Zitto awashambulia watangaza nia wa CCM

Zitto awashambulia watangaza nia wa CCM

Katika Hotuba ya Mbeya Zitto aliulizwa swali, Kwa nini hakutaja majina ya Walioficha pesa Uswisi.

Zitto akasema kutaja tu kama kutaja haina maana kwa sababu hata ukitaja halafu serikali isiwachukulie hatua za kisheria haisaidii.

Zitto akasema, Yeye alifunga safari kwenda Ulaya kuwajua ni akina nani Wameweka pesa Ulaya, Anasema Serikali ya Tanzania walipewa majina 99 ya walioweka pesa Ulaya, miongoni mwa waliokabidhiwa orodha hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa TRA na TAKUKURU, lakini je mpaka hivi sasa wamewafanya nini hao watu 99?

ZZK kuhusu kutaja majina tu, Akatolea mfano kipindi walipotaja orodha ya mafisadi 11 pale mwembeyanga mwaka 2008, Akauliza baada ya kuwataja Wamefanywa nini mpaka hivi sasa? . Akasema " Na Wengine si wanagombea Uraisi kwa tiketi ya CCM?" bila shaka hili lilikuwa dongo kwa Lowasa

Kwahiyo alifunga safari kwenda ulaya kuwajua ni akina nani wameweka hela huko.
Sasa kashawajua, ili iweje au alitaka kupata procedures za kuweka hela huko ili naye akweke za kwake?
 
Kwahiyo alifunga safari kwenda ulaya kuwajua ni akina nani wameweka hela huko.
Sasa kashawajua, ili iweje au alitaka kupata procedures za kuweka hela huko ili naye akweke za kwake?

Wenzake waliweka list of shame mwembe yanga yeye anaringa na majina ya walioficha fedha?
Anatumia hayo majina kusaka umaarufu tu hana lolote
 
Kwahiyo alifunga safari kwenda ulaya kuwajua ni akina nani wameweka hela huko.
Sasa kashawajua, ili iweje au alitaka kupata procedures za kuweka hela huko ili naye akweke za kwake?

Ali akusaidie kupata au kujua taarifa hizi mtu kama ambaye hata kusafiri kutoka mkoa uliozaliwa kwenda mkoa mwingine pengine ni jambo gum sana so huwez kufika uswisi na kupata taarifa kama hizi
 
Flip flopper.

Sasa kama kutaja tu hakuna maana kwa nini aliahidi kutaja majina?
 
Ali akusaidie kupata au kujua taarifa hizi mtu kama ambaye hata kusafiri kutoka mkoa uliozaliwa kwenda mkoa mwingine pengine ni jambo gum sana so huwez kufika uswisi na kupata taarifa kama hizi

Sijakuelewa kwa uandishi wako huo
 
Leo katika gazeti la mtanzania tena la kina Lowassa na team zake, Zitto Kabwe eti kawalipua Membe, Magufuli na Mwandosya, ilibidi nikimbie kulinunua gazzeti hili kusoma ndani nikagundua mtu huyu anatumika vibaya na Lowassa, kwanza kapewa milioni 200 ili afanye fujo zake hizo za kipuuzi.

Ukiangalia katika tuhuma hizo hapaswi kuacha kumsema Lowassa lakini yeye kwa makusudi anawashambulia ha niliowataja kwa kuwa pengine wanaogopwa kwenye siasa za kuwania urais.

Mfano,eti Magufuli haeleweki yupo upande upi kukemea rushwa? uuzwaji wa nyumba za serikali na kadhalika. Hizi ni hoja nyepesi sana kujibiwa na mwanasiasa kama Magufuli.

Mwandosya anamuhusisha na ubinafishaji wa mashirika ya Umma enzi za Mkapa (hakuna hoja hapa)

Kwa ufupi Zitto anatumika na Lowassa ! chunguzeni mfuatilie mtanielewa ninachokisema.

ww unatumika na nani
 
leo nimepita kwenye mitando mingi ya kijamii nieona watu wengi wameandika habari za zitto kutumiwa na wanasiasa wazee wanaotafuta kwenda ikulu na kuwachafua watu wengine kwa maslai ya wanaomtumia,wengine wamesema zitto alipofikia sasa ndo anafirisika kisiasa na wengine kusema tamaa za pesa ndo zinamuua kisiasa, na wengine kusema anawazalilisha elimu yake, na mengine mengi sana machafu yasiyostahili
wanajf msaidieni zitto kwa coment zenu najua atazisoma humu alipofikia sio anapotakiwa kuwa kama kijana na ajue kutumiwa na mazee wakati yeye ni kijana anazalilisha ujana wake na vijana wenzake,
nawasilisha wanajf



Mafisadi lazima muanikwe hadharani ili Taifa na wananchi wake wawatambue pamoja na unafiki wenu wa kudai mkipewa madaraka mtalifikisha Taifa letu mahali salama na pazuri. ZITTO endelea kuwaanika mafsadi wala usitishwe na maneno ya watu wenye umaskini wa Fikra akilin mwao
 
Nilichokigundua humu ktk mada hii ni kuwa wale wote mnaomshambulia ZITTO ni vibaraka wa makundi ya waliotia nia ktk Chama cha CCM na sababu ya kufanya hivyo ni uroho wa madaraka mliyoahidiwa au vijicent mnavyopewa. Ndiyo maana Mara nyingi sishangashai wajinga wachache wanapokuja na uzi wa kuwasafisha watu km akna Muhongo, Ngereja, Lowassa na wengine wengi kuwa siyo mafisadi Bali walisingiziwa. Ninachokuomba ZITTO endelea kuyaumbua hata Yale mafsadi yaliyodhan kuwa yameiba kiprofesa au kidokta na kwamba hayawez kugundulika au kubainika
 
Back
Top Bottom