Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Nimeshangazwa na majibu ya mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter.

Zitto alikuwa akimjibu mwananchi mmoja aliyekuwa akionyesha frustrations zake juu ya uamuzi wa chama cha ACT kujiunga na Serikali ya CCM huko Zanzibar katika kile kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mwananchi huyo anaonyesha kuwa kuingia kwa ACT katika hiyo serikali hakuwezi kusaidia wananchi kupata uhuru mpana waliokuwa wakitamani kuwa nao.

Katika hali isiyo ya kawaida, isiyo ya uungwana na isiyo ya kiuongozi mkuu wa chama cha ACT ndugu Zitto badala ya kutumia fursa hiyo kumuelewesha au atleast akae kimya wananchi watumie haki yao ya kutoa maoni, yeye anamjibu kwa ufedhuli na jeuri kuwa "Kama unaona tumekosea basi anzisha chama chako".

Kwa kweli sikutegemea kiongozi haswa wa upinzani kutoa majibu ya nyodo kama haya kwa wananchi wanapouliza maswali ya msingi juu ya mienendo ya kisiasa nchini.

Labda Zitto afahamu tu kuwa sababu mojawapo ya leo ACT-Wazalendo kuwa hapa ni haohao wananchi ambao leo anawajibu kwa nyodo kuwa "anzisheni chama chenu"

Lakini pia Zitto akumbuke kuwa kuna watu wamekifia hicho chama, Wakati akijibu kwa majibu ya "Anzisheni chama chenu" Je amelifikiria hili kuwa kuna watu wame-pay ultimate price kwa hicho chama au kwa course yake waliyoinadi kwao na kwa hiyo ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wana haki ya kuhoji ukinyongakinyonga wa misimamo iliyowafanya hapo awali wawe tayari kukipigania hicho chama?

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Viongozi wa ACT sasa hivi wameacha kujibu maswali magumu ya wananchi juu ya hatua yao ya kuingia kwenye SUK wakati waliitangazia dunia na nchi kiujumla kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa haramu, Zitto mwenyewe akaweka saini tamko la pamoja la Upinzani kuwa hawautambui uchaguzi ule pamoja na natunda yake, Sasa leo wananchi wakihoji wanaambiwa jamani eeh kama hamtaki tulichokifanya basi nendeni CCM, au NCCR yaani ni majibu ya kifedhuli uliopitiliza!. Sasa wameacha kutoa majibu kwa wananchi, wameanza kublackmail wanachama wa ACT na kutoa kauli za nyodo kwa wananchi, kuwa "ACT ina wenyewe na nyie kaanzisheni chama chenu"

Sasa leo tunaona kwa macho yetu, watu tuliodhani ni wakomavu wa kisiasa, tuliodhani kuwa mashambulizi yao kwa CCM basi wao labda wana ngozi ngumu na kwamba labda wao wakipewa nchi basi watakuwa humble, watakuwa na humility, watajibu hoja kwa hoja kumbe hawa jamaa ni arrogant(wenye viburi), intolerant(wasio wavumilivu) na wanajiona wao ni wamiliki wa taasisi kwa kuwa walizianzisha na si wahudumu tu wa taasisi ambazo wao ni wanachama.

Hawa wapinzani hawana blank cheque ya kutuletea jeuri sisi wananchi, Kwa miaka mingi tumekuwa tukiishabumbulia CCM, lakini na wenyewe hawana impunity, tutawaekeza ukweli maana hivyo vyama kwa namba moja au nyingine vinanufaika kwa jasho la wananchi iwe kwa ruzuku au wanasiasa wao kulipwa kwa kodi za wananchi n.k

Zitto acha jeuri kwa wananchi, Jibu hoja na frustrations zao kwa hekima, utulivu, nidhamu na utu. Bila wananchi usingekuwa hapa kuwa na humility.

Hebu kwanza tumsikilize Zitto wa baada ya uchaguzi kisha tusome kuhusu Zitto wa sasa na tweet zake za nyodo kwa wananchi:

View attachment 1649528

Kisha tazama majibu yake ya sasa mwezi mmoja na nusu tu baada ya uchaguzi:
View attachment 1648516

Na mahali pengine anamjibu mwananchi hivi:

View attachment 1648775

Pia ameanza kublock watu wanaomcriticize mitandaoni:

View attachment 1649138

Ila jamaa we Fake sana. Unataka watu Waishi unavyotaka wewe. Na mbaya zaidi wewe unanuka damu na ghasia. Hutaki Amani. Watu kama nyie mngetamani sana Kuwe na Vita Sijui kwa faida ya Nani. Nakwambia watz Ni watu Peace sana. Wanawajua watu wajinga na wapenda ghasia msio na kazi kama wewe. Sijui mkuu umeachika. Sijui una vyeti Fake. Sijui jambazi. Maandiko yako hayana hata dalili ya mtu mwenye maisha yake na majukumu.
 
Unazungumzia hisia ambazo hata maalim na Zitto hawawezi kukuamini. Siasa ni kujenga trust kwa wananchi sio kujenga tumbo lako. Hata wa Wazanzibar leo hawamwamini tena Maalim. Ni bahati mbaya ndo hatashiriki tena siasa za kuchaguliwa, ninaamini. lakini, angekuwa na umri wa kugombea 2025 ninakuhakikishia ni watu wachache sana angewakokota, wengi wameishamshtukia. SUK ilikuwepo kabla ya Maalim na Zitto kuungana na Chadema na vyama vingine kuharamisha uchaguzi na kuzitaka jumuiya za kimataifa kuishughulikia serikali ya CCM. Leo Maalim na Zitto hawaaminiki tena hata kwenye jumuiya za kimataifa! Hiyo IQ unayoisema iko kwenye matumbo yao haipo katika shida za wananchi!
Wazanzibar washafahamu nini kinaendelea ndio maana yalikywa mafungu 2 ikiwa ACT na CUF so kila kundi wakaona wengine wasaliti, nawanasiasa wetu USALITI WANAO SANA TENA SANA NDIO MAANA WANANCHI WAMECHACHOKA KUWASIKILIZA UKIANZIA UFISADI BAADAE MTU SAFI THEN WANAJIFICHA USO MWILI WANAUACHA nb bora upambane ukiwepo co kuagiza kma remote
 
Unazungumzia hisia ambazo hata maalim na Zitto hawawezi kukuamini. Siasa ni kujenga trust kwa wananchi sio kujenga tumbo lako. Hata wa Wazanzibar leo hawamwamini tena Maalim. Ni bahati mbaya ndo hatashiriki tena siasa za kuchaguliwa, ninaamini. lakini, angekuwa na umri wa kugombea 2025 ninakuhakikishia ni watu wachache sana angewakokota, wengi wameishamshtukia. SUK ilikuwepo kabla ya Maalim na Zitto kuungana na Chadema na vyama vingine kuharamisha uchaguzi na kuzitaka jumuiya za kimataifa kuishughulikia serikali ya CCM. Leo Maalim na Zitto hawaaminiki tena hata kwenye jumuiya za kimataifa! Hiyo IQ unayoisema iko kwenye matumbo yao haipo katika shida za wananchi!
CCM inajua sana kula na jumuiya za kimataifa, ndio maana wamedumu mpaka leo. Katika utawala wa Magu walioguswa sana ni wamarekani na wakanada. Nchi nyingine bado zinakula na CCM vizuri tu. Kwamfano: Uingereza ndio muekezaji namba moja TZ na hakuna hata rasilimali yake hata moja iliyoguswa moja kwa moja. Hawa ni rahisi kuzungumza na wamarekani na kuwapoza. Tigo, ni shirika linamilikiwa na waswidi - Walishiriki kikamilifu kuzuia mawasiliano wakati wa uchaguzi. Wamelaumiwa sana lakini waliamua kuufyata tu, kwa vile wanapata wanachokitaka toka kwa CCM.

Mimi ninaamini hata kwa ACT kuingia SUK baadhi ya jumuiya za kimataifa zimeshiriki sana kuwa wadau wa mazungumzo hayo. Nyuma ya pazia za hii SUK ya wakati huu kuna mambo mengi ambayo wewe na mimi hatutayafahamu. Ila moja ninauhakika, kuwa ZEC itajireform, kwa umbali gani? siwezi kueleza!

Ninachotaka kukueleza kikubwa ni kimoja tu, CCM iko tayari kuuza mali za nchi yote kwa wageni ili wabaki madarakani. Na hii ndio ilichokiwezesha chama hiki kuwa madarakani mpaka leo. Na kiukweli kwa ujanja huu hiki chama kitakaa sana kwasababu jumuiya za kimataifa wala hazina kipaumbele cha haki za binaadamu, bali wanaangalia iterest zao. Wala si jina ACT, CHADEMA AU CCM ndio wanachovutika nacho sana- hapana, ni nani katika vyama hivyo vinaweza kutoa dau kubwa kwao.
 
Back
Top Bottom