Zitto Kabwe apewa somo maridhawa Bungeni kuhusu kuilaumu Serikali mbaazi kushuka bei

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ambaye alikuwa akiilaumu serikali kuhusu mbaazi kushuka bei, amepewa somo na wa CCM kuhusu suala hilo

Mbunge huyo amesema kushuka kwa mbaazi haifai kulaumiwa serikali kwa kuwa India wenyewe ndio waliamua nchi yao isiingize mbaazi kutoka nchi nyingine kwa kuwa wakulima wa mbaazi wa nchi hiyo wanakosa soko, na ndipo ikapiga marufuku mbaazi kutoka nchi za nje na Malawi na Tanzania kuathirika

Kumbe bungeni kuna vichwa zaidi ya waropokaji kina zitto wasiofanya research..mama kumbe alikuwepo hadi bungeni india siku ya mjadala wa mbaazi..
Kina zito wanataka mbaazi ziuzwe tu nje kisha badae wanarudi wanasema serikali itangaze kuna njaa..kweli hawa wanasiasa uchwara kulikuwa na umuhimu sana wa kuwadhibiti kama magufuli alivyofanya..maana wanawapa sumu sana watanzania
 
Nchi ina Vituko hii!hivi wanajua sababu Kwann mbaazi ilizuiliwa kuingia india....angesema basi
Wakulima wana mbaazi mpaka zinawaozea
Subirini zamu ya choroko na dengu sasa....
Mtakuja kujibu blah blah hizo hizo

Ova
 
Zito alizungumzia Diplomacy Bussiness ichukue mkondo wake ila huyo mama naona kajikita kwenye sababu za kuanguka kwa soko la mbaazi ambazo kila mtu anajua.

Zito alikuja na solutions huyu kaja na ujinga tu
Umeshaambiwa wame over produce..sasa diplomacy business inaingiaje?? Yaani wanunue tu hivyo hivyo hata zikiwaozea wanunue tu..
 
Kumbe bungeni kuna vichwa zaidi ya waropokaji kina zitto wasiofanya research..mama kumbe alikuwepo hadi bungeni india siku ya mjadala wa mbaazi..
Kina zito wanataka mbaazi ziuzwe tu nje kisha badae wanarudi wanasema serikali itangaze kuna njaa..kweli hawa wanasiasa uchwara kulikuwa na umuhimu sana wa kuwadhibiti kama magufuli alivyofanya..maana wanawapa sumu sana watanzania
Under hidden ID unaropoka tu hapa, Zitto kichwa kubwa
 
Umeshaambiwa wame over produce..sasa diplomacy business inaingiaje?? Yaani wanunue tu hivyo hivyo hata zikiwaozea wanunue tu..
Hakuna cha ku-overproduce, unaijua India na population yake wewe? Juzi juzi nimetoka mji mmoja unaitwa Gandhinagar katika jimbo la Gujarat watu wanatafuta mbaazi siyo kawaida yaani kwenye masoko yao hazimo! Na kama utazikuta basi ni za kugombania! Tuache propaganda za kijinga!!
 
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ambaye alikuwa akiilaumu serikali kuhusu mbaazi kushuka bei, amepewa somo na wa CCM kuhusu suala hilo

Mbunge huyo amesema kushuka kwa mbaazi haifai kulaumiwa serikali kwa kuwa India wenyewe ndio waliamua nchi yao isiingize mbaazi kutoka nchi nyingine kwa kuwa wakulima wa mbaazi wa nchi hiyo wanakosa soko, na ndipo ikapiga marufuku mbaazi kutoka nchi za nje na Malawi na Tanzania kuathirika

Kwani anayeathirika ni Zitto au wakulima? Serikali imekaa ikitegemea soko moja, utashangaa kujua kuwa India wanauza nje mbaazi zao, serikali isipolaumiwa basi hatuna sababu ya kuwa na mabalozi nje, kazi yao huko si kuonesha wanavyoweza kuvaa suti na kufunga tai. Kuchekelea jibu la ccm ni ujinga ni sawa na kuwakebehi wakulima.
 
Hakuna cha ku-overproduce, unaijua India na population yake wewe? Juzi juzi nimetoka mji mmoja unaitwa Gandhinagar katika jimbo la Gujarat watu wanatafuta mbaazi siyo kawaida yaani kwenye masoko yao hazimo! Na kama utazikuta basi ni za kugombania! Tuache propaganda za kijinga!!
Jamani mwenye namba ya mwijage ampatie yuku mkuu ampe makavu live
 
Back
Top Bottom