Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Mi nilidhani kama KANU waliondoka kwa Harbinder , wazlendo wangeshangilia kama CCM itaodnoka kwa njia hiyo. Hapa nina maana Zitto hapambani na wafanyakazi fulani, anapambana na mfumo. Sasa kama mfumo huo una mteremko wa kuondoka kwanini awe na hofu?

Halafu kuna hoja alizotoa
1. Je, Ongangi alishiriki kuanzisha Gombe? Achilia mambo mengine ya familia, kasoma wapi ana wajukuu wangapi, gesi na mafuta n.k. Kinachotakiwa kujulikana ni kama ni mshiriki wa Gombe, baasi mjadala unaishi hapo

2. Je, kile kimemo ambacho sina uhakika nacho, ni kweli ZZK alichukua mshiko au ni uzushi tu?

3. Je, ZZK anaweza kuthibitisha kuwa wakili amekana mhuri huo.

Mbona mambo rahisi mnayarefu bila sababu?

Kauli ya Zitto ni hii hapa chini:
"Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia. Watanzania sio mabwege!"
Hiyo notion ya kuwa ana Hofu umeipata wapi?, kwa nini unamzushia tuhuma halafu unamjibia?
Mimi nilichokiona katika bandiko hilo la Zitto ni fact, na fact yenyewe ni kuwa Ufisadi huangushaga tawala, mfano mzuri ni serikali ya KANU ilivyoangushwa, sasa wewe utasemaje ana hofu kwa serikali ya CCM kuangushwa?. UNASPIN KAULI YA MTU WEWE KWA MAKUSUDI.
Zitto alishataka kuiangusha serikali ya Pinda, rekodi yake ya kutaka kuiangusha serikali ya CCM iko wazi na well documented, kuanzia bunge la Samweli Sitta, Kuzunguuka nchi nzima huku akimnadi dokta Slaa na Operation kibao za Chadema, sasa unawezaje kusema kuwa ana hofu ya CCM kuondolewa madarakani?

Nyinyi badala ya kuwaunga mkono Wananchi, na angalau kuwatia moyo waliojiweka on the line of fire kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi, nyinyi mnaleta siasa za chuki, vinyongo na visasi, huku mkijaribu kuua mshikamano wa umma kwa kijana aliyejiitolea kuongoza mapambano haya. WEWE BADALA YA KUMLAUMU ZITTO NA KUHOJI MOTIVES ZAKE, WEWE UMEKWISHA FANYA NINI KATIKA ISHU HII YA IPTL?- AU UMELIPWA KUSPIN PUBLIC OPINION KATIKA MTANDAO?. SHAME ON YOU!!!!
 
Tena basi watu tunahoji kwa kutumia maneno ya Zitto, hakuna neno la pembeni.
Sasa tunaambiwa tuna chuki, yaani ili mtu awe safi lazima amsifie zitto.

Hapana, lazima tuwe na fikra, tukiridhishwa na majibu hatuna tatizo na tutamuunga mkono.
Hii habari tumnaambiwa Gombe imeanzishwa na si ya biashara, wakati huo huo akikataa kusema kama Ongangi ni mshiriki inafikirisha.

Halafu, wanasema mtu anajitoa kupambana na ufisadi wa CCM, hilo tunasema ni jema.
Lakini anayepewa sifa hizo anatahadhirisha CCM kuwa Harbinder Singh ataungusha serikali yao.
Hizi conflicting information ndizo tunahoji.

Sidhani kama Zitto anapambana na watu, nadhani anapambana na mfumo, sasa kwanini aone huruma mfumo huo ukielekea kule walikopunzika KANU?

Huu utata hautakiwi kuhojiwa, tunatakiwa tubebe manyanga, na matawi ya majani tushangilie!

Hell ! no! lazima tutumie akili kabla ya kufikia conclusion na kabla hatujahimiza wake na ma girl friend wetu waanze kupiga vigelegele, nderemo na vifijo kwa Zitto. Kesho ikijulikana vinginevyo na tunavyokungumizwa kuamini tutarudi vipi kwa akina mama kuwaomba radhi

Mkuu, kuna kipindi hata mimi nilikiwa na kifua kama chako ilikuwa nikipishana/kukosana/kufarakana na mtu basi haiwezekani tukaelewana na huyo mtu kwenye hiyo mission, HASA ilikuwa kwa wale waliokuwa wamenizidi UKWASI au umaarufu au ujuzi.

Lakini muda wote huo niliendelea kujikuta badala ya kuitekeleza mission nikawa najihami kila wakati na huyu nimdhaniae adui yangu, bahati mbaya kila mwisho wa project nilikuwa najikuta nikifanikiwa chini ya malengo na nikikaa kufikiria nikagundua kabisa kiasi nilichofail ni kile ambacho kimetokana na uhasama wetu...!

Mkuu nimesoma maelezo yako na niseme tu umekuwa msaada wangu kwa muda sasa hapa JF lakini katika hili nimetofautiana na wewe pakubwa sana...

Kuna watu wanaisema conclusion ya Zitto kama mtu anayetoa tahadhari kwa maCCM, NAAM ni kweli ameitoa hiyo tahadhari, tahadhari yenyewe inatokana na kama serikali itashindwa/italipuuzilia sekeseke hili la escrow basi itaanguka...!

Mi naamini pamoja na kuwa tunataka kuuondoa mfumo wote wa serikali na kuuweka mwingine lakini bado wajibu wetu kwa serikali katika kuikumbusha kushughulikia mambo ya kifisadi unabakia palepale hata ikiwa ufisadi huo ukiachwa utaiangusha serikali...!

Maelezo ya wengi wanataka Zitto asiiamshe serikali ili ianguke kwa kuacha kuiasa dhidi ya escrow, lakini ktk uhalisia kila mmoja wetu anapiga vita ufisadi, sasa jiulize kwann tusiuache ufisadi uendelee ili serikali ianguke, why tunapiga makelele na tusiiache serikali iwe kiziwi ili ianguke vizuri...

Jamani tupunguze chuki tupate kuona sawia
 
Siyo Mbowe, Dr.Slaa, John Mnyika, Lema, Sugu, Mdee, Wenje, hakuna hata mmoja ambaye kaishaongelea huu ufisadi anaosema Zitto, najiuliza sana sipati majibu.

1) Escrow

2) IPTL

3) PAP
 
Siyo Mbowe, Dr.Slaa, John Mnyika, Lema, Sugu, Mdee, Wenje, hakuna hata mmoja ambaye kaishaongelea huu ufisadi anaosema Zitto, najiuliza sana sipati majibu.
Nasikia kwenye Sakata la Escrow, wapo pia viongozi kadhaa wa vyama vya Upinzani!!
Hofu yangu ni huu mtandao mpana wa hawa Mafisadi kula njama za kumdhuru Prezidaa ili asideal nao, maana Prezidaa huwa anafanya ishu zake polepole lakini kwa mahesabu ya hali ya juu!
 
Tatiza ninaloliona ni hoja kuachwa na kugeuka pigio la deki kwa watu! Jambo hili zito sasa limegeuka fursa ya kusafishana kisiasa! Jadilini hoja na si kusifiana binafsi na kwa malengo ya umimi! Hivi mwenye hoja ni nani hasa kati ya kafulila na zitto? Mbona sifa zote zinamuruka kafulila? Kuna nini hapo zaidi ya kusaka tu umaarufu binafsi? Jamani naombeni kamati ya PAC isitumike kutafuta na kutafutiana umaarufu!
 
Kinacho nishangaza kwenye hii issue watu wamejitoa ufahamu kabisa hakuna cha UKAWA wala Chadema.

kuna uzi upo humu umeandikwa Mkuu wa Wilaya Bagamoyo kaiba mifuko ya saruji, huku siyo mchezo pro-Chadema wamejaa eti wanapambana na ufisadi.

Lakini kwenye huu uzi wote wanaokuja wanakuwa wa mafisadi kisa hoja imeletwa na Zitto.
 
Tatizo nilionalo ni hoja hii kutumiwa na watu wenye akili ndogo kumsafisha mtu aliyepoteza uaminifu katika jamii! Watu kama hawa huweza kuharibu mada kwani badala ya kujikita kupigania maslahi ya umma wao huyatumia matatizo kisiasa hasa kujisafisha.hivi kwa nini asifiwe na kupambwa zitto kana kwamba ilikuwa hoja yake na wakati kaidandia juu kwa juu ikiwa imeibuliwa na kafulila? Leo anasifiwa mtu asiye na rekodi ya uaminifu badala ya kafulila? Zile tuhuma na kashifa zote zilizoingiliwa na huyu jamaa ziliisha katika mazingira yepi? Kuna hata moja iliyoleta tija kwa huu umma wa watz? Nadhani jibu mnalo!

Mkuu, lini kafulila kawa muaminifu...? Aliitwa sisimizi huyu
 
Waberoya na Wafuasi wa Zitto:

Mnajitahidi sana kufunika kombe mwanaharamu apite lakini Nirudie Tena, Kama nyinyi "hamtetereki", sisi "hatudanganyiki".
Adharusi, Hoja yangu ya msingi, na pengine wengi naowasoma humu doesn't question "upambanaji" dhidi ya mdudu ufisadi, Bali hoja ya msingi questions "mpambanaji" dhidi ya ufisadi (zitto).

Kiongozi anayepambana na ufisadi kwa Dhati huwa na integrity, na huwa transparent & responsible. Zitto wa baada ya "buzwagi" Hana Sifa hizi, he lacks integrity, he is hardly transparent, and he hardly assumes responsibility to see things through (eg Sakata la uswisi).

Tujikite zaidi Katika suala la integrity.
One of the qualities of good leadership Katika mazingira yetu ni integrity, huku lingine likiwa ni suala la political maturity, haya mawili ni unquestionable in a good leader, lakini kwa zitto, these two have become very questionable. Zitto ameonyesha political immaturity ya Hali ya juu sana Katika Sakata Zima la usaliti chadema.

Tukianza na political immaturity, maana yake Rahisi ni Hali ya kipngozi kuwa - self serving, vindicative and manipulative. Huyo Ndio zitto wa baada ya buzwagi. Badala ya kupambana na ufisadi kwa Dhati, anafanya hivyo kwa nia ya kujitafutia umaarufu, Wengine wanasema kujitafutia "vijisenti" (hajapinga Hili kwa hoja Zenye mashiko), lakini muhimu lingine ni kwa nia ya kujisafisha au kuwasahaulisha wananchi juu ya Madudu yake ya usaliti kwa mabadiliko.

Tukija kwenye suala pili yani - integrity, maana yake ni Kuwa kiongozi wa maamuzi magumu, lakini hasa kuwa na uwezo wa kufanya 'the right thing' Wakati wote, Katika mazingira yote, bila ya kuyumbishwa Wala kutetereka. Kiongozi mwenye integrity usually walks the talk, he/she's consistent, honest and hence trustworthy. Zitto Hana Sifa hizi.

Kwa miaka mingi sana, wananchi walikuwa wanatafuta mabadiliko nje ya CCM, na chadema ikageuka kuwa kimbilio la wengi sana, hasa vijana. Wananchi watafuta mabadiliko walimwamini zitto na Taratibu Kuanza kupata matumaini Kwamba kwa Mara nyingine Tena taifa linazaa Viongozi Wenye integrity na wanaoelekea towards political maturity, zitto akiwa ni mmoja wa viongozi hao. Lakini kulichofuata ni usaliti wa zitto kwa wananchi kwani his dishonest, lack of transparency and political immaturity became exposed.

Leaders lacking integrity can't be trusted with their followers or the public, na kitendo chenu akina waberoya et al kulazimishia umma kuendelea kuwekeza trust and hopes kwa failed leaders wa aina ya zitto ni kujishushia heshima kwa jamii, hasa vijana. Lazimisha lazimisha yenu ni kujenga migogoro na matatizo kwani kwa watafuta mabadiliko, na kwa vijana walio wengi, zitto is more of a liability than an asset.
Waberoya et al, Watanzania hawahitaji viongozi wa kufanikisha matukio tu, Bali viongozi wanaofanya hivyo with integrity and political maturity. Success (Kwa mfano suala la buzwagi, escrow), they come and go, lakini "integrity", this is a quality that lives forever.

Kujenga reputation of integrity takes many years, but it takes only a second to lose it all, and that's what happened to zitto. He has shown great political immaturity - he has become a self serving leader, He's vindicative, dishonest, lacks transparent, inconsistent, untrustworthy, irresponsible (mfano Sakata la uswisi) and he's very manipulative for personal gain.

Endeleeni kutotetereka, sisi hatudanganyiki.
 
Last edited by a moderator:
Tatiza ninaloliona ni hoja kuachwa na kugeuka pigio la deki kwa watu! Jambo hili zito sasa limegeuka fursa ya kusafishana kisiasa! Jadilini hoja na si kusifiana binafsi na kwa malengo ya umimi! Hivi mwenye hoja ni nani hasa kati ya kafulila na zitto? Mbona sifa zote zinamuruka kafulila? Kuna nini hapo zaidi ya kusaka tu umaarufu binafsi? Jamani naombeni kamati ya PAC isitumike kutafuta na kutafutiana umaarufu!

Nadhani Kafulila ana kesi mahakamani juu ya hili na hawezi kulizungumzia kwa sasa.

Sasa je tuachane na hili kwa sababu Kafulila ana kesi?naamini Kafulila na Zitto wanashirikiana kwenye hili.

LAKINI ata kama kamati ya Zitto imelishikiria hili haizuii Chadema pia kulishikia bango, hofu ya nin?sio kila wakati ni wa kucheza siasa wakati maslahi ya nchi yapo hatarini.

Tumeambiwa hapo, kuna viongozi wawili wa upinzani nao walipewa gawio la hiyo pesa, sasa huu sio wakati wa sie kushindana kwa ajili ya wanasiasa, bali sote kuungana kupambana na wizi huu kwani sote tunaumia na hii ni nchi yetu sote.
 
Waberoya na Wafuasi wa Zitto:

Mnajitahidi sana kufunika kombe mwanaharamu apite lakini Nirudie Tena, Kama nyinyi "hamtetereki", sisi "hatudanganyiki".
Adharusi, Hoja yangu ya msingi, na pengine wengi naowasoma humu doesn't question "upambanaji" dhidi ya mdudu ufisadi, Bali hoja ya msingi questions "mpambanaji" dhidi ya ufisadi (zitto).

Kiongozi anayepambana na ufisadi kwa Dhati huwa na integrity, na huwa transparent & responsible. Zitto wa baada ya "buzwagi" Hana Sifa hizi, he lacks integrity, he is hardly transparent, and he hardly assumes responsibility to see things through (eg Sakata la uswisi).

Tujikite zaidi Katika suala la integrity.
One of the qualities of good leadership Katika mazingira yetu ni integrity, huku lingine likiwa ni suala la political maturity, haya mawili ni unquestionable in a good leader, lakini kwa zitto, these two have become very questionable. Zitto ameonyesha political immaturity ya Hali ya juu sana Katika Sakata Zima la usaliti chadema.

Tukianza na political immaturity, maana yake Rahisi ni Hali ya kipngozi kuwa - self serving, vindicative and manipulative. Huyo Ndio zitto wa baada ya buzwagi. Badala ya kupambana na ufisadi kwa Dhati, anafanya hivyo kwa nia ya kujitafutia umaarufu, Wengine wanasema kujitafutia "vijisenti" (hajapinga Hili kwa hoja Zenye mashiko), lakini muhimu lingine ni kwa nia ya kujisafisha au kuwasahaulisha wananchi juu ya Madudu yake ya usaliti kwa mabadiliko.

Tukija kwenye suala pili yani - integrity, maana yake ni Kuwa kiongozi wa maamuzi magumu, lakini hasa kuwa na uwezo wa kufanya 'the right thing' Wakati wote, Katika mazingira yote, bila ya kuyumbishwa Wala kutetereka. Kiongozi mwenye integrity usually walks the talk, he/she's consistent, honest and hence trustworthy. Zitto Hana Sifa hizi.

Kwa miaka mingi sana, wananchi walikuwa wanatafuta mabadiliko nje ya CCM, na chadema ikageuka kuwa kimbilio la wengi sana, hasa vijana. Wananchi watafuta mabadiliko walimwamini zitto na Taratibu Kuanza kupata matumaini Kwamba kwa Mara nyingine Tena taifa linazaa Viongozi Wenye integrity na wanaoelekea towards political maturity, zitto akiwa ni mmoja wa viongozi hao. Lakini kulichofuata ni usaliti wa zitto kwa wananchi kwani his dishonest, lack of transparency and political immaturity became exposed.

Leaders lacking integrity can't be trusted with their followers or the public, na kitendo chenu akina waberoya et al kulazimishia umma kuendelea kuwekeza trust and hopes kwa failed leaders wa aina ya zitto ni kujishushia heshima kwa jamii, hasa vijana. Lazimisha lazimisha yenu ni kujenga migogoro na matatizo kwani kwa watafuta mabadiliko, na kwa vijana walio wengi, zitto is more of a liability than an asset.
Waberoya et al, Watanzania hawahitaji viongozi wa kufanikisha matukio tu, Bali viongozi wanaofanya hivyo with integrity and political maturity. Success (Kwa mfano suala la buzwagi, escrow), they come and go, lakini "integrity", this is a quality that lives forever.

Kujenga reputation of integrity takes many years, but it takes only a second to lose it all, and that's what happened to zitto. He has shown great political immaturity - he has become a self serving leader, He's vindicative, dishonest, lacks transparent, inconsistent, untrustworthy, irresponsible (mfano Sakata la uswisi) and he's very manipulative for personal gain.

Endeleeni kutotetereka, sisi hatudanganyiki.

Mkuu nikushtue tu, umeacha kupambana na ufisadi badala yake unapambana na Zitto- acha kuchepuka mkuu...

Hapa hatujadili matatizo ya Zitto na chama chake, bali tuhuma zinazozushwa wakati huu ambapo PAC inalishughulikia suala la IPTL kwa ukaribu kabisa...

Mkuu labda nikukumbushe tu, pamoja na mengine yote wananchi wanajua sababu kuu na ya Msingi ya Zitto kuchukiwa na ndani ya CDM ni kuutaka uenyekiti 2009 hayo mengine yazungumze tu kama kukuza mjadala...

Mkuu, nikukumbushe tena hata kama Zitto analifanya hili kwa ajili ya kujisafisha sisi hatujali, all we care about ni IPTL BRING BACK OUR MONEY...

Mkuu, hakuna asiyetambua siasa za Kiafrika kuwa tatizo kuu limekuwa NJAA YA MADARAKA, hata Mbowe analijua hili na ndio hata sababu kuu ya kubadilisha katiba kwa ajili ya kujiongezea muda wa kuongoza(japo itasemwa ilibadilishwa wa njia za kidemokrasia) ila ukweli kilichofanyika ni kama cha Blaise Compaore...

Kwahiyo unapozungumza kuhusu Zitto kujisafisha you have to bare in mind kisa na sababu za kuchafuka(by the way hajachafuka kama unavyotaka tuamini)

Kwa hiyo bwana mkubwa usiturudishe kwenye mambo hayo ya kichadema bali tusonge mbele tuilazimishe serikali itende vile wananchi tunataka na Mungu akijaalia maCCM yaondoke madarakani hapo 2015
 
Last edited by a moderator:
Kuna kitu kinachanganya watu. Ukisoma bandiko la Zitto hakika ni zuri kweli kweli.
Ukisoma na fikra, unatapa maswali mengi ynayohusu moral authority and motive behind.

Escrow ni tatizo kubwa sana la ufisadi na lazima lifanyiwe kazi.
Shida ni kuwa tatizo hilo limeambata na makando kando ambayo watuhawataki yasemwe.
Ndio chanzo cha Waberoya kuporomosha mitusi badala ya kusimamia hoja.

Bandikko lake hakujibu kama inavyopaswa kwa watu wenye weledi kuelewa. Amelijibu akijua wengi wanameza na wengine ni washabiki tu. Ukimuuliza hana jaibu. Nitaweka kipande hapa kuonyesha mapungufu.
Tuhuma #1 :

Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.

Majibu:

Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee'. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala
Jibu la kwanza la zitto lilitakiwa liwe kwa hoja ya kwanza inayohusu kuanzisha kampuni pamoja. Kuanzisha kampuni pamoja si tatizo, kinachotakiwa ni kuweka wazi. ZZK alitakiwa aseme hivi.
1. Ni kweli ameungana na Ongangi kuanzisha kapuni ambayo haishiriki katika masuala ya gesi bla bla bla n.k.
2. Si kweli kuwa wameanzisha kampuni na Ongangi, halafu bla bla bla n.k.

Ukomsoma, amekimbilia gesi na mafuta na kuacha jambo muhimu sana kiuchunguzi. Je uhusiano wao ni nje ya kampuni inayotuhumiwa au wanashiriki. Na kama ni washirika ni kwa kiasi gani kampuni hiyo ipo tofauti na tuhuma zinazowahusisha.

ZZK kakwepa kabisa hilo kakimbilia kutuambia Ongangi ana watoto, amesoma ana mke n.k.
Kama ameweza kusema hayo, nmini kinamshinda kusema kuwa Ongangi ni mshirika au la!
Hapa watu hawaoni logic wanashangilia tu, na sisi wengine tunahoji ili tuendelee kuupata ukweli wa Zitto na kumuunga mkono. kinyume chake tutahoji 'integrity yake'' hasa tukijua historia yake iliyohariobika siku za karibuni.

Huu ni mfano, tutaendelee kuwaonyesha wapi mnadanganyika.
Yes kuna Escow lakini hilo lazima tuliangalie sote kama tatizo, na wala lisitumike kisiasa.
 
Kuna kitu kinachanganya watu. Ukisoma bandiko la Zitto hakika ni zuri kweli kweli.
Ukisoma na fikra, unatapa maswali mengi ynayohusu moral authority and motive behind.

Escrow ni tatizo kubwa sana la ufisadi na lazima lifanyiwe kazi.
Shida ni kuwa tatizo hilo limeambata na makando kando ambayo watuhawataki yasemwe.
Ndio chanzo cha Waberoya kuporomosha mitusi badala ya kusimamia hoja.

Bandikko lake hakujibu kama inavyopaswa kwa watu wenye weledi kuelewa. Amelijibu akijua wengi wanameza na wengine ni washabiki tu. Ukimuuliza hana jaibu. Nitaweka kipande hapa kuonyesha mapungufu.
Jibu la kwanza la zitto lilitakiwa liwe kwa hoja ya kwanza inayohusu kuanzisha kampuni pamoja. Kuanzisha kampuni pamoja si tatizo, kinachotakiwa ni kuweka wazi. ZZK alitakiwa aseme hivi.
1. Ni kweli ameungana na Ongangi kuanzisha kapuni ambayo haishiriki katika masuala ya gesi bla bla bla n.k.
2. Si kweli kuwa wameanzisha kampuni na Ongangi, halafu bla bla bla n.k.

Ukomsoma, amekimbilia gesi na mafuta na kuacha jambo muhimu sana kiuchunguzi. Je uhusiano wao ni nje ya kampuni inayotuhumiwa au wanashiriki. Na kama ni washirika ni kwa kiasi gani kampuni hiyo ipo tofauti na tuhuma zinazowahusisha.

ZZK kakwepa kabisa hilo kakimbilia kutuambia Ongangi ana watoto, amesoma ana mke n.k.
Kama ameweza kusema hayo, nmini kinamshinda kusema kuwa Ongangi ni mshirika au la!
Hapa watu hawaoni logic wanashangilia tu, na sisi wengine tunahoji ili tuendelee kuupata ukweli wa Zitto na kumuunga mkono. kinyume chake tutahoji 'integrity yake'' hasa tukijua historia yake iliyohariobika siku za karibuni.

Huu ni mfano, tutaendelee kuwaonyesha wapi mnadanganyika.
Yes kuna Escow lakini hilo lazima tuliangalie sote kama tatizo, na wala lisitumike kisiasa.

Kwa maelezo yako hayo tunapataje PESA iliyoibiwa na IPTL

kama maelezo yako hayaleti pesa automatic unapambana na Zitto badala ya kupambana kupata pesa yetu

IPTL BRING BACK OUR MONEY
 
Nimejitahidi kusoma sana comments za watu hapa ili nizidi kupata darasa la kutosha. Kuna kitu nimekigundua hapa tuna wapinzani tu wala hatuna wanamageuzi. Mpinzani kazi yake ni moja tu kupinga kila hoja itokayo kwa adui yake. Inawezekana hapa kuna makundi mawili.

La kwanza ni lile lililoamua kuukumbatia mfumo wa utawala uliopo hata kama utaamua kuifilisi nchi. Wao wamejitolea kuupigania mfumo hata kama sio wanufaika wa moja kwa moja.

Kundi la pili ni la wapinzani walioamua kuchagua na kushabikia baadhi ya wanasiasa wao wanaowapenda. Hili kundi la pili laweza kuwa baya kuliko hata la kwanza kwani matumaini ya watanzania walio wengi walikua nyuma yao.

Haiwezekani leo hii uwe busy na Katiba kwa hoja za Idadi ya serikali 3 katikati ya lindi la ufisadi mkubwa kama huu wa 200bln alafu wategemewa wakabaki kimya kisa hoja imeibuliwa na watu wasiowapenda.

Leo ndo nimeziona rangi halisi za wapinzani wa Tanzania. Kusema kweli bado tuna safari ndefu sana kuyapata mageuzi ya kweli.

Zitto na Kafulila pambaneni watanzania tunaojitambua tuko pamoja nanyi kwani huu mtandao wa wezi wa raslimali za taifa ni mpana mno na yawezekana hata wale wa upande wa pili wanapiga kimya kimya ila hatujui. Lejea maneno ya Mwenyekiti KUCHUKUA FEDHA ZA FISADI SIO TATIZO BALI ISSUE NI UNAENDA KUZIFANYIA NINI.

Sijawahi kuwasikia hawa wachumia tumbo akina Mchambuzi na NguruV3 wakihoji kauli kama hizi wakati mtuhumiwa keshakiri kuchukua fedha lakini wao wameamua kuishi upande mmoja wa shilingi tena hata pasipo na ushahidi. Wametanguliza hisia balada ya facts... safari bado ndefu.
 
Ingawa hawajatajwa majina na ni fununu tu kuwa baadhi ya viongozi wa upinzani wamekatiwa bulungutu la escrow

Kwa nini viongozi wa ukawa hawajitokezi na kukanusha tuhuma hizo.....maana isije ripoti ikasema hamna ufisadi watu wakaamini kombe limefunikwa kuwanusuru mafisadi wakiwemo wapinzani
 
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.

Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege). Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.

Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.

Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari "Zitto na Filikunjombe wanatumiwa na Kenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu" zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.

Tuhuma #1 :

Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.

Majibu:

Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee’. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.

Tuhuma #2 :

Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia wa pasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel Knospe nyumba na gari ya kukodi.

Majibu:

Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya Bwana Ongangi kuthibitisha madai yao.

Tuhuma #3 :

Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwa kwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.

Majibu:

Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa Norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.

Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola za Marekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa. Uamuzi wa Kamati ya PAC kutaka mikataba yote ya Gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na wanataka umma wa watanzania usijue!

Tuhuma #4 :

Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafuta gesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji mkubwa Tanzania Bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.

Majibu:

Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari ina makubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya Petrobras ya Brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.

Tuhuma 5:

Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.

Majibu:

Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.

Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):

Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasa kwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.

Majibu:

Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa na Taifa lolote lile. Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo. Kwangu itikadi yangu ni ‘Uzalendo kwa nchi yangu’, ni jambo ambalo halina mbadala wake. Siku zote nasema “Right or wrong, my country first". Kurudia kurusha tuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.

Aidha, wanatuhumu kuwa “Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150 million kama deni likilipwa”

Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.

Tuhuma #7 :

Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale TANESCO. Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.

Majibu:

Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.

Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa “Naomba tuwe macho na Wabunge wetu achananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na Kampuni ya SHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza. Serikali ya Kenya na tapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na Kafulila”.

Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwa kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.

Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:

Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa TPDC kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya Gesi na Mafuta.

Pili, ni uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa kuanzishwa na kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200 ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12 zinalipwa na TANESCO kila mwezi kwenda kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth (50%) na watu wasiojulikana kupitia kampuni ya Simba Trust iliyosajiliwa na kufichwa nchini Australia (50%).

Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka TANESCO izalishe au isizalishe Umeme! Watanzania, PAP itaendelea kulipwa namna hiyo kwa miaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo Seth analindwa na baadhi ya watendaji Serikalini na hasa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya PAP. Seth pia anamiliki kitalu cha gesi Mnazi bay Kaskazini kupitia kampuni ya HydroTanz.

Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na Kamati yangu zimewapelekea kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili kutuogopesha na kutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala la uporaji wa fedha kutoka Benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye mstari. Mimi na wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na wabunge wenzetu kuhakikisha ukweli unajulikana na wezi kuchukuliwa hatua kali.

Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia. Watanzania sio mabwege!

Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC

Dodoma, 9 Novemba 2014
]

DUUH, nimejaribu kusoma na kurudia mara 3, kuna majibu mengne siyaoni kabisa.

MFANO: Mkopo kupitia Vivian/Smg za kuomba pesa ili jambo lipootwe kwenye kamati -/Kusaidia CEo kupata nyumba/
 
Waberoya na Wafuasi wa Zitto:

Mnajitahidi sana kufunika kombe mwanaharamu apite lakini Nirudie Tena, Kama nyinyi "hamtetereki", sisi "hatudanganyiki".
Adharusi, Hoja yangu ya msingi, na pengine wengi naowasoma humu doesn't question "upambanaji" dhidi ya mdudu ufisadi, Bali hoja ya msingi questions "mpambanaji" dhidi ya ufisadi (zitto).

Kiongozi anayepambana na ufisadi kwa Dhati huwa na integrity, na huwa transparent & responsible. Zitto wa baada ya "buzwagi" Hana Sifa hizi, he lacks integrity, he is hardly transparent, and he hardly assumes responsibility to see things through (eg Sakata la uswisi).

Tujikite zaidi Katika suala la integrity.
One of the qualities of good leadership Katika mazingira yetu ni integrity, huku lingine likiwa ni suala la political maturity, haya mawili ni unquestionable in a good leader, lakini kwa zitto, these two have become very questionable. Zitto ameonyesha political immaturity ya Hali ya juu sana Katika Sakata Zima la usaliti chadema.

Tukianza na political immaturity, maana yake Rahisi ni Hali ya kipngozi kuwa - self serving, vindicative and manipulative. Huyo Ndio zitto wa baada ya buzwagi. Badala ya kupambana na ufisadi kwa Dhati, anafanya hivyo kwa nia ya kujitafutia umaarufu, Wengine wanasema kujitafutia "vijisenti" (hajapinga Hili kwa hoja Zenye mashiko), lakini muhimu lingine ni kwa nia ya kujisafisha au kuwasahaulisha wananchi juu ya Madudu yake ya usaliti kwa mabadiliko.

Tukija kwenye suala pili yani - integrity, maana yake ni Kuwa kiongozi wa maamuzi magumu, lakini hasa kuwa na uwezo wa kufanya 'the right thing' Wakati wote, Katika mazingira yote, bila ya kuyumbishwa Wala kutetereka. Kiongozi mwenye integrity usually walks the talk, he/she's consistent, honest and hence trustworthy. Zitto Hana Sifa hizi.

Kwa miaka mingi sana, wananchi walikuwa wanatafuta mabadiliko nje ya CCM, na chadema ikageuka kuwa kimbilio la wengi sana, hasa vijana. Wananchi watafuta mabadiliko walimwamini zitto na Taratibu Kuanza kupata matumaini Kwamba kwa Mara nyingine Tena taifa linazaa Viongozi Wenye integrity na wanaoelekea towards political maturity, zitto akiwa ni mmoja wa viongozi hao. Lakini kulichofuata ni usaliti wa zitto kwa wananchi kwani his dishonest, lack of transparency and political immaturity became exposed.

Leaders lacking integrity can't be trusted with their followers or the public, na kitendo chenu akina waberoya et al kulazimishia umma kuendelea kuwekeza trust and hopes kwa failed leaders wa aina ya zitto ni kujishushia heshima kwa jamii, hasa vijana. Lazimisha lazimisha yenu ni kujenga migogoro na matatizo kwani kwa watafuta mabadiliko, na kwa vijana walio wengi, zitto is more of a liability than an asset.
Waberoya et al, Watanzania hawahitaji viongozi wa kufanikisha matukio tu, Bali viongozi wanaofanya hivyo with integrity and political maturity. Success (Kwa mfano suala la buzwagi, escrow), they come and go, lakini "integrity", this is a quality that lives forever.

Kujenga reputation of integrity takes many years, but it takes only a second to lose it all, and that's what happened to zitto. He has shown great political immaturity - he has become a self serving leader, He's vindicative, dishonest, lacks transparent, inconsistent, untrustworthy, irresponsible (mfano Sakata la uswisi) and he's very manipulative for personal gain.

Endeleeni kutotetereka, sisi hatudanganyiki.

Duh sijui akili umezipeleka wapi...hivi mtu mzima yeyote aliyefika walau kidato cha nne ata cha shule ya kata akipewa kichwa cha habari cha hii thread hivi kweli atakuja na insha hiyo?

Sikuhizi hauna tofauti na vijana wa waganga njaa wanaolamba matapishi ya mabwana zao, hii nguvu unayoitumia kujipendekeza kwa akina Mbowe ungeitumia kuwa mwanaharakati huru ungefanikiwa sana, lakini kwa hii style yako ya siasa HUTAFANIKIWA KAMWE KWENYE SIASA, UTAISHIA TU KUSUKUMA MAGARI YA VIONGOZI.

Nakumbuka nilikupa kura yangu kura ya maoni, najuta na kwa kweli unamuaibisha Mzee Mwambulukutu na unaaibisha walimu wako..

Hutupeleki watoto shule ili wawe wapambe, tunawapeleka shule ili mje muwe na mawazo yanayojitegemea yanayoweka mbele taifa na sio maslahi ya makundi madogo madogo yasiyo na faida kwa taif.Shame on You.
 
Last edited by a moderator:
Nimejitahidi kusoma sana comments za watu hapa ili nizidi kupata darasa la kutosha. Kuna kitu nimekigundua hapa tuna wapinzani tu wala hatuna wanamageuzi. Mpinzani kazi yake ni moja tu kupinga kila hoja itokayo kwa adui yake. Inawezekana hapa kuna makundi mawili.

La kwanza ni lile lililoamua kuukumbatia mfumo wa utawala uliopo hata kama utaamua kuifilisi nchi. Wao wamejitolea kuupigania mfumo hata kama sio wanufaika wa moja kwa moja.

Kundi la pili ni la wapinzani walioamua kuchagua na kushabikia baadhi ya wanasiasa wao wanaowapenda. Hili kundi la pili laweza kuwa baya kuliko hata la kwanza kwani matumaini ya watanzania walio wengi walikua nyuma yao.

Haiwezekani leo hii uwe busy na Katiba kwa hoja za Idadi ya serikali 3 katikati ya lindi la ufisadi mkubwa kama huu wa 200bln alafu wategemewa wakabaki kimya kisa hoja imeibuliwa na watu wasiowapenda.

Leo ndo nimeziona rangi halisi za wapinzani wa Tanzania. Kusema kweli bado tuna safari ndefu sana kuyapata mageuzi ya kweli.

Zitto na Kafulila pambaneni watanzania tunaojitambua tuko pamoja nanyi kwani huu mtandao wa wezi wa raslimali za taifa ni mpana mno na yawezekana hata wale wa upande wa pili wanapiga kimya kimya ila hatujui. Lejea maneno ya Mwenyekiti KUCHUKUA FEDHA ZA FISADI SIO TATIZO BALI ISSUE NI UNAENDA KUZIFANYIA NINI.

Sijawahi kuwasikia hawa wachumia tumbo akina Mchambuzi na NguruV3 wakihoji kauli kama hizi wakati mtuhumiwa keshakiri kuchukua fedha lakini wao wameamua kuishi upande mmoja wa shilingi tena hata pasipo na ushahidi. Wametanguliza hisia balada ya facts... safari bado ndefu.

Mwenye akili wamekusikia mkuu, maneno mazito sana haya.Ningekuwa kwenye desktop ningekupa like.
 
Waberoya na Wafuasi wa Zitto:

Mnajitahidi sana kufunika kombe mwanaharamu apite lakini Nirudie Tena, Kama nyinyi "hamtetereki", sisi "hatudanganyiki".
Adharusi, Hoja yangu ya msingi, na pengine wengi naowasoma humu doesn't question "upambanaji" dhidi ya mdudu ufisadi, Bali hoja ya msingi questions "mpambanaji" dhidi ya ufisadi (zitto).

Kiongozi anayepambana na ufisadi kwa Dhati huwa na integrity, na huwa transparent & responsible. Zitto wa baada ya "buzwagi" Hana Sifa hizi, he lacks integrity, he is hardly transparent, and he hardly assumes responsibility to see things through (eg Sakata la uswisi).

Tujikite zaidi Katika suala la integrity.
One of the qualities of good leadership Katika mazingira yetu ni integrity, huku lingine likiwa ni suala la political maturity, haya mawili ni unquestionable in a good leader, lakini kwa zitto, these two have become very questionable. Zitto ameonyesha political immaturity ya Hali ya juu sana Katika Sakata Zima la usaliti chadema.

Tukianza na political immaturity, maana yake Rahisi ni Hali ya kipngozi kuwa - self serving, vindicative and manipulative. Huyo Ndio zitto wa baada ya buzwagi. Badala ya kupambana na ufisadi kwa Dhati, anafanya hivyo kwa nia ya kujitafutia umaarufu, Wengine wanasema kujitafutia "vijisenti" (hajapinga Hili kwa hoja Zenye mashiko), lakini muhimu lingine ni kwa nia ya kujisafisha au kuwasahaulisha wananchi juu ya Madudu yake ya usaliti kwa mabadiliko.

Tukija kwenye suala pili yani - integrity, maana yake ni Kuwa kiongozi wa maamuzi magumu, lakini hasa kuwa na uwezo wa kufanya 'the right thing' Wakati wote, Katika mazingira yote, bila ya kuyumbishwa Wala kutetereka. Kiongozi mwenye integrity usually walks the talk, he/she's consistent, honest and hence trustworthy. Zitto Hana Sifa hizi.

Kwa miaka mingi sana, wananchi walikuwa wanatafuta mabadiliko nje ya CCM, na chadema ikageuka kuwa kimbilio la wengi sana, hasa vijana. Wananchi watafuta mabadiliko walimwamini zitto na Taratibu Kuanza kupata matumaini Kwamba kwa Mara nyingine Tena taifa linazaa Viongozi Wenye integrity na wanaoelekea towards political maturity, zitto akiwa ni mmoja wa viongozi hao. Lakini kulichofuata ni usaliti wa zitto kwa wananchi kwani his dishonest, lack of transparency and political immaturity became exposed.

Leaders lacking integrity can't be trusted with their followers or the public, na kitendo chenu akina waberoya et al kulazimishia umma kuendelea kuwekeza trust and hopes kwa failed leaders wa aina ya zitto ni kujishushia heshima kwa jamii, hasa vijana. Lazimisha lazimisha yenu ni kujenga migogoro na matatizo kwani kwa watafuta mabadiliko, na kwa vijana walio wengi, zitto is more of a liability than an asset.
Waberoya et al, Watanzania hawahitaji viongozi wa kufanikisha matukio tu, Bali viongozi wanaofanya hivyo with integrity and political maturity. Success (Kwa mfano suala la buzwagi, escrow), they come and go, lakini "integrity", this is a quality that lives forever.

Kujenga reputation of integrity takes many years, but it takes only a second to lose it all, and that's what happened to zitto. He has shown great political immaturity - he has become a self serving leader, He's vindicative, dishonest, lacks transparent, inconsistent, untrustworthy, irresponsible (mfano Sakata la uswisi) and he's very manipulative for personal gain.

Endeleeni kutotetereka, sisi hatudanganyiki.
......Nafikiri ifike mahali watanzania na vijana wenzangu tujifunze kusamehe na kusema(Let it go)..Jamani dunia unatucheka...Hata kama kuna mahala Mh:Zitto amewakwaza tusamehe twende mbele kwa masilahi mapana ya nchi yetu Tanzania...Hatuwezi kuwaacha hawa mafisadi/wezi wa rasimali zetu watambee na kutembea vifua mbele...Kuna watu humu Jf mungu kawapa(God gifted) upeo wa kipekee sana kujadili na kujenga hoja kwa hamasa,mashiko na weledi wa hali ya juu kwa mfano:MCHAMBUZI na wengine ila leo hii wamweshindwa kabisa kutuunganisha kwa pamoja kwa hoja zao makini dhidi ya wizi huu wa Tegeta Escrow wamebaki kumjadili Mh:zitto tu na kuacha hoja ya msingi, Kila binadamu ana mapungufu na hakuna binadamu aliyekamilika...Yatosha sasa ya Mh:Zitto yamepita tusonge mbele tuna mengi ya msingi sana ya kujadili...tunavyoongea sasa hakuna dawa mahospitalini Msd(Bohari ya dawa) wanaidai serikali zaidi ya billion 90 na wahisani wamegoma kabisa kuchangia budget yetu mpaka uchunguzi wa sakata hili la Tegeta Escrow utakapokamilika...Mwisho kama Taifa tusipojenga utamaduni wa kusameheana na kuamaniana siku zote adui yetu atakuwa anatumia udhaifu huo....Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom