mkuu naomba usimshambulie zitto. tupeane mawazo tu. mie huwa najiuliza israel wanapigana ukanda wa gaza wananyakua ardhi wanajenga makazi wayahudi wanapewa bure. sisi ardhi tunayo rasilimali tunazo hatutaki watanzania wapate makazi bora kweli?
dar kiwanja cha bei nafuu ni mil5 tena ukanunue ikwiriri. huyu mwalimu atapata wapi muda wa kusimamia mafundi. achilia pesa ya kununua cement mchanga na nondo.
duniani kote serikali ndo inajenga nyumba inawauzia wapangisha au kuwagawia wananchi wake. nenda uturuki urusi uarabuni afrika ya kusini uingereza marekani ni hivyo hivyo. mashirika ya umma yanajenga nyumba yanagawia wanauzia wananchi wake kwa mkopo.
Mkuu eddy
Kwa faida ya wasomaji wa JF unaweza kutupa sababu muhimu ni kwa nini NHC peke yao wapatr msamaha wa kodi.
Ahsante.
Mil 60 Ndo Nyumba Yenye Gharama Nafuu, Hata Kama Ni Nje Ya Mji.
Haya mashirika yakichukuliwa na wasanii na watu wengine wasioweza monitor issue ktk real time huwa mwihso wake ni mbaya sana.Waingereza na wengine huwa wanaweka macho haswa na uwekezaji wao huwa unawekwa kwenye ulinzi hata wa kidiplomasia.NSSf wacha wacheze urafiki na kupindisha habari.Zitto lazima awalinde mkurugenzi si swahiba.NSSF TAYRI INAISHI KWA KUDANGANYA UMMA.Nimeona watu wengi sana wana statements ambazo zinaonyesha makato ya Afya, uzazi yakiwa yameandikwa kuliko walivyopokea.Na mbaya zaidi NSSF hawatangazi hayo mafao km yanakatwa ktk michango ya mwanachama na yanapunguzwa ktk akiba yake.Hatari yake ni kwamba watu watatumia na NSSF watakata huduma kwa kiwango cha kifisadi toka ktk vituo vya afya, kingine ni hatari ya wizi wa maafisa wa NSSF kwa kila transaction inayoweza fikia mahali wastaafu wasipate kitu,na waliokula wameshakufa.KI UKWELI NSSF NA WENGINE NI MASHIRIKA YANYOENDESHWA KIUPATU UPATU KM UPATU MWINGINE,ILA WENYEWE WAMEHALALISHWA.KINACHOWALINDA NI UWEKEZAJI WA HIZO HELA AMBAO UNAHITAJI KUWA MAKINI SANA.SIKU ZOTE KM BANK WANATEGEMEA SANA ONGEZEKO LA AKIBA ZINAZOINGIA KULIKO WANAOTOA MICHANGO YAO.NSSF TAYRI IMESHAFIKIA SATURATION HAIWEZI WALIPA WOTE WANAOTOKA NDIO MAANA WANA DRAMA SANA KTK KUTOA HELA.HAWATOI MSAADA SANA KWA MWANACHAMA KUJUA NINI KIWE TAYARI ILI PATE.HII NI KWAVILE SLOTS WANAZOTOA HAZITOSHI MAOMBI YA KUJITOA.NDIO MAANA WANA HIZI JITIHADA,HADI WAKALETA MAOMBI YA KUZUIA FAO LA KUJITOA.SASA HIVI NSSF WAPO KTK RATE KUBWA YA KUJITOA KULIKO KUINGIA.NA MATUMIZI YAO, UWEKEZI USIO NA KIPIMO AU HAKIKA YA KURUDISHA HELA HARAKA NA MUDA MREFU KUWEZA SUSTRAIN WANAOTOKA HAUPO TENA.Haya mashirika ya Umma yanahitaji a very serious monitoring system Yanatakiwa hata investment zao ziangalie sehemu ambazo private sector wameshindwa lakini ambazo ni public utility Ni kosa kubwa Mashirika haya kutoa Mwanya wa Tax evasion kwa makampuni binafsi kupitia kandarasi
Kwa vile soul business ya NHC ni housing.NSSF na wengine ni pendion fund na kuwekeza ktk nyumba diversification tuu.Pia nao wanaweza wekeza kupitia NHC.Km waliwekeza ktk banking.Mbona wasiombe na banking pia BOT wabadili riba?sasa wakiomba kila sector waliyowekeza ipewe ruzuku serekali ya ccm itaweza?Haya mashirika yajifunze kuwekeza kwa akilina ufanisi km wanaona haiendi basi wajue hiyo idara si salama sana kwao.Mkuu eddy Kwa faida ya wasomaji wa JF unaweza kutupa sababu muhimu ni kwa nini NHC peke yao wapatr msamaha wa kodi. Ahsante.
Zungu, nadhani ni sahihi NHC kujenga nyumba na kuuza, halafu TBA (Tanzania Building Agency) hawa wakafanyakazi ya kupangisha nyumba hasa watumishi wa umma ambao huhitaji kuhama mara kwa mara, kuhusu nyumba zilizoko prime area NHC inajenga kwa ubia na private developers hili ni jambo la maana sana kwani maslahi ya shirika na maslahi ya wananchi yote yanalindwa kwa pamoja.
Tangia Zitto alipoingia kwenye hali y kutoelewana a Chama chake au niseme baadhi ya Viongozi wa Chadema Watanzania tumejenga chuki na uhasama usiona na msingi kwa Zitto. Tunayasahau mengi mzuri aliyowanyia na anayowafanyia Chadema na Watanzania. Tumekuwa wajinga tusiothamini uwezo na jitihada za Watanzania wezetu kwa kumshabikia mtu Fulani au kukubali na kauli ya Fulani bila kufanya uchambuzi wa kina na kuwa na marejeo ya kutosha kabla hatujaamua kuendeleza chuki zetu.Jana wakati wa kuhitimisha kikao cha bunge ulikuwepo mjadala wa kulipatia msamaha wa kodi shirika letu la NHC, binafsi nilifarijika sana na wabunge wetu walifarijika sana. Lakini wapo wabunge wengine akiwemo Zitto walishauri misamaha hiyo itolewe pia kwa mashirika kama PPF na NSSF, hapo ndo natofautiana na zitto.
Kwanza, NSSF na PPF sio jukumu lao kujenga nyumba (traditional business), jukumu lao ni kutunza mafao ya uzeeni (pension scheme), hivyo basi hawana wajibu wa kujihusisha na hii biashara na kama watahitaji kuwapatia wanachama wao nyumba za bei nafuu watazinunua NHC na kuwagawia na sio kuanzisha kandarasi za ujenzi.
Pili, hawa NSSF/PPF wamekuwa wakijihusisha na ujenzi wa majengo makubwa ya kibiashara yenye kuwaingizia faida kwa lengo la kuhifadhi akiba za wanachama wao, wamekuwa wakidai ujenzi wa nyumba za bei nafuu hauna tija sasa leo iweje walilie kuwekeza kwenye biashara isiyokuwa na tija? hapana.
Tatu, NSSF/PPF sio wajenzi hivyo wamekuwa wakikodi wakandarasi kutekeleza miradi yao hapa ni kutengeneza uchochoro wa kukwepa kodi kupitia makampuni yatakayopewa kandarasi za ujenzi, hapana kaeni pembeni.
Nne, Limekuwepo tatizo la NHC kujilipia garama za ujenzi wa miundo mbinu kama kuvuta umeme na maji na ujenzi wa barabara, ningeshauri serikali iwapatie ruzuku NHC pale wanapojiwekea umeme na maji au kulipa fidia kwa wananchi wanaopaswa kupisha mradi, kwani jukumu la kuweka miundombinu ni la serikali, basi inaposaidiwa ni bora ikafia kwa kutoa ruzuku.
Naamini kabisa NHC ikipewa support ya kutosha nyumba hizi zitauzwa mil tatu na kila mwananchi atamudu kununua nyumba badala ya mtindo wa sasa kila mtu kujijengea kijumba kwa tabu.
===========
Majibu ya Zitto:
Haya mashirika ya Umma yanahitaji a very serious monitoring system
Yanatakiwa hata investment zao ziangalie sehemu ambazo private sector wameshindwa lakini ambazo ni public utility
Ni kosa kubwa Mashirika haya kutoa Mwanya wa Tax evasion kwa makampuni binafsi kupitia kandarasi