Zitto natofautiana na wewe juu ya hili

Zitto natofautiana na wewe juu ya hili

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
17,079
Reaction score
12,309
Jana wakati wa kuhitimisha kikao cha bunge ulikuwepo mjadala wa kulipatia msamaha wa kodi shirika letu la NHC, binafsi nilifarijika sana na wabunge wetu walifarijika sana. Lakini wapo wabunge wengine akiwemo Zitto walishauri misamaha hiyo itolewe pia kwa mashirika kama PPF na NSSF, hapo ndo natofautiana na zitto.

Kwanza, NSSF na PPF sio jukumu lao kujenga nyumba (traditional business), jukumu lao ni kutunza mafao ya uzeeni (pension scheme), hivyo basi hawana wajibu wa kujihusisha na hii biashara na kama watahitaji kuwapatia wanachama wao nyumba za bei nafuu watazinunua NHC na kuwagawia na sio kuanzisha kandarasi za ujenzi.

Pili, hawa NSSF/PPF wamekuwa wakijihusisha na ujenzi wa majengo makubwa ya kibiashara yenye kuwaingizia faida kwa lengo la kuhifadhi akiba za wanachama wao, wamekuwa wakidai ujenzi wa nyumba za bei nafuu hauna tija sasa leo iweje walilie kuwekeza kwenye biashara isiyokuwa na tija? hapana.

Tatu, NSSF/PPF sio wajenzi hivyo wamekuwa wakikodi wakandarasi kutekeleza miradi yao hapa ni kutengeneza uchochoro wa kukwepa kodi kupitia makampuni yatakayopewa kandarasi za ujenzi, hapana kaeni pembeni.

Nne, Limekuwepo tatizo la NHC kujilipia garama za ujenzi wa miundo mbinu kama kuvuta umeme na maji na ujenzi wa barabara, ningeshauri serikali iwapatie ruzuku NHC pale wanapojiwekea umeme na maji au kulipa fidia kwa wananchi wanaopaswa kupisha mradi, kwani jukumu la kuweka miundombinu ni la serikali, basi inaposaidiwa ni bora ikafia kwa kutoa ruzuku.

Naamini kabisa NHC ikipewa support ya kutosha nyumba hizi zitauzwa mil tatu na kila mwananchi atamudu kununua nyumba badala ya mtindo wa sasa kila mtu kujijengea kijumba kwa tabu.

===========
Majibu ya Zitto:
Nashukuru sana kwa maoni yako mazuri sana. Kwanza, dhana nzima ya misamaha ya kodi ninaipinga. Nyumba ambazo NHC, NSSF, PPF, PSPF etc wanajenga zinanufaisha sehemu ndogo sana ya Watanzania. Kutoa msamaha wa kodi kwa nyumba hizi ni kugharamia kundi dogo la watu kwa gharama ya wananchi wote. Hoja ingekuwa na maana sana iwapo msamaha huu ungekuwa kwa vifaa vya ujenzi kwa ujumla ili kila Mtanzania afaidike.

Pili, ni kosa kubwa kuomba msamaha wa kodi kwa taasisi moja. Ni mtu ambaye hajui mfumo wa kodi vizuri anayeweza kusimama kuomba msamaha wa kodi wa Shirika moja. Kwa hiyo context yenyewe was wrong. Ndio maana nilishauri Bunge kuwa msamaha uwe kwa taasisi yeyote inayojenga nyumba kwa gharama nafuu iwapo tunaona ni muhimu kuwa na msamaha huo. Kimsingi napingana na wazo lenyewe in its totality. Ni wazo ambalo litafaidisha wakandarasi binafsi na sio wananchi. Zero rating system haina faida kwa mlaji wa mwisho bali kwa mzalishaji husika. Ilikuwa ignorance tu ya kamati husika katika kutoa pendekezo hilo.

Suluhisho la kudumu ni kutoa ruzuku kwenye vifaa ili viwe vya bei nafuu. Pia kuongeza uzalishaji wa vifaa vya ujenzi nchini kama saruji nk. Baada ya Dangote kuanza kuzalisha, bei ya Saruji inaweza kushuka hadi kwa 30% iwapo hataingia katika cartel na wenzake waliopo nchini. Lakini pia Serikali inaweza kutoa ruzuku kwa mtu yeyote anayenunua nyumba mpya kama inavyofanyika UK hivi sasa. Hata hivyo uchumi wetu bado mdogo kuhimili hilo na pia mfumo wetu wa kifisadi utapelekea skandali nyingi sana katika msaada wa aina hiyo.
 
Haya mashirika ya Umma yanahitaji a very serious monitoring system

Yanatakiwa hata investment zao ziangalie sehemu ambazo private sector wameshindwa lakini ambazo ni public utility

Ni kosa kubwa Mashirika haya kutoa Mwanya wa Tax evasion kwa makampuni binafsi kupitia kandarasi
 
Ni kwanini NHC ipewe msamaha wa kodi? Na hiyo maana yake ni nini? Kwamba ukinunua nyumba NHC basi hutatakiwa kulipa VAT? Ni wananchi wangapi wananufaika na nyumba za NHC? Tusipokuwa makini, hapa tutazidi kuwanufaisha matajiri. Na kwa jinsi hili suala linavyojengewa hoja,inaonekana kuna agenda ya siri (Kama anavyosema Ben Saanane hapo juu).

Mimi ni miongoni mwa watu ambao hatufurahishwi na utendaji wa NHC na hivyo natilia mashaka sana hoja ya sasa ya kutaka msamaha wa kodi kwa shirika hili. Zitto anataka msamaha huo pia uhusishe NSSF na PPF (What about LAPF and PSPF?). Pengine huko ndiko maslahi yake yalipolalia. Na ni juzi tu ametoka kutueleza kiasi cha mapato kinachopotea kutokana na misamaha ya kodi. Mpaka pale mtu atakapoweza kueleza wazi, ni kina nani watakaonufaika, na ni kina nani watakaopata hasara (Winners and losers/ political economy) kutokana na misamaha hiyo ndipo hoja hii itaeleweka.

Kwani Ndugu yangu eddy, wewe ukijenga nyumba yako ya kuishi, unapata msamaha wa kodi? Kama NHC wanastahili msamaha wa kodi, wewe hustahili msamaha? Kumbuka nyumba za NHC zinauzwa kwa watu binafsi ambayo ni sawa tu na wale wanaojenga nyumba zao wenyewe. Or else, what is the difference?
 
Last edited by a moderator:

Nyumba nyingi zinajengwa kwa ubia na kampuni binafsi. Kwa hiyo Kamati ilikuwa inaomba msamaha wa kodi kwa kampuni binafsi zinazofanya kazi na NHC. Wiki moja tu iliyopita tulikuwa tunapinga kwa mapovu misamaha ya kodi, leo tunatumia jukwaa hilo hilo kupigia debe misamaha. Kama sio umazwazwa ni nini?
 
Nadhani ni vizuri kupata maneno niliyosema (verbatim). Sikusema wapewe NSSF na PSPF tu, nilisema kuwa wanaojenga nyumba za gharama nafuu ni wengi hivyo huwezi kutoa msamaha kwa Shirika moja tu. Kama unatoa toa kwa yote ikiwemo GEPF, LAPF, PPF, NSSF etc. Lakini msingi wenyewe wa hoja ninaupinga kwani huo msamaha hautasaidia wanyonge
 
Sasa naelewa kuwa hoja hii unaipinga. Na sasa pia naelewa kuwa msamaha wa kodi unaozungumziwa ni kwa ajili ya makampuni binafsi yanayoingia ubia na NHC pamoja na makandarasi. Asante kwa ufafanuzi. Hili halikubaliki hata kidogo.

Nadhani mwanzisha thread anapaswa kufanya marekebisho. Inavyosomeka sasa ni kana kwamba Zitto aliunga mkono hoja ya msamaha wa kodi kwa NHC na akataka msamaha huo uhusishe pia NSSF na PPF wakati Zitto hakusema hivyo na anapinga hoja yenyewe kwa ujumla wake.

Zitto, karibu sana JF! Umeadimika mno kwenye jukwaa Mheshimiwa.
 
Nashukuru sana kwa maoni yako mazuri sana. Kwanza, dhana nzima ya misamaha ya kodi ninaipinga. Nyumba ambazo NHC, NSSF, PPF, PSPF etc wanajenga zinanufaisha sehemu ndogo sana ya Watanzania. Kutoa msamaha wa kodi kwa nyumba hizi ni kugharamia kundi dogo la watu kwa gharama ya wananchi wote. Hoja ingekuwa na maana sana iwapo msamaha huu ungekuwa kwa vifaa vya ujenzi kwa ujumla ili kila Mtanzania afaidike.

Pili, ni kosa kubwa kuomba msamaha wa kodi kwa taasisi moja. Ni mtu ambaye hajui mfumo wa kodi vizuri anayeweza kusimama kuomba msamaha wa kodi wa Shirika moja. Kwa hiyo context yenyewe was wrong. Ndio maana nilishauri Bunge kuwa msamaha uwe kwa taasisi yeyote inayojenga nyumba kwa gharama nafuu iwapo tunaona ni muhimu kuwa na msamaha huo. Kimsingi napingana na wazo lenyewe in its totality. Ni wazo ambalo litafaidisha wakandarasi binafsi na sio wananchi. Zero rating system haina faida kwa mlaji wa mwisho bali kwa mzalishaji husika. Ilikuwa ignorance tu ya kamati husika katika kutoa pendekezo hilo.

Suluhisho la kudumu ni kutoa ruzuku kwenye vifaa ili viwe vya bei nafuu. Pia kuongeza uzalishaji wa vifaa vya ujenzi nchini kama saruji nk. Baada ya Dangote kuanza kuzalisha, bei ya Saruji inaweza kushuka hadi kwa 30% iwapo hataingia katika cartel na wenzake waliopo nchini. Lakini pia Serikali inaweza kutoa ruzuku kwa mtu yeyote anayenunua nyumba mpya kama inavyofanyika UK hivi sasa. Hata hivyo uchumi wetu bado mdogo kuhimili hilo na pia mfumo wetu wa kifisadi utapelekea skandali nyingi sana katika msaada wa aina hiyo.
Mh Zitto nakubaliana na wewe kuhusu ruzuku kwenye vifaa vya ujenzi. Hii ilikua sera yenu CHADEMA wakati wa kampeni za uraisi za Dr Slaa. Nilipata kumsikia tena hata baada ya kampeni za urais akizunguzumzia ruzuku ya vifaa vya ujenzi. Lakini mh Zitto kama nia ni kusaidia watanzania maskini je vipi kuhusu wafanyabiashara wakubwa wanaojenga maghorofa makubwa?? je nao wapo titled na hizi ruzuku??
 
Last edited by a moderator:
Bongo bana yan mtu anapewa tuzo katika mchango wa kipekee ktkt jamii,tena kimataifa lkn nyumbani wanaponda,kweli mfalme atambi kwao.
 
Nyumba nyingi zinajengwa kwa ubia na kampuni binafsi. Kwa hiyo Kamati ilikuwa inaomba msamaha wa kodi kwa kampuni binafsi zinazofanya kazi na NHC. Wiki moja tu iliyopita tulikuwa tunapinga kwa mapovu misamaha ya kodi, leo tunatumia jukwaa hilo hilo kupigia debe misamaha. Kama sio umazwazwa ni nini?

Nakuelewa sana sana hoja yako hii

Pia ulipomjibu Eddy hapo juu umegusia Ruzuku kwa anayenunua nyumba mpya.

Ni kweli kwa mfumo huu corrupt itakua balaa zaidi hata kama economy ingekua inahimili.Mfumo wetu hauna tofauti na wa Nigeria

Nakumbuka Serikali ya Nigeria ilipotoa Ruzuku kwenye mafuta wafanyabiashara wakubwa walianza kuuza Ghana na nchi nyingine

Hapa kwetu uuzaji tu wa nyumba za Serikali ilirekodiwa ufisadi wa kutisha.System yetu ni mbovu sana

Pia sioni namna ya kumzuia Dangote asiingie kwenye Cartel na wafanyabiashara wenzake na kuna hatari wafanyabiashara na makampuni madogo ya Saruji yakapotea na kutengeneza ukiritimba mpya wa makampuni makubwa kwenye soko tena.

I'm worried!
 
Nadhani ni vizuri kupata maneno niliyosema (verbatim). Sikusema wapewe NSSF na PSPF tu, nilisema kuwa wanaojenga nyumba za gharama nafuu ni wengi hivyo huwezi kutoa msamaha kwa Shirika moja tu. Kama unatoa toa kwa yote ikiwemo GEPF, LAPF, PPF, NSSF etc. Lakini msingi wenyewe wa hoja ninaupinga kwani huo msamaha hautasaidia wanyonge

Lakini Zitto jana sikuelewa sababu za wewe kumtetea Lukuvi. Pengine unamfahamu zaidi, lakini nachelea kusema si rahisi kuwashawishi watu wengi kuwa Lukuvi ni mtu safi.

Hata kama unamfahamu sana, tuhuma zimeelekezwa kwake, kwa nini usimuache ajitete mwenyewe? Hata kama ulikuwa na dhamira safi kumtetea, inafanya baadhi yetu kutia mashaka kwa kuwa Lukuvi anaweza kujitetea mwenyewe. Na nilisikia ukimsihi Lugola amchunie Lukuvi kwa kuwa ni mshikaji? Au nilisikia vibaya?

Well, niliwahi ku-interact na huyu Mhe. Lukuvi wakati tukijaribu kufanya kazi fulani huko Mbomipa (Jimbo la Ismani). Nachelea kusema, zaidi ya 90% ya aliyosema Lugola ni sahihi. Nachotaka kusema, tuache double standards. Tukiamua kukataa ufisadi, hakuna cha ushikaji. Kila mtu ashughulikiwe kwa makosa anayofanya. Hili linataka kufanana na lile la kutowabana Gavana Ndullu na Waziri Mkuya kwenye sakata la escrow.
 
Mifuko ya Hifadhi ya jamii aka superannuation iko kwa maslahi mapana ya wananchama! Duniani kote mifuko hii hutumika kuwakomboa wananchi wake!

Liquidity kwenye mifuko hii ni muhimu sana muda wote! Miradi ya Ujenzi wa nyumba za Bei nafuu kwa wananchama wake ni muhimu sana kwani maisha bila nyuma hayakamiliki! Makampuni mengine yaendelee kufanya biasha za nyumba kwani mahitaji ni mengi zaidi ...

Naunga mkono hoja ya Zitto kuwa Mifuko inastahili misamaha ya Kodi kwenye Ujenzi same kwa wananchi wa kawaida..
 
Nashukuru sana kwa maoni yako mazuri sana. Kwanza, dhana nzima ya misamaha ya kodi ninaipinga. Nyumba ambazo NHC, NSSF, PPF, PSPF etc wanajenga zinanufaisha sehemu ndogo sana ya Watanzania. Kutoa msamaha wa kodi kwa nyumba hizi ni kugharamia kundi dogo la watu kwa gharama ya wananchi wote. Hoja ingekuwa na maana sana iwapo msamaha huu ungekuwa kwa vifaa vya ujenzi kwa ujumla ili kila Mtanzania afaidike.

Pili, ni kosa kubwa kuomba msamaha wa kodi kwa taasisi moja. Ni mtu ambaye hajui mfumo wa kodi vizuri anayeweza kusimama kuomba msamaha wa kodi wa Shirika moja. Kwa hiyo context yenyewe was wrong. Ndio maana nilishauri Bunge kuwa msamaha uwe kwa taasisi yeyote inayojenga nyumba kwa gharama nafuu iwapo tunaona ni muhimu kuwa na msamaha huo. Kimsingi napingana na wazo lenyewe in its totality. Ni wazo ambalo litafaidisha wakandarasi binafsi na sio wananchi. Zero rating system haina faida kwa mlaji wa mwisho bali kwa mzalishaji husika. Ilikuwa ignorance tu ya kamati husika katika kutoa pendekezo hilo.

Suluhisho la kudumu ni kutoa ruzuku kwenye vifaa ili viwe vya bei nafuu. Pia kuongeza uzalishaji wa vifaa vya ujenzi nchini kama saruji nk. Baada ya Dangote kuanza kuzalisha, bei ya Saruji inaweza kushuka hadi kwa 30% iwapo hataingia katika cartel na wenzake waliopo nchini. Lakini pia Serikali inaweza kutoa ruzuku kwa mtu yeyote anayenunua nyumba mpya kama inavyofanyika UK hivi sasa. Hata hivyo uchumi wetu bado mdogo kuhimili hilo na pia mfumo wetu wa kifisadi utapelekea skandali nyingi sana katika msaada wa aina hiyo.
Naunga mkono kwenye hoja kwamba, ikiwa ni misamaha basi iwe ni kwenye vifaa vya ujenzi ili idadi ya wanufaike iwe kubwa zaidi.

Hata hivyo, sikubalini na hoja kwamba, kutoa msamaha kwa nyumba kutanufaisha wachache... hili halikwepeki hata kama wataamua kutoa misamaha kwenye misamaha... sio wote watakaonufaika kv, hata kama bati litauzwa sh.5000/- bado si kwamba kila Mtanzania atakuwa na uwezo wa kununua bati... babu yangu kule kijijini ataendelea kuezeka majani wakati kodi yake ambayo ingesaidia kununua dawa kwa ajili yake imekuwa sacrificed kwenye vifaa vua ujenzi!

Heri hilo la mabati lakini kuna vitu kama kompyuta... sidhani kama kodi imerudishwa! Kodi iliyosamehewa huku huenda ingesaidia kununua madawati na kumsaidia mtoto wa maskini ambae, si ajabu katika uko wake wote hamna hata mmoja mwenye uwezo wa angalau kutumia achuilia mbali kununua laptop iliyosamehewa kodi... sana sana hapo napo wanaofaidika ni wachache wale wale!!!

Kutokana na hilo, suala la kuufaisha wachache ili mradi ni Watanzania isiwe ajenda! Kwangu mimi, ikiwa ombi la kupunguza ama kuondoa kodi kwenye nyumba ni ili kuzifanya nyumba hizo kuwa za bei nafuu kweli kweli then let it be na kweli tuone bei ya nyumba zimepungua with almost the same proportionality bila kujali amenufaika nani... wale wachache watakaonufaika, wata-route the surplus to other economic activities!

Aidha, lingine la kuzingatia isije kuwa watu wanasamehewa kodi halafu wana-route faida ya benefits za misamha ya kodi kwenye biashara isiyo lengwa... hili linafanyika sana kwenye maduka ya jeshi! Juzi hapa nilienda kwenye duka moja la jeshi nikakuta Tv inauzwa sh. 11 million... nikajiuliza ikiwa kweli Tv hiyo imewekwa kwa ajili ya wapiganaji wetu!

Hofu yangu nyingine hapa ni kwamba, isije kweli hao NHC wanapunguziwa kodi na gharama za ujenzi kushuka kwa (say) 20% lakini bei ya nyumba ikashuka kwa 2%...
 
Nne, Limekuwepo tatizo la NHC kujilipia garama za ujenzi wa miundo mbinu kama kuvuta umeme na maji na ujenzi wa barabara, ningeshauri serikali iwapatie ruzuku NHC pale wanapojiwekea umeme na maji au kulipa fidia kwa wananchi wanaopaswa kupisha mradi, kwani jukumu la kuweka miundombinu ni la serikali, basi inaposaidiwa ni bora ikafia kwa kutoa ruzuku.

Naamini kabisa NHC ikipewa support ya kutosha nyumba hizi zitauzwa mil tatu na kila mwananchi atamudu kununua nyumba badala ya mtindo wa sasa kila mtu kujijengea kijumba kwa tabu.
kwa mwenendo walio nao sasa NHC nadhani hata wakiondolewa huo msamaha bado nyumba wanazojenga zitanunuliwa na wenye pesa tu kwani wanaziuza kwa bei ya juu sana. Kwa Tanzania tabia hujenga mazoea kwani inawezekana punguzo la kodi likawa na malengo ya kupunguza gharama za ujenzi na hivyo kushusha bei za nyumba lakini baada ya taratibu kupitishwa mtakuja kunambia.

Tazama sakata la masuala ya umeme tu lilivyo. wakati wa shida kubwa ya maji bwawa la kihansi umeme ulipanda na tukaambiwa taraibu zitarejea katika hali ya kawaida lakini nambie leo hii ni watu wangapi wanalia kutokana na gharama za ujenzi

The Listener
Ex Detective
 
Hukumuelewa Zitto.

Simply alisema kwenye zama hizi huwezi kuondoa kodi specific kwa institution! Hiyo ni agaist sheria iliyopitishwa na Bunge hilo hilo tena muda ndani ya miezi 4 iliyopita!

In short kuwepo na pendekezo la namna ile ni aibu kwa Bunge letu. Meaning haliko makini.
 
Nyumba nyingi zinajengwa kwa ubia na kampuni binafsi. Kwa hiyo Kamati ilikuwa inaomba msamaha wa kodi kwa kampuni binafsi zinazofanya kazi na NHC. Wiki moja tu iliyopita tulikuwa tunapinga kwa mapovu misamaha ya kodi, leo tunatumia jukwaa hilo hilo kupigia debe misamaha. Kama sio umazwazwa ni nini?

Asante kwa ufafanuzi mkuu, nimekuelewa kuwa yanayo ombewa msamaha ni wakandarasi wa NHC na sio NHC yenyewe! sasa najiuliza kwa kuwa NHC biashara yake ni kujenga nyumba kwa ajili ya watanzania sasa kwanini lisiwe na kikosi chake cha ujenzi? kwani hiyo ndo tradditional business yao, wanaweza shirikiana na SUMA-JKT na idara ya magereza, kwa kufanya hivyo tutasaidia kutoa stadi za maisha kwa vijana wetu walioko jkt na vijana walioko magerezani amabao wengi wao walishajirudi.

Hili la kuwapigia chepuo wakandarasi huo ni mchoro wa dili, pili hili suala la kusamehe kodi vifaa vinavyo agizwa nje ya nchi napingana nalo kabisa, ni bora tukatoa msamaha kwa vifaa vinavyozalishwa nchi kwani kutahamasisha wafanyabiashara kujenga viwanda humuhumu nchini na kuleta ajira kwa vijana wetu.
 
hiv umewai kuulizia hizo nyumba za bei nafuu bei yake?hawana lolote nyumba hapewi mwananchi wa kawaida,wanataka kukwepa kodi tu.nyumba tujenge wenyewe.

Bei ziko juu kwa sababu nyumba yenyewe unailipia VAT na makorokoro ya kodi, maji umeme barabara wajijengee wenyewe, sasa kama tunaweza kumwekea umeme mwananchi kwa kulipia elfu 27, iweje NHC wasilipe elfu 27 tukawawekea umeme? kama tunaweza jenga barabara ya lami kwenda kwenye hotel ya mhindi sasa tunashindwa nini kuweka barabara ya lami kuelekea makazi yaliyojengwa na NHC? Je ni halali NHC kujinunulia transfomer badala ya tanesco kuwapatia bure au kugharimiwa na REA?
 
Nyumba nyingi zinajengwa kwa ubia na kampuni binafsi. Kwa hiyo Kamati ilikuwa inaomba msamaha wa kodi kwa kampuni binafsi zinazofanya kazi na NHC. Wiki moja tu iliyopita tulikuwa tunapinga kwa mapovu misamaha ya kodi, leo tunatumia jukwaa hilo hilo kupigia debe misamaha. Kama sio umazwazwa ni nini?

Zitto, naomba nitofautiane nawewe tena, nyumba haipaswi kutozwa kodi na ikibidi serikalai itoe ruzuku, kimsingi ukiwa na nyumba bado utalipa property tax, umeme utakaotumia utaulipia VAT, maji utakayotumia utalipa VAT hiyo kodi inarudi, hebu fikiria kwa miaka 50 ya uhai wa hiyo nyumba atakuwa amelipa kodi kiasi gani? nikwambie katika jambo linaloumiza watu ni kujenga nyumba ya kuishi.

Fikiria leo hii eneo la kujenga acha kiwanja kilichopimwa halipungui mil tano, huyu mwalimu polisi nesi dereva wa daladala na bodaboda watamiliki nyumba lini? Hili wazo kuwa watafaidika matajiri ni upuuzi pia, hivi mengi au bhakresa ataenda nunua nyumba ya chumba na sebule? ya nini? au matajiri gani tunaowazungumzia?
 
Hivi kwa nini NHC wasijenge nyumba za kupangisha? Hivi kuna namna nzuri zaidi ya kuboresha makazi zaidi ya kujenga nyumba ambazo watu wengi wanamudu kulipia kila mwezi? eddy anazungumiza traditional business. Traditional business ya NHC ni kuuza nyumba?

Kama mtu anataka kununua nyumba, si aende akanunue kwa makampuni binafsi? Mimi sina shaka lolote kuwa NHC inatumika vibaya kupora mali za umma, hususan prime plots zinazomilikiwa na shirika hilo. Na wanaonufaika zaidi ni viongozi wakiwemo wabunge na wafanyabiashara wakubwa.
 
Back
Top Bottom