Zitto, imetosha sasa

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
443
86
Rafiki Zitto,

Nakuandia ushahuri huu kwa dhati kabisa, una haki ya kuuchukua au kuupuuza.

Nakushauri kwamba kwa jitihada ambazo umekwisha kuzifanya mpaka sasa juu ya N.S.S.F kuuziwa Mgodi wa Kiwira, ni bora ukaishia hapo ulipofikia, umesema ya kutosha, kama kweli ni ushahuri ama wako binafsi ama wakamati yako ya Bunge ni vyema ukawaachia wote unaowashauri waufanyie kazi ushauri wako ama waukatae sababu hili swala litakuchafua zaidi.

Kumbuka kwamba Watanzania wenye nia ya kurejesha ustaarabu katika utawala wa nchi yetu wamekwishapoteza imani na wewe kutokana na actions zako za muda mrefu sasa, lakini kutokana na imani kubwa sana ambayo bado wanayo kwako wanakuchukulia poa hasa kwa imani kwamba Binadamu hatujakamilika na kukosea ni sehemu ya kujifunza hasa mkosaji anapoonyesha jitihada na kisha mafanikio katika kuhakikisha harudii kosa.

Mtazamo wangu ni kwamba, nguvu za mafisadi zinakuzidia nguvu kadri ziku zinavyokwenda, na Imani yangu ni kwamba hawakuzidi nguvu by coincidence bali ni strategically kwa kukutumia, na unawasiliana nao katika hatua zako zote ambazo wewe binafsi naona kama unadhani hiyo nafasi uliyonayo ya uenyekiti wa kamati ya bunge ni kinga tosha ya kusingizia kwamba unafanya kazi za taifa.

Unayo nafasi ya kujirekebisha, japo uwezo huo sidhani kama unao tena, hasa kutokana na uko ulikofikia sasa, umefika deep water my comrade. ZITTO mafisadi wamekuzidia kiasi kwamba sasa hauna nguvu kabisa za kuisonta serikali ukiwa katika spirit ya UMA/CHADEMA, sasa hata ukijitutumua kuisonta serikali unajificha kwenye kamati ya Bunge ya nini sijui!! Sio wewe

Sasa kwa kifupi ni kwamba, N.S.S.F wanayo idara inayojishughulisha na utoaji taarifa kwa UMA, waache wao wenyewe waje (Kama haujatumwa) na kuzungumza nasi ama kwa kutupa taarifa za mpango wao wa kununua Kiwira au kwa Mapendekezo,ila hii deal uliyonayo sasa ya kujustify kwa nini wao wapewe Kiwira mimi ntakuuliza swali, kwa nini wasipewe PPF, kwa nini wasipewe PSPF.Unatakiwa kuwa consistent kama unataka tuendelee kuamini kwamba akili yako bado ni nzuri na unathink Big. Idea nzuri kabisa lakini why do you narrow to NSSF.

Kazi ya Kamati yako ya Bunge sio kuwa maafisa miradi wa Mashirika ya UMA, toa ushauri then stop there, Kama watu wanapewa ushauri mzuri alafu wanaupuuza na wao hawaji na mbadala wa mawazo na matendo shauri waondolewe. Lula MwanaNzela na Mwanakijiji wametoa hoja za msingi kama maoni yao ya kupinga mpango huu na naona tayari Umeanza kupambana nao.

Hapo Nyuma tulimpenda sana Mkwere, Tulimpenda sana Lowasa walipotugeuka na sisi tumewakataa. Wewe sio exceptional
 
Umemalizia vizuri Mkuu kwenye mistari miwili ya mwisho...!
 
Taifa_ Kwanza ninakubaliana na wewe,

Hapa umesema kitu ambacho watanzania tunapaswa kukikataa, Hawa wenyeviti wa kamati za fedha za bunge inaonekana wanaanza kuhama kutenda majukumu yao waliyopewa na bunge na badala yake wakuwa wanafanya kazi za executives.Hii ni hatari kwa nchi yetu kuwa na wabunge waroho wa madaraka.

Tumeshuhudia hata mwenzake Augustino Lyatonga Mrema ameamrisha kukamatwa kwa afisa wa Halmashauri ya Rombo eti kwa ubadhirifu. Hawa wabunge wetu wamelewa madaraka ifike mahali nao wawajibike kwa kuingilia kazi za serikali.Kwa uelewa wetu mdogo ni kwamba Kamati za bunge zinawajibika kwa bunge na observations zao wanatakiwa kuziwasilisha kwa boss wao ambaye ni bunge. Leo wanaanza kufanya execution ni hatari.

Zitto nyamaza itafika mahali watu tuhoji competence yenu ninyi wenyeviti wa kamati za bunge.

Ni hayo tu
 
Hivi Kiwira kununuliwa na NSSF kuna tatizo lipi? au Kiwira ibaki ikijifia bila mtaji na wapewe wawekezaji wa nje bila ubia na Taasisi au mashirika ya ki Tanzania ndio vyema?

Nawashangaa sana wanaoona kuwa NSSF haipaswi kuwekeza Kiwira.
 
Kila hoja za upinzani, kwa dhana ya kuwa ni wapinzani, wakipinga hata mambo mema kwa Taifa, eti kwa kuwa wao ni wapinzani tu, hapo inakuwa upinzani wenye kasoro kubwa sana.

Upinzani upinge yasiyokuwa na manufaa kwa Taifa. Upinzani kupinga NSSF kuwekeza Kiwira, huo upinzani una jema ulitakalo hapo, au ndio fikra finyu kuwa tupinge yaharibike halafu tuseme si mnaona, hawafanyi?

Hoja na vitimbwi vyote vya upinzani vilenge katika kuleta maendeleo na si kubomoa maendeleo.
 
Napata shida kidogo kujua "boundaries" za majukumu ya kamati za bunge. Niliwahi kuanzisha thread iliyohoji nafasi ya waziri wa nishati na madini, kuwa ni nani kati ya William Ngeleja na January Makamba. Naona kuna mkanganyiko mkubwa sana wa muingiliano wa majukumu kati ya kamati na wizara. Na hii si kwa kamati ya nishati na madini pekee bali ni kwa kamati zote za bunge za msimu huu.

Inaonekana wenyeviti wa kamati na kamati zao kwa ujumla wamekuwa na sauti kubwa kushinda hata mawaziri husika. Tukichukulia kamati ya Zitto kwa mfano, inaitwa kamati ya hesabu za mashirika ya umma. Iweje leo iwe mstari wa mbele katika kuhakikisha ubinafsishwaji wa shirika? Hata kama hilo ni moja ya jukumu lake lakini naamini wanachopaswa ni kutoa ushauri tu na si kurasimisha ushauri wao kuwa matekelezo.

Nadhani Zitto umenisikia.
 
Napata shida kidogo kujua "boundaries" za majukumu ya kamati za bunge. Niliwahi kuanzisha thread iliyohoji nafasi ya waziri wa nishati na madini, kuwa ni nani kati ya William Ngeleja na January Makamba. Naona kuna mkanganyiko mkubwa sana wa muingiliano wa majukumu kati ya kamati na wizara. Na hii si kwa kamati ya nishati na madini pekee bali ni kwa kamati zote za bunge za msimu huu.

Inaonekana wenyeviti wa kamati na kamati zao kwa ujumla wamekuwa na sauti kubwa kushinda hata mawaziri husika. Tukichukulia kamati ya zito kwa mfano, inaitwa kamati ya hesabu za mashirika ya umma. Iweje leo iwe mstari wa mbele katika kuhakikisha ubinafsishwaji wa shirika? Hata kama hilo ni moja ya jukumu lake lakini naamini wanachopaswa ni kutoa ushauri tu na si kurasimisha ushauri wao kuwa matekelezo. Nadhani zito umenisikia.

mkanganyomkubwa
 
Najua hii ilipoanzia!

Ule mchezo wa kulipua jengo la Uwekezaji Nairobi na kufahamisha umma kuhusu mifuko mingine kutaka kutumika. Sasa naona mmeanza kuona NSSF inaelekea kupata faida kubwa na hivyo sifa kwa utawala wake mnaanza kushambulia watu wanaotazama mema ya nchi. Siasa wekeni kando na kamwe cha juu hamtapata kwa kuwa NSSF hatutoi rushwa.

Narudia sisi ni zero corruption zone na Hosseah anajua. Zitto achana na hawa
 
Pengine Zitto amekurupuka kutoa maoni yake, pengine waandishi wa habari walimbana naye kama mtoto mdogo (na ndivyo alivyo) akaingia mtegoni. Lakini sifikirii kuwa kauli ya Zitto ndio amri ya utekelezwaji wa aliyoyasema. Bila ya shaka aliyoyasema Zitto ni msimamo wa kamati yake, lakini yanayotoka katika kamati hayaishii katika utekelezwaji bali hufikishwa bungeni kwa mjadala. Huko kutatoka hoja na ushauri mwengine mpaka kufikiwa suluhisho la maana.

Binafsi napinga uwekezaji wowote (na hapa nampinga Zitto na Kamati yake), kupelekwa kwa mashirika ya umma, iwe NSSF au lolote lile kwani tumeshaona utendaji wao ambapo daima yamekuwa yakiendeshwa kwa hasara na kuwa mzigo kwa wananchi.

Kama mchangiaji tu, nahisi ni bora kuliwacha swali la uwekezaji wa Kiwira lipewe sekta binafsi ambao hawaombi pesa ya Watanzania, wanafanya kazi kwa kutaka faida na siyo kuvimbisha matumbo ya wachache na ufanisi ndio kusudio lao kuu. Wakiboronga, wanaacha ngazi kinyume na mashirika ya umma ambako wakiboronga wanajazwa mapesa waendelee kujaza matumbo yao.
 
Hawa wenyeviti wa kamati za Nishati na Madini (Makamba), mahesabu ya Serikali za Mitaa (Mrema) na mahesabu ya Mashirika ya Umma (Zitto) wanatumiwa tu kufanikisha mambo ya akina Mkwere na Rosti-tamu, pasipo kujali kuwa hao wenyeviti wanakiuka madaraka yao.

Baada ya mawaziri kama Ngeleja husika kuboronga (wakati akifuata maelekezo) kiasi cha kukosa moral credibility, sasa wametumika Januari Makamba na Zitto kujaribu kufanikisha mambo. Ila kwa kuwa nao wanafuata maelekezo kama Ngeleja, baada ya muda mfupi nao wameanza kukosa credibility. Kwishnei!
 
Kwa nini Zitto asipendekeze Tanesco - kampuni yenye wajuzi wa mambo ya umeme ikiwa kampuni ya umma pia - ndiyo ipewe - Kiwira kwa mkopo?
 
Mh Zitto

Zingatia mawazo ya watu unakoelekea siko ebu rudisha akili zako nyuma kuwa kama zitto wa zamani
 
Najua hii ilipoanzia!v Ule mchezo wa kulipua jengo la Uwekezaji Nairobi na kufahamisha umma kuhusu mifuko mingine kutaka kutumika. Sasa naona mmeanza kuona NSSF inaelekea kupata faida kubwa na hivyo sifa kwa utawala wake mnaanza kushambulia watu wanaotazama mema ya nchi. Siasa wekeni kando na kamwe cha juu hamtapata kwa kuwa NSSF hatutoi rushwa. narudia sisi ni zero corruption zone na Hosseah anajua. Zitto achana na hawa
Janja ya nyani unataka kutuaminisha kwamba kamati hii hawajapewa chochote mmh
 
Kawaida ukisifiwa mbio unapitiliza nyumbani Zito wewe ni binadam na nimtu mzima pima ukiona inafaa ongeza uangalifu katika utendaji wako
 
Hivi Kiwira kununuliwa na NSSF kuna tatizo lipi? au Kiwira ibaki ikijifia bila mtaji na wapewe wawekezaji wa nje bila ubia na Taasisi au mashirika ya ki Tanzania ndio vyema?

Nawashangaa sana wanaoona kuwa NSSF haipaswi kuwekeza Kiwira.

Wewe nyamaza kabisaaaaaaaa. NSSF ni pesa za wanachama. Sidhani kama Zitto ni member wa NSSF ataamuaje tu kuwekeza kwenye project yenye mgogoro kama hiyo. Wakati umefika sasa wa kuhoji uhalali wa matumizi ya pesa za mifuko ya pension kwenye uwekezaji usiofaa. Manaake naona wanaamua tu kuwekeza kwenye niradi hovyo hovyo isiyo na faida yoyote kwa sie tunaochangia pesa zetu kila siku.
 
.

Mtazamo wangu ni kwamba, nguvu za mafisadi zinakuzidia nguvu kadri ziku zinavyokwenda, na Imani yangu ni kwamba hawakuzidi nguvu by coincidence bali ni strategically kwa kukutumia, na unawasiliana nao katika hatua zako zote ambazo wewe binafsi naona kama unadhani hiyo nafasi uliyonayo ya uenyekiti wa kamati ya bunge ni kinga tosha ya kusingizia kwamba unafanya kazi za taifa.

HAHAHAHAHAHA. MWACHENI KIJANA MWENZENU
 
Back
Top Bottom