Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?

Fanya uchambuzi wa mada na utoe maoni yako, acha kumshambulia mtoa mada..........
 
Ndio maana watu wa kigoma wanapigwa Vita Sana kuliko watu wengine woote was mipka ya tz, hawa watu ni vichwa Sana , wanauwezo mkubwa was kufikiria na ni hatari kwa taifa letu , wanaweza kututawala
 
Ili haya uliyoyaandika yafanyike, inabidi kuwe na DIRA ya Taifa, kwa maana ya wapinzani na chama tawala na wadau wengine kajadili ilani za vyama vyote na baadae izalishwe DIRA Taifa ambayo itafuatwa na Rais wa chama chochote kitakachoshika hatamu.............

Ila siyo kwa mwendo huu wa kuendesha nchi kama mtu anavyoendesha familia yake...........
 
Ndio maana watu wa kigoma wanapigwa Vita Sana kuliko watu wengine woote was mipka ya tz, hawa watu ni vichwa Sana , wanauwezo mkubwa was kufikiria na ni hatari kwa taifa letu , wanaweza kututawala

Unaogopa kutawaliwa na Mtanzania mwenzako? au siyo waTZ hao jamaa........?Sasahivi utawaliwi?
 
NingefanyaTofauti

Na Zitto Kabwe

KWA miaka mingi nimekuwa mtu ninayeamini katika kujipa muda wa upweke na kutazama dunia iliyonizunguka na kujiuliza maswali ama kunihusu mimi binafsi au kuhusu nchi yangu na Afrika. Waingereza wangesema self reflection lakini ninapenda kutumia neno la lugha ya Kiswahili; kutafakari. Ninaamini kwamba ni muhimu kwa kiongozi kupata muda huu muhimu.

Siku chache zilizopita, nilijipa muda huo wa utulivu kwa ajili ya tafakari. Swali kuu nililokuwa nikijiuliza ni hili; kwamba kama ningekuwa nimepewa mamlaka ya kuongoza Tanzania nini ningefanya tofauti na wanaoongoza sasa?

Katika tafakari hii nilikumbuka safari niliyofanya wilayani Ludewa mwaka 2011 kukagua na kutoa nguvu kwa uwekezaji wa kimkakati wa uchimbaji wa madini ya chuma na makaa ya mawe na kuweka msingi wa viwanda mama nchini kwetu. Unaweza soma chapisho la blogu ya safari hiyo hapa An Eye Opener Week-long Visit to South Tanzania 1500MW Electricity Complex. Nadhani ningeanza na mradi huu kabla ya kitu kingine chochote. Nina sababu za kufikia hitimisho hilo.

Mchuchuma na Liganga ni nini?

Madini ya chuma na makaa ya mawe ndio msingi wa maendeleo ya viwanda duniani kote. Nchi yetu ina madini haya yote kwenye eneo moja, wilayani Ludewa mkoa wa Njombe. Hakika Mungu alitupenda, maana aliumba dunia na akaisanifu Ludewa na kuiweka Tanzania ili iwe chanzo cha viwanda mama.

Katika eneo la Mchuchuma kuna mashapo yenye tani bilioni 1.2 makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha Umeme 600MW kwa miaka 150. Makaa hayo pia hutumika kuyeyusha chuma na kuzalisha chuma cha pua. Vilevile eneo la Liganga lina mashapo ya madini ya chuma tani bilioni mbili ambayo ndani yake kuna madini yenye thamani kubwa ya Titanium na Vanadium.

Ujenzi wa kilometa moja ya reli unahitaji chuma cha pua (steel) chenye ubora wa hali ya juu kiasi cha tani 40 mpaka 60. Tanzania tunajenga kilomita 1200 za reli kwa sasa hivi na baadaye zitaongezeka kwa vipande vya Tabora - Kigoma, Kaliua - Mpanda - Karema, Uvinza - Musongati na miradi mingine kama Mtwara - Mbamba Bay, Ruvu - Tanga, Tanga - Musoma - Kigali nk. Kwahiyo basi, Tanzania itahitaji sio chini ya tani 500,000 za chuma cha pua (steel) katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Afrika nzima inajenga reli za kisasa na zote zinahitaji chuma kwa ajili ya kujenga njia za reli. Kenya na Ethiopia wamemaliza hatua za kwanza za reli zao ambapo Kenya imeshajenga kilometa 485 kutoka Mombasa mpaka Nairobi na Ethiopia kilometa 760 kutoka Addis Ababa mpaka Djibouti. Miradi yote hii mataruma ya reli yameagizwa kutoka nje na kuletwa Afrika na hivyo kuzalisha ajira huko kwenye nchi hizo (ambazo mataruma hayo yamezalishwa ).

Fedha za miradi hii zitakwenda nje ya nchi, Waafrika hawatafaidika kabisa. Tanzania nayo inakwenda njia hiyo hiyo licha ya kwamba ina madini ya chuma na makaa ya mawe ya kuzalisha chuma cha pua ambacho huzalisha mataruma ya reli na bidhaa nyingine kadha wa kadha za ujenzi wa reli. Tanzania ingeamua, ingeweza kulisha miradi yote ya reli chuma kutoka Ludewa katika nchi za Kongo, Zambia, Angola, Uganda na Rwanda ambao wote wana miradi ya ujenzi wa reli na wamepanga kuagiza chuma kutoka China na kwingineko.

Bei ya tani moja ya chuma kwenye soko la dunia ni dola za Marekani 600 mpaka 1000. Kwa hiyo Tanzania ikizalisha chuma tani milioni moja tu kwa mwaka, inaweza kupata mapato ya fedha za kigeni kati ya dola milioni 600 mpaka dola bilioni moja kwa mwaka. Kwa mashapo yaliyopo Tanzania, tunaweza kuzalisha kiwango hicho cha chuma kwa miaka zaidi ya 2000 na chuma cha Ludewa kisiishe.

Kwa hakika mahitaji ya chuma yatakuwa ni makubwa na tunaweza kuzalisha na kuuza nje mpaka tani milioni tano kwa mwaka. Hivi sasa nchi ya Australia ndio inaongoza duniani kwa kuuza chuma kingi zaidi. Mwaka 2017 waliuza tani milioni 49 za chuma na kupata dola za marekani bilioni 49.

Jambo kubwa sana ambalo Tanzania imebahatika ni kwamba mashapo ya chuma yana madini mengine yenye thamani kubwa zaidi. Kwa mfano Vanadium ya Ludewa inauzwa tani moja dola 50,000 katika soko la dunia. Katika kila tani milioni moja ya chuma kutoka Ludewa, kuna tani 80,000 ya Vanadium. Tukiuza madini haya tunapata fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni nne kwa mwaka.

[HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]

Unapokuwa na mamlaka ya uongozi wa nchi unakumbana na changamoto nyingi sana na moja ya changamoto ni kuamua uanze na nini katika vipaumbele vya nchi ili kupiga hatua za kimaendeleo. Kiongozi mwenye maarifa huanza na mambo ambayo yatamwezesha kupata rasilimali fedha ili atekeleze majukumu mengine. Ni dhahiri hapa Tanzania tuna changamoto ya miundombinu ya usafirishaji, reli, barabara na hata usafiri wa anga.

Viongozi wetu wa sasa wameamua kuanza na hayo kwa kutumia fedha za kodi au mikopo ghali yenye riba kubwa kutoka mabenki ya biashara ya nje. Wameanza na ujenzi wa reli wa dola bilioni saba, ununuzi wa ndege wa zaidi ya dola bilioni moja ( Dreamliner ‘Terrible Teen’) imenunuliwa kwa dola milioni 224 na hata ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Rufiji maarufu kwa jina la Stiglers Gorge litakalogharimu dola bilioni 3.5.

Yote haya yanahitaji kukamua kodi wananchi na kuchukua mikopo inayokuza Deni la Taifa. Yote haya yanasababisha mzunguko wa fedha nchini kuwa mdogo kwa sababu fedha zinatoka nje ya nchi kulipia wakandarasi na kununua malighafi kama chuma.

Ningekuwa na mamlaka ningeyafanya haya yote, lakini kabla ya kufanya hayo, ningeanza kwanza kwa kufanya jambo moja kubwa ambalo lingenipa fedha za kufanya hayo. Ningefanya tofauti.

Ningeanza na mradi wa Mchuchuma na Liganga kwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unaanza mara moja na uzalishaji wa chuma na makaa ya mawe unafanyika bila kuchelewa. Ningehakikisha kuwa ndani ya miaka 2 tunaanza uzalishaji wa chuma, Vanadium na Titanium.

Mauzo ya Vanadium peke yake ni sawa na dola bilioni nne kwa mwaka ambapo kwa kuwa haya ni bidhaa ambatana na chuma maana yake 80% ya mapato haya yangekuwa ya nchi. Kwa hiyo mwaka wa kwanza tu wa uzalishaji ningeweza kupata dola bilioni 3.2. Kwa fedha hizo, tungejenga reli kuanzia Dar mpaka Dodoma kwa mara moja bila kuungaunga na kubakia na chenji ya dola bilioni moja ambazo ningeweza kujenga hospitali tano kubwa kama Mloganzila katika kanda tano za nchi; Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma na Arusha.

Ningeweza kujenga vyuo vya VETA kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini ( Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji ) kwani unahitaji shilingi bilioni 750 tu kujenga vyuo hivyo vilivyokamili na vifaa vya kutosha vijana kupata mafunzo.

Ningeweza kujenga vyuo vikuu vipya vitatu aina ya UDOM kwani UDOM moja ina thamani ya shs bilioni 800 tu. Haya ni mapato ya mwaka wa kwanza tu. Kumbuka kuwa tunaweza kuendelea kuchimba chuma tani milioni moja kwa mwaka kwa miaka 2000!

Tungeamua kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka maana yake mapato ya Vanadium peke yake kwa mwaka yangekuwa dola bilioni 16 ambazo ni sawa na kumaliza reli yote mpaka Kigoma na Mwanza na kuiwezesha Air Tanzania kuwa na ndege kubwa na ndogo sawa na Shirika la Ndege la Ethiopia na hata kuzalisha umeme zaidi ya 10,000MW ndani ya miaka mitano kwa kutumia makaa ya mawe, geo thermo, gesi asilia, upepo na jua – yote hayo bila kuathiri hifadhi ya Selous.

Kwa kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka tungezalisha chuma, Vanadium na Titanium kwa miaka 400 mpaka kumaliza mashapo yote tuliyonayo. Kwanini hatuwekezi Mchuchuma na Liganga?

Kungoza nchi kunahitaji MAARIFA. Hakika [HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]
Aise duuu .hakika tunaangamia kwa kukosa maarifa .sijui wahusika wataona huu ushauri waufanyie kazi ??
 
Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?
Yaani kweli !!?? huu ndio mchango wako kahusu wazo zuri hivi.kweli ngombe wa masikini azai na akizaa anakufa .duu [emoji118] [emoji317] [emoji317] [emoji317]
 
Zitto subiri niwe Rais by 2040 nikiingia madarakani nitalifanyia kazi hili wazo lako!-nakumbuka ww ndio uliniii insipire nikasoma uchumi chuo kikuu.
 
Tanania ina miradi mingi yenye kutm ia pesa nyingi,miradi yote baba jesca nataka ikamilike ndani ya muda mfupi-hamna mradi hata moja ambao unaleta fedha ndani miradi yote inatoa pesa nje-wanaomshauri anko magu kwenye maswala ya kiuchumi wamefelin kabisa
 
Kuna kitu nimegundua katika mambo ya uongozi
Ukikaa pembeni unaona kiongozi flani anavyokosea na kuharibu lazima utamuona mjing/mzembe sana maana unaona anafeli kirahisi sana kwa maswala yanayohitaji akili ndogo tu kujiongeza
Lakini kiuhalisia ukipewa hicho kijiti ndipo utakapogundua how complex it is
Pale kila jambo linakuja mezani likisubiri wewe ndio ufanye maamuzi
Hapo unajua fika kila mtu anakuangalia wewe anangoja ukosee tu aite press conference akuchane
Kama huwezi kucalm down na kutumia hekima na busara iamue unaweza ukajikuta unavuruga kila kitu.
Tuwaombee sana hawa viongozi wetu maana wana changamoto nzito ambazo its almost killing them inside
Especially kwa wale wazalendo wa kweli
changamoto nzito zipi? kwanza katika viongozi ambao wangetakiwa wafanye makubwa wakiwa madarakani ni pamoja na viongozi wa Tanzania unafanya vitu huku huna presha kuwa kama ikitokoka madarakani utahukumiwa kufungwa
 
Hivi Zitto yale mabilioni ya pesa za rushwa uliyokuwa unachukua pale CRDB kwa Kimei kwa account tofauti tofauti ulikwishayarudisha? Tuanzie hapo...!!!!
jadili hoja iliyopo mezani acha kuharibu muda wako kuandika ambacho hakuhusiani na hoja
 
changamoto nzito zipi? kwanza katika viongozi ambao wangetakiwa wafanye makubwa wakiwa madarakani ni pamoja na viongozi wa Tanzania unafanya vitu huku huna presha kuwa kama ikitokoka madarakani utahukumiwa kufungwa
Yani issue ni kwamba mambo ni mengi na maamuzo magumu yanatakiwa yafanyike in most cases.
Changamoto ni nyingi hasa
Kutoka kwa mataifa nyonyaji
Kutoka upinzani
Kutoka kwa watendaji wasio waadilifu uliowachagua mwenyewe
Pia kutoka kwa wananchi waliochoshwa na ukali wa maisha
Wote hawa unatakiwa ufanye maamuzi ambayo yatawasatisfy wote maana wote wana influence kwenye ufanisi wa uongozi wako.
Ndomana ukisikia kwamba sheria mbovu or migodi + ardhi vilivyomilikishwa kwa wageni kinyemela
Sio vyote vimefanywa kwa uzembe
Wengine walikubaliana na hayo baada ya kupima conditions walizopewa wakaona ni bora wafanye hivyo kuliko otherwise
Hawaongeagi yote hawa viongozi wetu mengine wanakufa nayo mioyoni for the national interest
 
Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?
Nilitegemea ungempinga kwamba alichoingea ni Uongo mjifunze kujibu hoja
 
vitu hivi ni no brainer kabisa.Huwezi fika mapinduzi ya viwanda bila chuma ni kama ambavyo huwezi fika mapinduzi ya kilimo bila umwagiliaji. Viwanda ambavyo vipuri vyote unaagiza siyo endelevu. Kama jamaa hana kiburi hili suala atalifanyia kazi.
 
NingefanyaTofauti

Na Zitto Kabwe

KWA miaka mingi nimekuwa mtu ninayeamini katika kujipa muda wa upweke na kutazama dunia iliyonizunguka na kujiuliza maswali ama kunihusu mimi binafsi au kuhusu nchi yangu na Afrika. Waingereza wangesema self reflection lakini ninapenda kutumia neno la lugha ya Kiswahili; kutafakari. Ninaamini kwamba ni muhimu kwa kiongozi kupata muda huu muhimu.

Siku chache zilizopita, nilijipa muda huo wa utulivu kwa ajili ya tafakari. Swali kuu nililokuwa nikijiuliza ni hili; kwamba kama ningekuwa nimepewa mamlaka ya kuongoza Tanzania nini ningefanya tofauti na wanaoongoza sasa?

Katika tafakari hii nilikumbuka safari niliyofanya wilayani Ludewa mwaka 2011 kukagua na kutoa nguvu kwa uwekezaji wa kimkakati wa uchimbaji wa madini ya chuma na makaa ya mawe na kuweka msingi wa viwanda mama nchini kwetu. Unaweza soma chapisho la blogu ya safari hiyo hapa An Eye Opener Week-long Visit to South Tanzania 1500MW Electricity Complex. Nadhani ningeanza na mradi huu kabla ya kitu kingine chochote. Nina sababu za kufikia hitimisho hilo.

Mchuchuma na Liganga ni nini?

Madini ya chuma na makaa ya mawe ndio msingi wa maendeleo ya viwanda duniani kote. Nchi yetu ina madini haya yote kwenye eneo moja, wilayani Ludewa mkoa wa Njombe. Hakika Mungu alitupenda, maana aliumba dunia na akaisanifu Ludewa na kuiweka Tanzania ili iwe chanzo cha viwanda mama.

Katika eneo la Mchuchuma kuna mashapo yenye tani bilioni 1.2 makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha Umeme 600MW kwa miaka 150. Makaa hayo pia hutumika kuyeyusha chuma na kuzalisha chuma cha pua. Vilevile eneo la Liganga lina mashapo ya madini ya chuma tani bilioni mbili ambayo ndani yake kuna madini yenye thamani kubwa ya Titanium na Vanadium.

Ujenzi wa kilometa moja ya reli unahitaji chuma cha pua (steel) chenye ubora wa hali ya juu kiasi cha tani 40 mpaka 60. Tanzania tunajenga kilomita 1200 za reli kwa sasa hivi na baadaye zitaongezeka kwa vipande vya Tabora - Kigoma, Kaliua - Mpanda - Karema, Uvinza - Musongati na miradi mingine kama Mtwara - Mbamba Bay, Ruvu - Tanga, Tanga - Musoma - Kigali nk. Kwahiyo basi, Tanzania itahitaji sio chini ya tani 500,000 za chuma cha pua (steel) katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Afrika nzima inajenga reli za kisasa na zote zinahitaji chuma kwa ajili ya kujenga njia za reli. Kenya na Ethiopia wamemaliza hatua za kwanza za reli zao ambapo Kenya imeshajenga kilometa 485 kutoka Mombasa mpaka Nairobi na Ethiopia kilometa 760 kutoka Addis Ababa mpaka Djibouti. Miradi yote hii mataruma ya reli yameagizwa kutoka nje na kuletwa Afrika na hivyo kuzalisha ajira huko kwenye nchi hizo (ambazo mataruma hayo yamezalishwa ).

Fedha za miradi hii zitakwenda nje ya nchi, Waafrika hawatafaidika kabisa. Tanzania nayo inakwenda njia hiyo hiyo licha ya kwamba ina madini ya chuma na makaa ya mawe ya kuzalisha chuma cha pua ambacho huzalisha mataruma ya reli na bidhaa nyingine kadha wa kadha za ujenzi wa reli. Tanzania ingeamua, ingeweza kulisha miradi yote ya reli chuma kutoka Ludewa katika nchi za Kongo, Zambia, Angola, Uganda na Rwanda ambao wote wana miradi ya ujenzi wa reli na wamepanga kuagiza chuma kutoka China na kwingineko.

Bei ya tani moja ya chuma kwenye soko la dunia ni dola za Marekani 600 mpaka 1000. Kwa hiyo Tanzania ikizalisha chuma tani milioni moja tu kwa mwaka, inaweza kupata mapato ya fedha za kigeni kati ya dola milioni 600 mpaka dola bilioni moja kwa mwaka. Kwa mashapo yaliyopo Tanzania, tunaweza kuzalisha kiwango hicho cha chuma kwa miaka zaidi ya 2000 na chuma cha Ludewa kisiishe.

Kwa hakika mahitaji ya chuma yatakuwa ni makubwa na tunaweza kuzalisha na kuuza nje mpaka tani milioni tano kwa mwaka. Hivi sasa nchi ya Australia ndio inaongoza duniani kwa kuuza chuma kingi zaidi. Mwaka 2017 waliuza tani milioni 49 za chuma na kupata dola za marekani bilioni 49.

Jambo kubwa sana ambalo Tanzania imebahatika ni kwamba mashapo ya chuma yana madini mengine yenye thamani kubwa zaidi. Kwa mfano Vanadium ya Ludewa inauzwa tani moja dola 50,000 katika soko la dunia. Katika kila tani milioni moja ya chuma kutoka Ludewa, kuna tani 80,000 ya Vanadium. Tukiuza madini haya tunapata fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni nne kwa mwaka.

[HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]

Unapokuwa na mamlaka ya uongozi wa nchi unakumbana na changamoto nyingi sana na moja ya changamoto ni kuamua uanze na nini katika vipaumbele vya nchi ili kupiga hatua za kimaendeleo. Kiongozi mwenye maarifa huanza na mambo ambayo yatamwezesha kupata rasilimali fedha ili atekeleze majukumu mengine. Ni dhahiri hapa Tanzania tuna changamoto ya miundombinu ya usafirishaji, reli, barabara na hata usafiri wa anga.

Viongozi wetu wa sasa wameamua kuanza na hayo kwa kutumia fedha za kodi au mikopo ghali yenye riba kubwa kutoka mabenki ya biashara ya nje. Wameanza na ujenzi wa reli wa dola bilioni saba, ununuzi wa ndege wa zaidi ya dola bilioni moja ( Dreamliner ‘Terrible Teen’) imenunuliwa kwa dola milioni 224 na hata ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Rufiji maarufu kwa jina la Stiglers Gorge litakalogharimu dola bilioni 3.5.

Yote haya yanahitaji kukamua kodi wananchi na kuchukua mikopo inayokuza Deni la Taifa. Yote haya yanasababisha mzunguko wa fedha nchini kuwa mdogo kwa sababu fedha zinatoka nje ya nchi kulipia wakandarasi na kununua malighafi kama chuma.

Ningekuwa na mamlaka ningeyafanya haya yote, lakini kabla ya kufanya hayo, ningeanza kwanza kwa kufanya jambo moja kubwa ambalo lingenipa fedha za kufanya hayo. Ningefanya tofauti.

Ningeanza na mradi wa Mchuchuma na Liganga kwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unaanza mara moja na uzalishaji wa chuma na makaa ya mawe unafanyika bila kuchelewa. Ningehakikisha kuwa ndani ya miaka 2 tunaanza uzalishaji wa chuma, Vanadium na Titanium.

Mauzo ya Vanadium peke yake ni sawa na dola bilioni nne kwa mwaka ambapo kwa kuwa haya ni bidhaa ambatana na chuma maana yake 80% ya mapato haya yangekuwa ya nchi. Kwa hiyo mwaka wa kwanza tu wa uzalishaji ningeweza kupata dola bilioni 3.2. Kwa fedha hizo, tungejenga reli kuanzia Dar mpaka Dodoma kwa mara moja bila kuungaunga na kubakia na chenji ya dola bilioni moja ambazo ningeweza kujenga hospitali tano kubwa kama Mloganzila katika kanda tano za nchi; Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma na Arusha.

Ningeweza kujenga vyuo vya VETA kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini ( Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji ) kwani unahitaji shilingi bilioni 750 tu kujenga vyuo hivyo vilivyokamili na vifaa vya kutosha vijana kupata mafunzo.

Ningeweza kujenga vyuo vikuu vipya vitatu aina ya UDOM kwani UDOM moja ina thamani ya shs bilioni 800 tu. Haya ni mapato ya mwaka wa kwanza tu. Kumbuka kuwa tunaweza kuendelea kuchimba chuma tani milioni moja kwa mwaka kwa miaka 2000!

Tungeamua kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka maana yake mapato ya Vanadium peke yake kwa mwaka yangekuwa dola bilioni 16 ambazo ni sawa na kumaliza reli yote mpaka Kigoma na Mwanza na kuiwezesha Air Tanzania kuwa na ndege kubwa na ndogo sawa na Shirika la Ndege la Ethiopia na hata kuzalisha umeme zaidi ya 10,000MW ndani ya miaka mitano kwa kutumia makaa ya mawe, geo thermo, gesi asilia, upepo na jua – yote hayo bila kuathiri hifadhi ya Selous.

Kwa kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka tungezalisha chuma, Vanadium na Titanium kwa miaka 400 mpaka kumaliza mashapo yote tuliyonayo. Kwanini hatuwekezi Mchuchuma na Liganga?

Kungoza nchi kunahitaji MAARIFA. Hakika [HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]
Mheshimiwa ungefaa kuwa mshauri wa masuala ya uchumi
 
Yaani Zitto kila kitu wewe unajifanya unajua zaidi. Duh.
 
*Bei ya tani moja ya chuma kwenye soko la dunia ni dola za Marekani 600 mpaka 1000*

Sijaelewa
 
Mkubwa mwenzangu Zitto

Hilo ni jicho la kisiasa, kiuhalisia haliwezekani hata robo. Sayansi ya viwanda haiku kama unavyofikiri na haitakuwa hivyo. Kwanza niseme kitu kimoja ambacho kinaziumiza nchi zinazoendele kuwa ni wanasiasa, waweza waita watawala ili upinzani uonekane hauhusiki, lakini wote ni wale wale na wana lao moja. Mikataba mnayoingia ndo huwa inaharibu kila kitu hata kabla ya uzalishaji wenyewe. Mbaya Zaidi huwa mnafanya makusudi kwa kujua asilimia 100. Mfano mzuri ni nyumba za bei nafuu mlizojenga, sijui unafuu mliangalia watu wa kipato kipi. Hivyo waweza kuta chuma kutoka china kikawa na bei nafuu kuliko chuma cha mchuchuma na liganga, sababu ikiwa ni virushwa wakati wa kuingia mikataba.

Nije kwenye mada:
moja:
Chuma na makaa ya mawe tayari ni viwanda viwili. Mwekezaji haweza wekeza kwenye makaa ya mawe kwa ajili ya kulisha kiwanda kimoja cha chuma pekee, atapata hasara.
Kiwanda cha chuma hakiwezi kujengwa kwa kuangalia soko la reli pekee, ambalo huwa halizidi hata miaka kumi linakuwa limetosheka. Hapo yawezekana ndo anaanza kurudisha faida. Hii na hapo juu ni kwa sababu bei za za makaa ya mawe na chuma huhitaji uzalishaji mkubwa ili kutengeneza faida, ndiyo maana viwanda vingi bongo hutumia vyuma chakavu.

mbili:
Kiwanda cha chuma mchuchuma na liganga hakitakuwa na uwezo wa kuzalisha chuma cha pua (pure iron). Kupata chuma cha pua ni kiwanda kingine tena ambacho kitahitaji uhakika wa soko, (si reli pekee kama hapo juu)
Kiwanda cha chuma cha pua hakitaweza tengeneza mataruma ya reli, nacho kitahitaji soko tena Zaidi ya reli kuweza simika kinu cha kusafisha chuma kuwa PURE IRON.
Huyu wa pure iron hataweza tengeneza mataruma yareli, hivyo hicho ni kiwanda kingine ambacho kinahitaji uhakika wa soko kiweze kusimikwa.

tatu:
Kuna chemikali ambata na spea (reagents and spares) ambazo hatuna kiwanda cha kuzizalisha humu nchini, mwekezaji atahitaji uhakika wa kuzipata kwa bei nafuu na kwa wakati (SUPPLY CHAIN isiyo na longolongo wala rushwa!!)

nne:
Hivyo vyote wakati wa mwanzo vitahitaji wataalamu wa kuja kuwafundisha wazawa ambao huwa ni fly in/fly out katika muda mfupi mfupi

tano:
Ukiangalia mlolongo hapo juu, lazima kimoja kianze kistawi kiweze vutia cha pili yake, hivyo si swala la miaka mitano mtu aje azalishe pure iron baada ya mchuchuma kuanza.
Wa pure iron akianza, wa mataruma naye atachukua muda kupata uhakika wa soko kuanza kuzalisha tena.
Kwa mlolongo huo waweza ona kama una nia ya kujenga reli kwa chuma chako utachukua si chini ya miaka 15 mpaka huo uwezo upatikane.

Kuna mambo mengi, wanasiasa wanasema yaliyofichika, lakini yapo wazi hivyo ni bora kununua chuma na kujenga reli kuliko kusubiri viwanda ambavyo huna uhakika vitakamilika lini, hili la kusubiri laweza kuwa chanzo cha kuwabembeleza wawekezaji kwa kuwa kuna uhitaji, hivyo wakatupiga kama buzwagi na wengineo

MIMI NINGEFANYA KAMA MAGUFULI NA SERIKALI YAKE !!
 
Baada ya miundombinu na umeme wa kutosha, sheria na sera nzuri, viwanda mama vitafuata kaka. Time will tell.
 
Back
Top Bottom