Zitto: Serikali ya Magufuli imekopa zaidi ya tril 3 toka uswisi kufadhiri SGR na Stiglers yenye riba kubwa

Acha kupiga siasa mfu hapa jukwaani, nimekuambia tuna madeni toka enzi za Nyerere na hatujalipa mpaka tumefikia mahali pa kuomba kusamehewa, je pesa zako utaomba usamehewe? Halafu usichanganye advance payment na mkopo. Kama hujui tofauti ya mkopo na advance payment rudi shule ukajifunze. Na sasa hivi elimu ni bure hivyo hakuna kisingizio.

sawa kiongozi
 
"Serikali imekubaliana na Benki ya Standard Chartered kupata mkopo wa USD 1.5 Bilioni kwa ajili ya mradi wa Reli (SGR) na Benki ya Credit Suisse USD 500 milioni kwa ajili ya miradi mingine ikiwemo Stiglers Gorge. Mikopo Hii ni ghali sana" - Zitto Kabwe >>> https://bit.ly/2K9xVWB
Ndege zilinunuliwa cash tukalalamika kwanini tusichukue mkopo, SGR ilivyosemekana inajengwa kwa hela za ndani tukalalamika kwanini miradi mikubwa inatumia hela nyingi tusikope! Sasa imegundulika ni hela za mkopo napo ni tatizo!
 
Zito mbona hazungumzii ule mkopo wake wa milioni 800 bungen, na NSSF amekopa bilioni 1. 5 kufadhili ACT
Mkopo anaozungumzia Zito una uhusiano na sisi watz moja kwa moja kwani serikali isipolipa itawajibishwa nchi na inaweza kuathiri uchumi wetu.

Lakini huo mkopo wa Zito hauna mahusiano yoyote na watz kwani ni mkopo binafsi akishindwa kulipa mkopaji atawajibishwa.

Kwa utangulizi huo ninaona mchangia mada huna nia yenye afya kwa wasomaji ila kuwapumbazisha wawe wapumbavu wasiweze kutumia bongo zao kuchanganua.
Tetea maelezo yako kama ukishundwa nadhani utakuwa ni sehemu ya wale mh Rais anao waita wapumbav
 
Tufanye amekopa yeye ana atalipa yeye, kwa Nini waliomkesha hawajazingatia approval ya Bunge? Kwa hiyo Bunge sio hatua muhimu ili kukopeshwa.
Kama serikali imekopa kiasi hicho bila approval ya bunge basi lipo tatizo kubwa. Nchi haiwezi kuongozwa kwa utashi wa kisiasa wa mtu mmoja kama vile hakuna sheria!
 
Kukopa sio tatizo, ni namna ya kupata kiasi kikubwa cha hela kwa wakati mmoja ili miradi iweze kutekelezwa.

Makusanyo yetu ya ndani ambayo ndiyo tunayapata kwa kiasi yanatumika kulipa huo mkopo.
Hatuhitaji tukusanye kwanza ndiyo tuanze kutekeleza miradi wakati kuna taasisi zinafedha na zinaweza ku finance.

Fedha za ndani bado zinahusika..
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom