Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Status
Not open for further replies.
maamuzi magumu yanafanywa kwa vitendo sio porojo ulikuwa unaona raha sana kung'ang'ania fulani aondoke leo imekuja kwako inakuwia vigumu kama bado unaamini una mchango katika siasa zetu sioni sababu ya kubaki chadema nenda chama kingine
 
ZZK wew utakuwa wa mwisho kutoka chadema haya ni mapito tu kaza buti, uliowafanyia kampaini kwenye majimbo yao leo ndio wenye midomo mirefu
 
Maamuzi magumu ni kuomba msamaha na sio vinginevyo
uamuzi gani kuomba radhi..aombe radhi kwa kutaka kugombea uenyekiti wa cdm?. cdm inazidi kudhihirisha haina tofauti na vyama vingine vya upinzani. inaendeshwa kama kampuni binafsi.
 
Kama chadema ingekua inaondoa maovu basi shibuda angeondoka kabla ya zitto maana alisaliti tangu sikubya kwanza alipohudhuria kuapishwa kwa JK.zitto n tishio kwa nafasi ya mbowe kama mwenyekiti.undugu,uchaga na ukatoliki ndo umemuondoa zitto CDM
 
Ujinga uliopitiliza, hivi chadema wasio wakristo ni Zitto na Arfi tu? hivi wewe ndio ulikuwa moderator wa JF mtupu hivi? jamaa waliona mbali sana kukufurusha

Eti huyo nae alikua Moderator wa JF. Ndiyo maana JF ilipita katika majaribu sana Mwaka jana
 
Hakuna lolote la maana alilosema Zitto hapo. Alipaswa kutuambia ni vipi Katiba, sheria na kanuni inayompa uhalali wa kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Ni uamuzi gani tusioujua ambao hao wazee wake wamembariki?
Kama ni kuondoka CHADEMA sio issue tena kwa kuwa CHADEMA ilishatangaza hadharani kuwa haimtaki na sasa hata uanachama imemvua.

Inavyooneka tena wazi kabisa alipanga kutimka CHADEMA mwishoni mwa mwezi huu ila mahakama na CHADEMA vikamuwahi kabla hivyo project yake imeanza kuchuja kabla ya kuzinduliwa.
 
....chadema msikubali wala kurudi nyuma,onyesheni chadema ni taasisi.Hivyo mtu kama Zito ahangaike na sheria na kanuni za chama.Kama kuna sheria ya chama inayomhukumu basi lazima ahitii.



Hakuna msafi.
Zingefuatwa kanuni leo hii mbowe angekua sio mwenyekiti wa chama mana muda wake ulishakwisha kikatiba lakini pesa ikarubuni wajumbe wakakubali kubadili katiba kwa maslahi ya Mbowe.
Ilikua ni zamu ya Zito kuwa Mwenyekiti kakini wachaga wakaona maslahi yao ndani ya chadema yako hatarini kwani Zito ni mtu wa kupenda usawa.
 
Maamuzi gani ambayo yeye anajaribu kuyazungumzia!!? Ni zaidi ya yale ambayo hufanyiwa vibaka kule mtaani kwa mujibu wa magufuli?
 
Hakuna Uamuzi Mwingine Mgumu ambao ni makini anaopaswa kufanya zaidi ya Kuomba Radhi kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA na kusonga mbele

Kwenda chama Kingine itakua uamuzi mgumu lakini sio makini
Sasa braza aombe radhi kwa kosa gani?? Kutaka mahesabu ya vyama vya siasa yakaguliwe?? Kutaka kugombea uenyekiti chadema. ?? Kuonesha nia ya urais mapema??
 
Namshangaa sana Zitto kungangana na chama cha ovyo kama chadema...chadema ni chama cha wenyewe wakina mbowe na mkwewe mtei.hiki ni chama cha wakatoliki na wakaskazini iyo ipo wazi kabisa.chadema haina jipya kama walivo ccm
 
Maamuzi Magumu afanye Zitto? ... Shibuda aliwahi kumuuliza source ya ukwasi wake hadi kununua Hummer! alimpaka ile mbaya kuwa anawadanganya wenzie asichukue ujira wa MWIHA wakati yeye amekunja za CCM, Barrick, EPA nk... alimwambia kuwa Utajiri wa Mbowe na Ndesa Pesa una ABC ... Since then Zitto na timu yake walimuingiza kundini maana alikuwa anaharibu ile mbaya... ZItto anatakiwa awasikilize wazee badala ya EGO plus tamaa ya fedha na madaraka vilivyomtia UPOGO wa kuona umbali wa pua yake ...
 
Zitto ni makini na washauri wake ni makini pia, huenda maamuzi magumu anayotaka kufanya ni kuendelea na chama kwa kuomba msamaha. Maana hakuna kitu kigumu kama kuomba msamaha.

Kuomba msamaha ni mpaka ujue kosa lako ni nin, mpaka sasa Zitto hajui kavunja kanuni gani Chadema ndio maana alisema aambiwe kosa lake ili ajirekebishe.Maana yale yaliyosemwa ni uongo wa siasa za majitaka.

Sasa ni vyema ajue kwanza kosa halisi ni lipi, kama ni kutaka kugombea uenyekiti au kutangaza kutaka urais.Akijua hilo kosa itakuwa rahisi kuomba msamaha.
 
Kama chadema ingekua inaondoa maovu basi shibuda angeondoka kabla ya zitto maana alisaliti tangu sikubya kwanza alipohudhuria kuapishwa kwa JK.zitto n tishio kwa nafasi ya mbowe kama mwenyekiti.undugu,uchaga na ukatoliki ndo umemuondoa zitto CDM

Utamuondoshaje kama hajavunja katiba? Ujue kuna mtu kwa nje unaweza ukaona kama alifaa kuondolewa chamani lkn ukienda kwenye sheria na kanuni unakuta hamna sehemu anakutwa na hatia.Mtu huyo utamfukuzaje?
 
1.hatagombea ubunge tena katika jimbo analoongoza sasa
2.atafanya maamuzi magumu muda siyo mrefu
source: twitter yake


Maamuzi magumu ya kwanza kutokea hapa Tanzania ni yeye kufutwa uanachama. Ngoja tuone hayo maamuzi yake,japokuwa tayari ameshaonesha woga kwa kutogombea tena ubunge.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom