Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
We need social justice, Tanzanians must benefit from the countries vast resource wealth. We need a complete break from business as usual. We need a leftist leader, we need a Chaves a Morales. Is Zitto leftist enough?
 
Hivi yule kiongozi wa Korea Kaskazini ana umri gani vile...??

Unataka tule Madesa kwa Korea kumpata Rais wetu? Mvivu wa kufikiri huyu! Huyo dogo msimpe kiburi bado hajakomaa bwana! Urais ni taasisi inayohitaji mtu aliyetulia Zitto kwa sasa bado Jepesi!
 
Hivi yule kiongozi wa Korea Kaskazini ana umri gani vile...??

Mkuu nisome vizuri utambue nilichokimaanisha!! Hakuna nilipotaja umri!!
Pia mkuu kuifananisha Tz na huko kisiasa binafsi naona unakosea, siasa za wenzetu na demokrasia vimekomaa nchi inajiongoza, tofauti na hapa home ambapo nchi inahitaji kuongozwa!! Tz inahitaji mtu ambaye amekomaa kiuongozi, kisiasa na kidemokrasia!
Binafsi sina tatizo na Zitto kutangaza nia, isipokuwa naangalia je, ni mda muafaka kufanya hivo, Amekomaa?
Kiongozi unakiwa KUONWA sio KUJIONA!!
 
Unataka tule Madesa kwa Korea kumpata Rais wetu? Mvivu wa kufikiri huyu! Huyo dogo msimpe kiburi bado hajakomaa bwana! Urais ni taasisi inayohitaji mtu aliyetulia Zitto kwa sasa bado Jepesi!

Kwahiyo JK ametulia na ndivyo anavyoipeleka nchi hivi...?
Umdhaniaye ndie kumbe sie...! mnaweza kumpa nchi mtu msietarajia akafanya mambo ya maana kuliko hawa ambao mnaowatarajia.

Even dream makes you mad!!! what a man!
Waberoya unakumbuka umewahi kuandika nini kuhusu Zitto humu JF?

Hakuna kitu kibaya kama unafiki! Zitto ni mnafiki kama wewe!

Unakumbuka aliwahaidi nini wakazi wa kigoma? Eti 2015 hagombei ubunge bali Urais! Tena wakati huo Dr Slaa akigombea Urais! Huyu si ana matatizo ya akili!

Zitto kuingia Chadema akiwa na miaka 16 sio issue, Zitto kushiriki kuijenga Chadema ya leo sio issue pia kama hawezi kusimama kiitikadi na Chama; aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CDM na mbunge wa kwanza wa upinzani Tanzania Bwana Aman K. Amerudi CCM! Sembuse Zitto!

Eti haki yake msingi! Hiyo haki hata Matonya anayo Waberoya!
 
Alafu anakuja mtu kutwambia tu concentrate na ya Arumeru kwanza alafu yeye huyo huyo anakuja na statement za ajabu kipindi hiki kigumu kinachohitaji umoja! Kuna hekima hapo? Eti Mnyika hakuipenda CDM! Why now?
 
mwandishi analaumu kutawaliwa na kenya.anasema kenya wametuzuia kujenga barabara serengeti hapohapo anahoji wazalendo wako wapi.anasahau kuwa zitto ni miongoni mwa wa zalendo anaohoji wako wapi.
 
mwandishi analaumu kutawaliwa na kenya.anasema kenya wametuzuia kujenga barabara serengeti hapohapo anahoji wazalendo wako wapi.anasahau kuwa zitto ni miongoni mwa wa zalendo anaohoji wako wapi.
Ndio umeandika nini sasa? Hujielewi!
 
Kwanza ni zamu ya Wakristo. So long as Zitto ni mjahidina asubiri mpaka 2025
Wakristo tupo wengi pia,nadhani sasa ni wakati wa wapentekoste/sabato/lutheri/Anglikana maana wakatoliki mwalimu nyerere na Mkapa wanawatosha au unasemaje Nelsweeter?(Hili alikwisha lionya mwalimu kuwa dhambi ya ubaguzi haiishii kwa uislamu na ukristo tu bali itaendelea mpaka mtaanza kubaguana kwa vimo vyenu!!Sijui kwanini watanzania tuna mawazo mgando namna hii Aaaaghh!!)
 
Urais unahitaji hekima, Zitto hana kwa sasa, Urais unahitaji busara, Zitto hana kwa sasa, Urais ujasiri wa kweli Zitto hana kwa sasa,Urais unahitaji mtu wa kutafakuri, Zitto hana kwa sasa, Urais hauhitaji mtu mnafiki, Zitto kwa sasa ni mnafiki, Kwa ujumla Urais unahitaji mtu aliyepevuka, na Zitto bado hajapevuka.
Hizi sifa ulizozitaja zote rais wako wa sasa hivi anazo...?
 
Mwandishi na mleta mada inaonekana mna kinyongo na zitto!

Soma mada uielewe usikurupuke tu na kuandika. Sasa hapo mtoa mada anakinyongo gani na zitto penye ukweli unakubali. Kweli zitto hajaiva na bado ni muoga tumeona mengi akiwa ndani ya chama chake, akitofautiana na wenzake si mbaya kutofautiana lakini kuna mengine ambayo alikuwa anatofautiana na wenzake wakiwa tayari wameshakubaliana. Kuna mengi mazito ambayo siwezi kuyasema yote, ni kweli kabisa zitto bado hajawa tayari kutuongoza, Ni muoga, ajiamini, ni kigeugeu. Zitto hawezi kutoa maamuzi mwenyewe, zitto akiwa rais tutakuwa na kikwete part 2 au zaidi. Anatakiwa ajianda kwanza muda wake bado ache tamaa.
 
Upo sahihi kabisa ndugu! Wengi wameweka ushabiki mbele!
 
mwandishi analaumu kutawaliwa na kenya.anasema kenya wametuzuia kujenga barabara serengeti hapohapo anahoji wazalendo wako wapi.anasahau kuwa zitto ni miongoni mwa wa zalendo anaohoji wako wapi.
Unajaza server tu, sasa hiki ndo kitu gani?
 
mwandishi analaumu kutawaliwa na kenya.anasema kenya wametuzuia kujenga barabara serengeti hapohapo anahoji wazalendo wako wapi.anasahau kuwa zitto ni miongoni mwa wa zalendo anaohoji wako wapi.

Ukisoma kwa makini, utang'amua yote, tena kwa mapana!
 
Alafu anakuja mtu kutwambia tu concentrate na ya Arumeru kwanza alafu yeye huyo huyo anakuja na statement za ajabu kipindi hiki kigumu kinachohitaji umoja! Kuna hekima hapo? Eti Mnyika hakuipenda CDM! Why now?

Huo ndio ule mtoa mada kauita UNAFIKI. Tena hajamung'unya maneno, amesema peupe kabisa kuwa Zitto ni MNAFIKI
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom