari zinazoandikwa. Mheshimiwa Zito alikuwa na malaria na pia alikuwa akisumbuliwa na kipanda uso kwa muda mrefu ndipo muhimbili walipogundua kuwa kuna mirija kichwani ilikuwa imeziba, ndio maana wakam refer India kwa upasuaji.

Get well soon Zito!
 
So the whole thing took four hours which tells something on how serious an infliction was.

Altogether thanks God that the process went successfully and the vibrant politico has yet another lifeline to continue his campaign against irresponsible CCM. His contribution to the nation is extremely important especially during this period when everything goes chaotic.

Hoping will come back to put more pressure on the crook Mkulo until he steps down.
Pamoja mazee kama mkulo na failures
 
malaria iligundulika muhimbili na kuanza matibabu hapo hapo. kipanda uso ni sinus, na hiyo ndo ilikua haina sababu ya kuenda kutibiwa india. japo inapokuja kwenye afya kila mtu ana-panick na kutaka awe mzima ili aendeleze mapambano. toka 80's hizi operesheni zinafanyika hapa tz, hiyo endoscopy ni mbwembwe tu!
Hiyo aliitangaza mwenyewe Zitto, inaonesha hiyo katibiwa na akaona achukuwe na fursa ya kutibiwa na mengine yaliyokutikana.

Ingekuwa mimi ndio Zitto ningekubali kufa kuonesha uzalendo kuliko kwenda kutibiwa India, hivi Muhimbili hawawezi kutibu Malaria na huo sijui unanda uso sijui nini? Mwenzake Lema kakataa dhamana. Huku anajidai kukataa posho huku kwa malaria tu mbio mbio INDIA.
 
So the whole thing took four hours which tells something on how serious an infliction was.

Altogether thanks God that the process went successfully and the vibrant politico has yet another lifeline to continue his campaign against irresponsible CCM. His contribution to the nation is extremely important especially during this period when everything goes chaotic.

Hoping will come back to put more pressure on the crook Mkulo until he steps down.
Mwita25

have a good day
 
malaria iligundulika muhimbili na kuanza matibabu hapo hapo. kipanda uso ni sinus, na hiyo ndo ilikua haina sababu ya kuenda kutibiwa india. japo inapokuja kwenye afya kila mtu ana-panick na kutaka awe mzima ili aendeleze mapambano. toka 80's hizi operesheni zinafanyika hapa tz, hiyo endoscopy ni mbwembwe tu!

Zitto aliambiwa na Professor kuwa hawezi kufanyiwa hiyo 'surgery' hapa kwetu. Sasa wewe unaleta hizi taarifa zako ili upotoshe watu tu.
 
Ndio maana huwa nasema hawa upinzani sijui nini ni uongo mtupu linapokuja swala la matibabu wakati wenzao wanakwenda kutibiwa nje wao huwa wa kwanza kujidai wanafuja hela hata Malaria tu wanaenda nje, hata mafua tu wanaenda nje, sasa kiko wapi?

Mbona hizo hizo Malaria na Mafua yamempeleka kutibiwa nje? kwa fedha hizo hizo za walala hoi.
 
Back
Top Bottom