Simwamini sana huyu dogo. Akiwa India aliwahi kudai hanampango wa kugombea urais na kusisitiza hata katiba haimruhusu. Juzi kayala matapishi yake akidai anautaka urais. Tusubiri tuoneNaibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.
Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.
Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama, alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
Mara anataka kuwa lecturer.Wanaowasiliana naye wampe ushauri. Azungumze vitu vizito kama jina lake. Kwanini anajuzungumzia yeye tuuuuuuuu. Na tena wakati huuuuuuuuuuu !!! Hapo alipo tayari ni Kiongozi kwanini anacheza na manenoooooo !!! Mara nataka kuwa Rais mara nataka kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CDM !!! Anahangaika na nini???
Ben yupi? huyu Masalia ya Zitto Kabwe yaliyopukutishwa Chadema!?......geita labda kamuachia ben saanane.ni muda nasikia yupo huko na alipost picha huku
Yaah huyo huyo ila hana ofisi maalum, ofisi yake ni JF ni mwenyekiti wa CDM tawi la JF.Ben yupi? huyu Masalia ya Zitto Kabwe yaliyopukutishwa Chadema!?......
geita labda kamuachia ben saanane.ni muda nasikia yupo huko na alipost picha huku
Maji marefu yalitokana na kuzuiwa Zitto asigombee.,Sio kwamba Mbowe na maji marefu..Ila subirini safari hii "nahisi" kamanda John Magale Shibuda atagombea uenyekiti..Exactly mkuu, walianza kumpima Mbowe wameona maji marefu
na wewe unamuunga mkono?acha ujinga wewe
Wewe ndio uache ujinga EMT kumuunga mkono au kutomuunga mkono ni haki yake ya kuchagua na uhuru wake. Mimi simwamini Zito kuwa anasifa za kuwa Rais lakini nafikri ana haki ya kugombea. Alishasema wanachama na chama chake wakiamua ndipo atakuwa mgombea. Hiyo ni ambition ila sisi ndio tutajua anafaa au hafai kugombea urais lakini ni haki yake ya kidemokrasia.na wewe unamuunga mkono?acha ujinga wewe
Alizuiwa na nani asigombee.Maji marefu yalitokana na kuzuiwa Zitto asigombee.,Sio kwamba Mbowe na maji marefu..Ila subirini safari hii "nahisi" kamanda John Magale Shibuda atagombea uenyekiti..
Ben Saanane huyu Masalia ya Zitto yaliyopukutishwa CHADEMA?.........Yaani mtu ambaye hana sifa za kuwa kiongozi kwenye Baraza la vijana atapata wapi sifa za kuwa kiongozi wa chama? hapa ndipo ninapomkumbuka Makamba Sr visisimizi kama hivi alikuwa anaviponda kwa nyundo nzito.
mkuu hilo kundi haliaminiki.hapo kuna hesabu kali sana mwana.chadema watimueni tu hao
may be anataka amwachie Nafasi ya kugombea uwenyekiti BENARD SANANE. bkoz we cant know
Yeye tayari kashasema anautaka urais. Hivi vyeo vya chini tena vya kichama ni kujishusha hadhi.