Katika hili tafakuri yangu ipo hivi:
1. Membe hana ushawishi mkubwa, na hawezi kuusaidia upinzani kwa kiwango kikubwa kufikia athari chanya zilizoletwa na Lowasa, ikiwemo kuongezeka kwa kura za upinzani na hadi kupata wabunge. Hili hata Zitto Kabwe na Maalim Seif wanalifahamu.
2. Malengo ya ACT-Wazalendo katika uchaguzi huu sio kuchukua dola, ni kupata wabunge wengi. kwa hiyo, wakimpata Membe anaweza akawasaidia kuongeza wabunge hasa ukanda wa kusini anakotokea.
3. Kwa kuwa ACT-Wazalendo wanataka wabunge tu, wako radhi kushawishi Membe apewe nafasi ya kugombea urais wakijua kuwa hawezi kupata, lakini akawasaidia kupata wabunge wengi.
Nini cha kufanya?
4. Kama Membe anataka ajiunge na upinzani kweli, basi aje bila sharti hilo la kutaka agombee urais kwa sababu ataharibu saikolojia ya wapiga kura ambao wamejipanga kupigia kura mtu ambaye wanaamini kabisa ana roho ya upinzani piga ua! Wapiga kura walioko upinzani na CCM ambao wameamua mpaka sasa kumpigia mtu mwingine, lakini sio Magufuli wanatamani kumpigia kura mtu mwenye kumudu vilivyo Magufuli jukwaani na nje ya jukwaa, kama vyombo vya dola vinawekwa kando, na huyo hawezi kuwa Membe.
5. ACT-Wazalendo waachane na mtazamo kwamba Membe anaeza kuwasaidia kupata wabunge wengi, bali wajisimamie wenyewe kwa kuwatumia akina Bwege na watu mashuhuri ndani ya CCM ambao kiroho hawapo pamoja na CCM katika kupata Rais 2020, ambao ni wengi tu huko kusini kwenyewe ambako ni target yao.
6. Kama Zitto atalazimisha, kama inavyoonekana, kumvuta Membe kwa ahadi ya urais ataharibu kwa sababu ataanza kuandaa mapema utengano wa wapinzani ambao wameanza kuaminika kuelekea uchaguzi, yaani ACT-Wazalendo na Chadema.
lakini kubwa la mwisho katika ninachokiona sasa, na ambacho kinapaswa kutopuuzwa ni kwamba: Zitto ana historia ya kutumiwa na TISS, hivyo tusipuuze mtazamo kwamba Membe na Zitto wanaweza kushirikiana kupunguza threat kwa CCM. lazima mjue kuwa tofauti na wengi wanavyojidai, ukweli ni kwamba this time CCM kina wakati mgumu sana kuelekea uchaguzi mkuu. Hizo mbwembwe zinazoonyeshwa ni za nje tu ambazo ni sehemu ya propaganda, lakini anguko lake linaweza kuwa mwaka huu kupitia sanduku la kura!