Zitto, Habibu Mchange hana sifa za Kukunadi

sioni wapi vijana wa Tanzania na wasomi wake wanaweza leta ukombozi wa hii nchi.Na hii haishangazi kwani kwani hata tafiti zao zinaeitiriwa na Vyeti tuu na si vinginevyo.Kama tunaweza kuwa watu wengi hivi wapo tayari kupinga mabadiliko,wapo tayari kulinda himaya ya CCM ni wazi atakayekuja badili nchi CDM wakishindwa ni lazima awe dictator awachape wote na kuwaongoza kama robot hadi afe ndipo warudi kwenye ujinga wao.

Nyerere was so smart and very lucky kuwa that smart among fools.Disappearance yek ndiyo imefungulia all the dogs in town.Kwa ujumla tuna ujasiri wa kubaki ktk dhiki na kuzama kuliko kuondoka.Huwa tuna create bigger enemies wanaotosha tuhakikishia defeat katika fikra zetu kabla hata hatujaanza project.

Vijana wenye akili wana simama wanatetea ushenzi wa Zitto in the middle of the battle?Zitto naye anajua nini kipo at stake halafu anafanya matendo kama haya irresponsibly?Vijana waoga wanaona kwenda mbele ni kugumu zaidi ya kubaki na CCM huku wakidhani wanaweza secure nafasi za fadhila wanaua si nafsi zao tuu bali hata za watoto wao.WANAKOPA NGUVU NA DAMU ZA WATOTO NA KUZUTUMIA VIBAYA,WAFANYAYO YANAONGEZA KIASI CHA DAMU WATAKAYOMWAGA WANAFUATIA KTK NCHI HII ILI KUITOA KTK SHIMO TUNALOSUKUMIZWA NA CCM.sijui kwa nini hawaoni wanavyohalalisha kutawaliwa na huyu mwovu alieyebeba jina CCM na miwshowe CCM kupambana kwa vile atakuwa na imani kuwa kutawala kwa staili y akitumwa ni haki yake.

Halafu anadai udini na ukabila?Mbona nazidi thibitisha kuwa dini yake na kanda aliyotoka haiaminiki linapokuja suala la long and enduring journey.Huyu ana abuse tafsiri za udini ,ukabila, na ukanda.Anawasaliti waislam na watu wa kanda yake kwa kuact kama mtoto mdogo,kutowajibika kwa taifa na jamii aliyotoka zaidi ya kutaka watu wawajibike kwake.Conventional wisdom haimwambii kuwa CDM wanaweza pia kaa na kuashauriana wakapa best candidate kabla ya kuchukua form ili wapewe go ahead kuchukua form na uchaguzi uwe na matokeo mazuri na yenye kuweza changia ushindi na ukombozi kwa watanzania.

Kwa position CDM ilipo ni wazi kuwa watanzania wameweka matumaini kwao sana ya ukombozi na katk hii stage si Mbowe wala Slaa wanaweza fanya mzaha hawalafu wakawatazama watanzania.Zitto haoni kuwa na yeye ana wajibu mkubwa sana wa kuwa na busara.Kama aliingia katk siasa kama sehemu ya kupata mademu na sifa nyingine ajue alisaini mkataba mgumu sana.Keshachukua dhamana ya watananzia na sasa hawezi itia najisi kwa hizo sifa zake.talia kama yupo labour lakini lazima awajaibiki na kuwajibishwa.Sifa za kuwa anafaa kuwa jemedari halafu hawezi tumia busara hapa ni ukakasi mkubwa na ushahidi kuwa hawezi shika dhamana ya wananchi na kilichobakia ni kunajisi dhamani aliyopewa.

Mkubuke mkichezea nafasi basi hamtakaa muwe na nafasi tena ya kutoka katk hizi dhambi kwa kura au mtutu.Dunia siku hizi ina kataza mapinduzi ya mtutu,wasalaiti na waovu wengine hawawezi tena uwawa,watakuwepo nasi na watatumia haki za msingi kuwalinda ,huku wakiendelea fanya usaliti kwa raha zao.Miaka iliyopita jamii husika kama za kichina na nyingine za africa zilua waoga, wasaliti, watoa siri na wengine waliokuwa na elements za kurudisha move za jamii husika nyuma au hata kuhatarisha uhai wa kabila au taifa.Hawa walipotezwa ili kuokoa familia.Mjue sasa hivi Zitto na Shibuda hawawezi fanyiwa hivyo kwani haki za binadamu zinawalinda,na zitawalinda hata wanapowaangamiza watu wote,zitawalinda hata kipindi watakapotumi akila sababua jitete hata kama haihusiki na lengeo la mwanzo. Wata abusue sana democrasia,hawatawajibika na watataka mgao.

CCM is ganga of crooked evils ambao hata wao wanaihtaji msaada wa ukombozi wenu,wanachofanya ni kila mtu kuchukua chake mapema,ila hawajui watakwend aishi wapi na hicho wakitacho chao.Kuna hitaji la kuwato na kuawanyang`anya haraka, kabla hawajafanya uovu mkubwa zaidi ambao hautazibika na baadaye kujikuta tunahitajia watesa au kuwaua.
 
Lakini Tuntemenke unafikiri njia ya kukashfu watu na kuwa tukana kwenye mitandao na kuwadharirisha ndio suluhu pekee kwenye matatizo?
Mi nafikiri hii njia ndiyo inayo endeleza chuki na wala haijengi hata mara moja!
Kama kweli Mna mapenzi na chama na mnaona kuna tatizo kwa nini tutukane badala ya kuwafata na kuwaeleza?
Hii njia haijengi bali ina bomoa na kwenye wengi kuna mengi tena ugomvi ukiwemo na busara pekee ndio suluhu ya haya yote si matusi!

Kama kweli tuna kitakia mema chama na tunataka kweli kukijenga tunatakiwa kuwa chachu ya kuachana na ugomvi, matusi kupitia mitandao!

Mkuu mwita,
Labda katika utafiti wako kati ya Dr.slaa na Zitto nani anaongozwa kusemwa vibaya,kusimangwa kwenye mitandao ya kijamiii?
ukinpa jibu nitatoa nilichokuwa nataka kueleza mkuu
 
Kwa observation yangu Dr. Slaa ndiye anashambuliwa zaidi tena mbaya zaidi vijana wa Chadema ndio wanaongoza mashambulizi wakishirikiana na watu wa ccm. Zitto anashambuliwa na baadhi ya wanachadema lakini anaungwa mkono kwa nguvu sana na watu wa ccm kwa kushirikiana na wale vijana wa Chadema wanaomshambulia Dr. Slaa.

Mkuu Mwita Maranya,
Heshima mbele Kamanda. Nipo kwenye Mitihani Mkuu wangu, ndiyo maana nimepote kiaina. Nikimaliza ntarudi kulisogeza gurudumu la JF. Pamoja!

TUMBIRI (PhD In Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Mwampamba, Mchange, Juliana, Gwakisa ss hv Wanaganga njaa kwa kukishambulia chama na nina wahakikishia iko siku 2taleta ushaidi wa uhakika jinsi Mwigulu anavyowatumia na picha kabisa. Ila kwa mbozi mwampamba mambo yamemuwakia kwa kitendo cha kutukana viongozi wa kitaifa hasa Dr slaa. na vijana wa eneo la anapoishii MLOWA ( sijui kama nimepatia) walitaka kumtandika kwani wanasema walijitoa sana wakati alipogombea walijinyima kwa ajili yake lakini ss ameonyesha dharau kubwa WANASEMA ni heri alishindwa kwn angeshinda angewadhalilisha na asahau kugombea japo sasa anajitahidi kuomba msamaha ili wao wanasema wako tayari kumsamehe ila DR SLAA ndo aende akamuombee msamaha. hapo ndo anakwama.
Ni MLOWO Mkuu. Haka kajamaa kanajiamini kupita kiasi. Nilikutana nako pale Makao Makuu ya Chadema mwaka 2010 kama mwezi mmoja hivi kabla ya uchaguzi Mkuu nikamuuliza vipi yuko Dar wakati yeye ni mgombea na ndio kwanza moto wa kampeni umeshika kasi, akanijibu atafanya kampeni wiki 2 tu na tatashinda kwa sababu wazee wamemhakikishia atakuwa mbunge. Kilichotokea kila mtu anajua. Ajifunze kwa mwenzie Silinde.
Kuhusu ushiriki wake kwenye hujuma dhidi ya Dr Slaa naweza kusema huyu dogo na mchange hawana tofauti. Kwa wale wasiojua baada ya mchange kusambaratishwa wakati wa Uchaguzi wa Bavicha, wale wote waliokuwa kambi ya ZZK waliunganisha nguvu kwa huyu dogo wakisaidiwa kwa karibu sana na John Shibuda....Siku moja kabla ya uchaguzi walikamatwa maeneo ya Magomeni usiku wa manane wakiandaa mikakati ya kumpitisha Mwampamba na iliporitiwa kwa Katibu Mkuu iliundwa kamati ya haraka chini ya Marando ikawasambaratisha wote.....Hawa hwafai kwenye safari ya kuelekea kwenye uchaguzi wa 2015....Wanatumika na wamekubali kutumiwa. Waende huko Uvirus CCM, huko ndiko kwenye ujanja ujanja na majungu.
 
Haya ndiyo matokeo ya watu kutangaza urais mapema na kuunda makundi

Ni kweli mkuu.Na ndiyo maana nikiandika waraka maalum Kamati Kuu kuhusu haya mambo ya watu kujitangaza kugomvea urais na kuunda mitandao ya kihuni.Nadhani sasa Kamati kuu itanielewa na kuujadili waraka wangu.
 
Hawa ni vijana wanaotumika na Akina Mwigulu Nchemba na Shibuda kuivuruga Chadema

Ni kwanini wasihame waende huko CCM?

Mchange anatumia jina la Said Kulwa huko facebook kutukana viongozi na wanachama wa Chadema

Siku ya uchaguzi Shibuda aliweka mafuta kwenye magari waliyokua wakitumia.Mchange alikua akitumia gari ya Zitto na Ben alikua akitumia gari yake nyekundu.wote waliwekewa mafuta na shibuda.Mchange alichangiwa zaidi ya million 5 kwa ajili ya uchaguzi wa bavicha
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Ni kweli mkuu.Na ndiyo maana nikiandika waraka maalum Kamati Kuu kuhusu haya mambo ya watu kujitangaza kugomvea urais na kuunda mitandao ya kihuni.Nadhani sasa Kamati kuu itanielewa na kuujadili waraka wangu.

Mkuu hapo tatizo huyu mwenye kuyataka madaraka kwa namna yoyote,madaraka ya urais.niliwahitoa hoja siku za nyuma ni nani aliemhakikishia zitto kwamba hata kama umri wako uko chini atagombea tu na kwanini anatumia nguvu kiasi hicho kuyataka madaraka?kuna ajenda gani,mkuu mi nimeshindwa kuelewa hili kundi linaloshinda likitukana viongozi wa cdm mitandaoni si bure lina mtu anayejiita ana akili sana.kwakweli makao makuu wakae na kudraw njia sahihi vinginevyo ni fujo na badae balaa.
 
Huyo dogo ben saa8 alijaribu kupandikiza mamluki uvccm akina paul makonda na sango kasera tuliwashtukia mapema tukachinjia mbali na sasa ni zamu yenu lazima msambaratike
Alidhani akiidhoofisha uvccm atakua na uwezo mkubwa wa kuteka vijana Tanzania atakapokua mwenyekiti wa hicho kikundi kidogo cha Bavicha

Juzijuzi kulikua na thread apa alikua akilaumiwa kumpinga mbunge wake selasini alipompongeza Rais kujenga barabara ya Rombo na kuibatiza jina la JK Road.Hivi alipokua akijenga hoja na propaganda za kumnanga Selasini kuwa barabara ni haki ya warombo na rais aombe msamaha kwa kuchelewesha barabara tangu uhuru,mbona Mbowe kesho yake alimpongeza?
 
Tumeyasema sana takribani mwaka na nusu sasa.
Nilitumiwa ujumbe '' Kaa kimya usilete migongano kwa analysis zako pumba''
Juzi tukatoa tathmini ya uchaguzi, ah! tukaishia kuambiwa wavivu wa kufikiri kwa neno 'fulani et al'
Ukweli kuwa kuna tatizo tena kubwa huihitaji certificate au diploma, just a matter of time.

Niungane naMwita Maranya, katika vijana wanaosimamia kile wanachokiamini kwa hoja na mantiki Ben ni mmoja wapo.Maandishi yake yana ukomavu wa kisiasa. Hata pale anapopingwa bado husimama kutetea hoja zake kwa mantiki.

Hizi kauli za FB za vijana kuushambulia uongozi ni zile zile za UVCCM na matokeo yake tunayaona.
Kuwepo mawazo mbadala ni jambo zuri 'health' na chama cha siasa kinapaswa kiwe hivyo. Sijui kama kashfa na matusi navyo ni 'health' kwa ustawi wa chama! sina uhakika

Soma maoni ya Tuntemeke anayeamini kuwa maisha binafsi ya Dr Slaa yana mahusiano sana na ujenzi wa chama na harakati za ukombozi wa nchi! Utagundua kuwa anaongozwa na inda wala si sera au ubovu wa uongozi. Huyu ni sehemu tu ya kundi kubwa huko FB, sijui ndizo taratibu za Chadema au la, ninachojua ni kuwa huo ni mwanzo wa mtafaruku na analysis ya Mkuu Mkandara ifanyiwe kazi na si kudhihakiwa. Kuna tatizo!

Chadema, kila mara tunasema, ni lazima muwe taasisi na si kundi maarufu. Taasisi hufanyakazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na maadili no more no less!

Kama hamtaziba ufa basi mnaweza kushindwa kujenga ukuta maana utakuwa umeanguka.
Kwani maisha binafsi ya slaa hayana uhusiano na siasa za mabadiliko?
Ndiyo maana hapa juzi tumeambiwa kijana wao ben saanane alimtorosha demu wa kiongozi mwingine anaitwa mrashani?ndiyo maana vijana wake ben na mnyika wanashea demu anaitwa Hawa Mwaifunga mhasibu wa huko chadema?kwa staili hiyo si atakula ruzuku kama wamemkamata mhasibu hivyo?
 
Mkuu Mkandara nimesikitishwa sana na tishio/kusudio lako la kutaka kurudisha kadi ya Chadema kwasababu unaona Zitto anashambuliwa na ''vijana wa Chadema''.
Hivi inawezekanaje kukereka na mizimu ya JF inayojiita vijana wa Chadema to the extent ya kutaka kusitisha uanachama wako? Msimamo wako unanipa maswali kadhaa; Ulijiunga Chadema kumfuata Zitto ama ulivutiwa na sera za chama?
Je umewahi kusoma kwenye facebook kuona wanachoandika akina Mchange, Mtela, Juliana, Immaculate, Nyakarungu, Chagulani pamoja na wengine wengi wa kundi lao dhidi ya Dr. Slaa?
Hii notion ya kwamba kila mtu anayempinga Zitto anamchukia umeitoa wapi mkuu wangu mbona unakwenda mbali sana?
Hao vijana wanaokesha mitandaoni wakimtukana Dr. Slaa na kumtukuza Zitto ndio unawaona wa maana kuliko hawa wanaompinga Zitto? Nidhamu kwa viongozi unayoizungumzia hapa inakuwa na mashiko kwa upande mmoja tu ulio na maslahi nao au sijakupata vizuri kamanda wangu?
Duh, mkuu wangu ndio umeelewa hivyo?... Hapana ni ktk majadiliano tu kuna mtu hapa JF kanawekea vitisho ya kwamba Hata Kitila hatakiwi kuingilia umoja wa vijana wa Chadema Vavicha kwa kumuunga mkono Zitto. Ya kwamba vijana wamejiandaa kuchukua chama sijui na makolokolo mengine hivyo nikaema kama kweli haya ni maamuz ya chama basi nitairufisha kadi yenu..

Usinione naandika haya ukachukulia vinginevyo isipokuwa pale napoona upuuzi wa vijana wa Bavicha wanapoleta ugonvi wao hapa JF na kuanza kuwatukana hata viongozi wao. Zitto pamoja na makosa alokwisha yafanya bado ni NAIBU KATIBU wa chama na huwepo ktk vikao vyote vya kamati kuu. Mwandishi wa mada hii ana vita na Habib Mchange na kibaya zaidi ni mwana Bavicha ambaye anakuja kumvua nguo mwenzake humu JF huku akiwahusisha viongozi wa chama ktk ujinga huu wa makundi. Ya facebook yabakie FB maana kule ni uwanja wa mtu na ana kila haki ya kuandika akipendacho na kama inamkwaza Dr. Slaa yeye kama katibu wa chama ataweza kuwaita na kuzungumza nao.

Yeye Jiwe la Ukara (aaah ananikumbusha mbali) na Habib watajuana huko mitaani na FB, hakuna anayetaka kumjua Habib Mchange wala hakuna uchaguzi humu na sijaona mahala Mchange amekuja mzungumzia kiongozi yeyote vibaya. Sipendi kabisa huu mtind wa kuwaingiza viongozi wa chama ktk ujinga wa vijana wetu hasa pale maamuzi ya kichama yanapotumiwa kuwa kigezo cha ugonvi wao..

Sijawahi kuona kiongozi yeyote wa CCM wakifanya hivyo hata siku moja isipokuwa hivi vyama vyetu vya kuunga unga na hasa hawa vijana wa Bavicha hawana nidhamu kabisa kazi kugombania uongozi tu. Ridhwan yule pale hapendwi na kaleta vurugu kibao lakini umeona ama umesikia CCM wakipigizana makelele hapa JF.. Yao wanayalmaliza chumbani na sio vijiweni. All am saying ni kwamba yanayofanyika ktk vikao vya chama yanatakiwa kubakia ktk makabrasha ya chama na sio kuyaleta JF..Kama Zitto haonekani ktk mihadhara ya M4C ndivyo asivyoonekana Dr.Slaa, Kitila au Mbowe kila mtu kapewa majukumu yake na iheshimiwe..
 
Duh! sasa mko upinzani mna vurugu kama hizi! jee, mkikabidhiwa nchi tutafika kweli! CDM inaelekea kutumbukia kaburini kama waliotangulia kutumbukia wenzao NCCR-mageuzi!!

Duh, mkuu wangu ndio umeelewa hivyo?... Hapana ni ktk majadiliano tu kuna mtu hapa JF kanawekea vitisho ya kwamba Hata Kitila hatakiwi kuingilia umoja wa vijana wa Chadema Vavicha kwa kumuunga mkono Zitto. Ya kwamba vijana wamejiandaa kuchukua chama sijui na makolokolo mengine hivyo nikaema kama kweli haya ni maamuz ya chama basi nitairufisha kadi yenu..

Usinione naandika haya ukachukulia vinginevyo isipokuwa pale napoona upuuzi wa vijana wa Bavicha wanapoleta ugonvi wao hapa JF na kuanza kuwatukana hata viongozi wao. Zitto pamoja na makosa alokwisha yafanya bado ni NAIBU KATIBU wa chama na huwepo ktk vikao vyote vya kamati kuu. Mwandishi wa mada hii ana vita na Habib Mchange na kibaya zaidi ni mwana Bavicha ambaye anakuja kumvua nguo mwenzake humu JF kwa nini huku akiwahusisha viongozi wa chama ktk ujinga huu..

Yeye na habib watajuana huko mitaani, hakuna anayetaka kumjua Habib Mchange hakuna uchaguzi humu na wala sijaona mahala Mchange amekuja mzungumzia kiongozi yeyote vibaya. Sijawahi kuona kiongozi yeyote wa CCM wakifanya hivyo hata siku moja isipokuwa hivi vyama vyetu vya kuunga unga na hasa hawa vijana wa Bavicha hawana nidhamu kabisa kazi kugombania uongozi tu. All am saying ni kwamba yanayofanyika ktk vikao vya chama yanatakiwa kubakia ktk makabrasha ya chama na sio kuyaleta JF..Kama Zitto haonekani ktk mihadhara ya M4C ndivyo asivyoonekana Dr.Slaa, Kitila au Mbowe kila mtu kapewa majukumu yake na iheshimiwe..
 
Huyo dogo ben saa8 alijaribu kupandikiza mamluki uvccm akina paul makonda na sango kasera tuliwashtukia mapema tukachinjia mbali na sasa ni zamu yenu lazima msambaratike
Alidhani akiidhoofisha uvccm atakua na uwezo mkubwa wa kuteka vijana Tanzania atakapokua mwenyekiti wa hicho kikundi kidogo cha Bavicha

Juzijuzi kulikua na thread apa alikua akilaumiwa kumpinga mbunge wake selasini alipompongeza Rais kujenga barabara ya Rombo na kuibatiza jina la JK Road.Hivi alipokua akijenga hoja na propaganda za kumnanga Selasini kuwa barabara ni haki ya warombo na rais aombe msamaha kwa kuchelewesha barabara tangu uhuru,mbona Mbowe kesho yake alimpongeza?
Si rahisi kusambaratisha CHADEMA ama BAVICHA kwasababu ya husda uliyonayo kwa ben saanane,napenda nikuhakikishie kuwa kazi mnayoifanya ya kupandikiza chuki cdm twaifaham na kwa kweli si rahisi kama muaminivyo, Ben Saanane ni mwanaCHADEMA makini anayesimamia misingi ya chama iliyomlea na kumkuza. Kwa hiyo ku-attack CHADEMA kwa wivu wenu kwa Ben Saanane ni upofu. Ni usingizi wa pono kuishi kwa visasi na ni ukame wa fikra kwa vijana kama wewe kujenga hoja dhaifu ktk mambo ya msingi dhidi ya maendeleo ya taifa hili.

Jiamini na uishi kama kijana mwenye ndoto za kimaendeleo na si kuendeleza majungu na fitna, labda utueleze Ben Saanane wewe kakufanyia nini? Au ndo mambo yale ya msemakweli hapendwi? Acha kuwa kibaraka mkuu! Napenda tujenge nchi yenye upendo na mshikamano. Kila likija jambo Ben Saanane hata mada isiyomuhusu lazima mtie jina lake. Kama hakuna fikra zinazojitambua kaeni kimya.

Tz inatuhitaji mimi na wewe kuijenga na sio hao wataka madaraka kishari.
 
Me naona una turudisha kulekule wala hatupendi kusikia mambo binafsi ya watu wala haya tusaidii sisi, kwa nini mambo ya mitaani myalete kwenye mitandao? Huku ni kuvunjiana heshima kabisa.

Kwani maisha binafsi ya slaa hayana uhusiano na siasa za mabadiliko?
Ndiyo maana hapa juzi tumeambiwa kijana wao ben saanane alimtorosha demu wa kiongozi mwingine anaitwa mrashani?ndiyo maana vijana wake ben na mnyika wanashea demu anaitwa Hawa Mwaifunga mhasibu wa huko chadema?kwa staili hiyo si atakula ruzuku kama wamemkamata mhasibu hivyo?
 
laiti Zitto angekuwa na subira hadi wakati wa uteuzi ufike,leo hii mapandikizi yaliyofanikisha kusambaratisha NCCR, TLP yameingia kazini kujaribu kuipasua CHADEMA.

Sidhani huu ni wakati wa kujitambulisha na kundi la kiongozi fulani wakati huu wa kujenga chama imara kinachojipanga kuja kuchukua dola na kuwakomboa Watanzania.

Tutangulize maslahi ya chama na si ya binafsi.

Kama Mwigulu anasema kuwa cdm ya ukabila na udini,na wachangiaji hapa wako wanaokariri usemi huo na wanajifanya wana cdm jua mnatwanga maji kwenye kinu MMEINGILIWA.
 
Si rahisi kusambaratisha CHADEMA ama BAVICHA kwasababu ya husda uliyonayo kwa ben saanane,napenda nikuhakikishie kuwa kazi mnayoifanya ya kupandikiza chuki cdm twaifaham na kwa kweli si rahisi kama muaminivyo, Ben Saanane ni mwanaCHADEMA makini anayesimamia misingi ya chama iliyomlea na kumkuza. Kwa hiyo ku-attack CHADEMA kwa wivu wenu kwa Ben Saanane ni upofu. Ni usingizi wa pono kuishi kwa visasi na ni ukame wa fikra kwa vijana kama wewe kujenga hoja dhaifu ktk mambo ya msingi dhidi ya maendeleo ya taifa hili.

Jiamini na uishi kama kijana mwenye ndoto za kimaendeleo na si kuendeleza majungu na fitna, labda utueleze Ben Saanane wewe kakufanyia nini? Au ndo mambo yale ya msemakweli hapendwi? Acha kuwa kibaraka mkuu! Napenda tujenge nchi yenye upendo na mshikamano. Kila likija jambo Ben Saanane hata mada isiyomuhusu lazima mtie jina lake. Kama hakuna fikra zinazojitambua kaeni kimya.

Tz inatuhitaji mimi na wewe kuijenga na sio hao wataka madaraka kishari.

Mgaya,

Thank you. Safari hii ya mabadiliko ina changamoto. Ni lazima tuwe na wasaliti wa aina hii. Wanatuongezee chachu ya kupambana.Na kama hauko katika njia sahihi huwezi kupata wasaliti.

Tutawakomboa fikra zao hata wale wanaotutukana.Ila wasishushe heshima ya JF. Hili jukwaa si la matusi. Pia hili jukwaa halimilikiwi na chama cha siasa. Ni jukwaa ambalo watanzania wenye exposure ya kutosha wamekusanyika na kuunganishwa na uzalendo na kiu yao ya kutaka mabadiliko

Asante Mgaya
 
Nimeusoma kwa makini tena na kuurudia waraka au makala aliyoandika rafiki yangu habibu mchange juu ya nia ya Zitto Kabwe kugombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2015.

Pamoja na mambo mengi ya kijinga na kujikanyaga kwa mwandishi mchange mfano anaposifia oparesheni sangara anayodai iliasisiwa na zitto(buila kujua cdm ni chama na si mtu mmoja) ilhali akiiponda na kuidharau M4C kisa tuu haikuanzishwa na zittto na hapo hapo akisema kuwa zote mbili zinafanana na kushabihiana kwa malengo na utekelezaji.

Kuna kitu kimoja ambacho Mchange amekifanya kwa kujua au kutokuja, ameonyesha wazi jinsi ambavyo Zitto Kabwe na yeye pia walivyo na tabia ya ubinafsi.

Nitaeleza:
Kwanza kitendo cha kuisifu oparesheni sangara na kumilikisha zitto kuwa ndiye hasa muasisi wake ni kitendo cha hovyo sana. Mchange anasahau kuwa Zitto ni kiongozi wa CHADEMA na pia ni kiongozi wa kamati kuu na hakuna mipango yoyote ya chama isiyojadiliwa na kupitishwa na kamati hiyo bila kujali ilitolewa na nani. Inapopitishwa kwa utekelezaji, mipango hoyo inakuwa ya chama na kama itashindwa basi hakuna kiongozi wa chama anayeweza kukwepa lawama.

Pili, wakati akijibu hoja ya kwanini Zitto hashiriki M4C kama viongozi wengine, mchange alijisahau au bila kujua aliwamilikisha akina Mbowe hiyo oparesheni na kwamba hao ndio walioianzisha na kwa maana hiyo Zitto hawezi kuishiriki eti kisa tuu imeanzishwa na Mbowe. Hii ni alama ya wazi ya ubinafsi.

Tatu, Zitto mwenyewe analithibitisha hili pale alipoibuka na madai kuwa eti marehemu Regia Mtema ndiye hasa aliyeibua wazo la kumuona rais juu ya mchakato wa katiba. Zitto anasahau kuwa Regia naye kadhalika alikuwa ni mjumbe wa kamati kuu na hivyo hilo wazo kama halikupata baraka za kamati kuu akiwamo yeye lisingeweza kupita na pia hata ombi la kumuona rais halikuandikwa na Regia bali uongozi mzima wa CHADEMA.

Kimsingi Mchange anambomoa Zitto kuliko kumjenga kama anavyofikiri anafanya.
 
Back
Top Bottom