Zitto Kabwe: Msimlinganishe Bernard Membe na Edward Lowassa

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,196
2,000
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amewataka Wananchi kuondoa wasiwasi juu ya Bernard Membe endapo akipokelewa na kupewa nafasi kugombea Urais ndani ya Vyama vya Upinzani.

Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema upinzani kumpokea Membe wakati huu siyo sawa na kilichofanyika mwaka 2015 kwani Bernard Membe hajagombea Urais ndani ya CCM na kukatwa bali Bernard Membe amefukuzwa.

Pia amesema kuhusu uwezekano wa kumpokea Membe ndani ya ACT Wazalendo amesema hilo siyo suala la ACT peke yake bali ni swala la upinzani kwa ujumla. Na kwamba atatakiwa kushindanishwa na Wagombea wengine wa upinzani ambao wametia nia ya kugombea Urais.

Akizungumzia kuhusu kauli ya ofisi msajili wa vyama vya siasa kuwa upinzani umechelewa kuungana amesema upinzani bado upo ndani ya muda bado hawajachelewa kuungana. Kwa mujibu wa Zitto Kabwe sheria ya vyama vya siasa inasema vyama vinatakiwa kuungana miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Kwa maana hiyo kama uchaguzi ni mwishoni mwa oktoba bado muda upo.

Kuhusu kuwepo mkakati wa vyama vya upinzani kuungana Mheshimiwa Zitto Kabwe amewataka wananchi kuwa na subira muda ukifika watajulishwa. 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,957
2,000
"Syllogism" ya kishikaji 🤣 🤣 🤣 🤣
Major sttement: Membe---: Baada ya kufukuzwa kwa kuonyesha nia ya kugombea Urais kumpinga Mkulu akiwa na ushawishi mkubwa

Minor statement: Lowasa----: Baada ya kukatwa kugombea urais akiwa ameshinda kura za maoni

Conclusion: Cause and effect the same for both!
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
6,636
2,000
wanasiasa wana tabia za kimalaya hawana msimamo bahati nzuri tunaopiga kura ni sisi tunawajua vizuri wote wanafanana kitu kimoja wanakuja upinzani si kwa sababu wanapenda mageuzi bali waliamini kuwa wanastahili kuwa marais wa Tanzania na kwa sababu wapinzani wenyewe akili zao kama za kina Zitto wanajithidi kuwapamba waoneka wanamageuzi.

Zitto alikuwa anadai muda mrefu anataka kuwa mgombea urais kinachomzuia sasa hivi ni nini wakati umri unamruhusu au kwa sababu kipindi kile alikuwa anatumiwa kuvuruga upinzani?
 

Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,317
2,000
Kama Lowasa tu, Membe hawezi kukubali hayo mambo ya kwenda kushindanishwa tena na watia nia wa kwenye hivyo vyama vyenu! Never.

Uwezekano wa kushindwa ni 100% akishindanishwa na Lissu (kama hakutakuwepo maelekezo kutoka juu lakini) na Membe hawezi kukubali hiyo fedheha ya kuwa reject hadi huko!

Isitoshe tu Zitto anapaswa atambue wenzie walishafunga pazia la kutia nia urais toka June 15.
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
5,770
2,000
Binafsi mimi siungi mkono Membe kugombea urais kwa tiketi ya upinzani. Tujifunze kwa watangulizi wake. Sio watu waaminifu wenye mapenzi mema kwa Upinzani. Ni wabinafsi. Membe anaweza kuwa mbaya hata kuliko Lowasa na Sumaye.. Wapinzani wekeni mlio anza nao harakati..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom