Huo ndio ''Msimamo rasmi'' wa CHADEMA?
Tatizo sasa Zitto anasema hajui makosa yake ni yepi na ndio sababu mjadala ni muhimu kufanyika kwa kuwa jambo moja linaweza kuwa na maana tofauti kati ya watu wawili. Kuna mambo ambayo Zitto anaona labda sio makosa (kwa mfano kusema kwamba accounts za chama hazijakaguliwa na CAG..) wakati chama kinaona hilo ni kosa na usaliti wa hali ya juu kwa kuwa Zitto kama Katibu msaidizi, alikuwa na uwezo au nafasi ya kulifanyia kazi kabla ya ''kuropoka'' nje
He he patamu zitto ni tishio kwa uenyekiti wa mbowe
Akili yako ni mbovu, CCM haina bima ya kutawala taifa hili milele.
Asante kamanda Molemo, hakuna aliye juu ya chama.. Chama kwanza mtu baadae..
chadema bila zitto hawawezi kujiendesha kabisa hata iweje tulisema kitambo kwamba watampigia magoti tu.
Nadhani alipokwenda mahakamani aliomba Katibu Mkuu ampatie maamuzi ya Kamati Kuu na alipewa.
Namshauri asome kilichoandikwa mle ndiyo makosa yake.
Mwanasheria wake siku ile pale Serena Hotel alikuwa anasoma nini kama sio makosa yake?
Tuache jamani kujifanya tuko juu ya chama.Huu ni ujinga
Zitto kumaliza tofauti zake na chama chake ni jambo zuri,LAKINI si kwa kukipangia masharti kama hivyo,hapo ni kutaka kujiweka juu ya chama..na kama anategemea hilo kutokea atasubiri sana vinginevyo wataendelea kushirikiana tu bungeni kwenye maswala yanayohusu taifa na yenye tija kwa taifa letu
Kauli kama yako hiyo hazimsaidii ZZK bali zinamharibia; hatukatai kwama ZZK ni mwasiasa mahiri; bali hata yeye anajua "he needs a vehicle" and a strong vehicle; a 6x6WD; like CDM to achieve his political ambitions; kubali usikubali; ndio maana hata yeye mwenyewe alimshukuru Cmdr Mbowe kwa namna ya kipekee kwa ushirikiano wake katika sakata la Escrow; bila moral, political and intellectual support waliyompa Wanaukawa, asingetoboa; believe me you!! Ma CCM walikuwa tayari kumchinjia baharini; lakini ile collective voice; strong arguments; patriotic verve; viliwatisha Ma CCM mpaka wakakubali ku-compromise that much kiasi kwamba wamebaki lame ducks! wanaugulia maumivu ya ngumi za uso kutoka UKAWA
Usimuharibie ZZK; mwacheni afanye informed decisions pasi na ushabiki mandazi na fitina!
Hivi mathalani CHADEMA wakikataa hilo sharti alilowapatia Zitto, itakuwaje kwa Zitto?
Unajua sikatai mhalifu yeyote kutubu na kurudi kundini.Ni jambo Jema
Ninachokataa mimi ni kukipa chama masharti.Hilo kamwe sitalikubali.
Bora akina kafulila kuliko akina shonza na mwampamba....hawa BIG HAPANA wasirudi huku.
Sio Milele ila miaka 100 ijayo, CCM itaendelea kutawala!
Misukule mko CHADEMA, CCM wanajitambuaLabda itaendelea kutawala Lumumba na nyie misukule
Tehe teh amewapa WAHAFIDHINA masharti ya kumuomba radhi, tusubiri tuone."Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina; waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu; na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka."