Analyst kweli nimekukubali jinsi ulivyo jaribu kumuonya huyu kijana, lakini waswahili husema sikio la kufa halisikii dawa!!!!!!!Sitaki kukumbusha mambo yaliyopita lakini, uelewe jina lako limekua sana kwa kuwa wananchi wengi tuliamini una nia ya dhati ya kuondoa ufisadi unaokumbatiwa na serikali ya JK.
Siku za karibuni umekuwa unatoa matamko na kufanya vitendo vingi ambavyo vinawashtua wengi wetu na kujikuta wanahoji udhati wako katika kuwahudumia walio wengi na maskini. Sihitaji kukukumbushia maana unayajua na baadhi umeyatolea maelezo japo bado unaendelea kushutumiwa.
Leo nakupa ushauri wangu, tena bure na kukuonya. RA, JK na EL watakutumia sasa hivi na fedha utapata sana tu, kamatini, Bungeni kawaida, nk. Inawezekana ukawa miongoni mwa matajiri wakubwa sana miongoni mwa mafisadi uliopanda ngazi kwa kuwashambulia kama Karamagi na Lowasa. Ninachojaribu kukwambia hapa Kaka, ni kwamba jiangalie sana. TISS wanalinda watawala na si nchi. Ingekuwa nchi ufisadi wote mkubwa usingetokea kwa kuwa wana macho yaliyo-trainiwa kuona na ni wazi waliona lakini, haikuwa issue kwao.
Kubali kataa wewe ni silaha tu kwao. Utatumika leo kudhoofisha chama chako na walalamikaji wengine na mwishowe watakuacha hapo. CCM ilipofikia si wakati wa kina Tambwe, Wasira, Lamwai wala wengine waliofanikiwa kutukana weee na mwishowe wakapokelewa kundini walipoamua kurejea. Wewe kuna baadhi watakukataa maana tayari kuna wanaokuona Mzandiki kwa kujipendekeza kwa Mwenyekiti wao na kumpelekea majungu dhidi yao. Wanakujua na wakipata nguvu kidogo tu dhidi ya RA ujue huna chako.
Haya mambo unayojaribu kuyatetea wakati huu kama mitambo ya DOWANS, Kiwira nk wengi hatuelewi kama ni kweli una nia ya kusaidia kupatikana kwa umeme tu au unahangaikia posho yako na ahadi za RA.
Kama nia yako ni safi namwomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema akubariki sana na ndoto yako ya kuwa rais itimie mapema kuliko unavyotamani. But... kama umenunuliwa kweli (kwa fedha na ahadi) halafu unatumia mbinu hizo ili kuwaumiza wanyonge kwa maslahi yako binafasi kisiasa na kiuchumi, Zitto my Bro. nakwambia utaporomoka vibaya na utaona haya hata kuwasalimia wapiga kura wako.
I am sure (and I pray) Mwenyezi Mungu atakuadhibu kwa nguvu zote pale utakapokuwa umewahadaa wananchi walio wengi tena wanyonge na walioamini utawatetea kwa kuwa tu kuna fedha zaidi katika usaliti huo kuliko kule ulikoanzia.
Jiulize swali, Unadhani kwa fedha za mafisadi pasipo wananchi wanyonge lakini wenye matumaini na wewe Bunge ungeliona? Huoni kama wangepewa T-Shirt zao, kanga na kofia na kukutupilia mbali tangu mwanzo.
Nakuomba sana Zitto, please please jitafiti na ufikirie upya hiyo safari yako. Upande uliochagua ni mgumu kwako kuliko upande wa wanyonge. Amini usiamini utafail wakati you least expect.
Najua hii ilipoanzia!
Ule mchezo wa kulipua jengo la Uwekezaji Nairobi na kufahamisha umma kuhusu mifuko mingine kutaka kutumika. Sasa naona mmeanza kuona NSSF inaelekea kupata faida kubwa na hivyo sifa kwa utawala wake mnaanza kushambulia watu wanaotazama mema ya nchi. Siasa wekeni kando na kamwe cha juu hamtapata kwa kuwa NSSF hatutoi rushwa.
Narudia sisi ni zero corruption zone na Hosseah anajua. Zitto achana na hawa
Mh Zitto
Zingatia mawazo ya watu unakoelekea siko ebu rudisha akili zako nyuma kuwa kama zitto wa zamani
Huyu dogo anataka kutuletea ya Gagbo nini??????? Akaulize huko Ivory Cost watapelekana The Hague!!!!!!!! Mwenye macho haambiwi tazama!!!!!!Don't waste your time on this guy, sisi wengine hapa ni marafiki wakubwa wa huyu bwana na ni mwezi December tu mwaka jana tumemkalisha kitako juu ya masuala mengi sana tu na tukakubaliana.
Hivi leo kukifunuliwa chungu alichokifunika Kabwe uvundo utakaofumuka mle hata mama yake mzazi hatoamini kwamba kweli ni yeye tena ndani ya fukuto ambalo safari hii si kwa sauti pinzani ndani ya CHADEMA TU bali hadi dhidi ya vinara wa nndani ya vikundi mbali mbali ndani ya CCM yenyewe.
Huyu mwenzetu ni sikio la kufa eti kaambiwa anapewa uenyekiti wa kamati ili apate fedha za kutosha aje ajitokeze kugombea urais CHADEMA na mwisho kucheza kucheza KAMARI YA KALONZO MUSYOKA WA KENYA kwa kujipenyeza kati na kupewa eti Uwaziri Mkuu huku Lowassa akijimegea urais kwa wao kuunda serikali ya mseto.
Lakini hayo yote si vibya akajibembeleza roho yake kwa kuota ndoto mchana mchana tu, JAMBO LA HATARI ZAIDI HAPA NI UWEPO WAKE KWA MARA NYINGINE kwenye biashara ya KUFIKIRIA KUSHIRIKI KUCHUUZA DAMU YA BAADHI YA SAUTI PINZANI NCHINI (mpaka sasa ni wa 15) na baadhi ya wana-JF tukiwemo.
Zitto, Zitto, Zitto toka huko, Zitto achana na na tabia zako za kusimama mbele ya wanachokipenda umma wa Tanania lakini nyinyi hamipendi. Zitto huwezi kamwe kumfanya Lowassa awe rais kwa janja zozote bila Wa-Tanzania kuridhi kitu hapo.
Zitto ulizaliwa uchi ukaikuta fedha, nguo, magari na nyumba nzuri dunia na siku ya kuondoka kwako ahera hutoenda na chochote. Acha hizo tamaa za Lowassa ambaye tayari anaamini hela zake na za Rostam Aziz ni USAFIRI TOSHA KUFIKIA URAIS hata bila kuhitaji Wana-CCM wenzake.
Na ninasema kwa uchungu kwa taifa la Tanzania linawaangalia kila mlitendalo; Zitto, Makamba na Lowassa tunasema Tanzania inalia, wanyonge tunalia; wazee jamvi sasa tunalikunja!!!
Hivi mnambembeleza wa nini?kama kaamua kufuata mkondo huo achaneni nae,tatizo humu ndani kuna watu wanampenda huyu kijana(zitto) kupita kiasi,nashukuru kidogo sasa wanajamii wengi mmeanza kuuelewa upande wa pili wa Zitto mwaka juzi mpaka mwanzoni mwa mwaka jana ilikua ukimzungumzia zitto negative side unashambuliwa mpaka unajuta kuifahamu hii forum,wenye kumbu kumbu nzuri nadhani mnakumbuka mhariri wa gazeti la kulikoni enzi hizo alivyoshambuliwa na mashabiki wa zitto kwa kuandika upande wa pili wa (-ve) wa zitto akimhusisha na haya madudu mnayomuona nayo leo.
"Mwanangu si msikivu" Haya ni maneno ya Bi.Shida mama mzazi wa Zitto,sasa nyie mnaombembeleza hamuoni kwamba mnajaribu kumpigia mbuzi gitaa ili acheze?aah sijui bwana labda atacheza siku moja,mimi kamwe simlilii zitto.
Haya tena vyama vya siasa vya Bongo!! CCM waliwahi kusema kuwa wao ndio Baba wa wapinzani wote na sasa nakubali. Kumbe mna siri humu ndani ya vyama? Vikao vya vyama vinakuwa si suluhisho.
Ushauri wangu kwa CHADEMA: Ni bora huyo Bwanamdogo mwende nae au balaa kwenu!
Hivi Kiwira kununuliwa na NSSF kuna tatizo lipi? au Kiwira ibaki ikijifia bila mtaji na wapewe wawekezaji wa nje bila ubia na Taasisi au mashirika ya ki Tanzania ndio vyema?
Nawashangaa sana wanaoona kuwa NSSF haipaswi kuwekeza Kiwira.
Vijana mnanifurahisha mnavyomkaushia Majimshindo, hahahaaaaa Safi sana. Kuna wawili watatu ambao inabidi kuwakumbusha kuwa kuna watu humu ndani haifai kujibizana nao wala kuongea nao. BIG UP.
Kwa wanaomtetea Zitto kwa hili, naona hawaelewi tatizo liko wapi.
Tatizo si kuwa hatuna imani na NSSF. Ukweli mbona umeandikwa tangu jana?
NSSF hawana wataalamu wa kufua umeme ila wana hela zetu sisi. Sasa watakapoamriwa kutengeneza umeme/kuchimba makaa ya mawe basi watakuwa na option mbili: Kuchukua wabia wa serikali ambao ni TANESCO au kuchukua mbia mwingine ambaye ni ********.
Huyo ****** wengi wetu tuna wasiwasi kuwa atakuwa Richmonduli aka Dowans ambaye milele ofisi zake zipo Mirambo Street na kampuni mama ni CASPIAN. Huyu bwana huyu ni kama Boomerang. Kila ukimrusha na kumtupilia mbali, yeye anakurudia. Na hapo ndipo mzizi wa fitina kalala maana UFISADI wote wanaotaka kuufanya basi utaanzia hapo.
Barabara ya Chalinze hadi Msata ilikuwa ijengwe na Wakorea. Ila wakalazimishwa wawe na Sub-contactor ambaye alikuwa ni shirika la JKT kama sikosei na huku Kikwete Mdogo akiwa kajipachika kama kupe. Cha ajabu, hela zote walipewa hawa Wabongo ambao ni Sub-Contactor na jamaa wakalala mbele na hela. Matokeo yake ni kuwa hadi leo haijajengwa wala kipande (kupanulia). Mkorea kalizwa maana hajapata hata senti tano pamoja na kuingia Bongo na vifaa vyao.
Hii ndiyo Bongo ambao inabidi kuwamulika hawa jamaa kwelikweli. Sintashangaa hawa wanaokuja kutetea hapa na kuonyesha kuwa akina Zitto na Makamba wanafanya kazi kwelikweli, ndiyo hao hao wanaozisubiri hela zitoke. HAKUNA KULALA mwaka huu. Tutakupigieni kelele hata kama mtakuja JF na kusema huu ni USHENZI, UTOTO, UPUUZI, UJINGA na kila aina ya tusi mnalolifahamu. Wengine tukiwa JKT tumetukanwa sana na hatutajali sana.
Kama mkija na mapendekezo ya KUIPA NGUVU Tanesco na kuwaachia hatimaye wenyewe wafanye kazi na nyie mkisimamia tu, tutakuwa na nyie milele. Tanesco wamekuwa wakisumbuliwa tangu Mkapa aje na ile kampuni yake ya South Africa na wakala hela mwishoni mkawafukuza. Mkaja na mbinu nyingine nyingi tu na hadi leo mmeshaona kula kwenu kuko TANESCO tu.
Ingekuwa vema KUPIGA marufuku hawa wawezekaji wengine wa UMEME na Tanesco wabaki peke yao na huku akina Zitto, Makamba, Shelukindo nk nk wakisimamia tu. Kama kazi/umeme hauzalishwi, si mfukuzani tu CEO wa Tanesco na mlete mwingine? Badala ya kuwasikiliza akina CEO, kwa nini msiwalete Wahandisi na wao watoe maoni yao?
Kibaya kinachoniudhi hapa Tanzania ni hii tabia ya viongozi waliosoma mambo ya ABUSHIRI na Tip Tip, kukaa na kuamua mambo ya Umeme, barabara, mitambo, viwanda nk wakati hata Mwanga wa nini kinaongelewa hawana. Heri wizara ya Nishati angeliwekwa Prof. Mwandosya maana akikaa na Wahandisi wenzie, wanapeana mambo in detail. Sasa hawa akina Makamba, ukiwauliza hata Transformer inavyofanya kazi hajui. Ukimwuuliza Jet Injine inafanya kazi vipi hajui. Na huyu ndiye aagize mitambo ya umeme nje au kutafuta kampuni la kuzalisha umeme Tanzania. Kweli tatizo la umeme ni Tanzania ni UONGOZI (by Mwanakijiji).
Tatizo la Tanzania sasa hivi kila analysis ya jambo haifanywi tena objectively bali watu wanaangalia personalities zilizomo.Nani kasema nini, nani anatoka dini gani! TUTAFIKISHWA PABAYA KAMA SCOPE NA LENSE OF ANALYSING THINGS ITAKUWA NI DINI/UDINI! Pamoja na kwamba sijafuatilia sana huu mjadala nimeona watu humu wakiuliza " kwanini watu wanapinga NSSF kwanini hawaangaliii pia PPF!" Cha ajabu, PPF haijajikita kutaka kufua umeme! Utalinganisha vipi? Tuache huu mtizamo una bore sana.Tuangalie jambo lililopo tulijadili kitaalamu zaidi bila kujali nani yumo ndani ya taasisi.
Zitto hachafuki bila sababu, ana mambo mengi ya chini kwa chini yasiyolenga kuikomboa tanzania ndio maana maliberali tunaona bora CDM imtumulie mbali alalame poa tu.
Mtu huchafuka kwa matendo yake: mfano mwakyembe ni ccm mbona hapa jf cdm hawampondii?
Matendo matters than just to wear CDM combat na kujiita mwanaharakati