Zitto, Kwenye hili tayari umeshinda!

Zitto, Kwenye hili tayari umeshinda!

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na mtindo wa kurushwa kwa shutuma mbali mbali kutoka kwa viongozi wajuu wa CHADEMA wakitumia majina bandia kumuelekezea ndugu zitto kabwe.

Kwa makusudi kabisa viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti, katibu mkuu na wakurugenzi kadhaa wamekuwa wakirusha kila aina ya shutuma humu mtandaoni lakini kwa hofu kubwa ndio maana wanajificha kwa kutumia akaunti bandia.

Jana na juzi nimepokea sms, emails na simu nyingi sana kuhusu hiki kinachoitwa ripoti ya siri ya SLAA, MBOWE NA WAGAZA WENGINE dhidi ya ZITTO zikisema namie nimetajwa humo kuwa ninashirikiana na Zitto kukihujumu CHADEMA.

Bahati mbaya sana, hakuna ripoti ama shutuma zozote anazopelekewa Zitto kutoka kwa hawa majamaa ambazo hazinitaji, na kwentye hii nayo nimeshuhudia nikitajwa mara nyingi kupokea pesa kutoka kwa Zitto kukihujumu chama.

Bahati mbaya zaidi ni kwamba wafadhili wa mkakati huu ''OPERESHENI ONDOA ZITTO KWENYE HOJA ZENYE MASLAHI YA TAIFA'' wamekosa njia sahihi ya kutumia, wamekuwa wakiwatumia watu wale wale ambao kwa zaidi ya miaka na miaka tumekuwa tukikitetea chama kuwa si cha namna hiyo.

kitendo cha MBOWE na SLAA kuwatumia JOSHUA NASSARY, GODBLESS LEMA, MAMUYA na wengine, kinauthibitishia umma wa watanzania kuwa sio kweli kwamba zitto ni tatizo kwenye CDM, kitendo hiki cha kuwatumia watu wanaolalamikiwa kuwa wanabebana kimisingi ya ASILI ya wanakotokea kinatuthibitishia watanzania kwamba CHADEMA ni chama cha watu wa eneo hilo.

lakini wamefeli zaidi kumtumia LEMA kuwa eti ni KAMANDA mwenye uchungu na CHADEMA kuliko ZITTO, hiki pia ni kielelezo cha upeo mdogo wa kufikiri kwa watu hawa.

ZITTO ni mjenzi wa NYUMBA inayoitwa CHADEMA, Zitto ameshiriki mpaka kuijenga CHADEMA tangu ikiwa nyumba ya nyasi, mpaka ikawa ya udongo, ikaja ikawa ya tofali za kuchoma na sasa CHADEMA ni nyumba ya VIGAE,

LEMA ni mpangaji tu kwenye hii nyumba CHADEMA, hakuna jinsi yoyote mpangaji akawa na uchungu na nyumba kuliko mwenye nyumba, hakuna na haitaka itokee.

LEMA ni mpita njia tu kwenye CHADEMA, Kamwe hawezi kuwa na uhalali wa kumsema na kumtukana mtu aliyekijenga chama kilichomsaidia kumfikisha hapo alipo.

Nani humu jukwaani alikuwa anamfahamu LEMA mwaka 2006, NANI?. nani alikuwa anafahamu lolote kuhusu lema 2007,2008,2009 mpaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu?.

Nani anayemfahamu Lema kipindi hicho kwenye CHADEMA?. LEMA ni TUNDA LA KAZI NZURI YA KISIASA ILIYOFANYWA NA ZITTO KABWE.

Wakati Zitto anahangaika kushirikiana na viongozi wenzake kuijenga CHADEMA, LEMA alikuwa ni KIBARAKA wa MZEE AUGUSTINO MREMA wa TLP.

Wakati Zitto anaibua hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa kama BUZWAGI na nyinginezo, LEMA bado alikuwa hata hajui chaguo lake la kisiasa katika nchi hii, yaani lema hakuwa akijua aende chama gani cha siasa.

Wanaokumbuka na wenye akili timamu watakubaliana nami kuwa ni zitto aliyekwenda Arusha kumnadi mgombea wa TLP wa udiwani wakati wa uchaguzi wa marudio 2008 huku lema akiwa mpiganaji kibaraka wa augustino mrema wa TLP.

wanachadema wanafahamu kuwa wakati tunafanya uchaguzi wa ndani ya chama mwaka 2009 LEMA ndio kwanza alikuwa ana siku 4 za uanachama wake ndani ya CHADEMA.

LEMA anapita tu njia CHADEMA kwa kuwa yeye ni msaka tonge tu kama wasaka tonge wengine, ndio maana alipita NCCR, ILIPOKUFA AKAKIMBIA, AKAPITA TLP ilipokufa akakimbia na sasa yupo CHADEMA nayo ikiyumba sidhani kama hataacha kukimbia. LEMA hana hadhi ya kukubali kutumiwa na kina MBOWE na GENGE lake kumshambulia ZITTO, hana hiyo moral authority. mpangaji hawezi kuwa na uchungu sawa na mwenye nyumba,

Leo CHADEMA ikipasuka, leo CHADEMA ikiyumba, ikitetereka atakayeumia ni ZITTO aliyeijenga na si LEMA aliyeidandia.

Nasisitiza hapa kuwa Hakuna namna yoyote ile inayoweza kumshusha Zitto kwenye heshima yake aliyojijengea kwa kusambaza uwongo wa namna hii, hakuna na hitakaa itokee.

Hakuna namna yoyote ile ya kumshusha zitto kwenye orodha ya wanasiasa bora na makini kwa kuwatumia watu kama kina lema na nassary ambao wakati wanaomba kura waliomba wakisema WATUMWE WAENDE BUNGENI WAKAWE KAMA ZITTO.

Again, ni rahisi sana kumshusha zitto kama kuna lolote baya amelifanya lisilo na maslahi kwa umma wa watanzania. ni Rahisi sana kumshusha na kumchafua zitto kama njia anazopita sio sahihi, LAKINI SIO KWA UWONGO WA KIPUUZI NAMNA HII.

Pamoja na kukiri kuwa Zitto ndiye mwanasiasa ninayemuamini na anayenivutia kuliko mwanasiasa yoyote Tanzania, na pamoja na ukweli kwamba zitto sio rafiki kwangu bali ni kaka yangu. Lakini sijawahi hata siku moja kupokea pesa kutoka kwake ama kwa MPESA au kwa TIGO PESA tangu nimefahamiana nae mpaka leo.

Ndio maana ninawapa pole MBOWE na vijakazi wake wanaotunga uwongo wa namna hii bila hata kujifikiria mara mbili mbili.

Uchaguzi mkuu wa ndani ya chama unawatia homa kundi la Mbowe na wagaza wenzake, uchaguzi huo unawafanya waweweseke kutwa kucha, mchana usiku.

Hakuna sababu ya kuhangaika na Zitto, wanachadema wapo na wataamua kwa yale mliyoyafanya, Zitto yeye ameshawaacha mile 2000 kwenye siasa zenye tija kwa Taifa.

Nimelazimika kuandika maneno haya baada ya kuona kuna huu ujinga unaofumbiwa macho na viongozi wa CDM kwa makusudi kabisa.
iliwahi kuandikwa humu mtandaoni kuwa ''Zitto ni maporomoko ya Nile, hayazuiliki kwa kifusi'' amewashinda na anaendelea kuwashinda.

Narudia tena kusema KWENYE HILI TAYARI ZITTO AMESHASHINDA.

1. Aliwashinda kwenye uwongo wenu mliokuwa mkiusambaza wa kupokea rushwa TANESCO lilipobumbuluka wakina mnyika, lissu na nassary wote waliufyata.

2. Aliwashinda mlipounda tume ya kumchunguza kuasisi migogoro ndani ya chama.

3. Alishinda kwenye hoja ya Buzwagi

4. Alishinda kwenye hoja ya kuwatimua mawaziri vilaza kwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu

5. Amewashinda kwenye hoja ya kuficha mali nje ya nchi (kama mabilioni ya uswisi) leo mnatapa tapa kwa kuwa bossi wenu anamiliki mali uarabuni.

Naomba niwakumbushe kuwa zitto ndiye mwanasiasa pekee wa upinzania anayeweza kuilazimisha serikali ikafanya maamuzi kutokana na hoja yake hata kama haipendi kufanya hivyo kwa wakati huo. Mfano ni hiyo hapo juu.

Naomba nihitimishe kwa kusema, ni kweli kwamba uwongo unapanda ghorofa kwa kutumia klifti, lakini hauwezi kubadilisha ukweli wa mambo daima dumu. uwongo utabaki kuwa uwongo tu na utaendelea kupuuzwa milele na milele.

Ndimi,
Habibu mchange
0762178678
mchangehabibu@yahoo.com

Upeo wako mdogo ndio umepelekea uandike uliyoyaandika, tambua mjenzi wa nyumba siku zote ndio mbomoaji hivyo Zitto kutokana na kuijua vizuri CDM ndio maana anapita njia hizi kutaka kuibomoa CDM.
 
Ahsante bwana Mchange. Hakika umenena ya moyoni na yaliyo ya kweli

Hamna ukweli hapo,ni upuuzi mtupu. Huwezi furahia chakula kitamu kwenye sahani yenye harufu ya kinyesi.Mchange hata uongee ukweli hatutaupokea,unanuka kinyesi na wafuasi wenzio.Umeonyesha ushabiki wa kitoto kwenye hoja nyeti,huwezi kutuaminisha eti zitto ni bora kuliko mbowe,wakati zitto katengenezwa na mbowe.Mabega hayawezi shinda kichwa.
 
hawana jina zuri la kuwaita zaidi ya ''WAGAZA''.
kama mnaweza kukaa mkatunga uwongo na kuusambaza kwa kasi ya ajabu, mkautetea na kuufanya uaminiwe.

kama mnaweza mnkamshutumu mtu kwa usaliti baada ya kifo chake mkamuita kamanda,

kama mnaweza mkaweka mipango mpaka ya kutoa roho za wenzane kwa sababu ya madaraka ya duniani na ustawi wa KABILA LENU. kwanini sasa tusiwaite WAGAZA?.

kwangu mimi nyie ni WAGAZA na nitaendelea kuwaita hivyo daima dumu

wewe si ulifukuzwa lakini? endelea kutumika, CDM IPO NA ITAENDELEA KUWEPO.
 
Kama chadema wanataka kuendelea kukiimarisha chama basi wamfukuze mabere marando. Hao wengine ni vifaranga tu.

Mtiririko wa uchambuzi wa ripoti yenyewe haina tofauti na ule alioandika akihusisha uchunguzi kuhusu video rwakatare. Ilikuwa na mtiririko mzuri wenye ushawishi lkn ushahidi wote aliouweka wa nambaza simu, muda nk ulikuja kuonekana ni feki.

Hata zito kamtolea mfano wa jinsi nccr ilivyosambaratika na marando akiwa ndie msaliti

msaliti hatajwi kabisa kajikalia pembeni,
 
WACHAGGA

Ilikua code name ya kumaanisha "Wachagga" ndani ya PM-7

Karne hii tunaeneza chuki za kikabila kama msingi wa siasa.

Hii ni njia inayotumiwa na narrow minds kwenye siasa

Mkuu umenena. Chuki za kikabila na kidini ni mbaya kiasi kwamba huweza kumfanya mtu atembee na sumu mfukoni akimuwinda kiongozi wake kisiasa.
 
Siku zako zimebaki chache sana mkuu!


Acha vitisho

Mnaandika tamko refu la kutaja majina ya watu.Hesabu idadi ya jina "Lema" kwenye hilo tamko.Utaweza kugundua kiwango cha hasira na upeo mdogo wa mwandishi.Hayuko sawa kisaikolojia
 
Hii inaweza ikawa post yangu ya mwisho kwako, pengine utaelewa.

Hakuna anayedhani kwamba Mnyika au mwanaChadema yupo neutral bila upendeleo wowote. Na hilo siyo lengo langu na wala halipo katika asili ya binadamu. So, once more, inategemea na namna unavyopresent kutofautiana huko publically na pia nafasi yako kuproject hizo tofauti.

Huwezi kuona katika maandishi ya Mnyika akimpuuza Zitto kijinga kijinga kama wewe ulivyofanya kwa viongozi wako. Na hata kama Mnyika ikitokea ukahisi amefanya hivo, ana moral authority ya kufanya hayo. Anaweza kusimama akatetea mawazo yake kwamba "mimi ni Mbunge na kiongozi ndani ya chama, na nadhani fulani hauendi sawa".

Ona tofauti na wewe: "LEMA anapita tu njia CHADEMA kwa kuwa yeye ni msaka tonge tu kama wasaka tonge wengine"

Sasa, mwisho, ukiachilia mbali kwamba namna yako ya kuproject tofauti na waliokuwa wenzio haionyeshi humility kama mwanasiasa mchanga mwenye mwono wa kufika mbali kwenye chama, pia huna moral authority ya kumsema hivyo Lema. Na usidhani kwamba public itakupokea vizuri hata kama Lema amekosea (btw, ni mwanadamu). Na Mnyika wakati akiwa mchanga kwa level zako kisiasa, it would have been unthinkable for him to say such autrociously suicidal statements.
 
protocal kwa hili! my foot..,wenye iq ndogo mtakesha kwenye hili.

Mnyika ni mwenezi amelimaliza kwa niaba ya chama chake

Ni sahihi kabisa ki-protokol kwa Mnyika kuwasiliana na public. Lakini si sahihi kwa zitto kupata majibu kwa kumtumia Mnyika. Kwa kuwa Zitto amemuandikia Slaa; basi ki-protokol Slaa alitakiwa amjibu Zitto kimaandishi kabla ya Mnyika kuruhusiwa kuwasiliana na umma (public).
 
Mleta uzi ni kama vile unajua kuwa baadhi ya wana jf ni wapenzi wa taarab aka mipasho ndio maana umechukua muda mwingi kuwapa flava hiyo na ninaona wanaku back up vizuri.Binafsi nina uwezo wa kusoma facts kurasa elfu kuliko propaganda kurasa moja!After all we ni mwanachama wa CDM kwa sasa?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Akili yako inawaza pafupi tu?. ndio maana mnaandika uwongo uwongo kwa kupenda vifupi?. mbona ile ripoti yenu ndefu sana?

Machange lazima utakuwa na matatizo makubwa sana, Zitto ana akili ila nyinyi mnao jipendekeza ndo hamna akili, yeye Zitto kasema ndani ya CHADEMA hakuna mgogoro isipokuwa anachohisi ni kwamba kuna wahuni wasiokitakia mema chama ndo wanazusha upuuzi huo, leo hii unaleta uzi hauna kichwa wala miguu, hivi wewe kweli unajitambua, njaa zitawamaliza
 
Wa kumfukuza zitto chadema hajazaliwa,na siku akizaliwa na akamfukuza chadema ikuure!!

Hawezi kufukuzwa kwasababu hana madhara tena, kama ni joka limeshang'olewa meno, so halina sumu tena. Yeye na Shibuda kwasasa ni Majoka ya kibisa ya Magamba ndani ya Chadema
Joka ukishaling'oa meno, kuna haja gani ya kuliponda kichwa sasa. Ila amejua kwamba intelijensia ya Chadema ni dunia nzima inatisha!
 
Kheeh! Unampa sifa asizostahili.

Point of correction:Mleta mada si mwanachama wa CHADEMA.

Aliwahi kuwa mwanachama lakini akafukuzwa kwa tuhuma za usaliti na kuhujumu chama baada ya tuhuma kuthibitishwa pasipo na shaka(beyond reasonable doubt)
Ben.

Hivi Yericko ni mwanachama wa Chadema?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom