Zitto Kabwe ndie rais ajaye wa JMT 2025

Zitto Kabwe ndie rais ajaye wa JMT 2025

Haya ni maoni yangu,nasisitiza haya ni maoni yangu

Mbunge wa Kigoma Mjini ndg Zitto Kabwe kupitia chama cha ACT-Wazalendo,ndie anastahili kuvaa viatu vya JPM 2025.

Analysis zote nilizofanya zinaonyesha huyu kijana makini anafaa kabisa kuipeleka nchi kuwa taifa la uchumi wa kati duniani, tuache unafki huyu jamaa kafanya mengi yenye tija kwa taifa hili, hakuwahi kutanguliza maslahi ya chama siku zote ametanguliza maslahi ya taifa Tanzania.

Ndie mbunge pekee ambaye hachukui posho bungeni.

Kuna sababu nyingi zinazombeba na kumstahilisha kuwa rais ajaye baada ya JPM,pamoja na yote yaliyowahi kusemwa juu yake ila nimebaki kumuona kama kioo cha uongozi Tanzania.

Zitto Kabwe is my president in 2025
....Du! kweli haya ni maoni yako!! Sawa si utampa kura yako, basi atakuwa rais wako!!
 
mimi zamu yangu ni awamu ya 8 mwaka 2045 nitakuwa na miaka 56 ndio ninaanza maandalizi
 
Umetumwa? au ni bange? au umesahu kumeza dawa zako za Mirembe? Hata kama umetumwa wangetafuta mtu makini anaejua kujenga hoja japo majinga manne hivi yatakuelewa!
Mkuu Mimi ni mtanzania sifungwi na chama chochote
Sasa kama mnateua katibu mkuu kwa sababu aliongoza mgomo wa madaktari watu wakafa na kupata shida na mwenyekiti ana address mbele ya umma that damn reason, niwaweke kundi gani?
 
Sasa wewe mwanachama wa ACT, kuna wazo lingine unalo zaidi ya hilo?
Nani watampigia kura hata??
 
We we ni wakala wake? Atakuwa rais chini ya chama gani? Hachukui posho? Mbona alichukua mlungura wa kutosha tena kauchukulia Ujerumani? Kama asingekengeuka kwa CHADEMA,tungemuamini.Lakini kwa sasa tukimpa urais,atatuuza kwa wajerumani
 
eti saizi yake JPM.. haaa nimecheka sana nilipo soma post yake, ana maneno ya kanga sijawahi ona...haaa
 
Zitto anaupeo mkubwa sana ukiacha siasa zetu za mihemuko nina imani kubwa wanaomponda zitto midomoni mioyoni wanamkubali.

Hoja na umakini wake umesaidia kukuza chadema na upinzani kwa ujumla.

Kinachomponza Zitto sio mnafiki, nyeupe kwake nyeupe sio nyekundu. Tumezoea kudanganywa na hatuhoji, msema kweli hapendwi.

Tumeona uchaguzi uliopita, waliotoka chama tawala kwenda upunzani na kashfa zote tukalazimishwa ni wasafi na tukawashabikia tukiulizwa tunapewa majibu mepesi.

Zitto mtu makini na mwenye msimamo, kwangu mimi anaweza kuvaa viatu vya JPM
Hata ukimpamba nyau hawezi kuwa simba hata siku moja
 
We we ni wakala wake? Atakuwa rais chini ya chama gani? Hachukui posho? Mbona alichukua mlungura wa kutosha tena kauchukulia ujerumani? Kama asingekengeuka kwa chadema,tungemuamini.Lakini kwa sasa tukimpa urais,atatuuza kwa wajerumani
Haijalishi chama, tunaangalia mtu, nani alijua Lowassa atahamia CHADEMA siku moja, kumbuka Richmond ndio iliipa kick CHADEMA! Halafu kabla hujamnyooshea kidole zito, kamuulize mwenyekiti aliyedumu miaka 20 anayedai democrasia pesa ya ruzuku mbona haifiki majimboni kusaidia japo wagombea,
 
Kwanza twambie fedha alizokuwa anatumia kabla ya kampein kwenye chama chake alizitoa wapi na sasa anasoma
Harvard university je ni gharama zake ?
 
Kwa kuwa umesoma mahali kaandika kuwa yuoo masomoni havadi basi akili imekuruka na kuanza kumfikiria kwenye urais
 
SPOT ON , FOR ME IT HAS TO BE HIM OR AMBASSADOR DR DAU
 
Haya ni maoni yangu, nasisitiza haya ni maoni yangu

Mbunge wa Kigoma Mjini ndg Zitto Kabwe kupitia chama cha ACT-Wazalendo, ndiye anastahili kuvaa viatu vya JPM 2025.

Analysis zote nilizofanya zinaonyesha huyu kijana makini anafaa kabisa kuipeleka nchi kuwa taifa la uchumi wa kati duniani, tuache unafki huyu jamaa kafanya mengi yenye tija kwa taifa hili, hakuwahi kutanguliza maslahi ya chama siku zote ametanguliza maslahi ya taifa Tanzania.

Ndie mbunge pekee ambaye hachukui posho bungeni.

Kuna sababu nyingi zinazombeba na kumstahilisha kuwa rais ajaye baada ya JPM, pamoja na yote yaliyowahi kusemwa juu yake ila nimebaki kumuona kama kioo cha uongozi Tanzania.

Zitto Kabwe is my president in 2025
Naona umevimbiwa na makande wewe siyo bure
 
Back
Top Bottom