Sasa hapa ningependa wapenda ukweli wote wayapitie haya uliyoyaandika kwa makini halafu pumba na mchele vitaeleweka katika post yako hii.
Naawachia wadau wataamuwa kama kweli wewe ni mwanasiasa kweli au vipi!! Mimi binafsi hapa umeshanijibu dought zangu zote kwako umeziweka wazi mwenyewe hapa.
[Nashindwa kuelewa mtu anaposema fulani ana urafiki na Rostam sijui anamaanisha nini? Je,wanaofanya biashara na Rostam je? Kama una simu yenye laini ya VODA hufanyi biashara na Rostam?Mbona humfanyii Economic Embargo? Je ni Zitto pekee kwenye kambi ya upinzani mwenye urafiki na wana-CCM?
Hapa hatuongelea nadharia wala ununuzi wa bidhaa za RA bali tunaongelea mahusiano ya karibu au yale yasiyo ya kawaida kati ya Zito na RA. Mimi kwa kuwa ni mteja wa Vodacom, haimaanishi kuwa nina uhusiano binafsi na RA. Zito ana mahusiano binafsi ya karibu na RA. Hatushangai mahusiano ya RA na Zito eti kwa sababu RA ni mwana CCM bali kwa sababu RA ni mtu ambaye jina lake lipo katika kila kashfa kubwa ya fedha nchini. Pia huyu ni mtu ambaye licha ya kutokuwa ndani ya serikali lakini ndiye mgawaji wa vyeo ndani ya serikali (Rejea barua ya Rweyemamu. Rweyemamu alipotaka kupewa kazi ndani ya serikali ambayo aliipigia kampeni kupitia kalamu, alimwomba RA amkumbuke, hakumwomba JK, na baada ya muda akapewa nafasi hiyo aliyo nayo). Huyu RA, kwa Tanzania anaonekana kama mafia aliyeshindikana. Ufisadi wote unaopigiwa kelele na CHADEMA, katikati yake yupo RA, halafu mtu huyo huyo ni rafiki wa karibu wa Naibu katibu Mkuu (Zito) wa chama kinachomsakama.
Tuliwahi kumwuliza Zito atuambie ni nini alikuwa akijadiliana na RA pale Sea Cliff Hotel kuanzia saa 4 mpaka saa 7 usiku kwenye chumba maalum, wiki mbili tu kabla ya uchaguzi, Zito mpaka leo hajajibu. Zito ni mtata, ni vigumu sana kuelewa kilichomo moyoni na akilini mwake, yeye ndiye anajua anachokitaka LAKINI kwa tulio wengi tunamwona ni mtu hatari pengine kuliko hata hao CCM tunaowalaumu. Zito anaweza kufanya kazi, na hakuna mashaka juu ya uwezo wake lakini kuna mashaka makubwa juu ya uadilifu, uzalendo na dhamira yake. Ni mtu anayestahili kufanya kazi chini ya watu wengine ambao wakiona na kuhakikisha kuwa dhamira yake siyo safi, wanamwondoa LAKINI siyo yeye awe overall in charge wa nchi.
Wewe umechelewa sana tena bado uko mbali sana na dunia ya leo, hivi unadhani ni nani mwenye akili timamu anathamini makaratasi? wewe kama ni mtu makini unatakiwa umvalue huyo Yericko kwa alichokiandika na hapo ndipo utakapoipata Profile yake halisi na sio zile za kukariri darasani na kujaza mavyeti feki na udaktari feki kama Nchimbi.Mwenye PROFILE ya Yericko Nyerere aimwage hapa ili tujiridhishe kama ushauri wake ni wa kuzingatiwa au la. Mfano Livingstone Lusinde kwa profile yake hata aje na hoja nzuri kiasi gani mimi Ulukolokwitanga nitaipuuza tu...
Vyama vya siasa vingi vinapoteza mvuto kwa kukosa demokrasia. Mrema alipata kura nyingi 95 alikosa urais alitakiwa akae pembeni, Lipumba nae hivyo hivyo mwaka 2000 bado akangangania, maalim Seif zenji mara 3 anashindwa kwa kura asilimiaa chache. Tujifunze kwa wamarekani ukishakosa unakaa pembeni.
Kama unataka facts kuwa chama kilisema wewe ni usalama wa taifa hizi hapaMatola,
Nimekuambia nidhamu ni jambo muhimu sana.Tafadhali unapojenga hoja uwe na ushahidi.NAOMBA UTHIBITISHE kwamba chama changu CHADEMA kilisema kuwa mimi ni USALMA WA TAIFA.Njoo na facts hapa.
HATIMAYE uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) ulimazika jana kwa kumpata Bw. John Heche kuwa Mwenyekiti wa umoja huo.
Pamoja na kupatika kwa kiongozi huyo, uchaguzi huo uligubikwa na mizengwe mbalimbali ikiwemo rushwa na mambo ya 'kujuana' yaliyooneshwa wazi na viongozi wa chama hicho.
Kwa mujibu wa uchuguzi uliofanywa na Majira juzi usiku, uchaguzi huo ulifanyika huku kukiwa na makundi matatu, makundi hayo ni yale yanayomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe na lile lisilomuunga mkono mtu yeyote katika chama hicho.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa kundi linalomuunga mkono, Bw. Mbowe ndilo lilokuwa na nguvu zaidi na ndilo lilochukua kiti hicho kutokana na mwanzilishi wa chama hicho, Bw. Edwin Mtei kuliunga mkono kwa asilimia mia.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya Baraza la Wazee kilidokeza kuwa, maamuzi ya kufanya uchunguzi wa wagombea yalifikiwa baada ya kugopa kivuli cha Bw. Zitto ambaye ameonekana kuungwa mkono na vijana wengi ndani ya chama hicho.
Kilisema kuwa baada ya kubaini uwezekano wa kundi hilo kushinda, baraza la wazee lilikubaliana kutafuta mambo yatakayowamaliza wagombea hao ili wasipitishwe katika kugombea kiti hicho.
"Ndugu yangu napenda kusema kuwa chama hiki sasa kinaenda pabaya walitafuta kila njia ya kuwamaliza vijana na njia waliyoipata ni kuwatutafutia tuhuma zitakazowafanya waondoke katika kuwania nafasi hiyo...lakini tulipigana na ikashindikana," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
Alieleza kuwa tuhuma hizo ni kundi hilo kutaka kuunganisha nguvu katika uchaguzi huo ili kumpigia kura mtu moja jambo ambalo kamati ya wazee ilipingana na suala hilo ikidai kuwa ni jambo linalowagawa vijana ndani ya chama.
Chanzo hicho kilisema kuwa katika uchaguzi wowote makundi lazima yawepo ndo maana mgombea hawezi kupata kura kwa asilimia mia moja hata akiwa pekee yake.
Alisema tuhuma nyingine zilizofanya kuenguliwa kwa wagombea hao ni kupokea wajumbe kutoka Zanzibar jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote lakini kutokana na mizengwe iliyoandaliwa na kamati hiyo ilibidi watu hao waadhibiwe.
Alisema kuwa tuhuma nyingine ilikuwa ni kupiga kampeni kabla ya muda uliopangwa na tume hiyo hali iliyosababisha kuenguliwa dakika za mwisho katika uchaguzi huo.
"Tuhuma nyingine iliyoelezwa ni wagombea hao kutaka kupindua chama hicho kwa kuhamisha agenda za chama hicho na wengine walihofiwa kuwa ni usalama wa taifa," kilisema chanzo chetu.
Hata hivyo Mjumbe huyo wa baraza la wazee alisema kwa upande wa Bw. Heche nako kulikuwa na tuhuma za kupokea wajumbe ambao kamati haikutaja kuwa wanatoka katika mkoa upi lakini alijitetea kuwa ni ndugu zake.
"CHADEMA tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anapokosea tunataka awajibishwe, sisi leo mtu anakosea wakati wa mchakato wa uchaguzi lakini tunasema tunafanya uchunguzi je akipata madaraka tunamchukulia hatua gani kwani atakuwa tayari amepata madaraka," kilisema chanzo.
Chanzo hicho kiliendelea kuhoji ni kwa nini mgombea huyo aachwe na kuchukua madaraka huku akiwa na tuhuma hivyo akataka haki itendeke kwa wote.
Naye Tumaini Makene anaripoti kuwa;
Kamati ndogo maalum, kwa ajili ya uchunguzi wa uchaguzi huo iliyoundwa na kamati kuu ya chama hicho ilibaini kuwepo kwa vitendo vichafu ikiwemo baadhi ya wagombea kutaka kuundwa makundi ili kudanganya wapiga kura kwa nia ya kutaka ashinde mtu wanayemtaka kwa hila zao.
Akizungumza na majira jana akiwa katika uchovu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, pamoja na kutotaka kuzungumzia tuhuma hizo za rushwa kwa undani akisema "mengine yanahitaji maamuzi ya juu", alisema kuwa wagombea hao watatu walioenguliwa baada ya kuthibitisha kuwa wamekwenda kinyume na katiba na kanuni za chama, kifungu cha 10, wamekiri pia kuwa wao walijihusisha kutengeneza agenda ya BAVICHA.
"Sasa hilo ni suala kubwa agenda ya BAVICHA ni suala la mkutano na haliwezi kuwa la wao watatu lakini walibainika kujihusisha na kundi la Bw. Habib Machange ambapo ilibidi chama kiingie gharama ikiwemo wajumbe wa kamati hizo kufanya kazi tangu saa saba usiku wa juzi mpaka asubuhi jana na baadhi ya wajumbe walishindwa kurejea kwao," alisema Dkt. Slaa.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Majira ilibainika kuwa mmoja wa wabunge wa chama hicho alijihusisha na kusimamia vikao vya usiku wa manane vilivyokuwa vikitumika kuwalubuni wajumbe kugawa fedha, kuwanunulia pombe usiku wa kuamkia uchaguzi akitaka kuweka mtandao unaodaiwa kuwa na lengo la kusambaratisha chama hicho.
Mbunge huyo machachari kutoka Kanda ya ziwa ametajwa pia kutoa udhamini wa mmoja wa mgombea aliyeenguliwa kwa lengo hilo ambapo imeelezwa kuwa suala lake pamoja na vituko vingine vitafikishwa mbele ya Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.
Alipoulizwa juu ya tuhuma kwa mbunge huyo (jina tunalo), Dkt. Slaa hakuwa tayari kulizungumzia na kusema kuwa liko ngazi ya juu ya kamati kuu.
Wakati hayo yakiendelea Bw. Heche alisema yuko tayari kufanya kazi katika nafasi hiyo akishirikiana na wenzake ili BAVICHA iwe sauti ya kupigania maslahi ya wananchi wanyonge.
Akizungumza na majira jana, Bw. Heche alisema kuwa BAVICHA itasimama kwa maslahi ya nchi na chama hicho kwa jitihada za kuchukua dola kwa ridhaa ya wananchi.
Bw. Heche alipata kura 147 sawa na asimilia 56 ya kura zote zilizopigwa 267 ambapo kura tatu ziliharibika.
Walioenguliwa katika uchaguzi huo ni Greyson Nyakarungu, Mwampamba na Bernard Saanane.
Source: GAZETI MAJIRA. 30 May 2011
Kwanza ni zamu ya Wakristo. So long as Zitto ni mjahidina asubiri mpaka 2025
Kabila amepewa Urais akiwa bado kijana mdogo, sasa anatakiwa atoke ikulu akiwa bado umri wake ni kama kijana lakini sasa anang'ang'ania madaraka!! labda utueleze what is your point on this? i mis something.....Watakuambia Wade aligombea mara nne na mara ya tano ndio akaukwaa ila hawatakuambia kwamba baada ya kuutwaa akiwa mkongwe alitamani kufia Ikulu hadi aibu imemkuta jana!
Mwono wako unaonyesha wazi ni chuki au wivu........sijui umempima huyu Zito kwa kutumia vipimo gani?.....kama kuungombania urais basi ni haki yake ya Kikatiba.......mbona Nyerere alipochukua nchi alikuwa na umri mdogo na alikuwa hajakomaa kisiasa na aliwza kuongoza nchi hii kwa muda mrefu tu.
Tatizo la watanzania wengi hasa wa JF huwa wanasau upesi kwa sababu ya siasa za kishabiki.Mimi kwa kumbukumbu zangu Zitto wakati wa uchaguzi 2010 aliwaambia wapiga kura wake kuwa akirudi tena atarudi kama mgombe Urais.Bora Zitto anaeonyesha nia yake kwa uwazi kabisa kuliko Mbowe anaye tumia watu wake kumsemea.Mwacheni aonyeshe nia kama hamumtaki si mumuonyeshe kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wa ndani.Hivi katiba yenu CHADEMA inakataza mtu kuonyesha nia ya kugombea urais?
Narudia tena Ben Saanane hawezi kupita kwenye vetting yoyote makini ili awe Itelligence securty officer, sana sana tu anaweza akawa ni sehemu vya mainformer wadogo wadogo tu kupitia Zitto Kabwe through Jack Nzoka.Kama unataka facts kuwa chama kilisema wewe ni usalama wa taifa hizi hapa
Kabila amepewa Urais akiwa bado kijana mdogo, sasa anatakiwa atoke ikulu akiwa bado umri wake ni kama kijana lakini sasa anang'ang'ania madaraka!! labda utueleze what is your point on this? i mis something.....
Dr Slaa he was seek for one term Presidencial......Je una lingine?Mkuu nimewakumbusha hii habari huko nyuma lakini watu hawataki kabisaa kusikia. Mwaka 2010 kulikuwa na mgombea urais (dr. Slaa) ambaye kama angeshinda tulitegemea chama chake kimpe kipindi cha pili lakini Zitto akasema 2015 ataenda kuomba Urais. Baada ya Zitto kujitokeza na kurudia kusema kwamba anautaka Urais tunaambiwa timing mbaya! Hivi kati ya tangazo la sasa na tangazo la mwaka 2010 wakati tupo katikati ya kampeni ni hatuoni kwamba hapo ndipo kulikuwa na timing mbaya. Lakini sikusikia kelele!
Mtu aliyeshindwa uchaguzi na akabaki madarakani kwa nguvu bado unasema swala la katiba hapo? kuna katiba inayoruhusu kung'ang'ania madaraka?Nasubiri nione kama atang'ang'ania baada ya kipindi chake cha pili kikatiba kuisha. Sijaona ameng'ang'ania bado kwa kuwa yuko ndani ya vipindi vya katiba. Kwa hiyo Mkuu unataka wapewe wazee wakitoka wakutane na umauti?
Mkuu this is not a fact as you called it..............................Kama unataka facts kuwa chama kilisema wewe ni usalama wa taifa hizi hapa