Zitto awataja mafisadi wa mabilioni ya Uswisi!

Zitto awataja mafisadi wa mabilioni ya Uswisi!

Ukweli ni kwamba Zitto amewataja mafisadi wa mabilioni ya Uswiss, kwa kutumia busara yeye kama mbunge. Upande wa jeshi, fedha kwenye account za nje za viongozi hutolewa wakati wa manunuzi ya silaha na vifaa vya jeshi. Upande wa mafuta, makampuni ya mafuta hutozwa kiwango kidogo kulipia serikalini "exploration blocks" wanazopewa, kwa masharti kwamba waweke fedha kwenye account za nje za viongozi wa serikali ambao majina yao kampuni hizo hupewa.

Kwa kifupi basi, hizi hela zimeibiwa toka serikalini.Tusimlaumu Zitto kwa kutotaja majina, na sie tumsaidie kumalizia, kwani ameshatutafunia kila kitu. Hebu malizia, mie naanza; (List itakuwa updated kadiri wana JF wanavyotoa majina ya nani alikuwa kwenye nafasi zilizoorodheshwa katika kipindi kilichotajwa na Zitto)

Watu waliokuwa kwenye hizi nafasi kipindi kilichotajwa wamesemwa kuwa na fedha katika akaunti za Uswisi

1. Mawaziri Wakuu, 2003-2010; Sumaye, Lowasa
2. Mawaziri wa Nishati na Madini - 2003-2010; Ngeleja, Karamagi, Msabaha
3. Mawaziri Wizara wa Ulinzi 2003-2010; Kapuya,
4. Mkurugenzi Mkuu wa TPDC 2003-2010; Yona Killagane
5. Wenyeviti wa Bodi ya TPDC - 2003 - 2010; Robert Mboma
6. Makatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati 2003-2010; Patrick Rutabanzibwa, Arthur Mwakapugi
7. Makatibu Mkuu Wizara ya Ulinzi 2003-2010;
8. Wakuu wa Majeshi, 2003-2010; Robert Mboma,
9. Makamishna wa Nishati 2003-2010; Prosper Victus, Mrindoko
10. Wanasheria wa serikali, 2003-2010; Chenge,
11. Wajumbe wa Board ya TPDC, 2003-2010; Faida Bakari, Gosbert Blandes, Mudhihir Mudhihir, Emmanuel Ole Naiko, William Haji, Maduka Kessy, Prosper Victus, Mwalim A Mwalim, Ngosha Magonya

Source: Gazeti la Mwananchi, 9/11/2012: Kichwa cha habari; HOJA YA ZITTO YAIBUA MAJADALA MKALI,WABUNGE CCM WAIUNGA MKONO

:disapointed:Lakini hii si guessing tu? Kwani anao ushahidi wa documents angalau za hizo bank zikionyesha akaunti zao na kiasi wanachomiliki? Angalau la Chenge lilishathibishwa na kiasi alichonacho ambacho yeye aliita vijisenti.
 
Najiuliza, ina maana hakuna wana JF walio na interest ya kumalizia list kulingana na nafasi Zitto alizotaja, bali wote tunang'ang'ania Zitto ndio amalizie kutaja kila kitu?

Mbona inaonekana tunakuwa wepesi wa kuwaambia wengine watutolee viazi kutoka motoni ili tule? Hii vita ni ya Zitto peke yake?

zitto Mbuzi wa kafara!
 
Ukweli ni kwamba Zitto amewataja mafisadi wa mabilioni ya Uswiss, kwa kutumia busara yeye kama mbunge. Upande wa jeshi, fedha kwenye account za nje za viongozi hutolewa wakati wa manunuzi ya silaha na vifaa vya jeshi. Upande wa mafuta, makampuni ya mafuta hutozwa kiwango kidogo kulipia serikalini "exploration blocks" wanazopewa, kwa masharti kwamba waweke fedha kwenye account za nje za viongozi wa serikali ambao majina yao kampuni hizo hupewa.

Kwa kifupi basi, hizi hela zimeibiwa toka serikalini.Tusimlaumu Zitto kwa kutotaja majina, na sie tumsaidie kumalizia, kwani ameshatutafunia kila kitu. Hebu malizia, mie naanza; (List itakuwa updated kadiri wana JF wanavyotoa majina ya nani alikuwa kwenye nafasi zilizoorodheshwa katika kipindi kilichotajwa na Zitto)

Watu waliokuwa kwenye hizi nafasi kipindi kilichotajwa wamesemwa kuwa na fedha katika akaunti za Uswisi

1. Mawaziri Wakuu, 2003-2010; Sumaye, Lowasa
2. Mawaziri wa Nishati na Madini - 2003-2010; Ngeleja, Karamagi, Msabaha
3. Mawaziri Wizara wa Ulinzi 2003-2010; Kapuya,
4. Mkurugenzi Mkuu wa TPDC 2003-2010; Yona Killagane
5. Wenyeviti wa Bodi ya TPDC - 2003 - 2010; Robert Mboma
6. Makatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati 2003-2010; Patrick Rutabanzibwa, Arthur Mwakapugi
7. Makatibu Mkuu Wizara ya Ulinzi 2003-2010;
8. Wakuu wa Majeshi, 2003-2010; Robert Mboma,
9. Makamishna wa Nishati 2003-2010; Prosper Victus, Mrindoko
10. Wanasheria wa serikali, 2003-2010; Chenge,
11. Wajumbe wa Board ya TPDC, 2003-2010; Faida Bakari, Gosbert Blandes, Mudhihir Mudhihir, Emmanuel Ole Naiko, William Haji, Maduka Kessy, Prosper Victus, Mwalim A Mwalim, Ngosha Magonya

Source: Gazeti la Mwananchi, 9/11/2012: Kichwa cha habari; HOJA YA ZITTO YAIBUA MAJADALA MKALI,WABUNGE CCM WAIUNGA MKONO
ZITTO ATAJA VIGOGO WALIOFICHA FEDHA NJE..YUMO PIA MKUU WA MAJESHI MSTAAFU

Monday, November 11, 2013 | 2:49 PM

WAKATI ripoti ya kamati iliyoundwa na serikali kuchunguza tuhuma za vigogo walioficha fedha kwenye mabenki ya nje ya nchi ikiwa bado haijatolewa bungeni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amewataja vigogo watatu kuwa miongoni mwa wahusika.
1.jpg

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), ndiye muasisi wa hoja hiyo bungeni. Hivi karibuni alitishia kuwataja wahusika endapo serikali haitawasilisha ripoti hiyo kwenye mkutano wa Bunge

uliomalizika Jumamosi.
Mbunge huyo aliwataja vigogo hao juzi wilayani Kaliua mkoani Tabora wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kolimba. Bila

kutaja majina yao, Zitto aliwataja kwa nyadhifa zao walizowahi kushika akisema ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ulinzi wa zamani na aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi.
Alisema baada ya

kutoa hoja bungeni ya kuitaka serikali ifanye uchunguzi juu ya Watanzania walioficha fedha nje ya nchi, alichaguliwa kuongoza timu ya kufuatilia sakata hilo, kupitia taasisi ya Eurodad, ambapo alifanya ziara katika

sehemu mbalimbali ikiwemo nchini Uswisi na Uingereza.
Zitto alifafanua kuwa akiwa huko alikutana na wadau mbalimbali wa masuala ya kibenki pamoja na kuhudhuria mkutano wa Waziri Mkuu wa Uingereza uliokuwa ukizungumzia utoroshwaji wa fedha.

“Hawa watu wanajulikana na tutawataja kwa majina mchakato ukikamilika, lakini kwa sasa niwaambie miongoni mwa watu hao ni pamoja na waliowahi kuwa mawaziri na mmoja wa wakuu wa majeshi mstaafu,”

alisema Zitto.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali inaendelea kushikwa na kigugumizi cha kuwaanika watu hao hadharani licha ya Serikali ya Uswisi kuitaka isaini mkataba wa kubadilishana taarifa. Zitto alisema kwa sasa ameshawaagiza wasaidizi wake katika masuala ya kibunge kuandika utaratibu utakaowasilishwa bungeni

kwa ajili ya kuwadhibiti watu wanaoficha fedha nje bila kuwa na maelezo ya kutosha.
Aliongeza kuwa suala la kuwaanika hadharani watu wanaoficha fedha nje ya nchi linahitaji uungwaji mkono wa hali ya juu kwa kuwa ni kazi ya hatari inayowagusa watu wenye maslahi na uwezo mkubwa nchini. Kwa mujibu wa mbunge

huyo, mbali na Tanzania, nchi nyingi za Afrika zinaweka fedha nyingi Uingereza pamoja na visiwa vyake 15 ambapo katika kisiwa cha Jersey pekee kuna paundi bilioni 40 za Uingereza.
Zitto alisema baadhi ya nchi huwafilisi watu ambao wanabainika kuwa wameficha fedha nje na kuzitumia kwa shughuli mbalimbali za

kijamii.
Alisema kuwa wakati anafanya shughuli hiyo aliyosema ni ajenda ya kitaifa, alitegemea kuungwa mkono na watu wake wa karibu, ikiwa ni pamoja na walio ndani ya chama chake. “Hivi ni vita visivyohitaji

utengano, tunapoamua kulumbana sisi kwa sisi wenzetu wanapata mwanya wa kufanya mambo yao, nilitegemea katika hali hii CHADEMA tushikamane kuliangamiza hili dude CCM,” alisema Zitto.

Kuhusu migogoro
Zitto alisema CHADEMA hawama migogoro na kinachofanyika ni mikakati ya watu wachachahe wasio na shughuli kuamua kuwagonganisha viongozi.

“Kuna watu wachache sana ambao hawana kazi, shughuli yao ni kugonganisha viongozi ili wagombane na ikitokea hivyo wao ndiyo furaha kwao, sio ufahari hata kidogo kwa CHADEMA kuonekana ina migogoro,” alisema.
Zitto alisema mwaka 1995 kabla ya CHADEMA kuamua kuiunga

mkono NCCR-Mageuzi, Edwin Mtei na Bob Makani waligombea nafasi ya kutaka kuwania urais kupitia chama hicho na hakukuwa na misigano yoyote kwa kuwa walijua malengo yao ni kuwatumikia Watanzania.
Aliongeza kuwa hali ya watu kuwania nafasi moja ndani ya CHADEMA ilijirudia mwaka 1998, kwa nafasi ya

uenyekiti kuwaniwa na watu wawili tofauti na hakukuwa na mgogoro.
“Uchaguzi ndani ya CHADEMA ulifanyika mwaka 2009, tukapata viongozi na tukaingia kazini, mliona tulichofanya, tulivuna wabunge wengi, madiwani na wenyeviti wa mitaa. Lakini sasa hali inaanza kuwa ya ajabu ajabu

utafikiri kuna mtu aliyetangaza kugombea
,” alisema.
Kwa mujibu wa Zitto, hatua yake ya kugombea uenyekiti mwaka 2009 ilitokana na kile alichokuwa amekiona kuwa kutekeleza demokrasia ndani ya chama chake kutokana na waliomtangulia kujitokeza kuwania nafasi walizoona zinawafaa.

“Mimi ni binadamu, nina damu na nyama, katika umri huu mdogo nimepigwa mishale mingi sana ya kisiasa, ninaumia na damu inanitoka, sasa nimechoka kupigwa mishale, ni lazima viongozi tuambiane ukweli na tukemee hali hii,”

alisema Zitto.
Alisema kuwa mwanzoni hapakuwa na chama chenye nguvu kama NCCR-Mageuzi, lakini walipoanza kupigana kile alichokiita mishale, chama hicho kilisambaratika.

“Wakamchafua sana Mabere Marando kuwa ndiye msaliti, sasa Marando yuko wapi? Si ni kamanda wetu? Si ndiye huyu mwanasheria wetu? Lazima tuambiane ukweli na tuweze kuvikwepa vihunzi vya CCM, lazima sasa wanachama wanaoleta chokochoko washughulikiwe,”

alisema.
Alisema kuwa viongozi lazima waonye haya mambo, kwamba bila kuonya wataonekana wanashiriki. “Waha tuna msemo; ukiona kifaranga yupo juu ya chungu, jua mama yake yupo chini,” alisema Zitto.
Kapuya ajisalimisha

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), juzi alijisalimisha katika ofisi ya CHADEMA akimuomba Zitto azungumzie matatizo ya barabara katika jimbo lake ili aweze

kusaidiwa.
Kapuya alitoa ombi hilo katika ofisi za CHADEMA wilaya baada ya Zitto kuwasili eneo hilo saa 9.30 mchana kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara, ikiwa ni kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati

alipohutubia mkutano wa awali kwa njia ya simu wiki tatu zilizopita.
Akiwa ofisini hapo, Prof. Kapuya alihojiwa na Zitto akitaka kujua sababu ya kuikodishia Halmashauri ya Kaliua nyumba yake huku akiwa ni mmoja wa madiwani wa wilaya hiyo wanaopaswa kuhakikisha halmashauri inakuwa na majengo yake.

“Karibu mzee katika ofisi zetu, lakini unaweza kuniambia kama uamuzi wako wa kuikodishia halmashauri nyumba yako hauingiliani na vikwazo vya kuiwezesha kupata majengo yake?” alihoji Zitto.
Katika kujitetea, Prof. Kapuya alisema sababu ya kufanya biashara hiyo na halmashauri ni kutokana na wilaya kutokuwa na majengo yake binafsi.

“Ni kweli mimi ninakodisha, lakini kiasi ninachochukua ni kidogo kuliko kile anachochukua Waziri Magufuli katika Wilaya ya Chato, kwani naye anaikodishia halmashauri ya wilaya yake jengo linalotumika kama ofisi,”

alisema Kapuya.
Katika hali ya kuonyesha kuwa anaomba Zitto asizungumzie upungufu uliopo katika jimbo lake, Prof. Kapuya alimuomba azungumzie matatizo ya barabara. Zitto alisema kimaadili kiongozi anapofanya biashara sehemu anayoweza kuwa na uamuzi inasababisha hali ya kulinda maslahi ya kiongozi

huyo ikiwa ni pamoja na kukwamisha mradi wa eneo husika usikamilike au kujiongezea gharama katika biashara husika.
Alimueleza Prof. Kapuya kuwa kinachosabaisha Mkoa wa Tabora usiendelee, ni pamoja na

matatizo ya ubinafsi kati ya wabunge wa mkoa huo, huku akiwaambia waache tofauti zao na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta katika kuwatumikia wananchi.

----CREDIT: Tanzania Daima
 
Hakuna jipya yaleyale kama ya Tb Joshua kuna Rais atatekwa East Africa lakini siyo Kenya ila hataji ni nchi gani! Kazi porojo tu kama za Zitto.
 
yeye mtoto wa mkulima kama kuiba labda aibe matrekta

na anacheza na voucher za pembejeo tu.

anagonga kimya kimya tu za ndani ya nchi.

humo yote yamejaa makwapuaji tupu hakuna hata mwenye unafuu.

ni kizazi cha panya..................
 
Zitto awe makini maana mapatano ni kugelesha kutuzuga ngoma ipite ila akijipindua hao anaocheza nao ni hatar.
 
Zitto ameshindwa kutaja majina ya mafisadi walioficha fedha nje, aache wimbo wa kinafiki achape kazi ya kukijenga chama chake, aache ubinafsi arudi kundini.

Tulijua ni usanii wa Zitto hawezi kuwataja waficha fedha nje kwasababu yeye mwenyewe kuna ukakasi.
 
Hivi serikali ya ccm lazima iwakumbatie hao makupe mpaka wafe?

Hivi hujui jibu la swali lako au unajua jibu lakini hutaki kuamini?

Serekali ya CCM inawakumbatia kwasababu ndio makupe wenyewe.
 
Hivi kuweka pesa zangu uswiss nilizozitafuta kwa juhudi zangu ni kosa? Kuishi nchi zinazoendelea Bwana majungumajungu tuuu!!!!Kinachofurahisha ni kuwa kelele za chura hazimtishi mchota maji!!

Tatizo hatujui unamaanisha nini unvyosema juhudi zako na hasa kama ulikuwa serekalini. Na kama ni juhudi zako kweli kwanini usiweke wazi usifiwe
 
"Hawa watu wanajulikana na tutawataja kwa majina mchakato ukikamilika, lakini kwa sasa niwaambie miongoni mwa watu hao ni pamoja na waliowahi kuwa mawaziri na mmoja wa wakuu wa majeshi mstaafu,"

alisema Zitto.

Hivi huu mchakato bado au ndio watu wako mchakatoni? Manake hii ilikuwa ya Nov 2011....
 
Naye yumo kwenye list,labda ataje mtu mwingine yeye hawezi kujitaja(rejea siri ya Zitto)
 
Naona wote wababaishaji tu hakuna anayeweza kuwataja...............unadhani zitto kwa unafiki wake anaweza kumtaja kikwete?.............Tusubiri tuone

Zitto msanii tu. Ndio maana namueshimu msigwa alivyokomaa na kinana. Kwani kutaja jina pekeyake nikosa. Kwanza unaweza kutumia hata kisingizio cha kuuliza kama wanalipa kodi.
 
The Government itself encourages those in corridors of power to steal. Look what happened to Jairo's case. Look what happened to Chenge na vijisenti. It is stealing, embezzlement, corruption,etc. etc everywere. This is CCM and its Government at work.
 
“Hawa watu wanajulikana na tutawataja kwa majina mchakato ukikamilika, lakini kwa sasa niwaambie miongoni mwa watu hao ni pamoja na waliowahi kuwa mawaziri na mmoja wa wakuu wa majeshi mstaafu,”

alisema Zitto.

Hivi huu mchakato bado au ndio watu wako mchakatoni? Manake hii ilikuwa ya Nov 2011....
'When you want to shoot, shoot but don't talk'
'The Good The Bad and the Ugly'
 
kuna msemo unasema cheap popularity has got a price, muda wote zitto amekuwa akihubiri kuwa ana majina ya watanzania waliohifadhi mabilioni uswisi na mara ya mwisho aliwaahidi watanzania kuwa atawataja katika kikao cha bunge kinachoendelea sasa, baada ya mwanasheria mkuu kumbana sana apeleke hayo majina ili yafanyiwe kazi alianza kumkwepa na mwisho wa siku alivyobanwa sana alikiri TENA KWA KIAPO kuwa hana jina hata moja hii ni kwa mujibu wa werema, na yeye mpaka leo kakaa kimya hajalitolea ufafanuzi hili swala likiwemo la kiapo, KWA MWANASIASA MKUBWA KAMA YEYE NI AIBU SANA KUWADANGANYA WATANZANIA KWA MINAJILI YA KUTAFUTA CHEAP POPULARITY, kwa style hii taratibu anazidi kupotea ktk medani za siasa
 
Ukweli ni kwamba Zitto amewataja mafisadi wa mabilioni ya Uswiss, kwa kutumia busara yeye kama mbunge. Upande wa jeshi, fedha kwenye account za nje za viongozi hutolewa wakati wa manunuzi ya silaha na vifaa vya jeshi. Upande wa mafuta, makampuni ya mafuta hutozwa kiwango kidogo kulipia serikalini "exploration blocks" wanazopewa, kwa masharti kwamba waweke fedha kwenye account za nje za viongozi wa serikali ambao majina yao kampuni hizo hupewa.

Kwa kifupi basi, hizi hela zimeibiwa toka serikalini.Tusimlaumu Zitto kwa kutotaja majina, na sie tumsaidie kumalizia, kwani ameshatutafunia kila kitu. Hebu malizia, mie naanza; (List itakuwa updated kadiri wana JF wanavyotoa majina ya nani alikuwa kwenye nafasi zilizoorodheshwa katika kipindi kilichotajwa na Zitto)

Watu waliokuwa kwenye hizi nafasi kipindi kilichotajwa wamesemwa kuwa na fedha katika akaunti za Uswisi

1. Mawaziri Wakuu, 2003-2010; Sumaye, Lowasa
2. Mawaziri wa Nishati na Madini - 2003-2010; Ngeleja, Karamagi, Msabaha
3. Mawaziri Wizara wa Ulinzi 2003-2010; Kapuya,
4. Mkurugenzi Mkuu wa TPDC 2003-2010; Yona Killagane
5. Wenyeviti wa Bodi ya TPDC - 2003 - 2010; Robert Mboma
6. Makatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati 2003-2010; Patrick Rutabanzibwa, Arthur Mwakapugi
7. Makatibu Mkuu Wizara ya Ulinzi 2003-2010;
8. Wakuu wa Majeshi, 2003-2010; Robert Mboma,
9. Makamishna wa Nishati 2003-2010; Prosper Victus, Mrindoko
10. Wanasheria wa serikali, 2003-2010; Chenge,
11. Wajumbe wa Board ya TPDC, 2003-2010; Faida Bakari, Gosbert Blandes, Mudhihir Mudhihir, Emmanuel Ole Naiko, William Haji, Maduka Kessy, Prosper Victus, Mwalim A Mwalim, Ngosha Magonya

Source: Gazeti la Mwananchi, 9/11/2012: Kichwa cha habari; HOJA YA ZITTO YAIBUA MAJADALA MKALI,WABUNGE CCM WAIUNGA MKONO

Ni wakati sasa hili jipu kubwa kuliko yote na ambayo na amini likitumbuliwa haya mengine ya ndani njia inafunguka kiulaini. Kiasi tu cha Kodi itakayotokana na pesa zilizokwenda nje iwe kihalili ni kikubwa na niimani yangu hawajalipa Kodi au hofu ya kuwa pesa chafu.

cc. Mzee Mwanakijiji na wengine wa aina yake.
 
Huyu mbunge wangu nimekuwa nikifuatia kauli zake ila nilichokiona ni mnafiki,sio jasiri pia ni muibuaji wa hoja na kurudi kinyumenyume kudai rushwa hili tumempima kwa hoja ya buzwagi,majina ya walioficha hela nje ya nchi,sakata la miradi yenye giza la rushwa nssf akiwa kamati ya PAC.nitaweka ushahidi hapa,makonda kavaa ujasiri kutaja majina ya unga kwa sasa umevalia njuga kumtetea manji ili ukavute mshiko.Tunakuomba utupe listi ya walioficha hela nje
 
Back
Top Bottom