Zikiwa zimebaki siku chache kablaya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusuukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chinizinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi nabaadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu yaTanzania akaunti ya Escrow.
Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zinavielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikanakama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa naBwana Joseph Mkandege). Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.
Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazungukakwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadalakutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.
Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari "Zitto na Filikunjombe wanatumiwa naKenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu"zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habariili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.
Tuhuma #1 :
Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamojawameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, CertificateNo 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafutayanayofanya kazi nchini hapa.
Majibu:
Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited byGuarantee'. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewehaijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile nakampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars.Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.
Tuhuma #2 :
Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia wapasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel Knospe nyumbana gari ya kukodi.
Majibu:
Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapanchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana niuwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya Bwana Ongangikuthibitisha madai yao.
Tuhuma #3 :
Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwakwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na Mwananchi) mwandishimkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.
Majibu:
Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa Norway.Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wanguniliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namnayoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hiiwanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.
Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola zaMarekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi chamiaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa. Uamuzi wa Kamati ya PAC kutakamikataba yote ya Gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yotenchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusikakuingia mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba nawanataka umma wa watanzania usijue!
Tuhuma #4 :
Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafutagesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji mkubwa Tanzania Barakwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.
Majibu:
Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari inamakubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalunamba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya Petrobras ya Brazilkwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC.Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharauna kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.
Tuhuma 5:
Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchinimwetu.
Majibu:
Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hiiimeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishevinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidiya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata haowanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.
Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):
Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasakwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na Kafulila kuhakikishakwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa deni lake lisilotambulikakisheria nchini mwetu.
Majibu:
Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hatadiplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoatuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa naTaifa lolote lile. Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengineambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo. Kwanguitikadi yangu ni ‘Uzalendo kwa nchi yangu', ni jambo ambalo halina mbadalawake. Siku zote nasema "Right or wrong, my country first". Kurudia kurushatuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburicha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.
Aidha, wanatuhumu kuwa "Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150 millionkama deni likilipwa"
Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari.Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.
Tuhuma #7 :
Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale TANESCO.Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa hasira za kukosafedha za kitapeli za TANESCO.
Majibu:
Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibumambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs bilioni 200 kutokaBenki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma nikupungukiwa hekima na busara.
Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa "Naomba tuwe macho na Wabunge wetuachananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na Kampuni yaSHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza. Serikali ya Kenya natapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na Kafulila".
Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwakushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma kama hizihaziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisitutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni ummauujue ukweli wa mambo.
Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:
Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa TPDC kwakushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya Gesi naMafuta.
Pili, ni uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa kuanzishwana kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12 zinalipwa na TANESCO kila mwezikwenda kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth (50%) na watuwasiojulikana kupitia kampuni ya Simba Trust iliyosajiliwa na kufichwa nchiniAustralia (50%).
Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka TANESCOizalishe au isizalishe Umeme! Watanzania, PAP itaendelea kulipwa namna hiyo kwamiaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo Seth analindwa na baadhi ya watendajiSerikalini na hasa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, kuna fununukuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya PAP. Seth piaanamiliki kitalu cha gesi Mnazi bay Kaskazini kupitia kampuni ya HydroTanz.
Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na Kamati yangu zimewapelekea kugushinyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili kutuogopesha nakutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala la uporaji wa fedhakutoka Benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye mstari. Mimi na wenzanguhatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na wabunge wenzetu kuhakikisha ukweliunajulikana na wezi kuchukuliwa hatua kali.
Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotakakukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia.Watanzania sio mabwege!
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC