Zitto: Serikali ya Magufuli imekopa zaidi ya tril 3 toka uswisi kufadhiri SGR na Stiglers yenye riba kubwa


sawa kiongozi
 
Ndege zilinunuliwa cash tukalalamika kwanini tusichukue mkopo, SGR ilivyosemekana inajengwa kwa hela za ndani tukalalamika kwanini miradi mikubwa inatumia hela nyingi tusikope! Sasa imegundulika ni hela za mkopo napo ni tatizo!
 
Zito mbona hazungumzii ule mkopo wake wa milioni 800 bungen, na NSSF amekopa bilioni 1. 5 kufadhili ACT
Mkopo anaozungumzia Zito una uhusiano na sisi watz moja kwa moja kwani serikali isipolipa itawajibishwa nchi na inaweza kuathiri uchumi wetu.

Lakini huo mkopo wa Zito hauna mahusiano yoyote na watz kwani ni mkopo binafsi akishindwa kulipa mkopaji atawajibishwa.

Kwa utangulizi huo ninaona mchangia mada huna nia yenye afya kwa wasomaji ila kuwapumbazisha wawe wapumbavu wasiweze kutumia bongo zao kuchanganua.
Tetea maelezo yako kama ukishundwa nadhani utakuwa ni sehemu ya wale mh Rais anao waita wapumbav
 
Tufanye amekopa yeye ana atalipa yeye, kwa Nini waliomkesha hawajazingatia approval ya Bunge? Kwa hiyo Bunge sio hatua muhimu ili kukopeshwa.
Kama serikali imekopa kiasi hicho bila approval ya bunge basi lipo tatizo kubwa. Nchi haiwezi kuongozwa kwa utashi wa kisiasa wa mtu mmoja kama vile hakuna sheria!
 
Kukopa sio tatizo, ni namna ya kupata kiasi kikubwa cha hela kwa wakati mmoja ili miradi iweze kutekelezwa.

Makusanyo yetu ya ndani ambayo ndiyo tunayapata kwa kiasi yanatumika kulipa huo mkopo.
Hatuhitaji tukusanye kwanza ndiyo tuanze kutekeleza miradi wakati kuna taasisi zinafedha na zinaweza ku finance.

Fedha za ndani bado zinahusika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…