Japo namkubali sana ZZK, kwenye ule uzi wangu wa , nilimweleza weakness zake, miongoni mwake ni ni hii ya kukosa subra, ustahimilivu na uvumilivu when it comes to personal attacks!. Japo kwenye suala zima la kujenga hoja na kuwasilisha hoja kuna tofauti kubwa sana kuhusu hoja hiyo imeibuliwa na nani, inajengwa na nani na inawasilishwa na nani!. (Hata ile list of shame, walioijenga tunawajua, kilichofanyika pale Mwembe yanga ni kuwasilishwa tuu). Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa ZZK katika kujenga hoja na kuwasilisha hoja ila ZZK anakabiliwa na tatizo kubwa la "ego" linalompelekea kuwa na papara hivyo kum pre empty hata M/Kiti wake!.
Katika ule uzi wangu wa "Chadema Hijajipanga" , pia nililizungumzia hili la "lack of collective responsibilities!", haiwezekani kwenye chama hicho hicho kimoja ni kila mtu anatoa kauli kuhusu jambo hilo hilo moja!. Jana JJ Mnyika, leo Zitto, kesho ndio M/Kiti!. Mlitakiwa muwe na internal discipline mechanism kuwa katika suala la gesi, msemaji ni waziri atatoa msimamo wa wizara kivuli na M/Kiti ndiye atatoa msimamo wa Chama, mlipaswa kumuita ZZK awape full disclosure ya kila anachokijua kufuatia yeye kuwa ndiye Mwenyekiti wa POAC ambapo TPDC iko chini yake!.
Japo sijui ZZK atazungumzia nini, ila kwa vyovyote itakuwa ni kujitetea kwa personal attack alizovurumishiwa na Simbachawene. ZZK ni kijana wenu, akishutumiwa, mmeshutumiwa wote kama alivyo mchuma janga, hula na wa kwao. Haiwezekana mtoto wenu ashutumiwe alafu chama kikae kimya, ndio maana kaamua kujitokeza kuja kujitetea.
Kiukweli Chadema ina tatizo kubwa na "damage control", mgemsoma Nguruvi3 kwenye
Duru za siasa - Mgongano wa mawazo kuhusu somo hilo, haya yote yasingetokea!. Kuna shutuma zikivurumishwa, zinatakiwa kujibiwa promptly na sio za kusubiri, japo ZZK ana papara na pupa katika kujibu, kama chama kingekuwa na utaratibu rasmi, ZZK asingefika hapa alipofika!.
Najua wengi wa manazi wa Chadema, mnaamini kuwa ZZK is working in favor of CCM, the time will come, mtawajua wanaoifanyia kazi haswa CCM miongoni mwenu na hamtaamini!.
Pasco.