Zitto kuwa m/kiti wa CHADEMA taifa?

Waberoya,

Wee ni USALAMA WA TAIFA mkuu wangu na uko kazini haswaa kuivuruga CHADEMA.

Unatumia sana njia ya DEVIDE AND RULE.

Ulishatuelezea hapa Uhusiano Mkubwa wa Zitto na Ridhiwan na kuja na maneno kibao ya hadi kusalitiana kwenye migomo na mengineyo kibao............. Umeshamshambulia Mbowe mara kibao na tangu ile Makala, Zitto humshambulii tena ila kumtetea.

Sasa leo umekuja na mpya ya Urafiki wa Mbowe na Zitto.........tunashukuru tumelifahamu hilo. Kwa hiyo unataka kusema kuwa Mbowe akiondoka, Zitto ndiyo atachukua kiti na atampigia kampeni?

Nasubiri siku ukija na maneno ya Chadema ni chama cha watu wa kusini na hapo ndiyo ntakutwanga kwa maneno yako mwenyewe.

Mbowe alikuwepo Chadema miaka kibao. Zitto baada ya kusimamishwa bungeni, alianza kujipandisha chat mwenyewe na kuipandisha chat Chadema. Dr. Slaa alipoanza kurusha mabomu na kufanya ufanisi mkubwa katika kazi zake za ile Hospital ya mifupa na kule jimboni kwake, imemjengea umaarufu mkubwa sana kama Mchapa kazi na haogopi kumfunga paka kengele.

Alipotangaza kuingia kwenye uchaguzi wa Urais, pamoja na uhakika wa kushindwa (Ilijulikana hata akishinda, watachakachua. Na walichakachua kweli kweli) basi ashindwe ila atakipa chama NGUVU KUBWA. Sasa hivi kuwepo kwake Chadema, kunaijenga Chadema kama chama cha upinzani cha kutisha. Ni Slaa amewafanya CUF wawe chama cha pili cha Upinzani.

Slaa kwetu wengi atakuwa kama Mandela. Ingelikuwa furaha kumuona akiwa Rais kwa Term moja tu na huku akiacha Ameiweka katiba ya Tanzania katika hali nzuri. Kupunguza madaraka ya Rais, kuwaongezea madaraka viongozi wa Mikoani na Wilayani, kuongeza nguvu za Waziri mkuu, Mahakama kuwa na Nguvu na Bunge. Hii mihimili mitatu KUTENGWA na kuwekewa Mipaka ya kutokuingiliwa na hapa ina maana hata Jaji Mkuu, ni Majaji wapendekeze na Rais anachagua mmoja. Mkuu wa Usalama pia mchezo unakuwa huohuo kwa kupandisha watu vyeo na hadi mtu anafikia kuwa TOP na si kubebwa kama ilivyo leo......

Kuna mengi sana ya kufanya katika katiba ambapo kila mtu mwisho wa SIKU atakuwa CHINI YA SHERIA.

Waberoya, toka leo nakupa heshima sana maana USIJE UKANI-GHADAF bure mwana wa Sikonge.

Ahh, nimalizie kwa kusema "Zitto, wewe na JF ni kama Chanda na Pete." Hata usemeje, JF inakupenda?!?!
 
Wakuu,
Kuna habari za kuaminika kuwa Mh Zitto Kabwe ameanza harakati za kutaka kuukwaa uenyekiti wa Chadema Taifa. Nimeziita habari hizi tetesi kwa sababau sijui degree ya ukaribu kati ya Zitto na rafiki yake niliyeongea naye.

Yaani rafiki yako anayweza kukupa mkakati nyumbulufu namna hii hujui ana ukaribu kiasi gani na mtu maarufu kama Zitto? Fanyia kwanza basi "kazi ya nyumbani" tetesi yako kisha utuletee ikiwa imewiva kdogo;Tutakugongea senksi tuu usiwe na haraka sana.
 
1. Ndio maana kuna tuhuma nyingi juu ya Zitoanayeibua na kuzisambaza kwa uzushi ni Dr. Slaa, ndio maana tutahalikisha anaishia hapo alipo haendi mbali.

2. Slaa hajui kuwa Mbowe na Zito ni washikaji ..natamani niseme jambo naona keyboard inanizuia.

Leo naona umeamua kufunua nusu ya kile kiujazacho moyo wako,

1.Kwamba Dr. Slaa ndiye anayeibua na kusambaza uzushi inafanana sana na utetezi kwenye thread ya kutumika kukidhoofisha chama kwamba kuna baadhi ya viongozi wenzake wanachukua fitna na majungu hapa jf na kumjengea chuki, hapo nimewapata wote wawili, wewe na swahiba wako zitto. Lakini kwamba mtahakikisha kwamba anaishia hapo alipo nadhani hamtofanikiwa, ama mnampango wa kumtoa roho!!??manake nchi hii sasahivi kila mtu ajifanya mafia!! In a serious note, narudia tena, hamuwezi kumkwamisha Dr. Slaa, salamu zitaanza kumiminika kuanzia kwenye uchaguzi wa chama 2014.

2.Kwamba Dr. Slaa hajui kwamba zitto na mbowe ni washikaji, nadhani hapa unafanya masihara, ama vinginevyo umelewa uzittophobiasis!! how on the earth right here in Tanzania kwa mtu makini katika siasa za nchi hii asijue urafiki wa mbowe na zitto!!:teeth:

Kumbe ndio sababu ya wewe kila mara unaibuka kutoka huko ulikotoka kuja kuishambulia chadema huku ukimpamba zitto, sababu kubwa ni kwakuwa mnaamini kwamba slaa anamchukia na kumuogopa zitto. Kama kweli haya sio majugu, fitna na chuki, nikikopa maneno ya swahiba wako mh.zitto naomba umalizie na hilo unalolionea aibu na kusingizia keyboard. Labda nikuulize tu kidogo na wewe, sio kwamba mnamchukia slaa kwakuwa alimtemesha kibarua david kafulila???
 
Waberoya,

Wee ni USALAMA WA TAIFA mkuu wangu na uko kazini haswaa kuivuruga CHADEMA.


Ahh, nimalizie kwa kusema "Zitto, wewe na JF ni kama Chanda na Pete." Hata usemeje, JF inakupenda?!?!

Waberoya na GURTI the same ID kwahiyo husishangae, waberoya anajaribu kutema sumu kwa pande mbili kuangalia upepo lakini kagonga mwamba:embarassed2::lol::lol::lol::lol:
 
Kigoma is firmluy behind me and I dedicately serve them. Don't ever under estimate watu wa Kigoma.

Haya maneno ni ya kigadafi hivi au yule jamaa wa syria ya kuzani kuwa watu wataendelea kuwa wajinga milele. Kutokuwa na principles ni ujinga siyo sifa watu wa kigoma. Msaliti anatakiwa aonyeshwe njia
 
Gurti kwanza uelewe kuanzia leo..

Kuwa Zito na Mbowe ni washikaji tena sana tu....let this stick in your mind.

Ndio maana kuna tuhuma nyingi juu ya Zito anayeibua na kuzisambaza kwa uzushi ni Dr. Slaa, ndio maana tutahalikisha anaishia hapo alipo haendi mbali.

Slaa hajui kuwa Mbowe na Zito ni washikaji ..natamani niseme jambo naona keyboard inanizuia.

Na hili wengi hata humu hawalijui na tunapoona comments Zito aondoke wengine tunabaki tunacheka tu!

Bifu ni Slaa na Zito, Slaa ana chuki na anamuogopa Zito, najua kuwa alipopata kura milioni 2 aliringia na kusema Zito hajawahi kupigiwa kura kama hizo

Tulipotaka uchaguzi ufanyike na viongozi wa juu waondolewe wote kazi ikawa ni nani wa kuwapata

Mbowe is smart...very very smart..na KIKUBWA hana uroho wa madaraka...ukifikia muda ATAONDOKA TU, na kama chair anaweza kumpigia kampeni Zito atafanya hivyo...Mbowe kwa maneno yake anaonekana anampenda zaidi Zito.......mtafute muulize.



Inahisiwa hata ile vuguvugu la uongozi eti zito anataka kuwa mwenyekiti ni changa la macho..wengi mliingia king, hata mimi nilikuwamo humo

Nilichukia chadema, wazee, Mbowe na nilipokuja kugundua ukweli nikasema SIASA NI MCHEZO MCHAFU!!!

Hapo umejificha uso miguu na mwili vyote viko nje...tehtehe!

Akifanikiwa kuingia Ikulu utakuwa waziri wa Miundo mbinu nini? Mmh huu urais huu nyie watu wa Kaskazini kubalianeni nani ndiyo awe mgombea vinginevyo nyote mtashindwa na kuishia kupoteza vyote. For your information dola ikiparaganyika hakuna wakumzidi Slaa na ikibaki ilivyo the second best ni huyo ambaye wengi wana m under estimate including Web; mwambie mamvi pole sana anapesa lakini chess haiwezi akajifunze kwetu BK.
 
mkuu, tutabadilishana kadi, mh. akiwa m/kiti, naenda kurenew uraia wangu kule ssm. Kadi bado nonayo ila nimeisitishia ada mpaka ssm irudi msitarini na hii nakadiria mwaka 2047.
 
Wakuu,
Kuna habari za kuaminika kuwa Mh Zitto Kabwe ameanza harakati za kutaka kuukwaa uenyekiti wa Chadema Taifa. Nimeziita habari hizi tetesi kwa sababau sijui degree ya ukaribu kati ya Zitto na rafiki yake niliyeongea naye.
Mikakati ya kuusaka uenyekiti huo zimeshaanza na tayari ameanza kupanga safu ya uongozi hasa kwa ngazi ya Kitaifa.
Hoja ambazo ameaza kuisambaza chini kwa chini, kisiri siri sana na kwa umakini wa Hali ya juu ni kama zifuatazo;
HOJA ZA ZITTO ZUBERI KABWE kwa wapiga kura wake.
A) Uchaguzi uliopita alimpisha Mbowe kwa Ushauri wa Wazee kwa unyenyekevu wote, kwa hiyo safari ndugu yetu naye atawaomba wazee kuwa hii ni zamu yangu nami naomba nigombee na/au ikiwezekana nipite bila kupingwa kama Mbowe. Atawaomba wazee hivyo.
B) Hoja ya pili Chadema ni Chama kinachoungwa mkono sana na vijana hivyo, Dr Slaa siyo Chaguo bora kwa CDM kwa sasa kuwa mkiti ILA yeye ndiye Chaguo bora. Dr Slaa ni Mzee, Mbowe aachie kwa hiari hata kama katiba inamruhusu kwa kuwa ameongoza miaka 9 mpaka 2013 uchaguzi utakapofanyika.
C) Tatu, Chama chetu kinonekana au kinatuhumiwa kuwa chama cha Wachagga . Hivyo mimi nitamaliza hoja hiyo ili tushinde 2015. Ndani ya mkakati huu anategemewa kuchota kura toka mikoa yote isipokuwa wachaga. Wanategema kutumia fitina ikibidi hasa kama mbowe atagombea tena. Ikionekana Mbowe ana nguvu watamlazimisha kwa kashfa iwe iwavyo.
D) Mbowe na Slaa wote wawmetoka kaskazini, SASA ni muda muafaka na kanda zingine nazo ziongoze CHADEMA kama tumekomaa na tunataka kuingia ikulu.Hoja hii nayo inategewa kuwapa nguvu mikoa mingine. Tayari wapambe wako kazini isipokuwa kanda ya kaskazini.
E) Kete kubwa kuliko zote ni kuwa, kwa kuwa Chadema inatuhumiwa kwa udini na waislamu, mimi ndiye suluhisho pekee. Hapa tayari kuna watu wamesambazwa kwa wajumbe ambao ni waislamu ndani CDM ili wamwuunge hasa wale wanaoonekana kuwa wataweza kumaintain nafasi zao na kuwashawishi potetial leaders to be. Kumbuka uchaguzi wa taifa utafanyika baada ya chaguzi za ngazi ya chin kuisha kote nchini.

MIKAKATI
A) Viongozi ambao ni washabiki wake nchi nzima wamepewa fedha za kutosha kuhakikisha kuwa wale wanaomwuunga mkono wanashinda nafasi za kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa na Baraza kuu ili kumpitisha yeye mwaka 2013.
Kinachoshangaza kwa taarifa nilizo nazo toka moja wa marafiki zangu ambaye ni mtandao wake na asiyejua msimamo wangu ni kuwa fedha si tatizo katika kundi hili.
B) Washabiki wake ambao ni wanachadema na wasiowanachedema wanamchangia fedha nyingi sana. Wanakadiria kukusanya sh Bil moja. Hizi fedha nazo zilinipa mshangao nikizingatia kuwa alikuwa na confidence kupita kiasi.

NB; Alikana kabisa kuhusu watuhumiwa wa UFISADI kuwafadhili wao. Pia alikana kuwapo kwa mkakati wa kuhama Chadema ambao umekuwa ukirushwa katika jamiiforum ila alikiri kuwa bosi wao zitto anajua kila kitu katika JF kuhusu yeye. Ameamua kutojibu baadhi ya tuhuma huko JF na magazetini. Alisema, sasa tunampango wa kutumia sehemu ya fedha kusafisha majeraha ya mwahalisi, JF na magazeti mengine kwa mbinu yo yote. Sikuelewa maana ya Mbinu yo yote.
Kilichonishangaza kuliko zote.
Nilimwuuliza, je mkishindwa mko tayari kukubali matokeo? Alikataa kata kata kuwa kunakushindwa katika mikakati yao, piga ua gara gaza hakuna kushindwa. Iwe iwavyo lazima tutashinda.
Binafsi nilishindwa kumwelewa, nijuavyo, katika siasa kuna kushinda na kushindwa pia.
Wakubwa,
Humbly I submit.

Umelipwa kiasi gani/umeahidiwa cheo gani.muogope mungu wako what is needed is fact not porojo porojo,na usitumie sana mapenzi kwa mtu ndugu utaangamia ukimchezea chatu.
 
hoja za wanafiki na wote wanaotumwa na ccm naomba tusijibu ili akose la kusema siku nyingine wadau.
 
Rafiki yako hakukueleza ukweli nilichosikia mimi ni kwamba Zitto anaandaliwa kuwa mufti wa waislamu Tanzania kutokana na kuwa na elimu ya kuridhisha, kwani huyu mufti wa sasa hivi akikaa kikao meza moja na maaskofu hawezi kuwa napointi ya kuongea kwa sababu ni darasa la saba, huo ndio mkakati uliopo kwa sasa kwani licha ya swala la umri wake kuwa mdogo, imethibitishwa kwamba hakuna umri maalum wa kuwa mufti, na kuhusu kitakuwaje awe mufti wakati zitto haswali sala tano, hoja hiyo ilipanguliwa kwamba kuna viongozi wengi tu wa Bakwata ambao ni wakristo na wengine ni masheikh lakini wanamiliki bar za kuuza pombe, na wengine wameoa wanawake wakristo lakini hawajafunga ndoa za kiislamu. nitaendelea kuwapa update hizi kwa kadili ninavyozipokea.

Hapa patakuwa patamu pale Mufti wa Tanzania atakuwa hana mke, unless aoe mapema.
 
Back
Top Bottom