Samia Love yarejesha Tabasamu kwa Wagonjwa wa Nyonga, Goti

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wagonjwa walionufaika na matibabu ya upasuaji wa nyonga na magoti yaliyotolewa na jopo la madaktari wa mifupa na nyonga kutoka Los Angles, Marekani Agosti mwaka huu kupitia mpango wa 'Samia Love', wamerejesha tabasamu baada ya hali zao kuimarika.

Wagonjwa 45 waliofanyiwa upasuaji huo wameanza kupata nafuu huku wengine wakianzisha shughuli zao za kiuchumi.

Madaktari hao waliweka kambi kwa muda wa siku saba kwenye Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Cente (ALMC) inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.

Akizungumza leo Jumanne Oktoba 31, 2023 wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwatembelea wagonjwa waliotibiwa kupitia mpango huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Godwill Kivuyo amesema asilimia 90 ya waliofanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri.

Naye Mratibu wa mpango huo, Lazaro Nyalandu amesema wamezindua programu ya kuwatembelea wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji ambao wako Mikoa ya Arusha, Tabora, Mwanza, Singida, Dodoma na Dar es Salaam.

Nyalandu amesema wanatembelea wagonjwa hao kabla ya kutangaza ujio wa kampeni zingine kwa ajili ya matibabu.
 
Kumbuka Kuna mambo f kk k kufunga na kfu omba. Na kuna mambo yanahitaji Pesa. Yesu alipokufa wanamaombi wenzake wakina Petro, Yoha a na Yakobo walikimbia. Tajiri Mkristo Yusuph ndiye aliyeenda kuomba mwili wa Yesu auzike. Maana ilitabiriwa atazikwa na matajiri.

Pesa sio dhambi, ni kama kisu, unaweza kuulia mtu pia kuchinjia kuku upate kitoweo.
 
Back
Top Bottom