Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
hakuna cha kupongeza hapo, yeye si katoa taarifa tu? mnajuaje moyoni mwake kama kapendezwa na maamuzi ya secretariate? kweli humu wachanga wako wengi!!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.like name like they do.
peoples!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Congratulation Mh. Zitto!!! Hiyo ndiyo Democracy mze najua wabaya kinawauma, CHADEMA mwendo mdundooo!!!! Jamani huyu dogo Zitto upresida unamhusu for the futureeee!!!

Pia nawapongeza Chadema kwa ujumla, kwa kulimaliza hili swala vizuri, maana wabaya wake wlitegemea hapa kungezuka mgogoro wa kukata na shoka, hongereni sana.

Watu hawachelewi kupanga vichwa vya magazeti "Bundi atua Chadema rasimi" mwaka huu hakuna bundi, ila ni moto 3x3 kutwa mara 3 kila siku, hadi CCM ing'oke.
 
Zitto alipo onyesha nia ya kutaka kuwa kiongozi wa upinzani alishambuliwaaa!nakushutumiwa !!sasa hivi muungwana!!!!Ha ha ha ha!Washabiki wa chadema Jf kiboko!!!!
 
Tatizo kubwa la Zitto ni msimamo. Hana tofauti na Spika Mstaafu Sitta. Sisi wengine kwenye siasa za Nchi hii tumo tangu 1975! Hata sijui Zitto alikuwa wapi wakati huo.

Hii habari ya wewe kuwa kwenye siasa tangu mwaka 1975 inatuhusu nini sisi? Nina uhakika mwaka huo Zitto alikuwa ama hajazaliwa au alikuwa ni mtoto mchanga (Toddler).
 
Zitto alishutumiwa na wana ccm wa JF lakini ndani ya Chadema tulikuwa stable maana hatugombanii vyeo. Tuna staili tofauti sana na ccm.
 
Zitto anapongezwa kwa kipi au lipi? Ku-post maamuzi ya vikao kwenye facebook? I doubt him now than ever before!
 
Kingekuwa kichekesho kwa kweli. Zitto awe KUB, Anne Makinda awe Spika, Job Ndugai awe NS, Chenge awe Chief Whip wa wabunge wa CCM,....., Bunge la hovyo kabisa tangu uhuru!

Tuondoeni matongotongo hapo kwenye red tumezoea lugha yetu ya taifa
 
Hii habari ya wewe kuwa kwenye siasa tangu mwaka 1975 inatuhusu nini sisi? Nina uhakika mwaka huo Zitto alikuwa ama hajazaliwa au alikuwa ni mtoto mchanga (Toddler).

Ungeisoma pamoja na ile post nilioi-quote. Vinginevyo ipotezee tu kama kiswahili chenu cha sasa kilivyo!
 
Siyo jipya hilo kwani tulishasema jana kwamba kuna principle ya kumchagua leader of opposition na hata Zitto alikuwa analielewa hangeweza kunegate. Anachosema ni kuondoa shaka iliyokuwepo. Tunachoomba mshikamano uzidi na pipoz pawa!!!!
 
kutokana na mawazo na michango ya wana JF kuhusu Zitto kutumika kukigawa chama, leo imedhihirisha wazi kuwa watu bado hatujamwelewa Zitto Kabwe, dakika chache zilizopita Mhe. Zitto ame post kwenye facebook maneno yafuatayo "The party through its secretariat has adopted a westminster system to elect the leader of the opposition, following that Chadema caucus has endorsed Rt. Hon. Freeman Mbowe as the leader, Zitto Kabwe as his Deputy and Tundu Lisu as Chiefwhip." mimi kam mpiganaji wa miamvuli nasema nimependezwa na Mhe. Zitto kutoa kauli hii ambayo inaonyesha yeye binafsi amependezwa na hatua hiyo na kuwa yuko tayari kuwatumikia tanzania wote na mimi nikiwepo. Tuko pamoja. peoooopleeee

Chadema imeiva. haibabaishi kama wengine akina thithiem.
 
pongezi za nini wakati zitto alisema wazi kuwa ikiwa westminster system itafuatwa ambapo mwenyekiti wa chama ndiye anakuwa kiongozi wa upinzani basi yeye angekubaliana na uamuzi huo na kumuunga mkono mbowe lakini ikiwa american democracy style ingefuatwa basi angegombea...maana kimarekani huwa ni gombea goli..

mi nadhani Zitto ni mkomavu sana kidemokrasia kuliko wengi wetu hapa jamvini...na ni kwa sababu ya huo ukilaza wetu ndiyo kila mara tunamuona kama msaliti ingawaje ameshasema mara kadhaa...kamwe hatokisaliti chama alichoshiriki kukijenga..Zitto ameingia chadema akiwa sekondari kwao kigoma..si kama wengi wetu humu ambao mpaka juzi hapa 2005 tulimpigia kura kikwete.....ni baada ya slaa kulipua mafisadi pale TMK ndiyo baadhi humu wakaanza kujua alah..kumbe kuna upinzani!!!!

tofauti na wanasiasa wengi wa kiafrika na mashabiki wao...kwao upinzani maana yake ni kutaka kuleta mgawanyiko na ni uadui..hatujui kushindana kwa hoja...ni kwa mantiki hiyo mara nyingi zitto anashindwa kueleweka katika macho ya 'wanaojiita' wapinzani:smile-big:

Hatuwezi kuwazuia watu kutoa hisia zao hasa wakiwa na lengo la kuboresha kwa kukemea kile ambacho wanakiona kuwa kitaparanganisha chama. vilevile mshutumiwa anapo thibitisha ukomavu na kukidhi malengo ya wananchi wake hana budi kupongezwa. nani ajuaye kama maoni ya wana JF ndio yaliyopelekea malidhiano haya? Hongera Zitto kwa kuendelea kukidhi matakwa ya wananchi na wapenzi wa CHADEMA. vilevile tuliopigia CCM 2005 halikuwa kosa letu, kama lisivyo kosa kwa wakiopigia CCM mwaka huu. kwa takwimu hafifu nilizonazo CHADEMA imeonyesha kupata support kutoka maeneo yenye umeme ambapo watu wanaangalia TV na kusikiliza taarifa za habari kuliko vijijini. hivyo namaliza kwa kusema information is power. tuwaelimishe watu waelewe tusiwalaumu kwa kupigia cHAma cha Mafisadi. Hongera ZITTO
 
kutokana na mawazo na michango ya wana jf kuhusu zitto kutumika kukigawa chama, leo imedhihirisha wazi kuwa watu bado hatujamwelewa zitto kabwe, dakika chache zilizopita mhe. Zitto ame post kwenye facebook maneno yafuatayo "the party through its secretariat has adopted a westminster system to elect the leader of the opposition, following that chadema caucus has endorsed rt. Hon. Freeman mbowe as the leader, zitto kabwe as his deputy and tundu lisu as chiefwhip." mimi kam mpiganaji wa miamvuli nasema nimependezwa na mhe. Zitto kutoa kauli hii ambayo inaonyesha yeye binafsi amependezwa na hatua hiyo na kuwa yuko tayari kuwatumikia tanzania wote na mimi nikiwepo. Tuko pamoja. Peoooopleeee

nafikiri hili litakuwa ni funzo kwa wale wote ambao bado hawajatambua kuwa chadema is a governmnet in the making, and any govarnmnet has its procedure of doing things however good or bad. Chadema has now moved from stage ya kutumia hamasa kufanya mambo yake. Hivyo sote tunatakiwa kuifahamau na kuiheshimu katiba ya chadema na vyombo vyake vya maamuzi badala ya kila mtu kwa kutumia jina lake bandia katika jf, facebook, twitter n.k kuwa msemaji wa chadema.

sina maana kuwa chadema isikosolewe, ninachotaka kusema ikiwa kabla ya vikao vya chadema havijakaa na kutoa maamuzi watu watajichukulia madaraka ya kuvisemema vikao hivyo, hiyo sio swa hata kidogo. mfano halisi ni masuala haya mawili ya kub na viti maalum. Kabala kub haijamuliwa na vikao tayari baadhi yatu tulikuwa tushaanza kulipuka na kama tungekuwa sehemu moja natumai baadhi yetu wangerushiana hata ngumi. Katika suala la viti maalum vikao vya chama vimeshafanya uamuzi ni haki ya wanachama na wapenzi tunaweza kuendelea na kuunga mkono na kukosoa kama tupendavyo. Na natumaini wajumbe wa vikao hivyo watakuwa wanajifunza kitu kutokana na majadiliano yetu.

hivyo kama tutakuwa na informed discussions with facts tutakuwa tunakisaidia chama kupitia kwa wajumbe husika.

Nawatakia kila la kheri katila ili jukumu jipya la kuunda kambi ya upinzani, diama tukumbuke kuwa kudai haki bila kufuata taratibu hizo ni fujo!!!!!!!
 
chadema ni chama makini sana. basi kuna mivilaza, mingine inajipenyeza humu humu kutaka kuchafua chama.
 
Jamani mambo yote yanaenda poa wakuu, swali kunafununu yoyote kuwa upinzani wanasimamisha mgombea uspika mmoja? kwakuwa napata tomaini tunaweza kuwamwaga hawa mafisadi as wanamakundi.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom