Mtazamo: Kuteuliwa Kwa Naibu Waziri Mkuu ni ishara ya kuaminiwa kwa majukumu makubwa zaidi kimataifa PM Majaliwa na Rais Samia

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Tofauti na wengi wanaoona ,uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu umekuja kufuatia mamlaka kutomuamini Waziri Mkuu lakini mtazamo huo upo tofauti na mtazamo wangu.

Kwa mtazamo wangu, mamlaka imemuamini sana Waziri mkuu na uteuzi huu una lengo la kumuamini zaidi kwa majukumu makubwa ya kimataifa.

Sote tunamtambua Waziri mkuu Majaliwa ni mchapakazi kwelikweli na amefanya vema katika utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini akiwa kama Waziri Mkuu hivyo Sasa ameonekana anaweza kusaidia utendaji kimataifa na ndio maana uteuzi wa nafasi ya Naibu Waziri ukawepo na Naibu Waziri mkuu amepewa majukumu ya kuratibu shughuli za serikali ikiwa na maana kwamba Waziri Mkuu atakapokuwa katika majukumu mengine ya kimataifa serikali iendelee kuratibiwa na Naibu Waziri mkuu.

Kama tunakumbuka vizuri mwezi wa tano, Rais Samia aliunda tume kuchunguza utendaji wa wizara ya mambo ya nje katika kufanikisha diplomasia ya uchumi. Hatujasikia bado matokeo ya tume Ile lakini ninaamini mapendekezo yake ndio yameleta mabadiliko kwenye wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki.

Kwa kuwa waziri mkuu amefanya kazi nzuri hapa nchini ni wakati sahihi Rais ameona aanzishe cheo cha Naibu Waziri mkuu ili Waziri mkuu amsaidie kwenye masuala ya uratibu na usimamizi wa kimataifa. Huu ndio mtazamo wangu.
 
Kwani huyu naibu hawezi kuwa waziri mkuu kabisa?

Au mnaogopa nini kumtoa huyu ili huyu achukue hiyo nafasi, ukweli ni kuwa aliyepo ajiangalie, wanasema mtu mzima afukuzwi ila matendo na tabia za pale ulipo zitakuonyesha!.

Kuna uwoga unaonekana kupitia nafasi yenu hiyo ya unaibu waziri mkuu, pamoja na kuongeza mzigo kwa serikali mimi nimeona ni uoga wa kuipangua serikali baada ya kumtoa huyu aliyepo.

Hapo naona inaogopwa katiba ambayo uko kwingine inachezewa tu pasipo hofu!.
 
Back
Top Bottom