Baada ya mdahalo wa Vijana kura yangu ni Kwa Ruqqaya Nasir

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
322
255
Vijana wa Chama Cha ACT Wazalendo wamefanya mdahalo mmoja mzuri sana,ambao pia wameutumia kama uwanja wa kampeni.

Hoja nyingi zilielekezwa Kwa Mwenyekiti anayetetea nafasi yake katika Ngome hiyo Abdul Nondo,ambaye alizijibu Kwa umakini mkubwa.

Washindani wake Kwa kiasi kikubwa ukimuondoa Ruqqaya walijielekeza kukosoa uongozi unaomaliza muda wake badala ya kueleza watawafanyia Nini vijana

Hali imekuwa ni tofauti Kwa Ruqqaya,kila alipopewa maiki ni hoja zilikuwa zinajengwa,mwelekeo wa Vijana wajaonwa Chama hicho,ulionyeshwa katika taswira ya mazungumzo yake.

Hakuwa na pupa hakuwa na wahaka,alijieleza alifafanua na kutoa uongozi mzima wa mdahalo huo.

Wengine wamechagua kuelezea mazuri ya uongozi uliopita na kuyamiliki wao wakiwa ni Sehemu ya uongozi huo yale mabaya wakasema ni ya Mwenyekiti Abdullah
 
Huyo binti anajitambua sana, anastahili hiyo nafasi. Huyo nondo apishe ameshindwa kujijenga miaka 5 yote.
 
Back
Top Bottom