Zitto Kabwe ailipua Airtel bungeni dhidi ya TTCL

Zitto Kabwe ailipua Airtel bungeni dhidi ya TTCL

kil akukicha ni ufisad tu. Itafika wakati hata bajeti za nyumbani zichunguzwe na CAG maana hata dada wa kaz ukimtuma nazi ya 700 ananunua ya 500. Du! lini tutashinda katika hili?
 
Mumshupalie na makamba ang'oke sio tibaijuka na muhongo tu, hivi hili shirika linamtaji wa shs ngapi? lipate hasara ya bil 334.48 na bado linaendelea kutoa huduma, hii financhial statement ina walakini mkubwa.

Hii ni hasara kwa miaka karibu kumi inamaana kwa mwaka hasara ilikua karibu bil 30 na kitu hivi kulingana na maelezo ya PAC.
 
Upuuzi mtupu,Zitto anababaisha tu kwani kishawasoma Watz ni mapumbavu na hawana uwezo wa kufikiri,nakumbuka zamani ili upate simu ya TTCL inabidi uhonge milioni moja kwenda mbele kutegemeana na location,unaposema airtel wanaikandamiza ttcl kwenye soko utakuwa umelaanika kama ilivyolaanika TTCL. Ttcl ilikuwa na uwezo wa kuanzisha simu za viganjani hata kabla ya hao kina voda au airtel lakini kutokana rushwa hawakufanya,wacha wayakute na hata wakiachiwa litakufa tu,inashangaza Zitto anavyotetea hayo mashirika bila kuwa mkweli namna gani ilivyokuwa inatesa watu,wakafe mbele huko
 
Shida siyo makampuni ya toka Nje Shida ni sisi Watanzania-Tabia hii ya kuwaacha watendaji kugeuza Taasisi ya Umma kama kamapuni zao binafsi matokeo yake ndiyo haya.

Tatizo liko kwenye uteuzi wao. Wanateuliwa kwa urafiki wao na wanaowateua. Kwa maana nyingine wanawajibika kwa marafiki zao ambao hatujui chanzo cha urafiki huo ni kipi?

Angalia wateule wa Rais walivyo. Majority ni watu hovyo!
 
vipi mkongo wa taifa nao si uko ttcl au?

Mkongo wa taifa ni mali ya serikali, sema TTCL amekabidhiwa kuusimamia, kuufanyia maboresho na matengenezo inapohitajika kwa niaba ya serikali.
Mkongo wa taifa ni moja ya biashara kubwa kwa kuwa kuna bandwidth kubwa inanunuliwa na nchi jirani kama uganda,Rwanda,Burundi,Zambia na Malawi, hivyo kama TTCL akikabidhiwa moja kwa moja hakika itakuani moja ya faida kubwa kwa kampuni hii ya umma
.

PAC..... nawapongeza kutimiza wajibu wenu kuinusuru kampuni hii wa umma. lkn msiishie hapo, ubinafshishwaji wake ulikuwa ni wa wiziwizi tu chunguzeni hilo pia,hiyo aitel ikijulikana kama celtel chini ya mwenyekiti OMARI ISSA (mtu hatari sana) ni mali ya TTCL 100% lkjn ufisadi uliofanyika kuibabandua TTCL na kuwa kampuni mwenza na hapo ndipo ulipoanza uhuni wa kuifunga miguu TTCL isifanye lolote ,na ile simu 2000 ambayo mwenyekiti wake alikuwa mtoto wa Anna Mkapa , ambaye alimgawia mama yake mali kadha za TTCL nalo lichunguzwe pia. utiaji saini wake ambao ulikataliwa na mwenyekiti wa bodi wakati huo mzee LUHANGA BAADA YA KUKATA USHAULI WAKE AKAAMUA KUACHIA NGAZI, uchunguzwe pia, mhe Sumaye waziri mkuu wakati huo, Martin Lumbaka katibu mkuu ofisi ya rais, MHE Marck Mwandosya waziri wa mawasiliano wakati huo. Bw A Chenge (mzee wa dili kubwa) hawa woote wanahusika kuifikisha hapa kampuni hii, natamani tungelikuwa na sheria kama za China.
Mkuu nashukuru sana umelileta hili hapa leo maana Watanzania tuna akili ya kusahau sana sijui kwa sababu hatunywi mafuta ya samaki? Yaani kila kitu kina muda wake ukipita tu, ni historia ilopotea!
 
kil akukicha ni ufisad tu. Itafika wakati hata bajeti za nyumbani zichunguzwe na CAG maana hata dada wa kaz ukimtuma nazi ya 700 ananunua ya 500. Du! lini tutashinda katika hili?

haahaaha we kabyemera hata proff maro akikupa maksi ya haki unatamani ukate rufaa kwa ndumbaro uongezewe.pia
just kiding
 
Back to TTCL, pamoja na kwamba tunatakiwa kumlaumu sana Ben Mkapa na watu wake kwa uamuzi wake mbovu wa kuiua TTCL but management ya TTCL nayo inastahili lawama, wengi humu jamvini nadhani mtakua hamfahamu kua TTCL nayo ina simu za mkononi zinazo anzia na namba hi 073--, kwanini, sababu kwanza wala hutaona matangazo ya biashara either kwenye TV, Radio au magazetini, hilo moja lakini pia, hizo simu zao wanakulazimisha lazima uende ofisini kwao ukanunue line pamoja na hand set, kwenye hu ulimwengu wa kisasa ambao kila kitu kinafanywa na wakala kweli? Tena basi, line zao hazisomi kwenye simu zingine kama Nokia, Sumsang, Tecno n.k, ni lazima iwe Huewei tu, tena ile ulionunua kwao! Hu ni uzembe wa ajabu sana, naomba hili management waliangalie sana.

Mkuu baada ya miezi mitatu kuanzia sasa hayo uliyoyaeleza ambayo ni kweli kwa 100℅ yatakuwa ni historia. Uwekezaji wa mabilioni unaendelea hivi sasa ili kuhama kutoka kwenye CDMA iliyosababisha kero za kununua sim kwenye ofisi za TTCL tu na sasa watahamia GSM ambapo utanunua simu na line popote pale.

TTCL ilikuwa inaingia hasara maana core business yao ni mawasiliano. Kutokana na kutumia teknolojia ya CDMA ambayo haikuwa option ya TTCL bali ya wakubwa fulani huko kwa wakubwa TTCL ikajikuta inalazimika kufanya biashara ya kuuza simu na line. Kwaiyo ikawa kuna kitengo cha kushughulikia consignments za simu na line. Na supplier pekee akawa Huawei na ZTE. Hata mitambo na billing system ikawa TTCL wanalazimika kuchukua kutoka kwao. Implication yake ni kuwa gharama za kununua hizo simu ikawa kubwa sana supplier wakawa wanainflate price na TTCL ikalazimia ku subsdise ili 'iuze' hizo simu.

Pia gharama za kuzitunza na kuzihifadhi hizo simu ikawa ni mzigo mwingine kwa TTCL. Na kwa sababu ni 'slow moving items' nyingi zikawa zinaharibikia kule main store. Unampelekea mteja simu ambayo tayari imeshaharibika, hakuna mafundi wa kuzitengeneza na hazina spare parts. Kwaiyo TTCL ikajikuta inaingia kwenye shughuli ya kuwa na kitengo cha mafundi wa ku-repair vimeo vya CDMA. Hali ilikuwa mbaya lakini sasa inaelekea kuzuri. Nakuhakikishia ndani ya miezi hii mitatu shida hizo zitakuwa ni historia
 
Ukipata muda au kama una mbunge yeyote wa CCM ambaye ni ndugu yako muulize kwa nini Freeman Mbowe akisimama Bungeni kuzungumza wabunge wote wa pande zote wananyamaza kimya hata kuchati na simu zao wanaacha na kumsikiliza yeye? Jee wanafurahishwa na sauti yake au kuna nini?
Majibu utakayo pata ndio utajua yule ni level ingine kabisa, na kama hutaelewa basi utakuwa huna tofauti na Lusinde wa Mtera. Na kama uko level ya Lusinde basi ni bahati mbaya kuwa member JF

level nyingine kwako wewew kwa kuwa huna tofauti na lema wa arusha
 
Mkongo wa taifa ni mali ya serikali, sema TTCL amekabidhiwa kuusimamia, kuufanyia maboresho na matengenezo inapohitajika kwa niaba ya serikali.
Mkongo wa taifa ni moja ya biashara kubwa kwa kuwa kuna bandwidth kubwa inanunuliwa na nchi jirani kama uganda,Rwanda,Burundi,Zambia na Malawi, hivyo kama TTCL akikabidhiwa moja kwa moja hakika itakuani moja ya faida kubwa kwa kampuni hii ya umma
.

Sasa kama ndo hivyo huu mkongo wa taifa liwe shirika jipya la umma chini ya management mpya kuliko kuutumbukiza kwenye shirika lililotapakaa ufisadi kila kona, nasema hapana mkongo wa taifa kuwa chini ya ttcl tuunde shirika jipya.
 
Usiwe na papara. Serikali haifanyi biashara kwa mafanikio zaidi ya ufujaji mali kupita kiasi mashirika ya umma unadhani ni tanesco peke yake? Yako kibao yaliyokufa au umezaliwa tisini?....sorry for being behind. Tanesco will not last longer either...
Mdau nimekuuliza hapa kama serikali haifanyi biashara TANESCO inafanya nini?au wewe unapewa umeme wa ruzuku?sasa unaleta mambo ya utabiri hapa,
 
Mkongo wa taifa ni mali ya serikali, sema TTCL amekabidhiwa kuusimamia, kuufanyia maboresho na matengenezo inapohitajika kwa niaba ya serikali.
Mkongo wa taifa ni moja ya biashara kubwa kwa kuwa kuna bandwidth kubwa inanunuliwa na nchi jirani kama uganda,Rwanda,Burundi,Zambia na Malawi, hivyo kama TTCL akikabidhiwa moja kwa moja hakika itakuani moja ya faida kubwa kwa kampuni hii ya umma
.

Leo bungeni January Makamba ametamka wazi wazi kuwa wataunda kampuni nyingine ya kuusimamia na kuuendesha mkongo. Eti TTCL na yeye ni mteja wa mkongo kama ilivyo Tigo, voda na Airtel. Sasa TTCL kuu manage sio sawasawa. Ataunda kampuni independent kuu manage. Dah! Tanzania yetu inateketezwa na vijana wadogo kama January kwa kukosa uzalendo ili tu atimize matakwa yake ya kisiasa.
 
Wataunda lini?
After 9years ndo anawaza hayo?what a shame
 
Leo bungeni January Makamba ametamka wazi wazi kuwa wataunda kampuni nyingine ya kuusimamia na kuuendesha mkongo. Eti TTCL na yeye ni mteja wa mkongo kama ilivyo Tigo, voda na Airtel. Sasa TTCL kuu manage sio sawasawa. Ataunda kampuni independent kuu manage. Dah! Tanzania yetu inateketezwa na vijana wadogo kama January kwa kukosa uzalendo ili tu atimize matakwa yake ya kisiasa.

januari kasoma posti zetu hapa JF ndo akakumbuka, ila nampongeza kuwa msikivu
 
Back
Top Bottom