Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Kusema kweli huwezi kuamini jinsi chuki na roho mbaya zinavyoweza kuwafanya watu vipofu, jamaa wananikumbusha enzi za Abubakari Kombo wa ile timu ya zamani ya Sigara na baadae Simba aliyekamia kula Sahani moja dhidi ya Edibily Lunyamila wa Yanga!, Kila akikutana naye jamaa anakaa man to man, kiatu mtindo mmoja. Lakini Guess what, Jamaa alicheza viatu sana, Lakini lunyamila akigeuka tayari keshampiga mtu tobo, anateleza wingi ya kushoto anaweka majaro Kizota au Muhammed Hussein mmaching anatupia kiulaini!!, wakati huo Abubakari kombo anaishia kupewa Red card tu!!.

Huu ni mfano wa Zitto!, kuna watu wameamua kumkaba man to man, kwenye mitandao na popote pale!, Ni watu wazima na akili zao, na wanajua wananchokifanya lakini wameamua Kuharibu tu, kutokana na chuki zao zisizopimika dhidi ya mheshimiwa Zitto. Wao wako tayari TAIFA ZIMA LIKOSE, ILIMRADI ZITTO APOTEZE

Watu wa aina hii mimi nawaita makuwadi wa mafisadi, Mafisadi wa kisiasa, ndio ni mafisadi,kwa sababu If they walk like a duck, Swim like a duck and Quack like a duck then they must be ducks (Mafisadi kwa muktadha huu).

Eti wanataka Mtuhumiwa alete proof ya majibu yake, lakini wanajua kabisa the burden of the proof lies squarely on the accuser, WANAWAACHA WANAOTUHUMU WANA GO AWAY NA TUHUMA, THEN WANAKOMAA NA MTUHUMIWA ALETE USHAHIDI WA UTETEZI WAKE!!!, THIS IS JUST AN UNFAIRNESS OF THE HIGHEST ORDER!!.

Nadhani sisi wananchi tuliochukizwa kwa dhati na madudu haya ya Escrow, tuendelee kupambana kwa nguvu, kwa kuwaunga mkono makamanda wetu wa Upambanaji waliosimama kuhesabiwa, walio msitari wa mbele katika hili, MAKAMANDA HAWA NI MFANO WA "MAWE YALE WAASHI WALIOKATAA, SASA YAMEKUWA MAWE MAKUU YA PEMBENI", nayo ni mheshimiwa Kafulila na Mheshimiwa Zitto!.

Wale waliomua kula karamu na kugongeana Glasi za kifisadi, na ulevi wao kuwafanya wawarushie chupa kamanda wetu, hao sisi tunawaacha na hangover zao sisi tunasonga mbele, hawa watahukumiwa katika mahakama za kihistoria.

Jamaa hawathubutu kuona japo kale kaujasiri ambako kamanda wetu amejitolea, ndugu zanguni kama mnamchukia sana mheshimiwa Zitto, heshimuni basi hata sacrifice yake katika mapambano haya. WENGI TULIOWATEGEMEA WAPAMBANE KWA PAMOJA NASI KATIKA VITA HII WAMEKAA KIMYA, HAWADHUBUTU, NA YULE ANAYEHATARISHA MAISHA YAKE MBELE YA MTANDAO HATARI WA MAFISADI, NAYE BADO MNAMRUSHIA MAWE!!!, NYINYI MNAMUUNGA NANI MKONO?.

Ujanja mnaotumia hapa ni kwamba, kila tukileta hoja ambazo mnajua ni dhahiri hamna majibu, mnakimbia kwa muda ili vumbi litulie, kisha mnarudi na hoja zile zile baada ya kuhakikisha kwamba wafuatiliaji wa mjadala huu wamesha sahau hoja zetu za awali ambazo mmekimbia kuzifanyia ufafanuzi. Pengine ni vyema tukaanza kurudia yale yale tuliyojadili, mengine yakiwa addressed moja kwa moja kwako, Waberoya na wengine.

Nianze na hili (cc Ritz):

katika bandiko namba 630, tarehe 11/November, majira ya saa tisa na nusu za mchana Afrika mashariki, nilijadili hivi:

["Sisi hatumshindanishi zitto na mtu Bali tunamshindisha na Dhana ya integrity kwani tunaamini Kwamba hii ni Sifa ya msingi anayotakiwa kuwa nayo kiongozi yoyote anayeingia vitani kupambana na ufisadi.

Hatupo Hapa kujadili mbadala wa zitto, tupo Hapa kuchambua viongozi wote ambao wanajitokeza kutetea maslahi yetu wananchi ili tusije kuachwa solemba kama suala la fedha za uswisi n.k. Kwahiyo basi, kila kiongozi atakayejitokeza Katika hili, tutamchambua kwa hoja kwa nia ya kubaini iwapo anatufaa au hatufai kutetea maslahi yetu. Na nadhani mnatambua Kwamba tuna Haki ya kufanya hivyo."]

Nitajitahidi kurudia hoja zetu zote ambazo mmekuja na mkakati wa kuzikimbia and then when the dust settles, mnarudi and take advantage ya wachangiaji wageni humu kutafuta sympathy and support, wachangiaji ambao bado hawajapata nafasi ya kupitia hoja zetu za awali na kuzipambanisha na hoja zenu kwa nia ya kuchambua pumba na mchele katika upande wetu wa hoja, na pia pumba na mchele katika upande wenu wa hoja.
 
gamba @La NYOKA,

Umesema mengi kujaribu kuaminisha hoja za wadau kuhusiana Na Majibu ya Zitto ambyo ndio yanaongoza mjadala kuwa ni chuki tu kitu ambacho hakina ukweli hata chembe.

Kimsingi tunaohoji tunasimama katika mantiki ya Majibu ya Zitto ambyo ni kuhusiana na tuhuma alizopewa,Majibu yake yameacha baadhi ya tuhuma zikiwa hazina Majibu,Rejea Maswali ambyo yameulizwa na Nguruvi3 na Mchambuzi,Maswali yao yapo wazi na yamejikita kwenye Mjadala ambao umewekwa na Zitto mwenyewe.

Kusema/kuwaita ni makuwadi wa mafisadi huku maswali yao yakiwa hayana majibu ni matokeo yakutokuwa na majibu,Katika hali ya kawaida na kwa fkra huru ambzo hazina ukomo Majibu ya Zitto hapa yanaongeza/kuzidisha sintofahamu kuhusiana na tuhuma dhidi yake.

Hamna Mtanzania anayeunga Mkono ukwapuaji wa Bilioni 200 katika akaunti ya ESCROW Bali wapo wamoja ila haitoshi tu kuimba na kushangilia kila lisemwalo bila kwende mbele zaidi kwa wanaosema kuhusiana na dhamira zao kama kweli ni kwa ajili ya umma ama vinginevyo kuna mdau hapa amesema yakuwa Zitto anaonewa kwa kuwa tu anapata Credit maneno hayo yanaakisi kwa kiasi flani baadhi ya hisia za wadau.

Unamchukia Zitto kuliko CCM, full stop
 
Last edited by a moderator:
Ujanja mnaotumia hapa ni kwamba, kila tukileta hoja ambazo mnajua ni dhahiri hamna majibu, mnakimbia kwa muda ili vumbi litulie, kisha mnarudi na hoja zile zile baada ya kuhakikisha kwamba wafuatiliaji wa mjadala huu wamesha sahau hoja zetu za awali ambazo mmekimbia kuzifanyia ufafanuzi. Pengine ni vyema tukaanza kurudia yale yale tuliyojadili, mengine yakiwa addressed moja kwa moja kwako, Waberoya na wengine.

Nianze na hili (cc Ritz):

katika bandiko namba 630, tarehe 11/November, majira ya saa tisa na nusu za mchana Afrika mashariki, nilijadili hivi:

["Sisi hatumshindanishi zitto na mtu Bali tunamshindisha na Dhana ya integrity kwani tunaamini Kwamba hii ni Sifa ya msingi anayotakiwa kuwa nayo kiongozi yoyote anayeingia vitani kupambana na ufisadi.

Hatupo Hapa kujadili mbadala wa zitto, tupo Hapa kuchambua viongozi wote ambao wanajitokeza kutetea maslahi yetu wananchi ili tusije kuachwa solemba kama suala la fedha za uswisi n.k. Kwahiyo basi, kila kiongozi atakayejitokeza Katika hili, tutamchambua kwa hoja kwa nia ya kubaini iwapo anatufaa au hatufai kutetea maslahi yetu. Na nadhani mnatambua Kwamba tuna Haki ya kufanya hivyo."]

Nitajitahidi kurudia hoja zetu zote ambazo mmekuja na mkakati wa kuzikimbia and then when the dust settles, mnarudi and take advantage ya wachangiaji wageni humu kutafuta sympathy and support, wachangiaji ambao bado hawajapata nafasi ya kupitia hoja zetu za awali na kuzipambanisha na hoja zenu.

Unamchukia Zitto kuliko SHETANI(CCM)..!

yaani Zitto kuwa na rafiki mkenya we inakuuma, basi we ukawe rafiki yake wa kufa na kuzikana au vipi
 
Ujanja mnaotumia hapa ni kwamba, kila tukileta hoja ambazo mnajua ni dhahiri hamna majibu, mnakimbia kwa muda ili vumbi litulie, kisha mnarudi na hoja zile zile baada ya kuhakikisha kwamba wafuatiliaji wa mjadala huu wamesha sahau hoja zetu za awali ambazo mmekimbia kuzifanyia ufafanuzi.

Kuna tatizo hili la NYIE na SISI katika uchangiaji wa mdada humu ndani. A kind of mob pyschology that is ruining the quality of discussions and all sense of reason and logic katika arguments. That aside, the last engament na mkuu Mchambuzi umeniuliza maswali mawili nikayajibu ila badala tuendelee umeingia katika generalizations and mere assumptions. Hebu turudi kwenye hoja, may be kuna watu wamekufa useme uliyoyasema hapo juu ila please i beg you brother do not go into that NYIE na SISI mentality. This is not a competition, its a discussion!
 
aisee ZZk go go go wewe wala sio wa kulinganishwa na mbowe uko level zingine kabisa
 
zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kamati ninayoongoza ya pac kuwasilisha bungeni taarifa maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya tegeta escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka benki kuu ya tanzania akaunti ya escrow.

Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama vivian emmanuel sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na bwana joseph mkandege). Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.

Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za tegeta escrow anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.

Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari "zitto na filikunjombe wanatumiwa na kenya na uingereza kuvuruga na kudhoofisha uwekezaji nchini mwetu" zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.

tuhuma #1 :

zitto anaye rafiki yake mkenya aitwae rapahel ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha gombe advisors co. Ltd (registered on 24 november 2011, certificate no 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na makampuni ya gesi na mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.

majibu:

gombe advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘company limited by guarantee’. Haina kazi na kampuni yoyote ya gesi na mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la kigoma all stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.

tuhuma #2 :

zitto amemsaidia ongangi kupata uraia wa tanzania na kwa sasa ni raia wa pasipoti. Zitto na ongangi walimtafutia ceo wa shell aitwae axel knospe nyumba na gari ya kukodi.

majibu:

raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya bwana ongangi kuthibitisha madai yao.

tuhuma #3 :

mikataba ya statoil iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwa kwenye magazeti ya kenya ya hapa nchini (the citizen na mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo ceo wa shell.

majibu:

mkataba uliovujishwa wa statoil ulivujishwa na waandishi wa habari wa norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa ceo wa kampuni ya shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.

Ikumbukwe kuwa mkataba wa statoil utaipotezea tanzania mapato ya dola za marekani bilioni 12 (takribani tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa. Uamuzi wa kamati ya pac kutaka mikataba yote ya gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia mikataba serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na wanataka umma wa watanzania usijue!

tuhuma #4 :

kampuni ya shell imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafuta gesi na mafuta kule pemba. Vilevile shell haina uwekezaji mkubwa tanzania bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa bara.

majibu:

ukweli ni kuwa kampuni ya shell ina vitalu 4 huko zanzibar na tayari ina makubaliano na serikali ya zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya petrobras ya brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya tpdc. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.

tuhuma 5:

ongangi anapokea maelekezo kutoka serikali ya kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.

majibu:

nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.

tuhuma #6 (juu ya uingereza):

uingereza imekuwa inamfadhili zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasa kwa hiyo sasa hivi ubalozi wa uingereza unamlipa zitto na kafulila kuhakikisha kwamba standard chartered ya uingereza inalipwa deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.

majibu:

nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa na taifa lolote lile. Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo. Kwangu itikadi yangu ni ‘uzalendo kwa nchi yangu’, ni jambo ambalo halina mbadala wake. Siku zote nasema “right or wrong, my country first". Kurudia kurusha tuhuma kwa ubalozi wa uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.

Aidha, wanatuhumu kuwa “kafulila na zitto wamehaidiwa 15% ya usd 150 million kama deni likilipwa”

mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.

tuhuma #7 :

mbunge mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale tanesco. Kafulila na zitto wanalipwa na mkono kuvuruga serikali kwa hasira za kukosa fedha za kitapeli za tanesco.

majibu:

hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya tshs bilioni 200 kutoka benki kuu ya tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.

Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa “naomba tuwe macho na wabunge wetu achananeni na madai ya zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na kampuni ya shell na inasemekana analipwa na ubalozi wa uingereza. Serikali ya kenya na tapeli mkubwa mbunge mkono nae anawalipa zitto na kafulila”.

Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwa kushiriki wizi wa fedha katika benki kuu ya tanzania. Kamwe tuhuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.

hasira hizi zinatokana na mambo mawili:

moja ni uamuzi wa kamati ya pac kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa tpdc kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya gesi na mafuta.

Pili, ni uamuzi wa pac kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa kuanzishwa na kufungwa kwa akaunti ya tegeta escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200 ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12 zinalipwa na tanesco kila mwezi kwenda kampuni ya pap inayomilikiwa na harbinder singh seth (50%) na watu wasiojulikana kupitia kampuni ya simba trust iliyosajiliwa na kufichwa nchini australia (50%).

Ieleweke kuwa pap inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka tanesco izalishe au isizalishe umeme! Watanzania, pap itaendelea kulipwa namna hiyo kwa miaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo seth analindwa na baadhi ya watendaji serikalini na hasa ndani ya wizara ya nishati na madini. Aidha, kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya pap. Seth pia anamiliki kitalu cha gesi mnazi bay kaskazini kupitia kampuni ya hydrotanz.

Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na kamati yangu zimewapelekea kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili kutuogopesha na kutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala la uporaji wa fedha kutoka benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye mstari. Mimi na wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na wabunge wenzetu kuhakikisha ukweli unajulikana na wezi kuchukuliwa hatua kali.

Harbinder singh seth aliiangusha serikali ya kanu nchini kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha serikali ya ccm wakiendelea kumkumbatia. Watanzania sio mabwege!

zitto kabwe
mwenyekiti pac

dodoma, 9 novemba 2014
kwa hiyo mheshimiwa zitto hutaki serikali ya ccm ianguke?
 
Tafadhali rejea bandiko 768 la Mchambuzi kwaufahamu zaidi.

Swali aliloleta Zitto kama tuhuma linahusu kumtafutia bosi wa Shell,Knospe nyumba na gari akishirikiana na Ongangi.

Hapa tunaona Ongangi akitajwa tena katika ushirika nje ya urafiki wa kawaida.
Huko nyuma ametajwa kama mshiriki wa Gombejambo ambalo Zitto hajakanusha au kukubali.

Majibu ya Zitto, kama ilivyokuwa kwakampuni ya Gombe, halikutoa majibu .
Hoja ya kumtafutia nyumba Knospe haikujibiwakama alivyokwepa hoja ya ushirika wake na Gombe.

Zitto, je ni kweliulishirikiana na Ongangi kumtafutia nyumba bosi wa shell? Ndio au hapana?

Hivi mkuu katika majibu yake juu ya hii tuhuma hukuona hii sentensi: "Tuhuma hizi hazina msingi wowote ulemaana ni uwongo". Kuna jibu gani zaidi unalohitaji?

Jibu la tuhuma kuhusu nyumba,ni kituko.Hakuna mahali katika tuhuma Zitto ameulizwa kuhusu familia ya Ongangi. Hivyokututajia amesoma wapi, ana watoto na mke kwa kifupi ni anachronism. Ni njia yakukwepa tuhuma.

Hivi kweli bosi wa Shell anahitaji Zitto amtafutie nyumba!!! Does that really scan katika logic yako? Na the fact kwamba Zitto ameshasema kuwa Ongangi ni private citizen (angalia majibu ya tuhuma ya kwanza) and anajua kuwa kuwa ana mke na watoto ni jibu tosha kuwa yeye anamfahamu huyo mtu. Hivi kweli tunahitaji spoon feeding mpaka katika understanding ya simple logic kama hizi?!! Shutuma kuwa amemsaidia kupata uraia; who is Zitto to have that power to grant people from other nations citizenship. Does that really scan katika logic yako?!

Lakini kuonyesha Zitto alikuwa frantic ,akilenga ku delude the public, ni pale anapotaka watoa tuhuma waonyeshe passport ya Ongangi. Hivi passport ya Ongangi inawezaje kuwa mikononi mwa wabaya wa Ongangi na Zitto? Come on !
Who is suppose to prove kuwa Ongangi ni Mtanzania (kwa kusaidiwa na Zitto)? anayetoa tuhuma au mtuhumiwa?
Jibu la passport amelitoa akiwa disoriented, na hapo ndipo panafikirisha.

Hata ninyi watetezi wake mkisoma tuhuma jibu nina uhakika mnaona aibu nyuma ya keboard zenu.

Haya watetezi karibuni, tutaendele na critic ya mstari, neno hadi nukta.

Nimemuomba na mkuu Mchambuzi kuhusu hili swala la NYIE na SISI..this is a discussion not a competition mkuu. There will be no winner announced at the end. Tuache haya mambo ya kugeneralize na ku assume, hayana msingi.
 
Mkuu zito akiondoa kale kadharau ka kuto taka kushindwa, kuto heshim wakubwa zake coz kapata popularity ni kiongozi mzuri...-ni ushauri tu kwako bwana zito... niliyo sema ni msingi mkuu wa mafanikio popote pale kwa mtu anae jijenga kazini au kwenye siasa... tunakusuport kwenye hili but watch out. .. ukiwagawa watz na kutaka kuua CDM kisa unataka respect tutakutosa na ndo utakuwa mwisho wako kisiasa... big up zito..
Hapana!no!la !ni bora kuwa na mtu huru asiyeburuzwa!tusilete mambo ya chama hapa,tunataka mtu anaepigania nchi chama ni kitendea kazi tu!mwacheni zitto awe kama alivyo!
 
Hivi mkuu katika majibu yake juu ya hii tuhuma hukuona hii sentensi: "Tuhuma hizi hazina msingi wowote ulemaana ni uwongo". Kuna jibu gani zaidi unalohitaji?

Hivi kweli bosi wa Shell anahitaji Zitto amtafutie nyumba!!! Does that really scan katika logic yako? Na the fact kwamba Zitto ameshasema kuwa Ongangi ni private citizen (angalia majibu ya tuhuma ya kwanza) and anajua kuwa kuwa ana mke na watoto ni jibu tosha kuwa yeye anamfahamu huyo mtu. Hivi kweli tunahitaji spoon feeding mpaka katika understanding ya simple logic kama hizi?!! Shutuma kuwa amemsaidia kupata uraia; who is Zitto to have that power to grant people from other nations citizenship. Does that really scan katika logic yako?!

Who is suppose to prove kuwa Ongangi ni Mtanzania (kwa kusaidiwa na Zitto)? anayetoa tuhuma au mtuhumiwa?
Jibu la passport amelitoa akiwa disoriented, na hapo ndipo panafikirisha.

Nimemuomba na mkuu Mchambuzi kuhusu hili swala la NYIE na SISI..this is a discussion not a competition mkuu. There will be no winner announced at the end. Tuache haya mambo ya kugeneralize na ku assume, hayana msingi.

Hivi ugonjwa wa wivu na chuki unaitwaje kwa kiinglish, na dawa yake inapatokana hospitali gani kwa gharama zipi...!

Mkuu kama we ni Daktari tusaidie kuwapatia dawa akin Nguruvi & Mchambuzi, nina hakika kinachowasumbua SI majibu ya Zitto kwa tuhuma anazotuhumiwa bali ni ileile ROHO YA KWANINI, CHUKI, WIVU, MAFUNDO, CHOYO, ROHO YA MAPEPO, kwahiyo wangetibiwa haya kwanza ili warudi kwenye hali yao ya kawaida...
 
Kama unakumbuka..!

Wakati wa mabilions ya Uswisi tulifanya ujinga kama huu, badala ya kumuunga mkono tukaanza kumsema Zitto anatumika na maCCM, na kuwa amechukua Bil. 3 kuiua CDM, mara ukaibuliwa waraka ikabidi aache kupambania uanchama wake...

Tunarudia Yale Yale tuliyokosea kwenye issue ya mabillions ya uswisi mwisho wa siku akikata tamaa tuanze tena kumsema kuwa akianzisha hamalizii wakati kumbe sisi ndio tunamfanyia ujinga...!

Kwa sasa tunachotaka tu ni PESA YETU IRUDI, aina yoyote ya tuhuma kwa Zitto ni kujaribu kumvunja nguvu kitu ambacho hatutakikubali-watu hawajiulizi tu kwann tuhuma hizi zinakuja wakati huu...?

Yote ni katika mikakati yako ya kupindisha hoja. Nadhani umesha sahau kwamba wewe ni mmoja wa wachangiaji ambao mmekuwa mkiweka makundi ya nyinyi na sisi (see highlight in red), na umefanya hivyo kwenye mabandiko mengine mengi tu. All that said and done, usisi na unyinyi katika mjadala huu hauna uzito tena kuliko hoja iliyopo mbele yetu. Hoja nyingi za msingi bado hamjaleta majibu humu.
 
Unajitahidi kufanya kazi uliyotumwa kwa speed ya Super Sonic

Join Date : 21st March 2014
Posts : 962
Rep Power : 526
Likes Received356
Likes Given272​

Teh teh teh baki na hayohayo, SISI tunachotaka ni pesa zetu zirudi, hayo yenu matatizo ya kugombania madaraka ndani ya chama hayatuhusu
 
Yote ni katika mikakati yako ya kupindisha hoja. Nadhani umesha sahau kwamba wewe ni mmoja wa wachangiaji ambao mmekuwa mkiweka makundi ya nyinyi na sisi (see highlight in red), na umefanya hivyo kwenye mabandiko mengine mengi tu. All that said and done, usisi na unyinyi katika mjadala huu hauna uzito tena kuliko hoja iliyopo mbele yetu. Hoja nyingi za msingi bado hamjaleta majibu humu.

Mkuu, umesahau kuwa SISI tunachotaka ni pesa yetu irudi
 
Mkuu, umesahau kuwa SISI tunachotaka ni pesa yetu irudi

kwa kuazima neno lako la sisi, hata "sisi" tunataka pesa yetu irudi. Lakini je:

1. Za uswisi zimerudi? majibu ya kuridhisha hakuna.
2. Je kwanini tumuamini zitto kwamba anachopigania ni maslahi ya taifa na sio maslahi yake binafsi? mmedhihirisha kwamba anachotafuta zitto ni credit.
3. Je, kiongozi anayepigania pesa yetu irudi (KWA NIABA YETU SISI), je ana integrity? Majibu ya kuridhisha hakuna.
4. Je, nini majibu/ufafanuzi kwa maswali yetu mengi tu juu ya hoja za zitto kwenye bandiko lake namba moja? majibu ya kurudhisha hakuna.

Hapo ndio usisi na unyinyi unapokolea, lakini kwa lugha sahihi zaidi, upande wetu wa hoja na upande wenu wa hoja. Ni upande wenu wa hoja ndio upo nyuma kihoja. Tunaendelea kusubiri, na pengine hata mleta mada (zitto) atakuja kutoa ufafanuzi ili tuliweke hili sawa kwani ni dhahiri sasa kwamba mmeshindwa kumsaidia katika hili.
 
Ujanja mnaotumia hapa ni kwamba, kila tukileta hoja ambazo mnajua ni dhahiri hamna majibu, mnakimbia kwa muda ili vumbi litulie, kisha mnarudi na hoja zile zile baada ya kuhakikisha kwamba wafuatiliaji wa mjadala huu wamesha sahau hoja zetu za awali ambazo mmekimbia kuzifanyia ufafanuzi. Pengine ni vyema tukaanza kurudia yale yale tuliyojadili, mengine yakiwa addressed moja kwa moja kwako, Waberoya na wengine.

Nianze na hili (cc Ritz):

katika bandiko namba 630, tarehe 11/November, majira ya saa tisa na nusu za mchana Afrika mashariki, nilijadili hivi:

["Sisi hatumshindanishi zitto na mtu Bali tunamshindisha na Dhana ya integrity kwani tunaamini Kwamba hii ni Sifa ya msingi anayotakiwa kuwa nayo kiongozi yoyote anayeingia vitani kupambana na ufisadi.

Hatupo Hapa kujadili mbadala wa zitto, tupo Hapa kuchambua viongozi wote ambao wanajitokeza kutetea maslahi yetu wananchi ili tusije kuachwa solemba kama suala la fedha za uswisi n.k. Kwahiyo basi, kila kiongozi atakayejitokeza Katika hili, tutamchambua kwa hoja kwa nia ya kubaini iwapo anatufaa au hatufai kutetea maslahi yetu. Na nadhani mnatambua Kwamba tuna Haki ya kufanya hivyo."]

Nitajitahidi kurudia hoja zetu zote ambazo mmekuja na mkakati wa kuzikimbia and then when the dust settles, mnarudi and take advantage ya wachangiaji wageni humu kutafuta sympathy and support, wachangiaji ambao bado hawajapata nafasi ya kupitia hoja zetu za awali na kuzipambanisha na hoja zenu kwa nia ya kuchambua pumba na mchele katika upande wetu wa hoja, na pia pumba na mchele katika upande wenu wa hoja.
Mkuu Mchambuzi.

Nimekusoma kiduchu naona kama kuna mpambano hapa kati ya wanaomkubali Zitto kwenye ili suala na wale wanaompiga Zitto kutokana na sababu zao.

Umetumia maneno "Sisi hatumshindanishi" "Hatupo hapa kujadili mbadala wa Zitto" huo ni upande wenu.

Unatumia neno "Integrity" hii ni sifa ya msingi anayotakiwa kuwa nayo kiongozi, kwa faida ya JF unaweza kututajia walao kiongozi mmoja wa upinzani au CCM mwenye "Integrity" hatushindanishi mtu hapa tunaitaji kiongozi mwenye sifa tuwe nyuma yake.

Mkuu wangu ili la wananchi kuachwa solembe na wanasiasa wala siyo geni karibia wanasiasa wote wameishatuacha solemba.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom