Zitto Kabwe apewa somo maridhawa Bungeni kuhusu kuilaumu Serikali mbaazi kushuka bei

Nashindwa kuelewa kwanini kila hoja inayotolewa na mheshimiwa zitto inapingwa..!

Kama hiyo issue ya Mbaazi serikali isengepinga moja kwa moja badala yake itafute soko la mbaazi kusudi ziweze kuuzwa kwa bei nzuri kukuza uchumi wa nchi hii?
 
Hili ndio lingekuwa jibu sahihi tungeshaelezwa tangu siku nyingi sana maana ilikuwa rahisi sana kwa serikali kueleza hili.

Hapa tunadanganywa tu.Ni mwendo wa kuhamisha magoli!
Ipo thread tuliowahi kujadili hili labda kama wewe ndio mhamisha magoli
 
Zitto alishajibiwa hapa jamiiforums tangu February/March. Jibu lilikuwa hilohilo, hata ukisoma magazeti ya India, just google kuhusu maazi utakuta jibu ni hilohilo.
Msilazimishe majibu.
 
Nimecheka Sana hayo mambo nzito alishasema kitambo kuwa kulima kwa kutegemea Nchi Fulani pekee kuwauzia bidhaa ni shida sana

Je? Alipokuja waziri mkuu wa india hawakujua kuna siku wataoverproduce

Hata sasa tunawauzia madini wazungu, Siku wakikataa tutamuuzia nani?
 
Nchi ina Vituko hii!hivi wanajua sababu Kwann mbaazi ilizuiliwa kuingia india....angesema basi
Wakulima wana mbaazi mpaka zinawaozea
Subirini zamu ya choroko na dengu sasa....
Mtakuja kujibu blah blah hizo hizo

Ova
Wewe unakula mbaazi? Kama unakula, unanunua kiasi gani cha mbaazi kwa mwezi.

Seriksli Serikali, Serikali kila siku ndiyo kilio chenu! Kwani Serikali ni nani? Mtu analima zao hajui soko, du!
 
Kumbe bungeni kuna vichwa zaidi ya waropokaji kina zitto wasiofanya research..mama kumbe alikuwepo hadi bungeni india siku ya mjadala wa mbaazi..
Kina zito wanataka mbaazi ziuzwe tu nje kisha badae wanarudi wanasema serikali itangaze kuna njaa..kweli hawa wanasiasa uchwara kulikuwa na umuhimu sana wa kuwadhibiti kama magufuli alivyofanya..maana wanawapa sumu sana watanzania
Duh, alikuwepo bungeni India? Au sijakuelewe!!
 
Wewe unakula mbaazi? Kama unakula, unanunua kiasi gani cha mbaazi kwa mwezi.

Seriksli Serikali, Serikali kila siku ndiyo kilio chenu! Kwani Serikali ni nani? Mtu analima zao hajui soko, du!
Unachekesha sana.....Ulitaka mkulima a export mwenyewe hebu fikirisha ubongo wako

Ova
 
Brazil inaongoza kulima kahawa duniani,halafu ndo wanunuzi wakubwa wa kahawa duniani,ccm hawana akili
 
HUYU MAMA KATOA MAJIBU MEPESI SNA.UTAFIKIRI KAWAJIBU WANAFUNZ WA DRS LA PILI.NA WW MTOA MADA UNAKUBALIANA NA HUO UJINGA AU WW NDO HAO WANAFNZ WA DRS LA 2.SUALA LA MBAAZI NI SUALA LA DIPLOMASIA.MAAGENT WA MBAAZ KUNA KITU WAMEFANYIWA NDO MAANA WAKASUSA.

Mbona Na Wewe umekosoa kidarasa la pili
 
Unachekesha sana.....Ulitaka mkulima a export mwenyewe hebu fikirisha ubongo wako

Ova
Ubongo wangu ndio huo, ambao unaamini soko la ndani ndilo soko kuu, kwa kuwa mbaazi ni zao la chakula kwanza.
 
Ubongo wangu ndio huo, ambao unaamini soko la ndani ndilo soko kuu, kwa kuwa mbaazi ni zao la chakula kwanza.
Soko la ndani lingekuwa imara Wakulima wasidodewa na mbaazi huko shambani We unafikiri mkulima anapenda kuozeewa na mbaazi

Ova
 
Yaani inaeachukua zaidi ya miezi miwili kuja na jibu kama hili.

No wonder maswali magumu kama ya Lissu wasiojulikana ndiyo wanajibu!!
 
Back
Top Bottom