Zitto Kabwe ailipua Airtel bungeni dhidi ya TTCL

Zitto Kabwe ailipua Airtel bungeni dhidi ya TTCL

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
772
Hatimae jioni hii bunge limepata taarifa rasmi ya umiliki wa share za TTCL asilimia 35 by Airtel.

Sasa muda umewadia wa ukweli kujulikana na huyu mnyonyaji kuiacha kampuni hii ya kizalendo, itafahamika kwamba TTCL imekuwa na mazungumzo zaidi ya miaka mitano ya kumtoa mwanahisa huyu bila mafanikio huku akiendelea kuizuia kampuni hii ya kitanzania kutoa huduma zake kiufanisi.

Watanzania tuache unafiki tuungane Airtel aondoke zake. TTCL should be the next NHC

Tusubiri michango ya wabunge.

=====
TAARIFA MAALUM YA KAMATI KUHUSU HALI YA KIFEDHA NA KIUTENDAJI YA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA (TTCL)

Mheshimiwa Spika,tarehe 21 Januari 2015, Kamati ilifanya kikao cha mashauriano kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Msajili wa Hazina, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Menejiment ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Lengo la kikao hicho likiwa ni kutafuta namna bora ya kuikwamua TTCL kutoka katika hali mbaya ya kifedha na kiutendaji ili iweze kuhimili ushindani uliopo katika sekta ya mawasiliano nchini.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuelezea hali ya TTCL naomba nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa TTCL ilianzishwa kwa Sheria ya Kampuni ya Simu Tanzania Na. 20 ya mwaka 1993 na kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni Na. 212, tarehe 31 Desemba 1993 baada ya kuvunjwa kwa lililokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania mwaka 1993. Hadi hivi sasa Hisa za TTCL zinamilikiwa na Serikali na Bharti Airtel Tanzania B.V kwa uwiano wa asilimia 65 na asilimia 35 sawia na hivi sasa kuna mazungumzo kati ya Serikali na Bharti Airtel juu ya Serikali kununua hisa asilimia 35 za Bharti Airtel ili imiliki asilimia 100 za TTCL.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa, TTCL ilipata hasara ya Sh. 20.883 bilioni kwa mwaka 2012 na hasara ya Sh. 16.258 bilioni kwa mwaka 2013.

Mheshimiwa Spika, kutokana na TTCL kupata hasara kwa muda mrefu, takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na jumuisho kubwa la hasara ambayo kwa mwaka 2013 imefikia jumla la Sh. 334.48 bilioni. Ukubwa wa hasara hii umeiondolea TTCL mvuto wa kukopeshwa na Taasisi za Fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.

Mheshimiwa Spika, ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Aidha, tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali.

Mheshimiwa Spika,
kukosekana kwa fedha za kutosha kuendesha Kampuni kumesababisha TTCL kushindwa kuboresha au kukarabati miundombinu inayoendelea kuchakaa. Hivi sasa karibu asilimia 50 ya miundombinu ya TTCL ni michakavu (obsolete) na inahitaji kubadilishwa na mitambo ya kisasa.

Mheshimiwa Spika, wingi wa hasara ikijumuishwa na uhaba wa uwekezaji umepelekea TTCL kuwa na mtaji hasi wa wanahisa (Negative shareholders Equity) ambapo mpaka kufikia mwaka 2013 TTCL imekuwa na mtaji hasi wa jumla ya Sh.87.896 bilioni. Hii ikitafsiriwa kitaalamu inamaanisha kuwa TTCL ni Kampuni muflisi.

Mheshimiwa Spika, mnamo mwaka 2005 Serikali iliipa TTCL mkopo wa jumla ya Dola za Marekani milioni 28 kwa ajili ya kulipa wafanyakazi waliostaafishwa, deni hilo halijalipwa mpaka sasa na limefikiwa jumla ya Sh. 76.6 bilioni pamoja na riba. Aidha, ukiacha deni hili TTCL inadaiwa na TCRA jumla ya Sh. 25 bilioni hivyo kufanya jumla ya deni kuwa Sh. 101.6 bilioni.

Mheshimiwa Spika,
Kamati inaona kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa Kampuni hiyo ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa, ina wafanyakazi ( 1549) wanaotegemea ajira katika Kampuni hiyo na inatoa huduma ya internet kwa makampuni mengine ya simu nchini.
 
Hatimae jioni hii bunge.limepata taarifa rasmi ya Umiliki wa share za TTCL asilimia 35 by Airtel.
Sasa.muda umewadia wa ukweli kujulikana na huyu mnyonyaji.kuiacha kampuni hii ya.kizalendo...itafahamika kwamba TTCL imekua.na.mazungumzo zaidi ya.miaka mitano ya.kumtoa mwanahisa huyu bila mafanikio huku.akiendelea kuizuia.kampuni hii.ya.kitanzania kutoa.huduma.zake kiufanisi....
Watanzania tuache unafiki tuungane.Airtel aondoke zake....TTCL should be the next NHC
Tusubiri.michango ya wabunge....

bad idea

NHC ni disaster in the making... mark my words
 
Kwahyo tukisha mpokonya hisa ndio basi? Vipi kuhusu gharama ambazo kaziingizia TTCL kipindi chote ambacho aliahidi kuongeza mtaji bila kutimiza ahadi na mbaya zaidi alikuwa anatumia miundombinu ya TTCL kujitengenezea faida.
 
juzi hapa tumesikia TTCL kaingia mkataba na HUAWEI. Kunani huko TTCL???


Mkuu Mkataba wa juzi kati ya TTCL na HUAWEI ni kwa ajili ya kufufua Network ya TTCL ambayo haikufanyiwa uwekezaji kwa zaidi ya miaka 10.
Hivyo HUAWEI kazi yake ni Kusupply Mitambo mipya na technolojia mpya then analipwa kwa kazi hiyo pekee.Mkataba huo hau-husiana kwa lolote na hisa za TTCL. Hisa hizo zitabaki kua za TTCL.

Mkataba huo hauna tofauti na mikataba ambayo VODA au TIGO wanaingia na HUAWEI/ERICKSON kufanya manunuzi ya mitambo na technology then wanalipana na biashara inaishia hapo wakati hisa na biashara inabaki kuwa ya VODA au TIGO respectivly.
 
Kwakweli inashangaza saana jinsi kampuni hizi za nje zinavyoinyonyonya nchi yetu, ukitizama gharama ya kupiga simu Tanzania kutoka nje ya nchi ni karibu zaidi ya mara tatu ya unapopiga Kenya, South Africa na kadhalika.

Hiyo inatoka na gharama kubwa zinatozwa hapa nchini na TTCL kwa makusudi ili kuwanufaisha viongozi wasio na uchungu na nchi hii na hizi kampuni za simu zinaingia ubia usio na faida na nchi yetu.

Hizi kampuni zinajua wazi
 
Hii Nchi hatujifunzi.....hii mikataba ya kinyonyaji tangu nianze kusikia tunazulumiwa mpk Leo ni kama hii Nchi Haina mwenyewe,Kila anayekuja anafanya atakalo na kuacha maumivu na wala hakuna anayejali.
 
Unafahamu maana ya kulipua¿¿.

Hisa za Airtel zilikuwa wazi, kulikuwa hakuna siri yoyote.
 
[h=2]Tanzania Telecommunications Company Limited Key Developments[/h] Tanzania Plans To Buy Back Airtel 35% Stake In TTCL

Dec 14 13

Tanzania's government is planning to buy back 35% stake in Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) from Bharti Airtel Limited (BSE:532454). Tanzanian government tried to enforce an option to buy the stake from Zain, but the price being asked was higher than the government wanted to pay. Kamugisha Kazaura, Chief Executive Officer of TTCL said, “The Guardian noting that the move is intended to look at how the situation economically is in Airtel before buying the shares. The deal does not affect Airtel's mobile network, which it owns a 60% stake in.”


Mhe Zitto kupitia Kamati yenu ya PAC zoezi hili liharakishwa, na share ziuzwe kwa Watanzania ,pamaoja na baadhi ya Taasisi kama hizi Mashirika ya Mafao ya Jamii( NSSF,PPF n.k)
 
Last edited by a moderator:
Kwahyo tukisha mpokonya hisa ndio basi? Vipi kuhusu gharama ambazo kaziingizia TTCL kipindi chote ambacho aliahidi kuongeza mtaji bila kutimiza ahadi na mbaya zaidi alikuwa anatumia miundombinu ya TTCL kujitengenezea faida.

mkuu hakutoa hata senti kuwekeza ttcl kama m bia zaidi anataka alipwe bilioni 21 ili aondoke
 
Back
Top Bottom