Zitto, Kwenye hili tayari umeshinda!

Zitto, Kwenye hili tayari umeshinda!

haya yamesha kwisha Mnyika kesha toa majibu

ngonjera zote za nini ?!
 
Binafsi namukubali zito kama mwanasiasa kijana na machachali,ila nina maswali kadhaa juu ya sakata lake kilichodaiwa taarifa ya siri1. kwa nini kila issu ya zito hujadiliwa kwa misingi ya ukabila kuwa yeye hutengwa ka vile si wa kaskazini? mbona wapo wengi wasio wa kaskazini ndani ya chadema 2.kawa nini ccm kupitia wasira na nchemba walitabiri kifo cha chadema ndani ya miaka miwili? kama hakukuwa na mipango juu ya utabiri huo? kwa nini zito hakushirika kwa ukaribu kwenye m4c?3. kwa nini zito alihusishwa na uasi wa akina mwampamba? 4. hv kuna maslahi gani ndani ya chama katika malumbano haya? 5. hv hata kama zito yuko kwenye mpango mbaya kuingamiza cdm atakubali? naomba wapenzi kwa pamoja tujiulize maswali baadala ya ushabiki wa watu. naomba kama hakuna jambo la hivyo tukae chini na kujadili namna ya kukiimarisha chama.
 
Umeandika utumbo mwenyewe, utasoma mwenyewe ukishirikiana na masalia wenzako plus Lumumba project. Or else ni nani mwenye akili timamu atapoteza muda wake kusoma all this long rubbish?

Misukule ya Mbowe at work!
 
Zitto anavyokuzwa as if kafanya jambo la maana sana katika siasa za nchi hii!

Wako watu wamefanya mambo makubwa sana lakini hawajikuzi namna hii na kutumia migogoro kupata sympathy!

Ni ujinga sana mtu kujikuza bila sababu za msingi, Mbunge kama Lissu ana miaka mitatu bungeni na amefanya mambo makubwa sana lakini sijawahi kumwona akijikweza katika mitandao ya kijamii usiku na mchana kutwa!

Wewe Mchange ulitegemea Zitto asisafishwe kwa rushwa za Tanesco wakati huyohuyo ni mshauri wa Nishati na Madini wa Mkono Advocates & Co. Hata kamsaidia yule mjinga mwenzenu kupata tempo kule.

Mnachokera ni kukuza migogoro mitandaoni, alisafishwa kwa rushwa kwa kuwa na yeye anakula hela ya Tanesco kupitia Mkono!

Kwa akili yako fupi umeshasikia Zitto akizungumza lolote kuhusu gas au nishati popote pale nje au ndani ya Bunge au mtandaoni anakokesha tangu Prof. Muhongo awaumbue yeye na Mkono bungeni!

Akili yako ya kuku haikuoneshi alvyohama hoja na kuamia kwenye pesa uswisi?

Kumlinganisha Mbowe na watu wenye njaa na masikini kama nyie ni upumbavu wa hali ya juu!

rudi kwenye hoja ya ushindi wa zitto mkuu.
hizo hadithi zako nyingine kawapigie WAGAZA
 
Nilikuwa sijasoma jina lamuanzisha hii thread, niliposona na kujuwa kumbe ni yule mwizi wa simu basi nimeishia njiani.
Matola soma bandiko #116 hasa umsome niliye m-quote huyu ndo Zitto nliyekuwa nakwambia ni zaid.
The guy plays well his position as Sydney Bristow ndani ya SD6 & CIA.
 
Last edited by a moderator:
Halafu huu ujinga wa kujifanya nimepokea simu na e mail nyingi ni ujinga mwingine!

Wewe una umashuhuri gani wa kupigiwa simu na mail nyingi?

Ndio maana nawambia hizi tabia za kujikweza na political arrogance mliyofunzwa na huyo Zitto haitawafikisha popote!
 
Last edited by a moderator:
Matola soma bandiko #116 hasa umsome niliye m-quote huyu ndo Zitto nliyekuwa nakwambia ni zaid.
The guy plays well his position as Sydney Bristow ndani ya SD6 & CIA.

Mambo Teacher wangu?!

Muulize Matola ameona na kusikia shughuli tuliyoifanya ndani ya TFF?!
 
Last edited by a moderator:
ni kweli kuwa wewe UMEFUKUZWA CHADEMA? Kama, ni kweli, kwanini ulifukuzwa? nikizingatia ile ripoti ya kwenye mitandao, ilikuwaje wewe ufukuzwe na kisha Zitto asifukuzwe?

endelea kujiuliza mara mbili mbili
 
Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na mtindo wa kurushwa kwa shutuma mbali mbali kutoka kwa viongozi wajuu wa CHADEMA wakitumia majina bandia kumuelekezea ndugu zitto kabwe.

Kwa makusudi kabisa viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti, katibu mkuu na wakurugenzi kadhaa wamekuwa wakirusha kila aina ya shutuma humu mtandaoni lakini kwa hofu kubwa ndio maana wanajificha kwa kutumia akaunti bandia.

Jana na juzi nimepokea sms, emails na simu nyingi sana kuhusu hiki kinachoitwa ripoti ya siri ya SLAA, MBOWE NA WAGAZA WENGINE dhidi ya ZITTO zikisema namie nimetajwa humo kuwa ninashirikiana na Zitto kukihujumu CHADEMA.

Bahati mbaya sana, hakuna ripoti ama shutuma zozote anazopelekewa Zitto kutoka kwa hawa majamaa ambazo hazinitaji, na kwentye hii nayo nimeshuhudia nikitajwa mara nyingi kupokea pesa kutoka kwa Zitto kukihujumu chama.

Bahati mbaya zaidi ni kwamba wafadhili wa mkakati huu ''OPERESHENI ONDOA ZITTO KWENYE HOJA ZENYE MASLAHI YA TAIFA'' wamekosa njia sahihi ya kutumia, wamekuwa wakiwatumia watu wale wale ambao kwa zaidi ya miaka na miaka tumekuwa tukikitetea chama kuwa si cha namna hiyo.

kitendo cha MBOWE na SLAA kuwatumia JOSHUA NASSARY, GODBLESS LEMA, MAMUYA na wengine, kinauthibitishia umma wa watanzania kuwa sio kweli kwamba zitto ni tatizo kwenye CDM, kitendo hiki cha kuwatumia watu wanaolalamikiwa kuwa wanabebana kimisingi ya ASILI ya wanakotokea kinatuthibitishia watanzania kwamba CHADEMA ni chama cha watu wa eneo hilo.

lakini wamefeli zaidi kumtumia LEMA kuwa eti ni KAMANDA mwenye uchungu na CHADEMA kuliko ZITTO, hiki pia ni kielelezo cha upeo mdogo wa kufikiri kwa watu hawa.

ZITTO ni mjenzi wa NYUMBA inayoitwa CHADEMA, Zitto ameshiriki mpaka kuijenga CHADEMA tangu ikiwa nyumba ya nyasi, mpaka ikawa ya udongo, ikaja ikawa ya tofali za kuchoma na sasa CHADEMA ni nyumba ya VIGAE,

LEMA ni mpangaji tu kwenye hii nyumba CHADEMA, hakuna jinsi yoyote mpangaji akawa na uchungu na nyumba kuliko mwenye nyumba, hakuna na haitaka itokee.

LEMA ni mpita njia tu kwenye CHADEMA, Kamwe hawezi kuwa na uhalali wa kumsema na kumtukana mtu aliyekijenga chama kilichomsaidia kumfikisha hapo alipo.

Nani humu jukwaani alikuwa anamfahamu LEMA mwaka 2006, NANI?. nani alikuwa anafahamu lolote kuhusu lema 2007,2008,2009 mpaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu?.

Nani anayemfahamu Lema kipindi hicho kwenye CHADEMA?. LEMA ni TUNDA LA KAZI NZURI YA KISIASA ILIYOFANYWA NA ZITTO KABWE.

Wakati Zitto anahangaika kushirikiana na viongozi wenzake kuijenga CHADEMA, LEMA alikuwa ni KIBARAKA wa MZEE AUGUSTINO MREMA wa TLP.

Wakati Zitto anaibua hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa kama BUZWAGI na nyinginezo, LEMA bado alikuwa hata hajui chaguo lake la kisiasa katika nchi hii, yaani lema hakuwa akijua aende chama gani cha siasa.

Wanaokumbuka na wenye akili timamu watakubaliana nami kuwa ni zitto aliyekwenda Arusha kumnadi mgombea wa TLP wa udiwani wakati wa uchaguzi wa marudio 2008 huku lema akiwa mpiganaji kibaraka wa augustino mrema wa TLP.

wanachadema wanafahamu kuwa wakati tunafanya uchaguzi wa ndani ya chama mwaka 2009 LEMA ndio kwanza alikuwa ana siku 4 za uanachama wake ndani ya CHADEMA.

LEMA anapita tu njia CHADEMA kwa kuwa yeye ni msaka tonge tu kama wasaka tonge wengine, ndio maana alipita NCCR, ILIPOKUFA AKAKIMBIA, AKAPITA TLP ilipokufa akakimbia na sasa yupo CHADEMA nayo ikiyumba sidhani kama hataacha kukimbia. LEMA hana hadhi ya kukubali kutumiwa na kina MBOWE na GENGE lake kumshambulia ZITTO, hana hiyo moral authority. mpangaji hawezi kuwa na uchungu sawa na mwenye nyumba,

Leo CHADEMA ikipasuka, leo CHADEMA ikiyumba, ikitetereka atakayeumia ni ZITTO aliyeijenga na si LEMA aliyeidandia.

Nasisitiza hapa kuwa Hakuna namna yoyote ile inayoweza kumshusha Zitto kwenye heshima yake aliyojijengea kwa kusambaza uwongo wa namna hii, hakuna na hitakaa itokee.

Hakuna namna yoyote ile ya kumshusha zitto kwenye orodha ya wanasiasa bora na makini kwa kuwatumia watu kama kina lema na nassary ambao wakati wanaomba kura waliomba wakisema WATUMWE WAENDE BUNGENI WAKAWE KAMA ZITTO.

Again, ni rahisi sana kumshusha zitto kama kuna lolote baya amelifanya lisilo na maslahi kwa umma wa watanzania. ni Rahisi sana kumshusha na kumchafua zitto kama njia anazopita sio sahihi, LAKINI SIO KWA UWONGO WA KIPUUZI NAMNA HII.

Pamoja na kukiri kuwa Zitto ndiye mwanasiasa ninayemuamini na anayenivutia kuliko mwanasiasa yoyote Tanzania, na pamoja na ukweli kwamba zitto sio rafiki kwangu bali ni kaka yangu. Lakini sijawahi hata siku moja kupokea pesa kutoka kwake ama kwa MPESA au kwa TIGO PESA tangu nimefahamiana nae mpaka leo.

Ndio maana ninawapa pole MBOWE na vijakazi wake wanaotunga uwongo wa namna hii bila hata kujifikiria mara mbili mbili.

Uchaguzi mkuu wa ndani ya chama unawatia homa kundi la Mbowe na wagaza wenzake, uchaguzi huo unawafanya waweweseke kutwa kucha, mchana usiku.

Hakuna sababu ya kuhangaika na Zitto, wanachadema wapo na wataamua kwa yale mliyoyafanya, Zitto yeye ameshawaacha mile 2000 kwenye siasa zenye tija kwa Taifa.

Nimelazimika kuandika maneno haya baada ya kuona kuna huu ujinga unaofumbiwa macho na viongozi wa CDM kwa makusudi kabisa.
iliwahi kuandikwa humu mtandaoni kuwa ''Zitto ni maporomoko ya Nile, hayazuiliki kwa kifusi'' amewashinda na anaendelea kuwashinda.

Narudia tena kusema KWENYE HILI TAYARI ZITTO AMESHASHINDA.

1. Aliwashinda kwenye uwongo wenu mliokuwa mkiusambaza wa kupokea rushwa TANESCO lilipobumbuluka wakina mnyika, lissu na nassary wote waliufyata.

2. Aliwashinda mlipounda tume ya kumchunguza kuasisi migogoro ndani ya chama.

3. Alishinda kwenye hoja ya Buzwagi

4. Alishinda kwenye hoja ya kuwatimua mawaziri vilaza kwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu

5. Amewashinda kwenye hoja ya kuficha mali nje ya nchi (kama mabilioni ya uswisi) leo mnatapa tapa kwa kuwa bossi wenu anamiliki mali uarabuni.

Naomba niwakumbushe kuwa zitto ndiye mwanasiasa pekee wa upinzania anayeweza kuilazimisha serikali ikafanya maamuzi kutokana na hoja yake hata kama haipendi kufanya hivyo kwa wakati huo. Mfano ni hiyo hapo juu.

Naomba nihitimishe kwa kusema, ni kweli kwamba uwongo unapanda ghorofa kwa kutumia klifti, lakini hauwezi kubadilisha ukweli wa mambo daima dumu. uwongo utabaki kuwa uwongo tu na utaendelea kupuuzwa milele na milele.

Ndimi,
Habibu mchange
0762178678
mchangehabibu@yahoo.com

wewe ni gamba wala huwezi kuwachonganisha zito na viongozi wenzake,kauli tunayoijua sisi wana chadema ni aliyotoa mnyika kwamba chadema wala viongozi wa chadema hawajayasema hayo,hivyo tujuavyo sisi hayo ni maneno kutoka vinywani mwa Magamba. ccm subirini kifo chenu 2015
 
Ni sahihi kabisa ki-protokol kwa Mnyika kuwasiliana na public. Lakini si sahihi kwa zitto kupata majibu kwa kumtumia Mnyika. Kwa kuwa Zitto amemuandikia Slaa; basi ki-protokol Slaa alitakiwa amjibu Zitto kimaandishi kabla ya Mnyika kuruhusiwa kuwasiliana na umma (public).

e'mail ya Zitto na ufafanuzi wa Mnyika upi umetangulia?

Barua ya Zitto inataka maelezo ya Dr. Slaa kwa jambo lile lile ambalo lishaelezwa na Mnyika kabla
 
Umesahau pia kuuliza kwa nini Mbowe na Dr Slaa wamekaa kimya kwenue sakata hili
 
kibaraka leo umeamua kujitokeza hadharani hivi wewe bado ni mwanachama wa chadema
 
Hii inaweza ikawa post yangu ya mwisho kwako, pengine utaelewa.

Hakuna anayedhani kwamba Mnyika au mwanaChadema yupo neutral bila upendeleo wowote. Na hilo siyo lengo langu na wala halipo katika asili ya binadamu. So, once more, inategemea na namna unavyopresent kutofautiana huko publically na pia nafasi yako kuproject hizo tofauti.

Huwezi kuona katika maandishi ya Mnyika akimpuuza Zitto kijinga kijinga kama wewe ulivyofanya kwa viongozi wako. Na hata kama Mnyika ikitokea ukahisi amefanya hivo, ana moral authority ya kufanya hayo. Anaweza kusimama akatetea mawazo yake kwamba "mimi ni Mbunge na kiongozi ndani ya chama, na nadhani fulani hauendi sawa".

Ona tofauti na wewe: "LEMA anapita tu njia CHADEMA kwa kuwa yeye ni msaka tonge tu kama wasaka tonge wengine"

Sasa, mwisho, ukiachilia mbali kwamba namna yako ya kuproject tofauti na waliokuwa wenzio haionyeshi humility kama mwanasiasa mchanga mwenye mwono wa kufika mbali kwenye chama, pia huna moral authority ya kumsema hivyo Lema. Na usidhani kwamba public itakupokea vizuri hata kama Lema amekosea (btw, ni mwanadamu). Na Mnyika wakati akiwa mchanga kwa level zako kisiasa, it would have been unthinkable for him to say such autrociously suicidal statements.

You deserve to be future politician for this country,i wish zitto angesoma comment zako zote za kwenye huu uzi
 
rudi kwenye hoja ya ushindi wa zitto mkuu.
hizo hadithi zako nyingine kawapigie WAGAZA

Ndio maana nakufahamisha una akili za kuku na za kushikiwa, sasa ushindi hapo uko wapi?

Unataka kunilazimisha nijadili ushindi gani hapo?

Kwamba unataka kuhalalisha uchungu wa Zitto kwa CDM ni mkubwa kuliko wa Godbless J Lema kwa kuwa jamaa yako kalelewa na Mbowe tangu yuko UD au?

Unahalalisha lugha ya kuudhi aliyoitumia jamaa yako dhidi ya Lema kule Twitter iliyomfanya Lema kukasirika na kuja hapa kumwaga ugali?

Unataka ushindi gani kilaza wewe mwenye akili ya kuhongwa na kuhonga kila chaguzi?
 
Last edited by a moderator:
kwa kuongezea tu ... 1 kwa nini zitto anatetewa sana na wanazi wa ccm e.g kris lukosi, w. j. malecela, ritz, msalani etc. hayo mapenzi kwa mwanacdm yameanza lini?
 
Mchange ukihujumu CHADEMA!?? mbona unataka attention ambazo huna sifa nazo.. labda kwa kuiba simu...!!
 
Last edited by a moderator:
ni kweli kuwa wewe UMEFUKUZWA CHADEMA? Kama, ni kweli, kwanini ulifukuzwa? nikizingatia ile ripoti ya kwenye mitandao, ilikuwaje wewe ufukuzwe na kisha Zitto asifukuzwe?

Hili ndilo swali ninalojiuliza mie bila majibu,kama hili la Yericko Nyerere na SIRI ZA ZITTO limegundulika kuwa ni la UONGO,kuna uwezekano pia kuwa ile taarifa pia ya Usaliti wa Zitto kupitia PM-7 nayo ilikuwa ni sehemu ya uongo huu huu na ndio maana chama kilishindwa kumfukuza Zitto na kuuishia kuwatoa tu kafala hawa vijana ili kukatilia mbali uungwaji mkono wake kwenye chama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom