Mbunge mahiri na machachari kutoka chama makini Zitto Zuberi Kabwe ameweka wazi kuwa anautaka uraisi lakini akiwa atapata ridhaa kutoka kwa chama chake na wananchi kwa ujumla wao,
CHANZO: UDADISI: Rethinking in Action: ZITTO: "NDIO NATAKA KUWA RAIS"
Nafikiri Confedence ya kuongea kwenye forums sio tija ya kuwa Rais.Watanzania wanahitaji Rais mwenye uwezo wa kufanya maamuzi.Zitto analalamikia sekta ya madini! Alikua miongoni mwa wabunge waliosimamia hoja hii 2005.Alinyoteuliwa kwenye kamati na mweshimiwa JK. Hajawambia wadau kilichojiri.
Zitto anahaki ya kikatiba kugombea urais ILA kwa maoni yangu naona asanii mwingi kwake. Uchaguzi uliopita jimboni kwake alipata upinzani mgumu na kuambulia asilimia inayoonyesha wanajimbo wameanza kumchoka.
Nafikiri Zuberi anajiweka kwenye daraja la super young politicians yeye mwenyewe.Kabla ya kuingia Bungeni alifanya wapi kazi?