Zitto, Habibu Mchange hana sifa za Kukunadi

Mimi huwa najiuliza Udini wa Chadema utaisha lini?Hakika zitto hicho chama ni cha wakristo nakuhakikishia wanakusakama kwa sababu ya dini yako.Na sasa wanamfuata machange ujue udini unavyoitafuna chadema mbona hawamsakami katibu yule wa Tanga aliyetaka kuwa Rais.Na hiyo ukae ukajue ni Slaa ndo katengeneza yote haya.Mbowe kwangu sioni kama hisia za kidini kali kama alizonazo huyu mmbulu ni sumu kwako zitto na sasa anamshirikisha mambo ya chama hawara wake mbona mbowe hafanyi hivyo.Hakika slaa ni mdudu wa kuua sina huruma na watu kama hawa.Wambulu ni watu wa dini sana na wabinafsi waangalia watakavyojaa chadema kumfuata mmbulu mwenzao amini usiamini.
 
Kimagege

Makala ya mchange nimeisoma nikaielewa, Mchange alikuwa anamjibu Mwandishi mmoja aliyehoji ZITTO ATAGOMBEA URAIS KWA CHAMA KIPI?

Mchange akajibu, Zitto atagombea kwa tiketi ya CHADEMA.

Ndani ya ile makala akaelezea tuhuma zinazosemwa na watu kwamba Ooooh Zitto hashiriki M4C. Lakini ukweli ni kwamba Zitto si kwamba hashiriki M4C kama sisi tunavyotaka kuamini.

NAOMBA KULICHAMBUA JAMBO HILI KWA NAMNA HII.

Majukumu aliyonayo Zitto kitaifa kwa sasa ni tofauti kabisa na miaka ya Nyuma, Majukumu aliyonayo Zitto (ubunge, uenyekiti wa kamati ya POAC) ni tofauti na Dr. Slaa, Heche n.k ambao wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali kwenye vuguvugu la mabadriko.

Bunge linaisha, kama awamu iliyopita, Zitto anaingia kwenye safari za kwenda nje ya nchi na Kamati anayoingoza. Tulimwona akiwa Malaysia, Ujerumani na S. Africa.

Lakini pia muda mwingi anaonekana akiwa kweny vikao vya kamati yake hapa nchini.Muda wa kushiriki M4C kikamilifu kamatunavyotaka sisi ni vigumu.

Mbona anapopata nafasi anafanya mikutano mbalimbali nchini? Dr. Slaa na makamanda wengine walipokuwa Morogoro kwenye M4C, Zitto alikuwa jimboni kwa Rose Kamili.

DR. Slaa na makamanda wengine wamepumzika baada ya vurugu za Iringa, Zitto amefanya mikutano mikubwa Karatu na vijiji vyake.

Ndugu zangu, Operasheni sangara mbona Zitto alishiriki kikamilifu? UChaguzi mwaka 2010 ndiye mbunge pekee aliyezungukia mikoa yote akimnadi Dr. Slaa.

Je swala lipo kwenye M4C tu? Kwa imani yangu M4C ni sehemu ndogo sana kiasi cha kukuza mambo kiasi cha kuonekana Zitto si mshiriki wa kazi za chama.

Kuhusu swala la kumwona Rais,zitto alimtaja Regina Mtema kama mwanzilishi wa mada ya kwenda kumwona Rais na sio kama mmiliki wa ajenda hiyo. Otherwise hukuangalia muktadha wa hoja hiyo na ushiriki wa Regia Mtema.

LAKINI NAOMBA KUULIZA PIA KWANINI WANA-JF HUWA HAMHOJI HAYA MAMBO: Makamu mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA na ushiriki wake kwenye M4C? Au ni Naibu Katibu Mkuu tu ndiye anayeonekana?
 
Last edited by a moderator:
weel said yule Zitto ni wakala wa chama cha mabwepande
Sina hakika kama Maneno yako umefikiria kwanza au unahasira dhidi ya Zitto.

Si vyema kum-provoke mtu kitu ambacho huna uhakika nacho zaidi ya kusikia kelel za maadui wake wa kisiasa.

Ukiulizwa kivipi zitto ni wakala wa CCM, majibu yako yatakuwa huwa anakwenda na Rais nje kwenye mazishi Ethiopia.
Pia utasema Zitto anapendwa na rais.

Hizi nii hoja za kipuuzi, Kwa sababu mtu ambaye ni waka la CCM angethubutu kufanya haya?
1. Kukusanya saini za kumg'oa waziri mkuu wa serikali ya CCM?
2. Kufichua ufisadi mkubwa POAC ambao upo mikononi mwa serikali ya CCM?
3. Kulisimamia kidete sakata la pesa zilizofichwa Uswisi na vigogo wa CCM?

Kwa hiyo tunapotoa shutuma za kum-attack mtu ni muhimu tukawa na ushahidi
 
Who is Habibu Mchange, huyu ana ajenda za udini na ubinafsi tu. Zito bila Chadema si lolote wala chochote, kama wanabisha aondoke waone kama CDM itayumba. Mbona Mzee Nyimbo amesepa na kujimaliza mwenyewe.
 
huwa ninajiuliza ni kwanini zitto ana haraka sana ya kuwa Rais.
Ukiona hupati jibu,Jiulize tanzania tuna aina gani ya Demokrasia?
Jiulize kama umemsoma Zitto na sentesi zake zote za kuhusiana na Urais anaoutaja kama umezeelewa. Una nafasi ya kusoma na kurudi tena hapa utuambie umepata jibu?

Lakini ugeni wa siasa za ushindani licha ya kuwa nazo since 1992 lakini bado hatuzielewi. Tusijue tu kuwa inatakiwa kufanya uchaguzi,tujiulize mchakato wa uchaguzi,kupata mgombea unakuwaje kwa siasa hizi za mfumo wa vyama vingi.

So ipo siku utaelewa, hutauziwa mbuzi kwenye Gunia. Utamchagua Rais uliyemjua kiundani zaidi kuliko wagombea wote wa vyama vingine
 
TUNTEMEKE nyie ndio mnaomchafua kiongozi wetu Zitto, wew na wakina Mtela mwampamba na Juliana shonza ni wabinafsi na mnapenda kukichafua chama mitandaoni, kwa jinsi mnavyomtetea Zitto ndiyo jinsi mnavyomchafua kwani iwaje mchafu amsafishe msafi?

Muacheni Zitto kwani nyie hamna hadhi ya kumtetea otherwise ni kumchafua 2.
 
Ukiona hupati jibu,Jiulize tanzania tuna aina gani ya Demokrasia?
Jiulize kama umemsoma Zitto na sentesi zake zote za kuhusiana na Urais anaoutaja kama umezeelewa.Unanafasi ya kusoma na kurudi tena hapa utuambie umepata jibu?
Lakini ugeni wa siasa za ushindani licha ya kuwa nazo since 1992 lakini bado hatuzielewi.Tusijue tu kuwa inatakiwa kufanya uchaguzi,tujiulize mchakato wa uchaguzi,kupata mgombea unakuwaje kwa siasa hizi za mfumo wa vyama vingi,
So ipo siku utaelewa,hutauziwa mbuzi kwenye Gunia.utamchagua Rais uliyemjua kiundani zaidi kuliko wagombea wote wa vyama vingine​

kwa uelewa wako nitajie hata nchi 1 tu yenye demokrasia duniani!
 
Tuntemeke nikirefer tuhuma za kipumbavu ulizokuwa unazimwaga jf na sasa una-side na Zitto, unafifisha uwezekano wa zitto kupitishwa na chadema kugombea urais
 
Finally....Eventually...Hatimaye...!

Karibu sana Mkuu na Kamanda Tuntemeke. Kama nilivyogusia kule kwenye post nyingine, ni siku nyingi haujatembelea kwenye hili baraza. Karibu sana.

Hapa ndiyo JF, the home of GTs ingawa si wote ni maGTs.
 
Tukifanikiwa kuondoa ushabiki wa watu katika vyama tutafanikiwa sana kuijenga chadema ya mfano na yenye afya njema ili kuchukua nchi 2015,nafurahi kuona watu wakiibua mijadala lakini nasikitika mjadala unapoegemea ushabiki.

Ili tujenge CDM kama taasisi lazima tukubaliane kuwa sote tunajibika kama wanachama na si wapambe wa mtu,yeyote anapokwenda tofauti na wenzake ama utaratibu tunawajibu wa kumkumbusha kurejea ktk utaratibu. Tuntemeke umefafanua vizuri lakini nimepata shida kuelewa ni kwanini wewe umefafanua vizuri kuliko alivyofafanua Mchange ktk makala yake na pia kuliko mh. Zitto? Je, ni kwamba wewe unaelewa vizuri zaidi kuliko mh. Zitto juu ya mambo yake?

Nasema hivyo kwakuwa aliwahitoa ufafanuzi ulionesha kukebehi baadhi ya viongozi wenzake kuwa yeye ndo kawainua. Anyways mimi naamini ktk taasisi na kwakweli ninayoimani kuwa wajenzi makini wa cdm tuitakayo ili tukomboe nchi yetu ni wewe na mimi.
 
TUNTEMEKE nyie ndio mnaomchafua kiongozi wetu Zitto, wew na wakina Mtela mwampamba na Juliana shonza ni wabinafsi na mnapenda kukichafua chama mitandaoni, kwa jinsi mnavyomtetea Zitto ndiyo jinsi mnavyomchafua kwani iwaje mchafu amsafishe msafi?

Muacheni Zitto kwani nyie hamna hadhi ya kumtetea otherwise ni kumchafua 2.
Mkuu nimethamini mchango wako hapo kwenye nyekundu.Sitaki kuongeza neno.Mm si mtetezi wa zitto.
Asante.
 
Mimi huwa najiuliza Udini wa Chadema utaisha lini?Hakika zitto hicho chama ni cha wakristo nakuhakikishia wanakusakama kwa sababu ya dini yako.Na sasa wanamfuata machange ujue udini unavyoitafuna chadema mbona hawamsakami katibu yule wa Tanga aliyetaka kuwa Rais.Na hiyo ukae ukajue ni Slaa ndo katengeneza yote haya.Mbowe kwangu sioni kama hisia za kidini kali kama alizonazo huyu mmbulu ni sumu kwako zitto na sasa anamshirikisha mambo ya chama hawara wake mbona mbowe hafanyi hivyo.Hakika slaa ni mdudu wa kuua sina huruma na watu kama hawa.Wambulu ni watu wa dini sana na wabinafsi waangalia watakavyojaa chadema kumfuata mmbulu mwenzao amini usiamini.

Mkuu hizo RED zinaeleza msingi wa hoja yako, jiulize chuki yako ni dini au Slaa?

Finally....Eventually...Hatimaye...!

Karibu sana Mkuu na Kamanda Tuntemeke. Kama nilivyogusia kule kwenye post nyingine, ni siku nyingi haujatembelea kwenye hili baraza. Karibu sana.

Hapa ndiyo JF, the home of GTs ingawa si wote ni maGTs.
Nimekaribia mkuu,Kwa heshima na taadhima.Tegemea kuniona kwa muda mrefu zaidi.Huku namanyere Nework ipo full
 
Tuntemeke nikirefer tuhuma za kipumbavu ulizokuwa unazimwaga jf na sasa una-side na Zitto, unafifisha uwezekano wa zitto kupitishwa na chadema kugombea urais

Hazikuwa tuhumwa hewa mkuu,Ndio maana wenye kuwahusu wamezifanyia kazi.Na kwenye ngazi ya juu kabisa ya chama zilifika na kwenye vikao vya ndani zilijadiliwa.
Mm kutoa utetezi wangu wa hoja kwa zitto haina impliccation kwamba Zitto ni baba yangu.No,akili yangu imechambua swala hilo kwa mtizamo huo,pia mengine naweza chambua kwa mtizamo mwingine.
Mengi yote nakuachia wewe Mkuu
 
Nimekaribia mkuu,Kwa heshima na taadhima.Tegemea kuniona kwa muda mrefu zaidi.Huku namanyere Nework ipo full

Nafarijika kwa kuwa uwepo wako uko Namanyere utakuweka karibu na watu wa Sumbawanga Mjini. Hivyo wakati wa by election, utasaidiana na baadhi ya viongozi wa chama kumpigia kampeni na kuhakikisha ushindi kwa mgombea yeyote ambaye atakuwa amepitishwa na wananchi na chama.
 
Hazikuwa tuhumwa hewa mkuu,Ndio maana wenye kuwahusu wamezifanyia kazi.Na kwenye ngazi ya juu kabisa ya chama zilifika na kwenye vikao vya ndani zilijadiliwa.
Mm kutoa utetezi wangu wa hoja kwa zitto haina impliccation kwamba Zitto ni baba yangu.No,akili yangu imechambua swala hilo kwa mtizamo huo,pia mengine naweza chambua kwa mtizamo mwingine.
Mengi yote nakuachia wewe Mkuu
Mkuu hata kama uliyoyasema yamefanyiwa kazi bado hata ningekuwa mimi siwezi kukutazama vizuri katika muktadha wa kujenga chama. Ungefungua ID nyingine ndipo uanze kumtetea Zitto. Kwa ID hii mkuu unampakaza kinyesi Zitto, humsfishi, humfanyi kuwa presidential material
 
Back
Top Bottom