Wakuu,
Kuna habari za kuaminika kuwa Mh Zitto Kabwe ameanza harakati za kutaka kuukwaa uenyekiti wa Chadema Taifa. Nimeziita habari hizi tetesi kwa sababau sijui degree ya ukaribu kati ya Zitto na rafiki yake niliyeongea naye.
Mikakati ya kuusaka uenyekiti huo zimeshaanza na tayari ameanza kupanga safu ya uongozi hasa kwa ngazi ya Kitaifa.
Hoja ambazo ameaza kuisambaza chini kwa chini, kisiri siri sana na kwa umakini wa Hali ya juu ni kama zifuatazo;
HOJA ZA ZITTO ZUBERI KABWE kwa wapiga kura wake.
A) Uchaguzi uliopita alimpisha Mbowe kwa Ushauri wa Wazee kwa unyenyekevu wote, kwa hiyo safari ndugu yetu naye atawaomba wazee kuwa hii ni zamu yangu nami naomba nigombee na/au ikiwezekana nipite bila kupingwa kama Mbowe. Atawaomba wazee hivyo.
B) Hoja ya pili Chadema ni Chama kinachoungwa mkono sana na vijana hivyo, Dr Slaa siyo Chaguo bora kwa CDM kwa sasa kuwa mkiti ILA yeye ndiye Chaguo bora. Dr Slaa ni Mzee, Mbowe aachie kwa hiari hata kama katiba inamruhusu kwa kuwa ameongoza miaka 9 mpaka 2013 uchaguzi utakapofanyika.
C) Tatu, Chama chetu kinonekana au kinatuhumiwa kuwa chama cha Wachagga . Hivyo mimi nitamaliza hoja hiyo ili tushinde 2015. Ndani ya mkakati huu anategemewa kuchota kura toka mikoa yote isipokuwa wachaga. Wanategema kutumia fitina ikibidi hasa kama mbowe atagombea tena. Ikionekana Mbowe ana nguvu watamlazimisha kwa kashfa iwe iwavyo.
D) Mbowe na Slaa wote wawmetoka kaskazini, SASA ni muda muafaka na kanda zingine nazo ziongoze CHADEMA kama tumekomaa na tunataka kuingia ikulu.Hoja hii nayo inategewa kuwapa nguvu mikoa mingine. Tayari wapambe wako kazini isipokuwa kanda ya kaskazini.
E) Kete kubwa kuliko zote ni kuwa, kwa kuwa Chadema inatuhumiwa kwa udini na waislamu, mimi ndiye suluhisho pekee. Hapa tayari kuna watu wamesambazwa kwa wajumbe ambao ni waislamu ndani CDM ili wamwuunge hasa wale wanaoonekana kuwa wataweza kumaintain nafasi zao na kuwashawishi potetial leaders to be. Kumbuka uchaguzi wa taifa utafanyika baada ya chaguzi za ngazi ya chin kuisha kote nchini.
MIKAKATI
A) Viongozi ambao ni washabiki wake nchi nzima wamepewa fedha za kutosha kuhakikisha kuwa wale wanaomwuunga mkono wanashinda nafasi za kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa na Baraza kuu ili kumpitisha yeye mwaka 2013.
Kinachoshangaza kwa taarifa nilizo nazo toka moja wa marafiki zangu ambaye ni mtandao wake na asiyejua msimamo wangu ni kuwa fedha si tatizo katika kundi hili.
B) Washabiki wake ambao ni wanachadema na wasiowanachedema wanamchangia fedha nyingi sana. Wanakadiria kukusanya sh Bil moja. Hizi fedha nazo zilinipa mshangao nikizingatia kuwa alikuwa na confidence kupita kiasi.
NB; Alikana kabisa kuhusu watuhumiwa wa UFISADI kuwafadhili wao. Pia alikana kuwapo kwa mkakati wa kuhama Chadema ambao umekuwa ukirushwa katika jamiiforum ila alikiri kuwa bosi wao zitto anajua kila kitu katika JF kuhusu yeye. Ameamua kutojibu baadhi ya tuhuma huko JF na magazetini. Alisema, sasa tunampango wa kutumia sehemu ya fedha kusafisha majeraha ya mwahalisi, JF na magazeti mengine kwa mbinu yo yote. Sikuelewa maana ya Mbinu yo yote.
Kilichonishangaza kuliko zote.
Nilimwuuliza, je mkishindwa mko tayari kukubali matokeo? Alikataa kata kata kuwa kunakushindwa katika mikakati yao, piga ua gara gaza hakuna kushindwa. Iwe iwavyo lazima tutashinda.
Binafsi nilishindwa kumwelewa, nijuavyo, katika siasa kuna kushinda na kushindwa pia.
Wakubwa,
Humbly I submit.