Nilitegemea baada ya summary itafuatia Recommendation na Conclusion! Nimetafuta recommendation na conclusion nimevikosa.Hii ngoma imekuwa ndefu sana nipeni fursa kuweka SUMMARY,
- Wenye busara wamemshauri Zitto pamoja na nia yake nzuri ya kutaka kuwa rais aendelee kusoma alama za nyakati ili wakati ukifika aingie ulingoni akiwa na nafasi nzuri kushinda/ kuchaguliwa na chama chake
- Pro CCM members wamefurahia sana uamuzi huu wa Zitto, hii imewapa mashaka makubwa sana Pro CDM members kwamba kwa nini akina Ritz, Topical, Geniusbrain nk wamfurahie Zitto katika nia yake ya kugombea against chama chao? Kuna ujumbe mzito sana behind this scene...
- Wengine wameegemea kwenye age ain't nothing but a number kwamba ujana au uzee sio ishu sana kwani kuna vijana tumewaona ni wahuni kama Adam Malima na pia kuna wazee wengine hawana busara kama Wassira. Cha muhimu ni kuwa na sifa na uwezo wa kukabiliana na matatizo yaliyopo hapa nchini na sio changamoto kwa kuwa changamoto hata zisipotatuliwa hakuna wa kulaumiwa but matatizo kama ajira kwa vijana na umaskini lazima yamalizwe na rais ajaye, Na Zitto amesema anayajua vizuri sana
Zitto anafaa walau kuanzia 2025 atakuwa amepikwa na kukomaa vizuri.Kwa hivi sasa ni nafasi ya Dr Slaa.Dr Slaa kwa sasa hana mbadala ndani ya CDM.Ni kujilisha upepo kudhani kuna mtu mwingine atapitishwa kugombea Urais zaidi ya Dr wa ukweli walau kwa sasa.CDM ina vijana wengi na hakika huko Mbeleni kina Zitto na Mnyika na wengine ni hazina kubwa ya chama
Tatizo ningeweka Conclusion watu watatoka povu humu na kudai nimewasemea...Nilitegemea baada ya summary itafuatia Recommendation na Conclusion! Nimetafuta recommendation na conclusion nimevikosa.
kisha zeeka halafu tumemchoka cdm tuna utaratibu wetu mtu akigombea mara moja akishindwa basi aende akalime tu. Zitto hakika anafaa. Slaa kisha zeeka nchi ikiongozwa na mzee itaenda kizee slaa hafai tena bw.ege
WAKUU.
tusipotoshane hapa.
slaa sio mgombea urais wa chadema 2015 isipokuwa alikuwa mgombea 2010. yeye mwenyewe alitamka hadharani kuwa alikuwa hautaki urais lakini alilazimishwa. sasa kama kuna mtu amejitokeza kuutaka urais mimi nadhani anapaswa kuungwa mkono sana mana huwezi ivaa nguo nusiyoipenda ukaenda nayo safari. slaa alifanywa chambo na mbowe na sasa mnataka kumlazimisha kuwa yeye ndiye mgombea urais wa chadema.
shame on you.
Pandikizi la CCM hili tunalijua, kamwe wana CDM musikubali. Toka awe mjumbe tume ya madini hana tofauti na akina Chiligati. Hata hiyo 2025 kutakuwa na watu bora katika CDM kuliko Zitto.
Leo founder wa chama amekuwa pandikizi la CCM? Pandikizi wa ccm ni slaa anayekipeleka chama kuwa cha kimaeneo na watu wa mrengo fulani.ZItto,Mbowe hawa wapo neutral na wanaweza kupeperusha bendera ya CDM sio SLAa mropokaji. Ikulu inahitaji mtualiye balanced
Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.
Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!
Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.
Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com
Badala ya vyombo vya habari kuzidi kuanika hila zinazotaka kufanywa na wajanja kupokonya haki ya CDM kule Arumeru,leo magazeti yote yalikuwa yakitangaza nia ya mtu mmoja aliyetangaza rasmi nia yake ya kugombea urais 2015.Wito wangu kwa wanaCDM wote endeleeni kuungana katika kipindi hiki kigumu cha kufa na kupona kule Arumeru.Msikubali myumbishwe na yeyote.Nimepata taarifa mgombea wetu kule Arumeru amehuzunishwa sana na haya mambo ya kutangaza nia za urais leo.Ninampa moyo mgombea wetu huyo kwamba asiwe na hofu yeyote kwa sababu viongozi wote wenye nia ya kweli wako pamoja naye.Wanachama ondoeni hofu chama kiko imara kabisa na Arumeru tutashinda.Kutangaza kugombea urais si hoja bali hoja ni kuaminiwa na wenzako kwamba wewe ni mwenzao.Nani asiyejua hata msaliti Shibuda alitangaza nia ya kugombea urais 2010? Kwa hiyo wanachama wasishangae huenda Shibuda naye akatangaza nia yake kuomba kugombea urais kupitia CDM wiki ijayo.
kuna Kaushauri labda naweza kukutupilia kidogo..
kwanza ujue mimi nafurahi na kuunga mkono matamshi, michango na vuguvugu la wabunge wetu hasa Vijana wa vyama vyote vinavyoliunda Bunge, Kumbuka Mhe Sita aliwahi kusema vijana wabunge hukesha kwenye maktaba za Bunge wakikokotoa taarifa na kujenga semi zenye hoja na mashiko wanapowakilisha maada au wanapouliza maswali.. na Hutoa Changamoto chanya kwa serikali. Na Kumbuka Mhe Zitto ulijichotea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi yako. kuna kitu kina nituma niwaze kwamba kipindi kile ulikuwa wewe kama wewe Zito ukitegemea hazina ya mawazo na utashi wako. Lakini Zito wa Leo umebadilika sana, sizuiliki kuwaza pia kwamba umezungukwa na mamluki wapambe ambao inawezekana kula yao inategemea na uhai wako, na wapambe hao mara zote ni ndio mzee, na ushauri wao daima umekuwa ukikuzuzua, ukikulimbuka. sidhani kama una muda wa kusoma na kuelewa utitiri wa vyombo vya habari ambavyo kila kukicha kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakikuandika, kwa maana hiyo mara zote lazima utegemee taarifa za marafiki na "feedback" zako. Nadhani hupewi taarifa sahihi kutoka kwa wapambe hawa. mara baada ya uchaguzi ulikumbwa na wingu baya la kuchukiwa sana na wale waliokupenda, na unakumbuka mama mmoja alipiga magoti ndani ya Ndege alipowaona mabosi wa chama chako akiwalilia wakung'oe kwenye chama haraka ila nadhani mabosi wale walimjibu vizuri kwa hakma ingawa hawakutarajiwa kupatwa na ugeni ule ndani ya chombo cha usafiri.
Najua wewe ni mwoga sana inapotokea kitu physical atack, ndio maana mara zote kwenye mikiki ya chama hutokei anyway hakuna mwenye nafasi ya kukuhukumu kwa hilo kwa sababu sisi binaadam wote tuna degree tofauti za woga. lakini una uwezo wa kushawishi ambao ni kitu kizuri kwenye medani ya siasa. SASA niseme kwa uwazi tu kwamba UMEKOSA WASHAURI WAZURI. na ukiendelea na tabia hii utajikuta unatokomea gizani kwenye pori la wasiojulikana tena kwa aibu.
Hoja yako uliyolimwa na mwana zuoni ambaye unajua ni si wa chama chako, unatutumuka this way kumjibu sidhani kam ni dhana yenye mantiki.. mwanasiasa gani aliyekomaa yuko hivi. ina maana kila post ikiandikwa kuhusu wewe lazima uijibu?, zito kanya karimjee..."utajibu", zito kaiba kuku .. "Utajibu" zito kampiga flan.. ujibu, utajibu mangapi.. si kujibu kunako leta maana but why now, why soon.. Yaani huna moyo wa kusikiliza neno na kulihifadhi.. Unashindwa hata na Lowassa, kasemwa mangapi na hawa "mboga za CHAMA" .. mwaka mzima ila jamaa yuko kimya na ilipotengwa CC ya chama chake akajimimina vilivyo, sasa wewe hata hujui wapi useme nini kiongozi gani Jukwaa hili na majukwa mengine yote ya mitandaoni ni majukwaaa huria. Yanatiwa mikono na raia wa aina mbalimbali, watoto kwa wakubwa.. seuze ni mwanafunzi tu wa chekechea aliyeleta hoja ile umejitutumua this way kumnanga kwa majibu. Wewe kiongozi wa wapi usiyejua kwamba kuna vikao halali ndani ya Chama ambavyo unaweza kuweka vuguvugu lako. Upwayukaji wa namna hii mapema kiasi hiki unanipa shaka sana. Si bure unaweza kuwa na kasoro. Wagonjwa wengi walioathirika na propaganda za kisiasa si rahisi wakakiri kwamba hapo kuna tatizo. Usikariri siaza za kizayuni na za nje wala historia. Jamii ya Tanzania ni tofauti sana na jamii za Nchi nyingine Duniani. Nakushauri Pata washauri makini, linda sana Kinywa chaweza ponza kichwa. .. Kama una maarifa utaelewa usipoelewa hayanihusu.. if you lost who cares.. na akina muddy mdogo (mtoi) watalost vilevile..