Zitto Kabwe ndie rais ajaye wa JMT 2025

Zitto Kabwe ndie rais ajaye wa JMT 2025

Kwahiyo ilikua inafahamika hivyo muda wote huo alipokua pale mpaka akaondoka?

Ofcause jamaa ni msaliti asilimia mia moja unadhani ni kwanini alikuwa na mawasiliano na Jack Zoka kipindi chote cha uchaguzi wa mwaka 2010.
 
Kwa hivyo unataka kusema kuwa ACT-Wazalendo ni CCM?
 
Haya ni maoni yangu,nasisitiza haya ni maoni yangu

Mbunge wa Kigoma Mjini ndg Zitto Kabwe kupitia chama cha ACT-Wazalendo,ndie anastahili kuvaa viatu vya JPM 2025.

Analysis zote nilizofanya zinaonyesha huyu kijana makini anafaa kabisa kuipeleka nchi kuwa taifa la uchumi wa kati duniani, tuache unafki huyu jamaa kafanya mengi yenye tija kwa taifa hili, hakuwahi kutanguliza maslahi ya chama siku zote ametanguliza maslahi ya taifa Tanzania.

Ndie mbunge pekee ambaye hachukui posho bungeni.

Kuna sababu nyingi zinazombeba na kumstahilisha kuwa rais ajaye baada ya JPM,pamoja na yote yaliyowahi kusemwa juu yake ila nimebaki kumuona kama kioo cha uongozi Tanzania.

Zitto Kabwe is my president in 2025
Ni mnafiki hawezi kuja kuwa rais. Ni mtu wa majungu majungu ndiyo maana alifukuzwa CHADEMA! Na akikombea hiyo 2025 lazima tumkate tu maana hafai kabisa kuwa hata mjumbe wa nyumba 10.
 
Haya ni maoni yangu,nasisitiza haya ni maoni yangu

Mbunge wa Kigoma Mjini ndg Zitto Kabwe kupitia chama cha ACT-Wazalendo,ndie anastahili kuvaa viatu vya JPM 2025.

Analysis zote nilizofanya zinaonyesha huyu kijana makini anafaa kabisa kuipeleka nchi kuwa taifa la uchumi wa kati duniani, tuache unafki huyu jamaa kafanya mengi yenye tija kwa taifa hili, hakuwahi kutanguliza maslahi ya chama siku zote ametanguliza maslahi ya taifa Tanzania.

Ndie mbunge pekee ambaye hachukui posho bungeni.

Kuna sababu nyingi zinazombeba na kumstahilisha kuwa rais ajaye baada ya JPM,pamoja na yote yaliyowahi kusemwa juu yake ila nimebaki kumuona kama kioo cha uongozi Tanzania.

Zitto Kabwe is my president in 2025

Mleta mada na baadhi ya watu mnakosea sana. Kwa nini Urais unafikiria 2025 na si 2020? Kwa nini tunataka kujenga kasumba mbaya kuwa ukisha kuwa Rais lzm umalize miaka 10? Katiba inasemaje? Ni miaka 5 tu.
 
Zito ashapotea nyota saiv imemuwakia kijana wetu Makonda
 
Umetumwa? au ni bange? au umesahu kumeza dawa zako za Mirembe? Hata kama umetumwa wangetafuta mtu makini anaejua kujenga hoja japo majinga manne hivi yatakuelewa!
 
Wachangiaji wote waliochangia huu Uzi chuki na roho za kwanini zimewajaa,
 
Hhhaahaah anaweza kuwa rais wa chama cha wavuvi Kibirizi au rais wa body ya Mawese labda
 
Raisi ajaye anamjua Mungu!!, Labda tungekuwa tunakaribia uchaguzi ndio mada kama hizi zitolewe. Tujaribu kwenda extra mile sio kukurupuka kutoa mada, au ndio kujipendekeza, acha hizo.
 
sitapiga kura tena!

Nami narudia tena sitopiga kura tena kama tume ya uchaguzi haitokuwa huru ikajisimamia yenye.
Tume inayoongozwa na chama kimoja ni sawa na nchi kuotokuwa na vyama vingi.
Siwezi ni kaungua juani nakwenda kusindikiza waliokwesha teuliwa sio waliochaguliwa.
 
zitto ni mwanasiasa alietimia na mtu mwenye upeo kuliko mtu yoyote katika kile chama alichokijenga wakamfitini
Ndiyo maana Rais kawaambia muache kucheza pool mkalime, sasa mmeacha pool mmehamia humu.mnasheeeda
 
Labda Rais wa Kigoma Tanzania haiwezi kuongozwa na mpenda sifa Zitto by the way hivi chama chake kina wabunge wangapi labda tuanzie hapo.
Chama chake kina mbunge mmoja kama kile cha UKAWA cha Mbatia.
 
Back
Top Bottom