Zitto Kabwe: Msimlinganishe Bernard Membe na Edward Lowassa

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amewataka Wananchi kuondoa wasiwasi juu ya Bernard Membe endapo akipokelewa na kupewa nafasi kugombea Urais ndani ya Vyama vya Upinzani.

Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema upinzani kumpokea Membe wakati huu siyo sawa na kilichofanyika mwaka 2015 kwani Bernard Membe hajagombea Urais ndani ya CCM na kukatwa bali Bernard Membe amefukuzwa.

Pia amesema kuhusu uwezekano wa kumpokea Membe ndani ya ACT Wazalendo amesema hilo siyo suala la ACT peke yake bali ni swala la upinzani kwa ujumla. Na kwamba atatakiwa kushindanishwa na Wagombea wengine wa upinzani ambao wametia nia ya kugombea Urais.

Akizungumzia kuhusu kauli ya ofisi msajili wa vyama vya siasa kuwa upinzani umechelewa kuungana amesema upinzani bado upo ndani ya muda bado hawajachelewa kuungana. Kwa mujibu wa Zitto Kabwe sheria ya vyama vya siasa inasema vyama vinatakiwa kuungana miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Kwa maana hiyo kama uchaguzi ni mwishoni mwa oktoba bado muda upo.

Kuhusu kuwepo mkakati wa vyama vya upinzani kuungana Mheshimiwa Zitto Kabwe amewataka wananchi kuwa na subira muda ukifika watajulishwa.




Huu ni muda wa waache wafu wazike wafu wao,Chadema isimame yenyewe,hakuna kuachiana jimbo wala kuungana.😃.
 
Hivi Zitto aliwahi kusema juu ya Membe kuitelekeza nafasi ya kugombea urais?
 
Back
Top Bottom