Jiwe la Ukara
Member
- Jul 15, 2011
- 44
- 31
Na. Martin M. Malima
Tangazo la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe la kugombea Urais kama atapitishwa na Chama chake cha Chadema linaripotiwa na vyombo vya habari kuzua tafrani ndani ya Chadema. Binafsi sina hakika na uwepo wa tafrani hii ndani ya Chadema kwani naamini Chadema ni zaidi ya Mzee Edwin Mtei na wanachadema wachache katika mitandao ya kijamii.
Baada ya Tangazo hili wamejitokeza marafiki wawili wa Zitto wakitetea na kuunga mkono Tangazo hilo. Hawa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Kitila Mkumbo na aliyekua mgombea wa ubunge wa Chadema katika uchaguzi mkuu 2010 Jimbo la Kibaha Mjini Habibu Mchange. Ingawa ninayo maoni juu ya makala ya Dkt. Kitila Mkumbo lakini katika makala haya nitajadiri makala ya Habibu mchange. Nitajikita kujadili kama Habibu Mchange anazo sifa za kisiasa za kumnadi Zitto na hoja alizotoa kumnadi.
Kuna mwanasiasa mmoja wa Chadema aliwahi kuniambia kuwa ukitaka kukosana na Habibu Mchange basi mpinge au tofautiana na Zitto. Mwanasiasa huyo aliniambia kuwa Mchange huwa yuko tayari kutofautiana na mtu yeyote ambaye aliwahi au huwa anatofautiana na kile anachokiamini hata kama suala linalojadiliwa ni kweli.
Kwa kile kinachoitwa siasa za makundi ndani ya Chadema Mchange anajipambanua kama mfuasi mtiifu kwa Zitto. Katika siasa za majukwaani na nje ya majukwaa ufuasi wake unaonekana. Kumwamini mtu flani katika jambo lolote la kisiasa, kijamii na kiuchumi ni kawaida. Ila si kawaida kumwamini mtu kiasi cha kutokutofautiana nae au kushindwa kuona udhaifu wake. Katika harakati za kisiasa mwanisiasa anapaswa kuwa na marafiki wanaoweza kuthubutu kumwambia madhaifu yake.
Anapswa kuwa na marafiki ambao zaidi ya kumpongeza kuthubutu kutangaza nia, pia watamwambia kuwa kusema kuwa waliozaliwa kabla ya uhuru wasigombee urais ni ubaguzi wa rika. Mtu mbaguzi wa namna yeyote ile hafai kuogoza. Leo atawabagua watu kwa umri wao, kesho kwa dini, jinsia, taaluma , makabila, mikoa na wilaya zao. Sitashangaa akianza kuwabagua hata kwa vyuo walivyosoma. Maama aweza kusema wenye kufaa kuongoza ni wale waliosoma Chuo kikuu cha Mzumbe pekee, na sio Chuo Kikuu cha Zanzibar. Kama Mchange ni ndio Mzee kwa Zitto ni wazi kuwa si mtu wa msaada sana katika harakati za kuelekea Ikulu ya Magogoni mwaka 2015.
Zitto na Machange ni wanasiasa wanaofanana katika baadhi ya mambo. Ukifuatilia kauli zao katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii utagundua. Hawa ni wanasiasa wanaoamini wanafahamu kuliko wengine. Wanawaona wale wasiorandana na mawazo yao kuwa hawajui. Katika mitandao ya kijamii Mchange huwaita wale anaotofautiana nao viraza. Katika makala yake amewaita wavivu, waoga na wafitini . Ni maneno makali yanayowafaa wauaji, mafisadi na walarushwa.
Katika harakati za kisiasa mwanasiasa anakutana na watu wenye lugha za kuudhi na kukatisha tamaa. Kwa bahati mbaya hakuna mwongozo wa spika katika siasa za ushindani. Chadema kama chama kinachojiandaa kuchukua dola kimekumbana na maneno ya namna hii kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na hivi karibuni kutoka Chama cha Wananchi (CUF). Uvumilivu katika kutoa mawazo ni turufu katika siasa. Zitto anahitaji watetezi watakao kua tayari kukabiliana na wananchi watakao kuwa na maswali mazuri kwake na ya kuuzi.
Wapo watakoa hoji uhusiano wake na mmoja wa wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Tiafa, Jack Zoka, anayetuhumiwa na Chama chake kupanga mpango mchafu wa kumuua Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Ubungo John Mnyika na aliyekua mbunge wa Arusha, Godbless Lema. Anachotakiwa kufanya Zitto ni kuandaa majibu ya kuridhisha na kushawishi na sio dhihaka za Mchange.
Uadilifu na uajibikaji wa Habibu Mchane
Katika kuwahikikishia watanzania kuwa anaweza kuwa Kiongozi Mkuu wa nchi, Zitto anajinasibu kuwa ni muadilifu. Sio mla rushwa. Bila shaka hana urafiki pia wanarushwa au watuhumiwa wa ufisadi. Mchange anaposimama kumnadi Zitto anapaswa afanane nae pasipo shaka.
Habibu Mchange aligombea nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Taifa. Kabla ya mchakato Mchange alinza kampeni chafu za rushwa. Aliwatumia baadhi ya wajumbe pesa kinyume na taratibu za uchaguzi ndani ya Chadema.
Wajumbe wa kamati ndogo ya CC ya Chadema chini ya wanasheria nguli Mabele Marando, Prof. Abdalah Safari ilimkuta Mchange na hatia ya kutumia Sh. 2, 561,000 kama hongo kwa kuwasafirisha baadi ya wajumbe kutoka mikoani hadi Dar es Salaam na kuwaandalia malazi.
Barua ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Mwanza Liberatus Mlebele kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroud Slaa ulikua ushahidi tosha kumwengua Mchange katika uchaguzi huo. Katika barua yake Mlebele aliambatisha kiwango cha pesa, namba ya simu aliyotumia Mchange kutoa rushwa kwa wajumbe na nakala ya kitabu cha wageni cha Hitel ya Bondeni One ya Magomeni.
Mchange alikili mbele ya CC ya Chadema kwamba simu iliyotajwa na Mlebele kupeleka fedha ni yake, na kwamba alimhonga Mlebele kiasi kilichotajwa na kulipa sehemu ya gharama za hoteli, na kumuagiza akusanye wajumbe wa mkutano wa uchaguzi. Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa Mchange hajaweza kuwashawishi wanachadema na vijana asilimia 60 wa Tanzania anaoamini watampeleka Zitto Ikulu kua ni mwadilifu. Mchange anaposimama kumnadi Zitto huku anaelea katika lindi la tuhuma za rushwa ambazo hajawi kuzikanusha ni dhihaka.
Zitto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma kwa vipindi viwili mfulizo mpaka sasa. Kama ishara ya ya utendaji wake mzuri mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Anapotangaza kugombea urais anamaanisha kuwa ameshinda majukumu aliyonayo anahitaji ridhaa ya kupatiwa majukumu zaidi. Itakuwa ni turufu nzuri kwa Zitto kama watakao mnadi ni watu wenye rekodi nzuri ya utendaji kama yeye.
Sababu nyingine ilyopelekea Mchange kufutwa katika uchaguzi wa BAVICHA Taifa ni kushindwa kuwajibika katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Temeke. Katibu wake alimtuhumu Mchange kushindwa kutimiza wajibu kwa kutokuudhuria vikao tangu kuchaguliwa kwake. Tafsiri ya madai haya ni kwamba Mchange ni Mshindwa Kazi, anayemnadi Zitto, Mshinda Kazi. Hili ni doa katika harakati za Zitto.
Mchango wa Zitto katika kujenga Chama
Makala ya Mchange inaonesha kuwa hamfahamu vizuri Zitto. Chadema ni taasisi. Kazi za kueneza sera za chama zinafanywa na wote kama timu moja. Mafanikio ya chama hiki ni matokeo ya ushiriki wa wanachama wote wa chadema, na sio viongozi wa makao makuu pekee. Unapozungumzia mafanikio ya Chadema huwezi kumwondoa mwanachama mtiifu wa kijiji Kajiungeni, Urambo, Tabora. Hivi ndivo Zito anavyoamini pia.
Kuna tabia inazuka miongoni mwa wanachama wa Chadema ya kutambua mchango wa mtu mmoja mmoja katika mafaniko ya chama. Kuliwahi kujitokeza hoja katika chombo kimoja cha habari juu ya nani alitoa wazo la Chadema kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kuhusu Sheria ya Mabadiriko ya Katiba. Mara baada ya hoja za Chadema kukubaliwa na Rais ilizuka hoja ya kibinfsi ya kwamba nani mwanzilishi wa hoja ya kwenda kumuona Rais. Wengine walisema ni Zitto Kabwe na wengine marehemu Regia Mtema. Kimsingi sikuona mantiki katika hoja hii kwa kuwa Chadema ni taasisi.
Mchange anakuja na hoja za kibinafsi na u-mimi toafuti na mtazamo wa Zitto anayemtetea. Anaamini kuwa kazi ya kujenga chama aliifanya Zitto wakati wa Oparesheni Sangara aliyoiassisi yeye (Zitto). Anakwenda mbali kwa kuwataja baadhi ya wabunge wa Chadema kama udhihirisho wa kazi nzuri ya Zitto. Anakiweka Chama na wanachadema wengine pembeni.
Ni kweli matunda ya Oporesheni Sangara yalionekana wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010, lakini si kipimo sahihi unapowaataja wabunge kama uthibitisho pekee. Mwamko wa wananchi kupigia kura Chadema ndio matunda dhahiri. Watanzania walijitokeza kwa wingi kuipigia kura Chadema katika nafasi za udiwani, ubunge na uraisi. Isingekwa mifumo mibovu ya uchaguzi tuliyonayo, vinginevyo pengine Chadema ingekuwa inashika dora au kuwa na idadi kubwa zaidi ya wabunge na madiwani.
Mwanachama makini ni anayeheshimu na kushiriki kikamilifu kazi za kisiasa. Kazi hizi ni kueneza sera na falsafa za chama kwa wanachama wapya. Chama kinapaswa kubadirika kimkakati na mbinu katika kueneza siasa. Chama chenye kutumia mbinu zile zile za kisiasa kinakbiliwa na changamoto ya ubunifu ambayo inapelekea kifo cha kisiasa. Kampeni ya Vuguvugu la Mabadiriko (Movement for Change) au M4C ni kazi halisi ya kisiasa iliyobuniwa na Chadema. M4C ni nimwendelezo wa Oparesheni Sangara. Mwanachama wa Chadema anaposhindwa kukubali mkakati wa chama kujitanua na kuwafikia wananchi wengi zaidi anakosa nia njema kwa chama.
Mchange anajikanganya. Anaikubali Oparesheni Sangara, anakejeli M4C. Anasema kuwa kushiriki M4C si kipimo cha mtu kutokupitishwa kugombea Urais. Anajenga hoja kuwa kazi ya kueneza chama si kigezo cha kuteuliwa kugombea urais. Tangazo la Zitto ni kugombea kupitia Chadema. Kama angetangaza kugombea kama mgombea binafsi hoja ya Mchange ingekuwa na mashiko, lakini kwa kuwa Zitto ataomba ridhaa ya wanachadema ili ashinde zaidi ya kuishia kugombea, hana budi kushiriki harakati za kueneza na kujenga chama mpaka vijijini. Naamini Zitto anafanya hivyo.
Kwa kile kinachoonekana ni kujibu hoja za watu wanaopinga hoja zinazotolewa na wapinzani wa Zitto, kuwa (Zitto) amekuwa hashiriki katika mikutano ya Kampeni ya Vuguvugu la Mabadiriko, Mchange anasema kuwa kazi ya kukuza chama inafanywa bungeni na katika vikao vya ndani vya chama. Kwa lugha nyepesi M4C si chochote. Ninavyofahamu M4C si mikutano inayoratibiwa na Chadema makao makuu peke yake. Hii ni kampeni inayopaswa kufanywa katika ngazi zote za chama na inaendelea hata wakati huu ambako hakuna timu kutoka makao makuu inayoongozwa na Dkt. Slaa au Freeman Mbowe. Ukiichukulia M4C kama kampeni inayopaswa kuongozwa na timu kutoka makao makuu, utaoona ushiriki hafifu wa Zitto, lakini ukichukilia kampeni hii kwa mapana yake lazima utaona ushiriki mzuri wa Zitto.
Mchange anaingia katika mtego wa wanaompinga Zitto. Anakubaliana na hoja ya Zitto kutokushiriki katika M4C na anafanya kazi ya kumtetea kwa kushusha harakati za chama chake, Chadema. Tafasiri ya hoja ya Mchange ni kwamba kampeni ya kueneza chama ya M4C ni kampeni dhaifu isohitaji ushiriki wa Zitto.
Ni kweli wabunge wa Chadema wamefanya kazi kubwa bungeni. Watanzania wachache wanaofuatilia vikao vya bunge ni mashuhuda. Hata hivyo mchango mzuri wa wabunge wa bungeni haiwezi kutumiwa na chama makini kama njia ya kutegemea kueneza chama. Kazi ya siasa inafanywa waliko wananchi. Huko ndiko unaweza kuona uhalisia wa maisha ya watanzania. Si nia yangu yangu kuzalau bunge, lakini ni wazi kuwa bungeni utaambiwa Uchumi unapaa wakati uhalisia ni kwamba kipato cha wananchi wa kijiji cha Ngoma wilayani Ukerewe ni Tsh. 800 kwa siku. Mwanasiasa Mchange anaamini ndani ya bunge na vikao vya ndani vya chama ndio njia za kueneza chama hadi vijijini na M4C.
Moja ya Changamoto inayoikabili Taifa ni watanzania wengi kukosa nishati ya umeme. Chombo cha habari kinachomwezesha mtanzania kufuatilia vikao vya bunge moja moja ni televiheni. Katika nchi ambayo nishati ya umeme ni tatizo huwezi kutumia televisheni kama njia kuu ya kupeleke ujumbe wa ushawishi. Chombo pekee cha habari kinachoweza kuwafikia wananchi wengi kwa muda mmoja ni redio. Kwa bahati mbaya hakuna redio inayorusha moja mikutano ya bunge. Katika mazingira haya njia mwafaka ya kuwafikia watanzania popote walipo ni mikutano ya siasa. Mchange anaona anachofanya Zitto Bungeni kinatosha, na hakuna haja ya M4C.
Katika siasa unapata ujasili pale mawazo yako yanapokubalika. Unapata nguvu zaidi pale wanakubaliana na wewe wanakuelewa vizuri na hoja zako kwa ufasaha, na wana sifa na hoja za kushindana na wale wanaokupinga. Sina hakika kama Habibu Mchange ametumwa na Zitto au ametumia tu haki yake ya kikatiba kutoa maoni, lakini nikionana na Zitto nitamwaambia Zitto, Habibu Mchange hana sifa za kukunadi.