gwijimimi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2011
- 7,344
- 3,623
juzi hapa tumesikia TTCL kaingia mkataba na HUAWEI. Kunani huko TTCL???
Itakua network management pamoja na vifaa
The same to other companies
Eartel Ericson
Voda
Tigi Huawei+ericsson
juzi hapa tumesikia TTCL kaingia mkataba na HUAWEI. Kunani huko TTCL???
bad idea
NHC ni disaster in the making... mark my words
Naomba nieleweshwe, airtel anawezaje kuwa mbia wa TTCL wakati na yeye anafanya biashara hiyo hiyo independently? Mbia gani anaweza kumsaidia mpinzani wake kibiashara afanikiwe?
Serikalii haifanyi biashara zitto aache ubabaishi.Hilo sshirika lina drain resources za nchi should be gone to hell long ago.
labda nikudokeze mkuu, kampuni ya apple ndo most valuable company in then world, kampuni hii ina mshindani mkubwa ambae ni samsung kwa sasa, ila hao hao samsung ndo walikuwa watengenezaji wa processors za apple ambazo zinaitwa A SERIES na ndio zinaifanya simu za apple ziwe faster kuliko hata simu za samsung (iphone are the top selling smartphones mpaka sasa ila chip wananunua samsung kwa mda mrefu sasa kama mbia wao) ***business is complicated, its more than what we study in classes)
Hatimae jioni hii bunge limepata taarifa rasmi ya umiliki wa share za TTCL asilimia 35 by Airtel.
Sasa muda umewadia wa ukweli kujulikana na huyu mnyonyaji kuiacha kampuni hii ya kizalendo, itafahamika kwamba TTCL imekuwa na mazungumzo zaidi ya miaka mitano ya kumtoa mwanahisa huyu bila mafanikio huku akiendelea kuizuia kampuni hii ya kitanzania kutoa huduma zake kiufanisi.
Watanzania tuache unafiki tuungane Airtel aondoke zake. TTCL should be the next NHC
Tusubiri michango ya wabunge.
=====
TAARIFA MAALUM YA KAMATI KUHUSU HALI YA KIFEDHA NA KIUTENDAJI YA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA (TTCL)
Mheshimiwa Spika,tarehe 21 Januari 2015, Kamati ilifanya kikao cha mashauriano kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Msajili wa Hazina, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Menejiment ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Lengo la kikao hicho likiwa ni kutafuta namna bora ya kuikwamua TTCL kutoka katika hali mbaya ya kifedha na kiutendaji ili iweze kuhimili ushindani uliopo katika sekta ya mawasiliano nchini.
Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuelezea hali ya TTCL naomba nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa TTCL ilianzishwa kwa Sheria ya Kampuni ya Simu Tanzania Na. 20 ya mwaka 1993 na kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni Na. 212, tarehe 31 Desemba 1993 baada ya kuvunjwa kwa lililokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania mwaka 1993. Hadi hivi sasa Hisa za TTCL zinamilikiwa na Serikali na Bharti Airtel Tanzania B.V kwa uwiano wa asilimia 65 na asilimia 35 sawia na hivi sasa kuna mazungumzo kati ya Serikali na Bharti Airtel juu ya Serikali kununua hisa asilimia 35 za Bharti Airtel ili imiliki asilimia 100 za TTCL.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa, TTCL ilipata hasara ya Sh. 20.883 bilioni kwa mwaka 2012 na hasara ya Sh. 16.258 bilioni kwa mwaka 2013.
Mheshimiwa Spika, kutokana na TTCL kupata hasara kwa muda mrefu, takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na jumuisho kubwa la hasara ambayo kwa mwaka 2013 imefikia jumla la Sh. 334.48 bilioni. Ukubwa wa hasara hii umeiondolea TTCL mvuto wa kukopeshwa na Taasisi za Fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.
Mheshimiwa Spika, ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Aidha, tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali.
Mheshimiwa Spika, kukosekana kwa fedha za kutosha kuendesha Kampuni kumesababisha TTCL kushindwa kuboresha au kukarabati miundombinu inayoendelea kuchakaa. Hivi sasa karibu asilimia 50 ya miundombinu ya TTCL ni michakavu (obsolete) na inahitaji kubadilishwa na mitambo ya kisasa.
Mheshimiwa Spika, wingi wa hasara ikijumuishwa na uhaba wa uwekezaji umepelekea TTCL kuwa na mtaji hasi wa wanahisa (Negative shareholders Equity) ambapo mpaka kufikia mwaka 2013 TTCL imekuwa na mtaji hasi wa jumla ya Sh.87.896 bilioni. Hii ikitafsiriwa kitaalamu inamaanisha kuwa TTCL ni Kampuni muflisi.
Mheshimiwa Spika, mnamo mwaka 2005 Serikali iliipa TTCL mkopo wa jumla ya Dola za Marekani milioni 28 kwa ajili ya kulipa wafanyakazi waliostaafishwa, deni hilo halijalipwa mpaka sasa na limefikiwa jumla ya Sh. 76.6 bilioni pamoja na riba. Aidha, ukiacha deni hili TTCL inadaiwa na TCRA jumla ya Sh. 25 bilioni hivyo kufanya jumla ya deni kuwa Sh. 101.6 bilioni.
Mheshimiwa Spika, Kamati inaona kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa Kampuni hiyo ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa, ina wafanyakazi ( 1549) wanaotegemea ajira katika Kampuni hiyo na inatoa huduma ya internet kwa makampuni mengine ya simu nchini.
Probably but how?
Wanafanya hivyo na wala hakuna kitu ambacho shule hawafundishi labda alikimbia topic zake za financial management, decision making and business strategy of course with a little bit of creativity needed kutoka kwa graduate.Sio kweli na uache uongo kama hujui kitu usilazimishe kuonekana unajua
Juzi tu Samsung kamlipa apple billions of dollaZ KWA THE SAME CASE (BEING COPY CAT)WE UNAKUJA KULETA UTUMBO WAKO HAPA SIJUI UNADHAN WATU WOTE JF NI MAMBULULA?HV DO U EVEN KNW TECHNOLOGIA YA SIMU IKOJE KWELI?KUANZIA PPROGRAMING LANGUAGE ZAKE MPAKA MFUMO?WHAT A SHAME
BESIDES LETS ASSUME NI KWELI(KITU AMBACH SIOKWELI) HATA UNGEKUA WW UNAWEZAJE KUMTENGENEZEA BIDHAA NZURI MSHINDANI WAKO KULIKO ZAKO MWENYEWE?U CUD HAVE ATLEAST USE UA MIND KABLA YA KUJA KUJATIBU KUTUDANGANYA
DUDE PLZ
Sio kweli na uache uongo kama hujui kitu usilazimishe kuonekana unajua
Juzi tu Samsung kamlipa apple billions of dollaZ KWA THE SAME CASE (BEING COPY CAT)WE UNAKUJA KULETA UTUMBO WAKO HAPA SIJUI UNADHAN WATU WOTE JF NI MAMBULULA?HV DO U EVEN KNW TECHNOLOGIA YA SIMU IKOJE KWELI?KUANZIA PPROGRAMING LANGUAGE ZAKE MPAKA MFUMO?WHAT A SHAME
BESIDES LETS ASSUME NI KWELI(KITU AMBACH SIOKWELI) HATA UNGEKUA WW UNAWEZAJE KUMTENGENEZEA BIDHAA NZURI MSHINDANI WAKO KULIKO ZAKO MWENYEWE?U CUD HAVE ATLEAST USE UA MIND KABLA YA KUJA KUJATIBU KUTUDANGANYA
DUDE PLZ
Serikalii haifanyi biashara zitto aache ubabaishi.Hilo sshirika lina drain resources za nchi should be gone to hell long ago.
Ndio maana kila siku tunasema jamaa sio wabunifu kabisa sana sana subiri uone wakiwa kwenye faida watakavyoanza kudai mishahara na posho za ajabu yote kwa sababu serikari yenyewe aina targets za kibiashara, wao wakiona kitengo chenye faida wanafikiria kodi au wakilambe kama walivyochukua hisa za airtel.Ni jana tu tulikua tunajadiri na mke wangu jinsi ambavyo wafanyakazi wa sekta kadhaa wasivyo wabunifu, mazungumzo yetu yalianzia pale ambapo kipindi cha Dira ya dunia ikiendelea kupitia Star TV, mara matangazo yakakatwa, tokea mambo ya ving'amuzi yaanze, Star TV wamekua hawataki TV yao kuonekana kupitia ving'amuzi vingine isipokua Continental, swali letu likawa hivi; hivi co-business ya Sahara Media ni ipi? uuzaji wa ving'amuzi au TV na Radio? Kwanini azuie ving'amuzi vingine kama Dig Teck, Azam n.k visishike TV yao? Haoni kama anajikomoa mwenyewe? ITV pamoja na kua na king'amuzi chao bado ving'amuzi vingine vinakamata, tena wanakuelekeza wenyewe kabisa kua king'amuzi Fulani ITV inashika No ngapi, kwanini;sababu ni rahisi tu, co-business ya IPP sio biashara ya ving'amuzi bali Television, Radio, magazeti n.k.
Back to TTCL, pamoja na kwamba tunatakiwa kumlaumu sana Ben Mkapa na watu wake kwa uamuzi wake mbovu wa kuiua TTCL but management ya TTCL nayo inastahili lawama, wengi humu jamvini nadhani mtakua hamfahamu kua TTCL nayo ina simu za mkononi zinazo anzia na namba hi 073--, kwanini, sababu kwanza wala hutaona matangazo ya biashara either kwenye TV, Radio au magazetini, hilo moja lakini pia, hizo simu zao wanakulazimisha lazima uende ofisini kwao ukanunue line pamoja na hand set, kwenye hu ulimwengu wa kisasa ambao kila kitu kinafanywa na wakala kweli? Tena basi, line zao hazisomi kwenye simu zingine kama Nokia, Sumsang, Tecno n.k, ni lazima iwe Huewei tu, tena ile ulionunua kwao! Hu ni uzembe wa ajabu sana, naomba hili management waliangalie sana.
Mkuu Mkataba wa juzi kati ya TTCL na HUAWEI ni kwa ajili ya kufufua Network ya TTCL ambayo haikufanyiwa uwekezaji kwa zaidi ya miaka 10.
Hivyo HUAWEI kazi yake ni Kusupply Mitambo mipya na technolojia mpya then analipwa kwa kazi hiyo pekee.Mkataba huo hau-husiana kwa lolote na hisa za TTCL. Hisa hizo zitabaki kua za TTCL.
Mkataba huo hauna tofauti na mikataba ambayo VODA au TIGO wanaingia na HUAWEI/ERICKSON kufanya manunuzi ya mitambo na technology then wanalipana na biashara inaishia hapo wakati hisa na biashara inabaki kuwa ya VODA au TIGO respectivly.
Yes, keep it up Zitto. January Makamba anafanya nini? Iweje shirika linaingia hasara na wanaolisababishia hasara wanaachwa tu humo kazini? Hii nchi ikoje? kila sector ni hasara...why?? Kuna umuhimu ccm kuachia nchi maana inatupeleka pabaya sana.