Asalaam wana jukwaa,
Napenda kuwaomba tumuunge mkono ndg Zitto Kabwe aweze kuimiliki hii kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa ni mtu mwenye focus ya kiutu uzima na hana ushabiki wa kivyama, anasimamia maslahi ya nchi na watu wake, na pia ana siasa na kistaarabu.
Walikuwepo akina mzee Cheyo Mrema nk ambao wao waliamua kufanya kazi za ccm na kusahau majukumu yao kama wabunge wa upinzani. matokeo yake wameyaona wao wenyewe na hawakutegemea kama itakuwa hivyo.
Ni suala la muda tu lakini ipo siku ZITO utalitizama kupitia tv.
Zitto ni mpinzani?
Ni ccm team bZitto ni mpinzani?
Haa haaa Zitto ana malengo ya mbali anajua ili aweze kuchukua mikoba ya PAC atahitaji kura za wabunge wa CCM hata wapinzani wakisusa kumpatia kura bado atakuwa mwenyekiti.
hawa sijui wanafikiri kwa kutumia nini? wanamdai maalim saif wakati wabunge wa cuf Zanzibar wako ndani ya bunge, nilitegemea wangegoma kuingia hadi boss wao maalim saif atakapoingia bungeni.
Kama Mh Zitto unamuona anafaa kuwa KUB ungemuunga mkono kwa kuchagua wabunge wa chama chake.
Sheria, kanuni na taratibu bila kusahau utamaduni wa bunge kama ilivyo kwa Waziri mkuu lazima atokane na Chama chenye wabunge wengi. Hali kadharika KUB lazima atokane na Chama chenye wabunge wengi wa upinzani.
Uchaguzi ujao (2020)onyesha mahaba yako kwa Zitto kwa kuchagua wabunge wengi wa chama chake. Kwa bunge hili hawezi kuwa KUB. IMPOSSIBLE!

Dada hamida habari yako!WanaJF,
UKAWA wanazidi kuvuliwa nguo na wasomi na watu wenye akili kutokana na nidhamu yao mbaya walioonyesha Bungeni. Kada mbalimbali kwenye jamii ikiwemo asasi zisizo za kiserikali, wanazuoni, makundi mbalimbali ya wanawake wameendelea kuwaona UKAWA ni watu wa ajabu ambao hawajakomaa kisiasa.
Pia baadhi ya wanasiasa nguli nchini nao wameendelea kuwaponda UKAWA na siasa zao za kishamba za kuzomea na kususia Bunge. Mathalani haya ni machache tu ambayo yamesemwa na ndugu Zitto kuhusu utovu wa nidhamu wa UKAWA ndani ya Bunge:
View attachment 306797
Source: Ukurasa wa FB wa Zitto
WanaJF,

Mrema alikuwa mbunge pekee na kukifuta chama chake na yeye mwenyewe akajifuta.Na Zito ameanza tabia ileile ya Mrema kuunga mkono Serikali.Naona safari ya Zito kujifuta imekoleaZitto ni mpinzani?