Zitto, imetosha sasa

It is hard to let this thread pass. For the love of JF, CDM and Zitto I will sit on the rails and watch.

Gone are the days when Zitto was Daruso Prime Minister (he remains to be the first Daruso PM) and Albert the Speaker.....age has caught with us. And so many things more.

I am all ears and eyes!
I concur with you Mr. Speaker, Msando!
 
Umeongea kwa uchungu sana na naamini mhusika kakuelewa. Ila inaonekana unayafaham mengi kuhusu Zitto ila haujayasema hapa!!??
HUYU NI MWANA MPOTEVU ALIYESAHAU NJIA YA KURUDI KWA BABAYE, HATA TULIE VIPI HATAREJEA HUYU. MAY HE HIS SOUL RIP. He is beyond repair this young man. Believe me people. Nowadays i dont want even to remember that there once was Zitto for he is no more.
 
Jamani mbona nyuma ya pazia kuna mengi. Tufumbueni macho wenzenu ambao ni maamuma
 
CCM 2011 NA MAKAMBI YAKE YAFANANAYO KAMA MAFUTA TAA NA MAJI:

1. CCM- Uadilifu (Wazee wenzake na Mwalimu Nyerere ambao ni watulivu, wakomavu na masikini wa kutupwa kwa kuipenda sana nchi na wenye moyo kuitetea Tanzania).

Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Msuya, Samwel Malechela, Ole Sendeka, Salim Ahmed Salim, Mzee Kisumo, na wengine wachache.

2. CCM- Ufisadi ( Ni kundi dogo linalojiita Wanamtandao au kumbakumba wa kila dili / mchecheto wa kila senti irukayo hewani wenye utayari wa kuuza hata mtoto wake alimradi fedha ipatikane zaidi kufanyia kila aina ya uchafu unaoweza kufikiria; ni wale ambao mpaka hivi sasa wamepepetwana pembeni wasio na kitu na kubakia RA + EL).

3. CCM-Unguja (Chama cha Wazanzibara kama Vuai wa Kondoa na Hussein Mwinyi wa Kisarawe Umatumbini).

4. CCM-Yatima (Ni wale akina Sumaye, Kigoda, Mungai, banduka, Komanya, Ngulume, na wengine waliokua chini ya BWM).

5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli) + Zitto Zuberi Kabwe + Mbunge Kafulia wa Chigoma ...

6. CCM-Mwandosya / Mangula / Mwakyembe / Mwakyusa (Kanda ya Juu Kusini)

7. CCM- Six/John Liquor Ma-Padlocks aka Mzee wa Chato (Kanda ya Ziwa)

8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini) + Lipumba + Cheyo

9. CCM-Uislamu (Pwani/ Tanga / Mashariki na Pemba) + Maalim Seif

Sasa hapa mtu unapoongelea CCM ni sharti uwe makini sana sana na ijulikane kwamba unazungumzia CCM ipi hasa.


Wa-Tanzania tuwatambue viongozi wetu kwa matabaka yao ndani ya CCM pana lakini kubwa zaidi tujihadhari sana tena sana na
CCM kambi ya 2 na ya 5 hapo juu!!!!
 

5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli) + Zitto Zuberi Kabwe + Mbunge Kafulia wa Chigoma ...

sina uhakiaka kama nchimbi hana hela ila ana hisa katika kampuni ya Supper FEO
 
Don't waste your time on this guy, sisi wengine hapa ni marafiki wakubwa wa huyu bwana na ni mwezi December tu mwaka jana tumemkalisha kitako juu ya masuala mengi sana tu na tukakubaliana.

Hivi leo kukifunuliwa chungu alichokifunika Kabwe uvundo utakaofumuka mle hata mama yake mzazi hatoamini kwamba kweli ni yeye tena ndani ya fukuto ambalo safari hii si kwa sauti pinzani ndani ya CHADEMA TU bali hadi dhidi ya vinara wa nndani ya vikundi mbali mbali ndani ya CCM yenyewe.

Huyu mwenzetu ni sikio la kufa eti kaambiwa anapewa uenyekiti wa kamati ili apate fedha za kutosha aje ajitokeze kugombea urais CHADEMA na mwisho kucheza kucheza KAMARI YA KALONZO MUSYOKA WA KENYA kwa kujipenyeza kati na kupewa eti Uwaziri Mkuu huku Lowassa akijimegea urais kwa wao kuunda serikali ya mseto.

Lakini hayo yote si vibya akajibembeleza roho yake kwa kuota ndoto mchana mchana tu, JAMBO LA HATARI ZAIDI HAPA NI UWEPO WAKE KWA MARA NYINGINE kwenye biashara ya KUFIKIRIA KUSHIRIKI KUCHUUZA DAMU YA BAADHI YA SAUTI PINZANI NCHINI (mpaka sasa ni wa 15) na baadhi ya wana-JF tukiwemo.

Zitto, Zitto, Zitto toka huko, Zitto achana na na tabia zako za kusimama mbele ya wanachokipenda umma wa Tanania lakini nyinyi hamipendi. Zitto huwezi kamwe kumfanya Lowassa awe rais kwa janja zozote bila Wa-Tanzania kuridhi kitu hapo.

Zitto ulizaliwa uchi ukaikuta fedha, nguo, magari na nyumba nzuri dunia na siku ya kuondoka kwako ahera hutoenda na chochote. Acha hizo tamaa za Lowassa ambaye tayari anaamini hela zake na za Rostam Aziz ni USAFIRI TOSHA KUFIKIA URAIS hata bila kuhitaji Wana-CCM wenzake.

Na ninasema kwa uchungu kwa taifa la Tanzania linawaangalia kila mlitendalo; Zitto, Makamba na Lowassa tunasema Tanzania inalia, wanyonge tunalia; wazee jamvi sasa tunalikunja!!!
Haya tena vyama vya siasa vya Bongo!! CCM waliwahi kusema kuwa wao ndio Baba wa wapinzani wote na sasa nakubali. Kumbe mna siri humu ndani ya vyama? Vikao vya vyama vinakuwa si suluhisho.

Ushauri wangu kwa CHADEMA: Ni bora huyo Bwanamdogo mwende nae au balaa kwenu!
 
HUYU NI MWANA MPOTEVU ALIYESAHAU NJIA YA KURUDI KWA BABAYE, HATA TULIE VIPI HATAREJEA HUYU. MAY HE HIS SOUL RIP. He is beyond repair this young man. Believe me people. Nowadays i dont want even to remember that there once was Zitto for he is no more.

Pengine upande wa pili wa kesi hii ndio wenye tatizo sio Bwanamdogo.( Ni fikira tu msinishambulie)
 
"Politics is like opium addiction"......the more you take the more you become useless,ask this prince,he knows
 

Attachments

  • Ranariddh+02+%2528PPP%2529.jpg
    Ranariddh+02+%2528PPP%2529.jpg
    33.4 KB · Views: 31
ina maana 2015 kabwe 4 President kwa tiketi ya Cdm au chama kingine? Dr Slaa atagombania tena ubunge au itakuwa ndio siasa hataki tena?
 
Watu mabingwa wa conspiracies.

Yaani mtu akitofautiana na watu katika misimamo huyo anakuwa amenunuliwa. Kuna watu hapa waliwahi kuombwa ushahidi hawakuutoa. Ipo thread ya Waberoya (km sijakosea) pitia na yeye alikuja na conspiracies zake.

Tatizo wengi tunaamini katika kuandamana au kupinga jambo lolote ili tu nchi ikwame na si kwamba tunaamini katika kutafuta ufumbuzi. Kwa hili ninatofautiana na nyie. Hivi kwanini mara zote hatuji na alternatives (mbadala) wa yanayotukwaza zaidi ya kupinga?

Huyo aliyeandika thread hii ukiitazama ni kweli ana uchungu lakini je alitaka kufikisha nini zaidi ya kulalamika? Mbona analalama hasemi Zitto amemkwaza nini? Au hana hoja anaiga tu kulalama?

Tujenge nchi tuache maneno mengi bila kufikiria suluhu ya yale tuyaotayo.
 
Watu mabingwa wa conspiracies.

Yaani mtu akitofautiana na watu katika misimamo huyo anakuwa amenunuliwa. Kuna watu hapa waliwahi kuombwa ushahidi hawakuutoa. Ipo thread ya Waberoya (km sijakosea) pitia na yeye alikuja na conspiracies zake.

Tatizo wengi tunaamini katika kuandamana au kupinga jambo lolote ili tu nchi ikwame na si kwamba tunaamini katika kutafuta ufumbuzi. Kwa hili ninatofautiana na nyie. Hivi kwanini mara zote hatuji na alternatives (mbadala) wa yanayotukwaza zaidi ya kupinga?

Huyo aliyeandika thread hii ukiitazama ni kweli ana uchungu lakini je alitaka kufikisha nini zaidi ya kulalamika? Mbona analalama hasemi Zitto amemkwaza nini? Au hana hoja anaiga tu kulalama?

Tujenge nchi tuache maneno mengi bila kufikiria suluhu ya yale tuyaotayo.
Mkuu siasa nchi hii zilipofika lazima plan B itumike maana hizo njia mbadala zimeshatolewa sana lakini hakuna kinachofanyika.

Kulalamika kupindukia kwa wananchi (sio CDM) ni dalili za kuishiwa uvumilivu. Zitto tunamfahamu vizuri toka kwenye harakati za ubunge wake 2005, si Zitto wa sasa na kivipi imeshajadiliwa sana humu! Hili la nssf linazidi kutoa uelekeo, mfano hali ya umeme ni mbaya zaidi vp kuhusu ule ushauri wake wa kununua DOWANS? Mbona hazungumzii? Hili la NSSF, kwanini NSSF tu!? Na kwanini anatumia nguvu kubwa namna hii hadi kuzua mtafaruku kwa wenye mawazo mbadala kama Mwanakijiji?

Mbona hatumuoni akiweka nguvu kama hizo kwenye maandamano ya chama chake kudai mambo ya msingi na hii utagundua ni issue yoyote itayoibomoa CCM hashiriki na kuimba wimbo mpya wa CCM wa eti njia wanazotumia cdm hazisaidii nchi, yaani CDM wafanye siasa kwa mtindo wataopenda CCM!

Zitto anayo karama ya utendaji lakini anaitumia vibaya na siasa anayofanya sasa si kujenga chama chake kichukue dola bali eti maslahi ya nchi! Maslahi gani bila kuondoa utawala wa miaka 50 ya CCM tukaweka utawala na mifumo mipya? Namheshimu Zitto kwa karama alizo nazo lakini kutosikia kwake kutamuangusha sana na sio kisiasa tu bali hadi maisha binafsi na naomba afunuliwe anguko lake ndotoni ili aokoke!
 
Hivi kwa nini CDM wasimtimue Zitto mapema? Ya nini kukaa na mtu kama huyu ndumilakuwili wa ajabu kabisa.

CDM wajikaze kisabuni wamtimue Zitto, kama ANT-CDM watasema katimuliwa kwa sababu ya dini yake poa with time yatasahaulika.

zitto anaondoa ladha ya cdm kabisa
 
Kwanza kumbukeni huyu ni member mwezetu hapa jamvini, tusimfanye achukie na mwisho ajitoe jamvini...:washing:
Si kwa zama hizi ukifanya vizuri watu wata kusifia ukifanya madudu watu wanatabika tu hakuna cha wanachama mwenzetu bona JK tunampa kubwa!!!!!!!!!!
 
Mmmh kazi kwelikweli,Mungu uliye HAI jidhihirishe kwa kutumia watu wenye nia njema na Tanzania kama ulivyomtumia Daudi kwa Waisraeli toka kwa Sauli.Amen
 
Rafiki Zitto,

Nakuandia ushahuri huu kwa dhati kabisa, una haki ya kuuchukua au kuupuuza.

Nakushauri kwamba kwa jitihada ambazo umekwisha kuzifanya mpaka sasa juu ya N.S.S.F kuuziwa Mgodi wa Kiwira, ni bora ukaishia hapo ulipofikia, umesema ya kutosha, kama kweli ni ushahuri ama wako binafsi ama wakamati yako ya Bunge ni vyema ukawaachia wote unaowashauri waufanyie kazi ushauri wako ama waukatae sababu hili swala litakuchafua zaidi.

Kumbuka kwamba Watanzania wenye nia ya kurejesha ustaarabu katika utawala wa nchi yetu wamekwishapoteza imani na wewe kutokana na actions zako za muda mrefu sasa, lakini kutokana na imani kubwa sana ambayo bado wanayo kwako wanakuchukulia poa hasa kwa imani kwamba Binadamu hatujakamilika na kukosea ni sehemu ya kujifunza hasa mkosaji anapoonyesha jitihada na kisha mafanikio katika kuhakikisha harudii kosa.

Mtazamo wangu ni kwamba, nguvu za mafisadi zinakuzidia nguvu kadri ziku zinavyokwenda, na Imani yangu ni kwamba hawakuzidi nguvu by coincidence bali ni strategically kwa kukutumia, na unawasiliana nao katika hatua zako zote ambazo wewe binafsi naona kama unadhani hiyo nafasi uliyonayo ya uenyekiti wa kamati ya bunge ni kinga tosha ya kusingizia kwamba unafanya kazi za taifa.

Unayo nafasi ya kujirekebisha, japo uwezo huo sidhani kama unao tena, hasa kutokana na uko ulikofikia sasa, umefika deep water my comrade. ZITTO mafisadi wamekuzidia kiasi kwamba sasa hauna nguvu kabisa za kuisonta serikali ukiwa katika spirit ya UMA/CHADEMA, sasa hata ukijitutumua kuisonta serikali unajificha kwenye kamati ya Bunge ya nini sijui!! Sio wewe

Sasa kwa kifupi ni kwamba, N.S.S.F wanayo idara inayojishughulisha na utoaji taarifa kwa UMA, waache wao wenyewe waje (Kama haujatumwa) na kuzungumza nasi ama kwa kutupa taarifa za mpango wao wa kununua Kiwira au kwa Mapendekezo,ila hii deal uliyonayo sasa ya kujustify kwa nini wao wapewe Kiwira mimi ntakuuliza swali, kwa nini wasipewe PPF, kwa nini wasipewe PSPF.Unatakiwa kuwa consistent kama unataka tuendelee kuamini kwamba akili yako bado ni nzuri na unathink Big. Idea nzuri kabisa lakini why do you narrow to NSSF.

Kazi ya Kamati yako ya Bunge sio kuwa maafisa miradi wa Mashirika ya UMA, toa ushauri then stop there, Kama watu wanapewa ushauri mzuri alafu wanaupuuza na wao hawaji na mbadala wa mawazo na matendo shauri waondolewe. Lula MwanaNzela na Mwanakijiji wametoa hoja za msingi kama maoni yao ya kupinga mpango huu na naona tayari Umeanza kupambana nao.

Hapo Nyuma tulimpenda sana Mkwere, Tulimpenda sana Lowasa walipotugeuka na sisi tumewakataa. Wewe sio exceptional

Zitto,

ndugu yangu mi nakupongeza sana kwa kazi zako nzuri sana na zenye nia thabit kwa maslahi ya watanzania na uwezo wako mkubwa wa kuweza kusoma alama za nyakati.

Mkuu endeleza harakati hizo hizo za kutetea maslahi ya wanyonge waliokuchagua na hata kama itawaudhi Chama chako Chadema. Elewa kuwa umechaguliwa na watu na sio Chadema. Mfano mzuri unao wa Rafiki yako Kafulila.
 
Kila hoja za upinzani, kwa dhana ya kuwa ni wapinzani, wakipinga hata mambo mema kwa Taifa, eti kwa kuwa wao ni wapinzani tu, hapo inakuwa upinzani wenye kasoro kubwa sana.

Upinzani upinge yasiyokuwa na manufaa kwa Taifa. Upinzani kupinga NSSF kuwekeza Kiwira, huo upinzani una jema ulitakalo hapo, au ndio fikra finyu kuwa tupinge yaharibike halafu tuseme si mnaona, hawafanyi?

Hoja na vitimbwi vyote vya upinzani vilenge katika kuleta maendeleo na si kubomoa maendeleo.

Mtoa hoja mmoja amesema kama kamati walichopaswa kufanya ni kushauri na hilo wameshalifanya,kilichobaki ni ther part ku-take action pale Zitto anaposhika bango ndipo watu wanapojiuliza kulikoni?au ana maslahi binafsi??ishu siyo kupinga ishu ni wapi boundary ya kamati yake kwenye kutekeleza majukumu yake,na hakuna tatizo wakipewa NSSF lakini swali kwa nini wao tu? tungeweza kuwa tunazungumzia mashirika mawili matatu then mwisho litakalokuwa limekidhi vigezo vyote lipewe!!
 
Huku kwenye Taasisi za mifuko ya Jamii(Social Security Fund) kuna kitu kimejificha sana hiyo ni michango ya watu lakini bado hatuna maamuzi nayo,watu wanajilambia tu wapendavyo .
Ni kama wachangiaji wengine walivyosema Kamati imetoa ushauri,isiwe watekelezaji tena wa ushauri huo kwa kulazimisha na kukejeli ushauri wa wengine
 
Back
Top Bottom