Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Oct 14, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mhe, Zitto Kabwe (MB) atakuwa na Press Conference kesho Oktoba 15, mida ya saa 6 adhuhuri Cortyard Hotel - Dar es Salaam.

  Press Conference hii itahusiana na Mgawo wa Umeme unaoendelea. Kwa waandishi mlio Dar tunatarajia mtatufahamisha kinachoendelea. Kama kawaida, JF itatuma mwakilishi wake kutufahamisha kilichojiri.

  Stay tuned


  Update 1: Hiki ndicho alichoongea:


  TAMKO LA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI NA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA, NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE KUHUSU MGAWO WA UMEME NCHINI.

  COURTYARD HOTEL, DAR ES SALAAM
  OKTOBA 15, 2009.


  UTANGULIZI

  Kwanza niwashukuru ndugu zangu wana habari kwa kukubali kuja kunisikiliza, hatua ambayo kwangu ni fursa ya kuzungumza na umma wa Watanzania hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa letu lipo kwenye matatizo mengi, na kwakweli linapita kwenye kipindi kigumu sana kisiasa, kiuchumi na hivyo kijamii. Najua tunakabiliwa na matatizo mengi sana kama Taifa, kiasi kwamba ni vigumu kama kiongozi kuchangia mawazo kuhusu ufumbuzi wa matatizo yote yanayotukabili.

  Ni kwa msingi huo, leo nimeona nizungumze nanyi kuhusu hali tete ya mgawo wa umeme unaolikabili Taifa kwa sasa. Mwanzoni mwa mgawo huu sikupenda kusema chochote pamoja na kuulizwa sana na waandishi wa habari na wadau mbalimbali. Sikutaka kusema chochote nikiamini kwamba Shirika la TANESCO, Serikali, na kwa upande wa bunge, Kamati ya masuala ya Nishati na Madini, wangeweza kutoa majibu ya tatizo linatukabili. Badala yake, juhudi nyingi zimetumika kutafuta chanzo cha tatizo na kuchelea kutoa suluhu. Pia kumekuwa na shutma mbalimbali, mojawapo ikidai kuwa baadhi ya watendaji wa TANESCO wanajaribu kuthibitisha madai yao ya kitaalumu ya kununua mitambo ya DOWANS. Shutma kama hizi, ni dhahiri zinauelewa finyu juu ya vyanzo vya mgao wa umeme uliopo sasa, ambao unasababishwa na uhaba wa mashine na upungufu wa maji. Uelewa huu finyu si tu hauna manufaa, bali hautoi ufumbuzi juu ya tatizo lililopo sasa ili kuepuka madhara ya kiuchumi kwa taifa na wananchi wake.

  Kwa maendeleo yote duniani, nishati ya umeme ni msingi mmojawapo wa kujenga uchumi. Kwa utambuzi huu nchi mbalimbali duniani, hata zile zinazoweza kutoa huduma ya umeme kwa asilimia 90 kukidhi mahitaji yake, zinajaribu kuimarisha sekta zao za nishati kama msingi wa ujenzi wa maendeleo kwenye viwanda na wananchi wake. Nchi yetu ya Tanzania, huduma ya umeme inauwezo wa kuhudumia asilimia 12 tu na bado kunamgao.

  Ni kweli changamoto za kuendeleze sekta ya umeme ni kubwa sana, na mipango ya muda mrefu ipo ingawaji haitekelezwi kwa sababu mbalimbali, lakini si lengo la mazungumzo yangu ya leo. Kwa mazingira tuliyonayo sasa, hasa katika kufuatia kuporomoka kwa uchumi duniani, hatua za haraka hazinabudi kuchukuliwa kuliepusha taifa katika uporomokaji wa uchumi wa kitaifa unauweza kuzuilika. Huu ni wakati ambapo serikali inapaswa kufanya tathimini ya haraka ili kufikia muafaka wa taratibu zipi zichukuliwe kuepuka hasara zitakazoletwa na mgao wa umeme, na hivyo maongezi yeyote yajikite kutafuta suluhu ya kuondoa mgao wa umeme kwa haraka zaidi. Badala ya hali ya sasa ambayo mijadala na hatua mbalimbali zimejikita kutafuta chanzo cha tatizo bila kutoa suluhisho, huku madhara ya mgao yakiendelea kuwaumiza watanzania.

  Tumeambiwa na TANESCO kuwa Mgawo wa umeme wa masaa 14 kila siku msingi wake ni upungufu wa 90MW za umeme. Kwa mgawo huu TANESCO wanapoteza mapato ya takribani shilingi 200 milioni kwa siku! Lakini hii ni kwa upande wa TANESCO tu, bado kunamadhara mengi kwa upande wa wananchi na taifa kwa ujumla.

  MADHARA YA MGAWO WA UMEME KWA UCHUMI WA TAIFA.

  Ndugu zangu, mgawo huu una madhara makubwa sana, kuanzia kwenye uchumi mkubwa wa taifa (macro economy) hadi uchumi mdogo wa makampuni na mtu mmoja mmoja. Madhara ya mgawo wa umeme yana athiri mpaka wasio na umeme;

  • Katika sekta ya Ujenzi, mfano wa viwanda vya Simenti gharama za uzalishaji zimeongezeka sana. Kwa mfano Kampuni ya Twiga Cement hutumia dola za Marekani 10 kama gharama ya kuzalisha umeme iwapo wanatumia umeme wa TANESCO. Gharama hizi huongezeka mara 4 na kufikia dola 40 kwa Tani wakati wa mgawo. Hii maana yake ni kwamba bei ya Saruji itapanda kwa shilingi 1000 zaidi kwa kila mfuko wa Saruji. Watakaoumia hapa ni raia wa kawaida wanaojiwekea akiba ili kujenga nyumba zao.

  • Nimeambiwa sekta ya Mabenki inaathirika sana na mgawo wa umeme kwani gharama za kuwasha umeme katika matawi yao imeongezeka sana. Mfano, Benki ya CRDB sasa itatumia shilingi 400 kwa mwezi kwa gharama za umeme na Benki ya Barclays itatumia zaidi ya shilingi 210 milioni kwa mwezi. Zote hizi zinaongeza gharama za biashara na hivyo kupunguza kodi ya serikali.

  • Katika sekta ya Mawasiliano gharama za kuendesha minara ya simu zimeongezeka kutokana na kampuni za kugharamia mafuta ya kuwasha minara. Takwimu zinaonesha kuwa Kampuni ya Simu ya Zain sasa inatumia shilingi 700 milioni zaidi kwa mwezi kwa sababu ya mgawo. Kampuni ya Vodacom inatumia zaidi ya shilingi 800 milioni zaidi kwa ajili ya kuwasha minara yao. Hii maana yake ni kwamba gharama hizi zitapunguza kodi za makampuni ambazo kampuni zitalipa serikalini. Zaidi ya hapo mgawo husababisha matatizo ya mawasiliano kwa watu kushindwa kutumia simu zao kutokanana ukosefu wa umeme.

  • Madhara ya mgawo wa umeme yanamuathiri kila Mtanzania, Mkulima kwa mfanyakazi, wafanyabiashara wakubwa kwa wafanyabiashara wadogo. Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu, Kamati yangu ya Mashirika ya Umma tulifanya utafiti mdogo kuangalia madhara ya mgawo wa umeme kwa watu wa kawaida, tulikuta salooni moja wakatwambia wanatumia 8000/= pakiwa hakuna mgawo lakini pakiwa na mgawo wa umeme wanatumia hadi 68000 kwa ajili ya umeme wa jenereta, sawa na gharama ya ziada ya shilingi 60,000/= kwa siku. Hivyo mgawo unawaumiza sana wajasiriamali wadogo wadogo na kuharibu mitaji yao na hivyo kuongeza umasikini.

  • Hivi juzi nilikuwa nazungumza na watu wenye mashine za kusaga nafaka huko Nzega naambiwa , pakiwa hakuna umeme wanatumia mafuta ya diesel na gharama za uendeshaji ni mara tatu ya gharama wanazotumia umeme ukiwepo. Hii maana yake ni kuwa madhara ya mgawo yanamgusa mwananchi wa kawaida kabisa vijijini kwa kuongeza bei za vyakula na hivyo kuongeza mfumuko wa Bei.

  • Nimekwenda Internet café moja hapa Dar es salaam, wanasema bei ya huduma ya internet kwa saa siku za mgawo wa umeme ni shilingi 2000 wakati siku umeme ukiwepo ni sh1000. Hii ni mifano ya maeneo machache tu kuhusu mgawo, ambayo kwa ujumla inaonesha wazi kuwa mgawo wa umeme unapandisha gharama za maisha (cost of living) wakati mapato ya mtanzania yakiwa duni.
  Serikali na Taifa linapoteza mabilioni ya fedha kutokana na mgawo huu wa umeme. Naamini baadae Benki kuu itakuja kufafanua hili. Lakini Taifa linapokuwa kwenye mgawo uchumi wa unayumba. Nimewaambia kwamba mgawo wa 2006 peke yakeuliporosha uchumi kwa nukta moja ambayo ni sawa na shilingi billion 250. Na sasa ninawaambia, tukiacha mgawo huu uendelee hata kwa miezi miwili, taifa litatetereka vibaya sana.

  • Mfumuko wa bei utazidi kupanda(cost push inflation),
  • Uwiano wa malipo ya nje utaathirika kwasababu ya kutumia pesa nyingi za kigeni kununua mafuta nje(import),
  • Gharama za uzalishaji viwandani zitapanda sana na kusababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha ambayo ingekusanya kama kodi.
  Inaumiza sana kuona kuwa tunaendekeza siasa rahisi tunaposhugulikia masuala mazito ya kitaifa kama Nishati. Inasikitisha zaidi pale tunapoona kuwa serikali inashindwa kuchukua hatua mahususi za kuhami uchumi wa Taifa letu. Serikali na Bunge hazitoi suluhisho la hali hii na ni wazi kuna kutupiana mpira wakati nchi inaumia. Serikali imewekwa madarakani ili ifanye maamuzi na tuihukumu kwa maamuzi hayo. Serikali ni lazima sasa iamue.

  3. HATUA NINAZOPENDEKEZA
  Nimesema mwanzo kwamba, kuendelea kwa mgawo huu wa umeme ni udhaifu wetu wa uongozi kushindwa kufanya maamuzi magumu lakini ya msingi, na badala yake kujikita katika kutafuta nani mchawi kila tunapokabiliwa na tatizo. Ni bahati mbaya sana hata vyombo vya habari vimejikuta vikiendelea kutoa taarifa za mchawi anatafutwaje badala ya kueleza madhara ya mgawo kama njia ya kushinikiza ufumbuzi wa tatizo.

  Wakati Taifa linakabiliwa na upungufu wa 90MW za umeme, na uchumi wa kila mtanzania unaathirika, hapa nchini tuna mitambo ya IPTL yenye uwezo wa kuzalisha 100MW, ambayo imezimwa kwa sababu ‘eti’ ina kesi dhidi ya serikali. Majadiliano kuhusu mgogoro huu bado yanaendelea bila kwisha. Hapa nchini tuna mitambo ya Dowans yenye uwezo wa kuzalisha 125MW, ambayo ni ya kuwasha tu. Lakini kwasababu tu serikali imeshindwa kufikia maamuzi, inaendelea kuwepo nchini huku Taifa linayumba kwa giza.

  Kama nilivyoeleza hapo awali, nishati ya umeme ni kichocheo kikubwa sana cha ukuaji wa uchumi na hatimae maendeleo ya kiuchumi. Kwahiyo kama kiongozi sikubaliani kabisa kuona nchi inaendelea kuwa gizani na kugharimu uchumi wa Taifa, kuongeza gharama za maisha ya mwananchi wa kawaida na hata kupunguza mapato ya serikali.

  Ninapendekeza;

  • Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.
  • Kwa kuwa mapendekezo ya TANESCO ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans yalipingwa na baadhi ya wanasiasa wenzangu na hatimaye kutonunuliwa na hivyo kusababisha mgawo uliopo hivi sasa, na kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu, na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans.

  4. HITIMISHO

  Mgawo huu wa takribani mwezi sasa umeshaligharimu Taifa kwa kiasi kikubwa sana. Mgawo huu ukiendelea kwa wiki tatu zijazo, madhara yake ni makubwa kiasi cha hata maamuzi ya serikali kuhami uchumi (stimulus Package) yaliyotajwa na Rais Kikwete mjini Dodoma mwezi Juni yatakuwa hayana maana kabisa kwani mfumuko wa bei na kudorora kwa shughuli za uchumi kutaporomosha ukuaji wa uchumi uliotarajiwa na mkakati huo.

  Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.

  Asante sana.

  KABWE ZUBERI ZITTO,MB
  Dar es Salaam.
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...chochote kile, I'll still say NO to Dowans!!
   
 3. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Atarudia tu yale aliyoyaandika na kuchapisha leo katika gazeti la Tanzania Daima... hana jipya ila kujigamba kwamba I told you so.... hana suluhisho huyu kijana zaidi ya kuifagilia Tanesco na Dr Rashid.... NEXT......
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 14, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Miafrika bana...they are still struggling with electricity!! Shame on them.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nitakuwepo na nitasema kama kutakuwa na kitu tofauti na hicho .
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Anatarajia kujaribu tena kuipigia debe mitambo ya Dowans. Kwa kuwa mgao umeshika kasi, basi atasema: "Siliniwaambia? Sasa kiko wapi?"

  Atasema mtambo wa Dowans utamaliza tatizo kwani mashine zile bado ziko pale Ubungo badala ya kuamriwa kuondolewa -- ni kubonyeza tu button -- na lo! umeme huoooooo!!!!! hakuna mgao tena!!!!!
   
 7. A

  August JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  mitambo ya wizi ni a big no, yeye azungumzia jinsi watakavyo maliza mjadala wa richmond nov, watuhumiwa waadhibiwe na kufilisiwa kama hili neno lina maana yeyote ? ndipo kutaifisha mitambo kuje au mumpe huyo mwizi apeleke anakojua.
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Hivi huyu kijana hana washauri? Kwa nini asiwaachie serikali wakahangaika na mizengwe yao ya umeme? Naona anafanya mchezo wa kununu kesi kama nilivyosikia kuwa kuna kabila fulani linapenda sana mchezo huo. Kama ningeweza kumshauri, ningemwambia afunge mdomo wake. Damage aliyoipata kwa kauli zake kuhusu Dowans ni kubwa sana kiasi kwamba hatakiwi kuanzisha mijadala mingine isiyokuwa na tija. Anyway, sikio la kufa....!
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Oct 14, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Babu, all buffoonery and foolishness aside, machungu ya mgao wa umeme mimi nayajua. Kinachonitatiza mimi ni swali moja tu: inachukua muda gani kulitatua hili tatizo la umeme? Karne nzima?

  Tokea niko shule ya vidudu tatizo la umeme lipo kitu ambacho kinaashiria lilikuwepo hata kabla sijawa fikra ama wazo katika vichwa vya wazazi wangu.

  Mbona majuu hili tatizo halipo? Ndio, hata majuu umeme hukatika lakini itokeapo hivyo kunakuwa na sababu nzuri na ya msingi. Hivi watu wa majuu wao wanafanya fanyaje? Aaagh I'm just tired.....
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hiyo ndiyo tofauti. Hapa kwetu ukikatika tu, tunategeneza mamilionea wa kuchonga!
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Watabiri wengiiiiiiiiiii si msubiri kesho tusikie atasemaje?...si wataalum wakiheshimiwa kuliko wanasiasa till then nchi itasogea...shame to wansiasa.
   
 13. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wanatumia Nuclear technology...je watakuruhusu wewe (Tanzania) kabla kukuweka kwenye list...
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwani hapa kuna kutabiri tena? Dogo ataongelea mgao wa umeme na msimamo wake katika hili unajulikana. Kama siyo kuja kuchafua hewa nini? Ingewezekana akanyamaza tu. Amini usiamini chance ya kuwachefua watu ni >75%!!
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Oct 14, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Nani aturuhusu? Kwani wao nani aliwaruhusu?
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Siasa ndio inaharibu kila kitu, hata masuala ya kitaalamu siku hizi yanatafutiwa ufumbuzi kisiasa
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Waganga wa mvua JF wengi kweli....
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,568
  Trophy Points: 280

  Natumai hatasema kwamba alikuwa right alipopigia debe ununuzi wa mitambo ya kifisadi ya *~Dowans.
   
 19. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Do people still take him serious?
   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwenye siasa wakati mwingine kukaa kimya kunaweza kuwa na faida kuliko kuongea.
   
Loading...