Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea...

Tunalia kwa vile Zitto kasema Dowans wasipolipwa watakamata mali za Tanzania Abroad!

Legally, what has to be the way forward with regard to this issue? Any suggestion my friend Fundi Mchundo.

Mimi si mwanasheria kama my learned friend alivyonikumbusha. Hapa nionavyo mimi ni kuwa hatuna recourse bali kuheshimu maamuzi ya arbitrators. Kitu pekee tunachoweza kufanya ni kuwachukulia hatua za kiutendaji wale ambao waliotufikisha hapa. Bahati mbaya historia inaonyesha kuwa hatuna hiyo political will.

Athari ya kutoheshimu uamuzi huu ni kubwa kuliko huko kukamatwa assets. Credibility yetu katika international arena itashuka na wale wote watakaoingia mkataba nasi watatutoza zaidi ( kwa mfano kusisitiza kiasi kikubwa cha bond kiwekwe kwa ajili ya kulipia vitu kama hivi vikitokea) ingawa wengi watakataa tu kufanya biashara nasi. Hii itatuacha na matapeli kama hawa Dowans na Richmond maana wanajua wana njia zao za kutuchuna!

Amandla.....
 
Mimi si mwanasheria kama my learned friend alivyonikumbusha. Hapa nionavyo mimi ni kuwa hatuna recourse bali kuheshimu maamuzi ya arbitrators. Kitu pekee tunachoweza kufanya ni kuwachukulia hatua za kiutendaji wale ambao waliotufikisha hapa. Bahati mbaya historia inaonyesha kuwa hatuna hiyo political will.

Amandla.....

Hakuna jinsi zaidi ya kuwalipa Dowans. Zitto could be right again.

Happy new year to you Fundi Mchundo and all JF members.
 
I beg to differ. The fact that we agreed to enter into arbitration with Dowans makes the issue of its legality moot. Hivi tunataka kusema kama award ingekuwa against Dowans tungekataa kupokea kwa sababu hiyo kampuni ni dubious? Tuweke pembeni huu uzalendo feki na tukubali kuwa watu tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha wametuangusha. Tulipe halafu tugeuke na kuwashikisha adabu wale waliotuingiza katika hii predicament. Ukweli ni kuwa mpaka hapo tutakapo-demand accountability kutoka kwa wale ambao tunawapa dhamana ya kutuongoza tutaendelea kuwa "kichwa cha mwendawazimu". Kuendelea kukataa kulipa kutazidi kudhihirisha ukweli huo. Zitto yuko sahihi kwenye hili.

Amandla........
lakini si tumeisha ambiwa ya kuwa ili hukumu hii iwe legally binding, lazima isajiliwe mahakamani? kama ni hivyo huoni kama ndio sehemu ya kuanzia kuupinga huo uamuzi?
matatizo mengi ya hii kadhia ni ya kupikwa
1.kuanzia jambo la tununue au tusinunue, ni la watu hao hao katika dhima yao ya kutaka kutuibia ndio wanaosema hivyo, na sisi jambo hilo lilipingwa tumelipinga.
2. kuhusu kuvunja mkataba nalo ni suala la watu hao hao kutafuta njia mbadala ya kutuibia baada ya jambo la kwanza kushindwa.
3. na hitimisho la jambo hilo kwenda kwenye hicho kitu icc/abbitration nako ni muondelezo wa hatua hizo mbili za mwanzo kama njia nyingine tofauti bila ya sisi kujua ila kupewa huo uamuzi na mambo ya kisheria, ambayo inakuwa ni ngumu kwa mtu asiye jua sheria/ asiye na nyaraka muhimu za hii kesi kuliongelea kwa ufasaha jambo hili.
hitimisho hakuna haja ya kumsifia au kumuunga mkono mtu yoyote anaye halalisha iwe ununuzi au kulipwa fidia kwa wahusika wa hii kampuni, infwact wafadhili wanaliangalia vizuri tu hili jambo na kuwaona serikali yetu ina watu wa namna gani, iwe ni jk, pinda, ag, pcccb, na wabunge uchwara
 
Mkuu. Hii si hukumu bali ni uamuzi. Ninavyoelewa mimi, mahakama wala haihusiki.

Bottom line ni kuwa mambo ya kiutendaji tuwaachie watendaji (technocrats). Huu mchezo wa kufanya maamuzi technical kisiasa ndio uliosababisha yote haya. Kuvunja mkataba si kitu cha kufanyia mashara hata siku moja.

Na ndio, wafadhili wanaangalia kama tutaheshimu maamuzi ya chombo kinachotambuliwa dunia nzima.

Amandla.....
 
Zitto is old news!
Tanesco must pay Dowans. Period!
This will be a big time lesson for other politicians like Prof. Tibajuka:embarrassed:
Raj Patel JR,

Do you also have a power of attorney to receive payment from wananchi aka " vichwa vya wendawazimu"?
Just present it to Werema.
 
Waberoya,

..Zitto alikuwa amepotoka kuhusu suala hilo.

..mapendekezo yake yalikuwa mitambo ya dowans ITAIFISHWE na serikali.

..kuna mambo mawili yalijitokeza. hoja ya kwanza ilikuwa kununua mitambo ya Dowans, na hoja ya pili ilikuwa inahusu uhalali wa mkataba wa Dowans na kama Tanesco wavunje mkataba au la.

..hoja ya kwanza ilipingwa na wabunge na wananchi. badala yake mapendekezo yalikuwa Tanesco inunue mitambo yake yenyewe, na zaidi iepukane na middlemen.

..sijui kwanini Tanesco walivunja mkataba. they really owe us an explanation on this issue.

NB:

..kuna watu wanajaribu kutumia "hukumu" hii kama mtaji wa kisiasa.
 
Me nishasema sijaona mwanasiasa TZ hii ambae anataka kweli kutuletea maendeleo,wote wachumia tumbo tu,dhuluma na ubabaishaji ndo umewajaa mioyoni mwao. Kambarage peke yake ndo alikua na nia thabiti na hii nchi,wengine wote wababaishaji na wezi wakubwa

Ndugu Macheda ningependa nikupinge. Dr Slaa ni kiongozi ambaye sio mwizi, dhulumati, anachumia tumbo, mbambaishaji na asiye na nia ya kweli na nchi hii. Kama huamini toa ushahidi kuonyesha ushahidi unaothibitisha ana moja ya mambo hayo matatu! Na ndio maana umeona watu wengi wamejitokeza kumchagua hadi kumpatia kura nyingi ye na chama chake.
 
Tumfanyeje Huyu Rostam maana tunalalamika tuuu na yeye anazidi kutumaliza hebu semeni sasa tufanyeje?!!

Mkuu,

Jibu rahisi. Ni kukaa kwenye key board tu, tuandike, tuandike, hasira zikiisha tutapata jibu la nini kifanyike.
nini ufanye, nini nifanye na nini tufanye!!
In the mean time endelea kubonyeza vitufe vya key board yako.

Au washauri wale "watu" waliofikiria yule mkuu wa majeshi wa zamani kuwa ni jambazi, watusaidie katika hili.

Nani yule?? Mboma!!???
 
Fundi Mchundo said:
Mkuu. Hii si hukumu bali ni uamuzi. Ninavyoelewa mimi, mahakama wala haihusiki.

Bottom line ni kuwa mambo ya kiutendaji tuwaachie watendaji (technocrats). Huu mchezo wa kufanya maamuzi technical kisiasa ndio uliosababisha yote haya. Kuvunja mkataba si kitu cha kufanyia mashara hata siku moja.

Na ndio, wafadhili wanaangalia kama tutaheshimu maamuzi ya chombo kinachotambuliwa dunia nzima.

Amandla.....

Fundi Mchundo,

..ningekuwa serikalini i would been very tempted to tell Dowans to go f.u...themselves.

..kuna Valambia anaidai serikali na hajalipwa mpaka leo, sasa ije kuwa hao Dowans.

..sidhani kama wawekezaji wataacha kuja nchi hii kwasababu tumekataa kuwalipa Dowans.

..nchi hii ina madubwana[gold,uranium,gas..] kibao na hayo yanasababisha "wakubwa" wavumilie madudu ya kila aina yanayofanywa na serikali yetu.

..sekta za mafuta, nishati, na madini, ndiyo uchochoro wa vigogo kujichotea mapesa nchi hii. Dowans ni mradi wa vigogo.
 
Ni "Uamuzi" that is why it has to be registered in order to make it legal binding. na kuwa registered wapi? Mahakamani.
kuhusu hayo mengine uliyo yaongelea ya technorants/wanasiasa nk ni kwamba hili jambo lina scenario nyingi ambazo zimejengwa mahususi na watu walioteuliwa iwe kisiasa au kitaaluma ili kufanikisha wizi huu. yaani kikibimburuka mwana siasa ana mkingia kifua mwana taaluma, na vivyo hivyo mambo yakienda mrama kwa mwana siasa, mwana taaluma ana kuja na kauli ya kitaaluma kumtetea huyo mwana siasa, na ndio sindima/ngoma inayo chezwa sasa kuanzia Wizara husika/AG/PM magazeti na wabunge uchwara.
Sasa ukiangalia hilo suala la kuvunjwa kwa Mkataba ni nani aliye fanya na kwa nia gani? utakuta ni hao hao wanasiasa/technorants wetu ambao wako katika utatu mtakatifu wa kulindana.
Lakini hapo hapo tuchukulie scenario yako kwamba tumewaachia technorants walifanyie uamuzi jambo hili, lakini kwa makusudi mazima mtu huyo apindishe taaluma yake apendele kitu fulani? je kwa nchi iliyo adilifu hato tokea kiongozi/mwanasiasa aliye na nia ya dhati aka-kemea jambo hilo? au akachukua hatua zifaazo katika kum-discipline huyu technorant. juzi juzi kulitokea tatizo la umeme Dar nk ikasemekana Bosi moja ambaye ni technorants alitoa ushauri/uamuzi mbaya ulio leteleza mitambo kuharibika.
Je ni mara ngapi technorant kama Purchasing officer akafanya uamuzi mbovu? tena kwa hapo tanesco mifano ipo mingi tu toka enzi za Mzee Mosha/Mhavile nk ambapo wana siasa wetu walikuwa hawaingili kwa sana mambo ya utendaji wa kila siku wa Tanesco.
Je ni mara ngapi hao Technorants kama wahasibu wameliibia shirika la Tanesco.
Hitimisho ni kwamba si suala la technorants kuachiwa kufanya mambo kitaaluma tu, bali kuwepo na utawashi wa kufanya jambo kitaaluma, kitu ambacho hakipo au kina chezewa kutokana na outside influence.
kuhusu ku-heshimu huo uamuzi ni jambo la kichekesho ikiwa binadamu mwenye akili zake timamu akavua nguo zake mbele ya kadamnasi na umati huo ukamwachia tu huyo juha kufanya hivyo bila kumpa adhabu stahili, halafu baada ya hapo unaenda mahakamani kuomba msaada wa kisheria au unawafuata hao benki ya dunia/imf, eu g8 nk kupeleka kibakuli chako kisa eti uliadhibiwa kwa kuvua nguo, sasa unaomba wakupe suruali/sketi nk nk. watakuuliza ilikuwaje mpaka wa kakupora hiyo kaptura/suruali nk nk. na tuna uhakika gani tukikupa hiyo suruali hutaenda kuivua tena.
Je
 
Serikali yetu imeshapoteza sifa za kuiongoza nchi, na kibaya zaidi hata hawalitambui hilo. Waziri wake mkuu anatangaza kuwa kuna watu hatari ambao serikali haiwezi kuwashitaki maana wanaweza kuipindua nchi. Rais wa nchi anampa maelekezo mkurugenzi wa kupambana na Rushwa watu wa aina gani wakamatwe na wepi wasiguswe. Mwanasheria mkuu anakataa kukata rufaa ya kesi ambayo hawezi kueleza wananchi ni nini ushauri wa ofisi yake katika huu mkataba kabla haujafikiwa na ulivunjwa na nani na kwa kukiuka sheria ipi. Wakati huo mkataba unavunjwa nchi ilikuwa haina serikali ila sasa baada ya kuamuliwa hii kampuni hewa kulipwa ndio AG anajifanya kuzinduka na kuonyesha kwamba serikali ni madhubuti kuwapa watu haki ambao hata hawajulikani na pesa yao iwekwe kwenye account na bank zisizojulikana kwa umma. Hii ni kwa namna ya mtindo ule ule wa kampuni ya kagoda ya mmiliki asiejulikana kurudisha pesa zilizoingizwa kwenye account isiyojulikana na kwa bank ya kufikirika. Kweli huu ni usanii usiyo kifani. Nathubutu kusema toka nchi hii ipate uhuru haikuwahi kuwa na uongozi dhaifu kama huu wa awamu ya tano. Ndio maana Nyerere alikuwa akiona mbali na alitumia nguvu kubwa sana kumzuia Jk dhidi ya mkapa, na hata kama angekuwa hai wakati wa awamu ya tano asingeweza kuuruhusu udhaifu kutamalaki namna hii.
Naweza kuona muunganiko wa mafisadi na mpango wa kumwondoa Sitta ktk uspika maana walijua kamwe asingeweza kukubaliana na upuuzi huu wa kijinga. Yule mama speaker yeye ni mtu wa kuwekwa tu na sidhani kama ana ubavu wa kuruhusu mjadala huru bungeni juu ya hii hukumu ya kuwapora wendawazimu wa kidanganyika pesa zao. Mungu lirehemu taifa hili linaloonekana kuwa la kiuenda wazimu.
.
 
Fundi Mchundo,

..ningekuwa serikalini i would been very tempted to tell Dowans to go f.u...themselves.

..kuna Valambia anaidai serikali na hajalipwa mpaka leo, sasa ije kuwa hao Dowans.

..sidhani kama wawekezaji wataacha kuja nchi hii kwasababu tumekataa kuwalipa Dowans.

..nchi hii ina madubwana[gold,uranium,gas..] kibao na hayo yanasababisha "wakubwa" wavumilie madudu ya kila aina yanayofanywa na serikali yetu.

..sekta za mafuta, nishati, na madini, ndiyo uchochoro wa vigogo kujichotea mapesa nchi hii. Dowans ni mradi wa vigogo.

Mkuu. I share your sentiments. Ukweli ni kuwa serikali imebanwa na haina jinsi. Arbitration kama hizi zinazosimamiwa na ICC ni tofauti na kesi zetu za nyumbani kwa vile kile ni chombo ambacho kinatambuliwa kimataifa na mahakama zetu ni zetu. Hii ndiyo maana katika mikataba mikubwa arbitration inapendelewa zaidi maana ni enforcable nje ya mipaka ya nchi. Dowans anaweza kwenda kokote ambako Tanzania ina assets na kudai kupewa kutokana na uamuzi wa arbitrators wakati maskini Valambia hawezi.

Kwenye biashara, ICC ni kama the Hague. Wawekezaji wa MAANA ( sihesabu wachina miongoni mwao) wanataka uhakika kuwa nchi wanakowekeza wanafuata sheria hata kama inawauma. Wawekezaji kama hao watasita kuja nchini na kama wakija wataweka masharti magumu mno.

Katiika extractive industries tutawaona maana mwisho wa siku wenye hasara ni sisi. Hayo madini ni finite na iko siku yatakwisha na tutabaki na mashimo na uharibifu mwingine. Lakini kwenye investments za maendeleo kama viwanda, teknolojia,huduma etc. hatutawaona. Jiulize makandarasi wote wa maana wameenda wapi?

Amandla.......
 
Ni "Uamuzi" that is why it has to be registered in order to make it legal binding. na kuwa registered wapi? Mahakamani.
kuhusu hayo mengine uliyo yaongelea ya technorants/wanasiasa nk ni kwamba hili jambo lina scenario nyingi ambazo zimejengwa mahususi na watu walioteuliwa iwe kisiasa au kitaaluma ili kufanikisha wizi huu. yaani kikibimburuka mwana siasa ana mkingia kifua mwana taaluma, na vivyo hivyo mambo yakienda mrama kwa mwana siasa, mwana taaluma ana kuja na kauli ya kitaaluma kumtetea huyo mwana siasa, na ndio sindima/ngoma inayo chezwa sasa kuanzia Wizara husika/AG/PM magazeti na wabunge uchwara.
Sasa ukiangalia hilo suala la kuvunjwa kwa Mkataba ni nani aliye fanya na kwa nia gani? utakuta ni hao hao wanasiasa/technorants wetu ambao wako katika utatu mtakatifu wa kulindana.
Lakini hapo hapo tuchukulie scenario yako kwamba tumewaachia technorants walifanyie uamuzi jambo hili, lakini kwa makusudi mazima mtu huyo apindishe taaluma yake apendele kitu fulani? je kwa nchi iliyo adilifu hato tokea kiongozi/mwanasiasa aliye na nia ya dhati aka-kemea jambo hilo? au akachukua hatua zifaazo katika kum-discipline huyu technorant. juzi juzi kulitokea tatizo la umeme Dar nk ikasemekana Bosi moja ambaye ni technorants alitoa ushauri/uamuzi mbaya ulio leteleza mitambo kuharibika.
Je ni mara ngapi technorant kama Purchasing officer akafanya uamuzi mbovu? tena kwa hapo tanesco mifano ipo mingi tu toka enzi za Mzee Mosha/Mhavile nk ambapo wana siasa wetu walikuwa hawaingili kwa sana mambo ya utendaji wa kila siku wa Tanesco.
Je ni mara ngapi hao Technorants kama wahasibu wameliibia shirika la Tanesco.
Hitimisho ni kwamba si suala la technorants kuachiwa kufanya mambo kitaaluma tu, bali kuwepo na utawashi wa kufanya jambo kitaaluma, kitu ambacho hakipo au kina chezewa kutokana na outside influence.
kuhusu ku-heshimu huo uamuzi ni jambo la kichekesho ikiwa binadamu mwenye akili zake timamu akavua nguo zake mbele ya kadamnasi na umati huo ukamwachia tu huyo juha kufanya hivyo bila kumpa adhabu stahili, halafu baada ya hapo unaenda mahakamani kuomba msaada wa kisheria au unawafuata hao benki ya dunia/imf, eu g8 nk kupeleka kibakuli chako kisa eti uliadhibiwa kwa kuvua nguo, sasa unaomba wakupe suruali/sketi nk nk. watakuuliza ilikuwaje mpaka wa kakupora hiyo kaptura/suruali nk nk. na tuna uhakika gani tukikupa hiyo suruali hutaenda kuivua tena.
Je

August. Hilo la registration silijui lakini sidhani kama mahakama yetu ina uwezo wa kukataa kurejesta kama inapaswa kufanya hivyo.

Mimi ninachozungumzia kuhusu technocrats ni accountability. Technocrats anaweza kuchukuliwa hatua kirahisi kuliko wanasiasa. Mlingwa alitupwa lupango wakati waziri wake anapeta. Jamaa wa BOT nao hivyo hivyo. Sasa kama technocrat anaachiwa aibie shirika bila kuchukuliwa hatua utamlaumu nani? Kama technocrat kakabidhiwa shirika halafu analiangusha bila kuchukuliwa hatua tutamlaumu nani? Ninavyoona mimi ni kuwa siasa imepenyeza mno katika utendaji kiasi ambacho hao technocrats wanalindwa kisiasa na si kiutendaji. Watendaji wanawekwa kwa sababu za kisiasa na si kutokana na uwezo wao na ndio maana wanapobolonga tunashindwa kuwachukulia hatua. Haitakiwi kuwa hivyo.

Amandla......
 
rais wenu kikwete amesema nini na yeye ndiye kila kitu,

Guys lets join hands let us think, say aloud, and demonstrate that..

1. JK should step down
2. AG should step down
3. all who knew for sure what will happen while abrogating this matters should step down
 
Mh. Ziito Kabwe kweli aliona mbali kuhusu dowans wakati alipo kubaliana na mpango wa mitambo hiyo kununuliwa na serikali kwa Tshs 100bn. Leo hii, tunalazimika kuilipa dowans Tshs 97bn kama fidia ya kuvunja mkataba na mitambo hiyo bado itabakia kwenye miliki ya dowans. Hapo hamwoni kuwa Ziito msimamo wake ulikuwa wa kuangalia mbali zaidi na kwa kujali maslahi ya taifa zaidi, kuliko wakati ule wakina Slaa walimpinga na kumuona msaliti. Leo hii maneno na ujasiri wake umethibitika kwani dowans hatuna jinsi ni lazima italipwa tu.
 
Are you talking about Ziito, or Zito...
 
Kumekucha GB ... habari ya asubuhi mkuu.... naona zomba ame log out ... Genius Brain ume log in
 
umbali wa kuona wa akili ya zitto na yako ni sawa tu.

Wewe uliona wapi mtu unaambiwa ulipe Tshs 100 bn umiliki mitambo Bunge likakataa kwa kupingwa vikali na wakina Slaa wakati huo . Madhara yake leo hii Tshs 97bn zinalipwa na mitambo inabakia ya kwao. Kumbe nawe huelewi , habari ndio hiyo !
 
Back
Top Bottom