Bibi Ntilie
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 245
- 8
Mheshimiwa Zitto,
kwanza hongera sana kwa kuteuliwa kwako. Hii ni dalili kwamba kazi zako kama mbunge zinathaminiwa na watu wengi hata nje ya nchi yetu.
Ila tu mimi pia nina ushauri, pamoja na kushiriki kwenye tume mbalimbali, weka juhudi zako kubwa kwenye kuendeleza jimbo lako la Kigoma. Mafanikio yako kama mbunge yatakuwa judged na juhudi zako za kuwakomboa wana jimbo lako kuliko kitu kingine chochote.
Ukianza kushiriki hizi tume na kamati mbalimbali ni rahisi mno kujisahau na kukuta jimbo linabaki pale pale.
Mafanikio mema katika shughuli zako.
Zitto Hongera.
Naungana na Mheshimiwa 'Mtanzania' kumtahadharisha Zitto, na kuongeza kwamba mara nyingi hizi posts za kimataifa huwa zinalevya! Tanzania ilivyo sasa inahitaji kwa asilimia mia nguvu za vijana kama Zitto wenye uchungu wa kweli na taifa hili.
Zitto, usije ukawa kama akina wengine ambao wamepata uwakilishi Bunge la Afrika Mashariki tu na hatuwasikii tena wakivalia njuga ama kujihusisha ipasavyo na masuala ya ndani ya nchi kama ilivyokuwa huko nyuma.